UCHUNGUZI WA IMAM MAHDI
 

 

IMEANDIKWA NA: AMIR ALY DATOO

BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM
IMAM MAHDI KWA MUJIBU WA WANAZUONI WA AHLI SUNNA
Katika sehemu hii ninajaribu kuwaleteeni makala haya juu ya Uthibitisho wa kuwapo kwa Imam Mahdi a.s. kwa mujibu wa Wanazuoni wa Ahli Sunna1 kwa sababu yatasaidia kutoa utata juu ya swala hili la kuwapo kwake kwani wengi wanazua kuwa mambo yote juu ya Imam a.s. yapo yamezuliwa na Mashiah.

(1). HADITH YA KWANZA
Hadith hii ifuatayo inatuonyesha dhahiri kuwa kuna haja ya kuwapo kwa Imam wa zama na kumtii yeye ni faradhi kwetu sisi,kama vile wanavyoinakili Maimamu wa Kishiah na vile vile Wanazuoni wa Ahli Sunna pia wananakili vivyo hivyo katika vitabu vyao. Hadithi mashuhuri ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. inayopokelewa na madhehbu yote ni kama ifuatavyo: "yeyote yule atakayekufa bila ya kumtambua na kumjua Imam wa zama zake basi mtu huyo atakufa mauti ya ujahili (yaani atakufa kifo cha ukafiri)."

Uzito wa Hadith hii itaeleweka vyema na umuhimu wake pia utakapoelewa kuwa mwana wa khalifa wa pili Abdullah bin Omar alipopata habari kuwa Abdul Malik amekuwa khalifa na hizo habari zilipomfikia akiwa Madina wakati wa usiku,basi aliondoka wakati huo huo na kumwendea mdhalimu huyo Hajjaj nyumbani mwake.Hajjaj alimwuliza sababu ya kufika kwake wakati huo wa usiku na hapo alimwambia kuwa amefika kumtolea bay'a (ahadi ya utiifu) ya baba yake Abdul Malik.

Hajjaj alimwelezea kuwa hakuwa na fursa wakati huo hivyo amwijie kesho yake.Hapo Abdullah bin Omar alisikitika mno na kusema "je nikifa usiku wa leo,basi nitakuwa nimekufa bila ya kufanya bay'a ya imamu wa zama zangu na kwa mujibu wa kauli ya Mtume Mtukufu s.a.w.w.,basi nitakuwa nimekufa mauti ya ujahiliyya ambavyo ni ukafiri.Hivyo vyo vyote vile,lazima chukua bay'a yangu."

Hajjaj alimwita ndani (hivyo inamaanisha kuwa mtoto wa khalifa Omar alikuwa bado yupo nje) ya nyumba yake na kumwambia kuwa alikuwa anashughulika na hivyo mikono yake ilikuwa mashghuli hivyo atoe bay'a yake miguuni mwake. Hivyo huyo masikini mtoto wa khalifa Omar aliifanya bay'a miguuni mwa Hajjaj kwa ajili ya utiifu wa Abdul Malik.Baada ya kufanya hivyo,alirejea nyumbani akiwa amefurahi mno.
(Sharh ya Nahjul Balagha - Ibn Abi al-Hadid,j.3,uk.362.Chapa ya Misri)

Jambo la kustaajabisha ni kwamba Abdullah ibn Omar katika zama za ukhalifa wa Amiral Muminiin Imam Ali ibn Abi Talib a.s. hakufanya bay'a na alikaa kimya na baada ya kupita miaka minne na nusu alipitisha kipindi hicho bila ya kumtambua Imam wa zama zake na wala hakuwa na khofu ya kufa mauti ya kafiri ! Vyema Hadith hii inatuonyesha waziwazi kuwa katika kila zama kuna ulazima wa kuwapo kwa Imam wa zama hizo na ambavyo maarifa yake ni lazima yaelekee kwa kila mtu na vile vile katika 1 Katika sehemu ya kwanza ya kitabu hiki,tumezungumzia juu ya 'dalili za kudhihiri kwa Imam Mahdi a.s.kwa marefu na undani zaidi.Hivyo hii ni sehemu ya pili ya kitabu hiki juu ya uthibitisho wa kuwapo kwake. Makala haya yametarjumiwa kutoka itmam-i-Hujjat cha S.S.Akhtar Rizvi katika lugha ya Urdu na yamewahi kuchapishwa katika Sauti ya Bilal no.6 Juzuu XXII Novemba 1988.

