Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

KWA JINA LA MWENYE ENZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU .
MALENGO YA SITE YA KIISLAMU YA IMAMAINI ALHASANAINI, NI KUUSOGEZA MBELE UISLAMU KWA KUPITIA NJIA YA USAMBAZAJI WA MAANDIKO YA MTUME PAMOJA NA MAIMAU (S.A.W.W), MAANDIKO AMBAYO YAMETUFIKIA SISI KWA KUPITIA KALAMU ZA WANAZUONI
LENGO LETU HASA NI KUUSAMBAZA UTAMADUNI WA UISLAMU HALISI NA KUILEA JAMII KWA KUIRAHISISHIA NJIA YA KUVIPATA VITABU ASILI PAMOJA NA MASOMO YENYE KUPANDISHA ELIMU. NA HAZINA HII IKO WAZI KATIKA SITE HII KWA KILA MTU MWENYE SHAUKU YA UCHUNGUZI WA KIELIMU.
KUTUMIA NYENZO ZA KISASA ZA MAWASILIANO KAMA VILE INTERNET KATIKA KUFANYA TABLIGHI NA KUSAMBAZA ELIME YA KIISLAMU AMBAYO CHIMBUKO LAKE NI AHLUL-BAIYT, NI JAMBO LILILOTILIWA MKAZO SANA NA KITENGO CHETU, NA KWA MSINGI HUU BASI NDIYO MAANA TUKAWEKA MAKTABA MAALUM KATIKA SITE HII ILIYOBEBA NDANI YAKE MAUDHUI TOFAUTI ZA VITABU NA MAKALA, KAMA VILE VISOMO VYA QURAN, HUTUBA NA MAWAIDHA, MASOMO YA HAUZA (DARSA MAALUM), DUA NA ZIARA, KASIDA, PAMOJA NA MAOMBOLEZO YANAYOWAHUSU MTUME PAMOJA NA ALI ZAKE (S.A.W.W).