zama zetu hizi pia yupo Imam ambapo inatuwia faradhi kuwa na ilimu na maarifa yake,ama sivyo atakayekufa bila ya kumjua na kufanya bay'a yake atakufa kifo cha kikafiri. Vile vile kuna wataalamu wa kuwapotosha watu kuwa wao wanadai kuwa neno Imam linamaanisha Quran Tukufu.Je watu kama hawa hawawezi kuelewa kuwa Mtume Mtukufu s.a.w.w. hakulitumia neno la Imam peke yake bali alitumia Imamu wa zama ? Yaani kusudi lililopo hapa ni kule kubadilika kwa Imam katika kila zama yaani baada ya Imam mmoja atafuatia Imam wa pili na kuendelea. Jee na Quran imekuwa ikibadilika katika kila zama au jee kuna taarifa yoyote ya kuja kubadilika ?Jee baada ya Quran moja itafuatia ya pili na kuendelea ?.Kwa hakika sisi tusipotoshwe na wazushi kama hao kwa kutumia hila zao.

(2). HADITH YA PILI
Madhehebu yote ya Islam kwa pamoja yanaelezea Hadith ifuatayo na ambayo ni uthibitisho wa ukweli wa Kiislamu na vile vile Sahih Bukhari na vitabu vingine vyote vya Hadith pia vinaelezea kuwa Mtume Mtukufu s.a.w.w. alisema: "Baada yangu watakuwapo Maimamu kumi na wawili ambao watatokana na Maqureish."

Hadith zenye madhumuni kama haya yamepewa milango makhsusi katika vitabu vya Hadith. Na Hadith hii ipo yenye umuhimu mkubwa mno kwetu sisi kwani twaitegemea mno na kuweza kuelezea usahihi na ubatilifu wa Ukhalifa. Jambo lililowazi katika Hadith hii ni kuwa,iwapo kutapungua kwa idadi au kuzidi katika idadi ya kumi na wawili ama kutokea nje ya Qoeish basi mfululizo huo wa makhalifa utakuwa si ule aliouelezea Allah swt kwa kupitia Mtume Mtukufu s.a.w.w..Kwani haiwezekani kamwe kuwa Allah swt alIssahau au kufanya kosa katika kuelezea idadi ya makhalifa wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na ambavyo kwa hakika idadi hiyo sivyo au labda kwa ajili ya kufanya kubadili au labda inawezekana Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliutoa huo ubashiri bila ya kupokea Wahyi (ufunulio kutoka kwa Allah swt). Haiwezekani kamwe kwa Allah swt kusahau au kutenda bila ya maarifa au kusema kwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. bila ya kupokea wahyi ,basi itawezekanaje kwa idadi ya makhalifa aliyoielezea Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. iwe imekosewa? Kwa hakika itatubidi tuyakini kuwa ijma',Istikhlaf,shuraa au taratibu zinginezo ambazo ndizo ziizotokezea utawala wa ukhalifa baada ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na ambao makhalifa wao hawakubakia katika idadi ya kumi na wawili au tawala hizo hazikuwa zile zilizopendwa au kubainishwa na Allah swt.

Kwa kifupi, Mashiah wanayo fakhari kwa kuwa na Makhalifa kumi na wawili tu kama vile alivyothibitisha Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na vile vile alibashiri majina,idadi na kabila lao pia.

(3). HADITH YA TATU
Allamah Syed Jamal ud-Din Muhaddath ambaye ni mwachuoni mkubwa wa Ahli Sunna,anaandika katika kitabu chake Rawdhat ul-Ahbaab kwa kumnakili Sahaba Ja'abir ibn Abdullahi Ansari wakati Allah swt alimfunulia Aya hii Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.:- "Enyi mlioleta Imani! Mtiini Allah swt na Mtume wake na vile vile mumtiini 'ulil Amr'."

"Basi mimi (anaendelea Bwana Jaabir) niliuliza "Ewe Mtume wa Allah swt! Sisi tunaelewa Allah swt pamoja na Mtume wake.Lakini jee ni wakina nani hao ambao wanajulikana kama 'ulil Amr" ambao utiifu wao umefaradhishwa kwetu sisi?" Hapo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alitoa majibu haya yafuatayo:
"Wao watakuwa Makhalifa baada yangu na wa kwanza miongoni mwao ni Ali ibn Abi Talib na amfuataye atakuwa ni mwanae Hasan na atamfuatia Hussein na baadaye atafuatia Ali ibn al- Hussein na baadaye Mohammad ibn Ali na anatambulika katika Tawrati kwa umashuhuri wa jina la Baqir na ewe Jaabir! Karibu utafikia zama zake na hapo tafadhali naomba unifikishie salamu zangu.

Baada yake atakuja Ja'afer as-Sadiq bin Mohammad na baadaye Musa ibn Ja'afer na baadaye Ali ibn Musa na baadaye Muhammad ibn Ali na baadaye Ali ibn Mohammad na baadaye Hasan ibn Ali na baadaye Muhammad ibn al-Hasan ambaye atakuwa juu ya ardhi hii kama hujjatillah na bakiyallah katika wamchao Allah swt. Huyo ndiye atakayepata ushindi wa mashariki hadi wa magharibi wa dunia hii. Na yeye mwenyewe ambaye atakuwa hayupo mbele ya wafuasi (Mashiah) wake na wale wampendaye hadi kwamba hao hawatabakia katika itikadi ya Uimamu illa wale tu ambao Allah swt ameshawachukulia mitihani ya nyoyo zao." Jaabir r.a. anaelezea kuwa "mimi sikusita kumwuliza Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. "Ewe Mtume wa Allah swt! Je katika zama za Ghaibat, wafuasi (Mashiah) wake wataweza kufaidika naye?"

Hapo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alijibu:
"Naam ! Kwa kiapo cha Allah swt ambaye amenituma nikiwa Mtume wake,kuwa katika zama zake za Ghaibat ,Mashiah wake watang'arika kwa nuru yake na kufaidika kwa Ukhalifa wake kama vile watu wanavyofaidika na jua hata kama litakuwa limejificha katika mawingu." Hadith hii tukufu ambayo imenakiliwa na mwanachuoni mashuhuri wa Ahli Sunna kutokea kwa Sahaba Jaabir ibn Abdullahi ansari r.a. ambaye ni mmaarufu na mwenye kuheshimiwa katika Islam.

Hivyo inatudhihirishia katika Hadith hizi tatu, wazi kuwa dunia haiwezi kubakia tupu illa kwa Makhalifa kumi na wawili na ni faradhi kwa kila Mwislamu kuwa na maarifa na ilimu yao na hao wote kwa pamoja wameshakwisha tambulishwa kuwa ni nani hao na kwamba Khalifa wa kumi na mbili hatakuwa akionekana machoni mwa watu (atakuwa katika hali ya ghaibat) na kipindi hicho kitakuwa kirefu kiasi kwamba nyoyo zilizokwisha imtihaniwa,nyoyo zao zitakuwa salama na nyoyo zisizojaribiwa na zisizo na imani zitakuwa zikifanya mzaha na kuyapitisha kwa kicheko na Muumin watakuwa wakifaidika nae kama vile wanavyofaidika kwa jua hata kama litakuwa mafichoni.

Vivyo hivyo haiwezekani kwa Mtume Mtukufu s.a.w.w. amekwishatubashiria juu ya Ghaibat bila ya kutubashiria juu ya dalili na kudhihiri kwake 2 Napenda kuwaleteeni baadhi ya Hadith zinazozungumzia juu ya kudhihiri kwa Al-Mahdi a.s. na uthibitisho wa kuwapo kwake. Kwa hakika Hadith zote ni mutawatir na hivyo hazihitaji dalili za ziada kwa sababu Shia na Sunni wote kwa pamoja wanaitikadi kuwa Imam Mahdi Sahib az-Zamaan a.s. anatokana na kizazi cha Bi.Fatimah az- Zahra a.s na kwamba atadhihiri katika kipindi cha karibu na Qiyama.

(4). HADITH YA NNE
Imam bu Dawud ameandika katika kitabu chake Sunan na Imam Tirmidhi anaandika katika Sahih Tirmidhi kwa kumnakili Abu Said Khudhri,kuwa:
" Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema:
' Mahdi anatokana nami na mwenye uso unaong'aa na pua yake iliyo ndefu ataijaza ardhi kwa uadilifu na haki kama vile itakavyokuwa imeshajaa kwa dhuluma na ufIssadi, na atatawala kwa kipindi cha miaka saba.' "

(5). HADITH YA TANO
Imam Abu Dawuud katika Sunan amendika kwa kumnakili Sayyidina Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s :
"Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema kuwa iwapo kwisha kwa dunia hata kama ni siku moja itakayobakia,hivyo pia Allah swt atamtuma mtu mmoja kutokana na Ahlul Bayt yangu (kizazi changu) humu duniani ambaye ataijaza dunia kwa uadilifu na haki kama vile itakavyokuwa imejaa kwa dhuluma na ufIssadi."

(6). HADITH YA SITA
Imam Abu Dawud amemnakili Ummul Moominiina kufuatilia mfululizo huo wake kuwa: Mtume Mtukufu s.a.w.w amesema kuwa 'Mahdi atatokana na Itrati (kizazi) yangu,yaani atatokana na kizazi cha Fatimah az-Zahra a.s.'

"

(7). HADITH YA SABA
Imam Bukhari katika Sahih Bukhari , Imam Muslim katika Sahih Muslim na Kadhi ibn Mas'ud Baghawi katika Tasnif Sharh al-Sunnah. Wote wanamnakili Abu Hurayrah akisema: "Amesema Mtume Mtukufu s.a.w.w. 'Je hali yenu itkuwaje wakati Mtume Issa a.s. atakapoteremka kwenu na Imam wenu atakuwapo ametokea miongoni mwenu?'"

(8). HADITH YA NANE
Imam Tirmidhi katika Sahih Tirmidhi na Imam Abu Dawud katika Sunan Abu Dawud wanamnakili Abdullah Ibn Mas'ud akinakili riwaya: " Amesema Mtume Mtukufu s.a.w.w. kuwa dunia haitakwisha hadi hapo mfalme wa Kiarabu hatatokea kutokana na kizazi changu,na ambaye jila lake litakuwa kama jina langu."

(9). HADITH YA TISA
Imenakiliwa na Maimamu wa Ahli Sunna katika Sahih zao,riwaya ifuatayo: Amesema Mtume Mtukufu s.a.w.w. "Atatokezea mtu mmoja katika Ahlul Bayt yangu,atakayetawala na jina lake litakuwa kama jina langu."

(10). HADITH YA KUMI
Imam Abu Is-haq Tha'alabi katika tafsir yake anamnakili Anas bin Malik kuwa: Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema kuwa " Sisi wana wa Abdul Muttalib ni viongozi wa watu wa Jannah,yaani mimi , Hamza, Ja'afer na Ali na Hasan , Hussein na Mahdi." Dalili zote hizi zimefanya wazi kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ametuthibitishia nidhamu ya ukhalifa kwa urefu na undani katika maneno yaliyo wazi na yenye balagha na katika maelezo hayo yaliyokuwa na umuhimu zaidi ni juu ya Imam Mahdi a.s. na kipindi chake cha Ghaibat na vile vile kuhusu kudhihiri kwake.

Iwapo kutakuwa na watu ambao wataendelea kushuku kuhusu Hadith hizo,basi hapa chini ninawaleteeni shahada walizozitoa Wanazuoni na Maulamaa wa Ahli Sunnah kwa kuthibitisha itikadi ya Imam wa kumi na mbili yu bado hai na kwamba yupo katika Ghaibat na atadhihiri katika kipindi cha kabla ya Qiyamah Na itikadi hii inaaminiwa na Ahli Sunna na Mashiah. (1). Allamah Abdul Wahab Shu'arani
Ni mwanachuoni mkuu katika Ahli Sunna na ambaye amesifiwa mno na Shah Waliullah Dehlavi kuwa ni Sahabi Fadhail na Makarim Aarif Muhaqqiq Awliyaullah na kumshirikisha katika Irthani Rasulullah.

"Na miongoni mwao wapo Sheikh Saleh,Abid al-Zahid mwenye kashif sahih na bwana adhimu Sheikh Hasan Iraqi,na umri wake ulikuwa kadiri ya miaka mia moja na thelathini,na mara moja mimi na Abul Abbas Harashi,tulimwendea,naye alituambia kuwa mimi ninataka kuwaambieni jambo moja ambalo nyie munaweza kuelewa hali yangu ya ujana hadi wakati ule (utakaouelezea)." Sisi tulimwelezea kuwa atuelezee.Naye alisema kuwa "mimi wakati huo nilikuwa kijana kamili na huko Shaam (Damascus) nilikuwa nikijifunga nguo ya kujivika shingoni hadi miguuni (abaa) na nilikuwa sijizuii katikakutenda madhambi(kwani nilikuwa nikijivunia juu ya nafsi yangu). Basi siku moja mimi niliingia katika chuo cha Bani Umayyah,na huko nilimwona mtu mmoja amekaa juu ya kiti akielezea juu ya Imam Mahdi a.s. na hali ya kudhihiri kwake. Basi hapo moyoni mwangu nilijawa na mapenzi yake Imam Mahdi Sahib az- Zamaan a.s. na nikaanza kuomba duaa kwa Allah swt kuwa anikutanishe naye Mahdi a.s.

Ulipita kiasi cha mwaka mmoja hivi nikiwa nikiomba duaa hiyo,siku moja baada ya magharibi nilikuwa katika Msikiti wa Jamea na mara nilimwona kwa ghafla mtu mmoja wa makamo akiingia Msikitini akiwa amevaa kilemba cha kama Waajemi na amevaa jubba lililotengenezwa kwa ngozi ya ngamia,na akiwa amegusa mabega yangu,alisema: "Je kwa nini unataka kuonana nami ?" Nami nilimwuliza, 'Je wewe ni nani ?' Alijibu, "Mimi ni Mahdi."

Basi mimi nilibusu mikono yake na nilimwomba aje nami hadi nyumbani kwangu,naye alinikubalia na kuwa mgeni wangu kwa muda wa siku saba na alinifundisha dhikiri ya Allah swt na alinihukumu kuwa niwenikifunga saumu siku za katikati na kila siku niwe nikIssali sala za rakaa mia tano na kwa ajili ya kutaka kulala,nisiwe nikiuweka uso wangu hadi usingizi utakapokuwa ukinighalibu kabisa.Baadaye alitaka kuondoka,na kuniambia, "Ewe Hasan! Sasa baada yangu usiende kwa mtu yeyote yule na chochote kile ulichokipata ktoka kwangu kinakutosha kabisa na ujue kuwa kile walichonacho wengine ni kidogo na khafifu kuliko kile ulichonacho wewe,kwa hivyo usichukue hIssani za wengine zisizo na faida.Mimi nilisema sam'an wa ta'atan! ,na nilimshukuru na kumruhusu kuondoka na nilitaka kumsindikiza,lakini nilipofika mlangoni,alinizuia nisiendelee na kuniambia nirudie hapo.

Basi mimi nilibakia katika hali hiyo kwa miaka.Nami nilimwuliza Imam Mahdi a.s.kuhusu umri wake,naye alinijibu,Ewe Mwana! Umri wangu kwa sasa hivi ni miaka 620." Sheikh Hasan Iraqi anaelezea kuwa mazungumzo haya yamepita miaka mia moja iliyopita(yaani wakati huo umri wa Imam Mahdi a.s. ulikuwa wa miaka 720). 'Allamah Abdul Wahab Sha'arani anaelezea kuwa mimi nilimwelezea hayo Ali Khawasi na ambaye aliwafikishia umri wa Imam Mahdi a.s. na ile ya Sheikh Hasan Iraqi."

Kutokana na kisa hicho cha hapo juu si kwamba tu Allamah Abdul Wahab Su'arani bali hata Sheikh Hasan Iraqi na Ali Khawasi,hawa wazee watatu wanatupatia uthibitisho wa Itikadi zao za kuwapo kwa Imam Mahdi a.s. na mmoja wa watatu hao alibahatika kuupata ugeni wa Imam Mahdi Sahib az- Zamaan a.s. na vile vile kupata fursa ya kuelimishwa na Imam Mahdi Sahib az-Zamaan a.s. Vile vile Allamah Abdul Wahab Shu'arani ameandika katika kitabu chake mashuhuri Yanaqut wa Jawahir katika sura ya sitini na tano juu ya dalili za kukaribia Qiyamah,anaelezea dalili ya kwanza ikiwa ni kudhihiri kwa Imam Mahdi Sahib az-Zamaan a.s. na baadaye akielezea dalili zingine anaandika wakati ambapo Din itakapokuwa ikififia,basi:
"Wakati huo ndio unaotakiwa kumsubiri Imam Mahdi a.s. adhuhuri na huyo Imam a.s. atakuwa ni mtoto wa Imam Hasan al-Askari a.s. na alizaliwa tarehe 15 Sha'aban mwaka 255 Hijriyyah. Naye yu hai na ambaye yu bado hai hadi atakapoungana na Mtume Issa bin Maryam a.s. Umri wake wakati huu ni miaka 958,miaka 706 imeshakwisha."

(2). Mawlana Ali Akbar Mawdudi
Huyu ni miongoni mwa Maulamaa wakubwa mutakhirina naye ameandika, yanayojulikana kwa jina la Makashifat na mwandishi huyu katika kuelezea juu ya Ali ibn Sahil il-Isfihani,anaandika: "Watu wanasema kuwa kutokufanya makosa katika hukumu au maamrisho ya Din ni sifa ya Mitume tu,lakini Sheikh r.a. amekhitilafisha jambo hili miongoni mwa watu katika Hadith ile ambayo imeshuka juu ya Mahdi a.s. akiyeahidiwa Babu yake a.s..Baadaye katika sura ya arobaini na tano ameandika kuwa Sheikh Abul Hasan al-Shadhili r.a. amesema kuwa zipo dalili kumi na tano za Qutb - Shakhsiyya ya pekee kiongozi - mfano kwamba uthibitisho wake unatokana na ucha Mungu wake,kutokuwa na madhambi,rehema,ukhalifa na niaba na kudura huwa vinamsaidia na kudhihirisha waziwazi dhati yake na sifa zake na kadhalika,n.k."

Basi kwa kauli hii (kuwa katika Qutb kuna kuwapo na ile sifa ya kutokuwa na madhambi) inathibitisha kwa usahihi kuwa madhehebu ya wanaoamini kuwa wapo Maasum (wasio na madhambi) mbali na Mitume......kwa sababu kuwapo kwa utawala wa al-Mahdi Maw-ud (aliyeahidiwa) a.s. (yaani yeye ni Qutb baada ya baba yake Imam Hasan al-Askary a.s. kama vile Imam Hasan al-Askary a.s. alivyokuwa Qutb baada ya baba yake hadi hapo huu mfulululizo unamfikia Imam Ali ibn Abi Talib a.s. ) inatuelezea ishara ya kuwa rutuba hii inakuwa makhsusi kwa ajili ya kizazi hiki tu(Baada ya Imam Ali ibn Abi Talib a.s. kuwa Qutb hadi al- Mahdi al-Maw-ud a.s.,na wala si kabla ya Imam Ali s.a.).

Hivyo yeyote yule atakayekuwa Qutb basi atakuwa ni katika niaba ya al-Mahdi al-Maw-ud a.s. kwa sababu Imam Mahdi Sahib az- Zamaan a.s. yupo ghaibu mbele ya macho ya watu na papo hapo huwa anaonana na baadhi ya watu makhsusi na huwa sikatika hali ya ghaibu mbele yao...... Hivyo imekuwa ni lazima kuelewa kuwa kila Imam a.s. katika Ithna-Asheria ni Maasum (wasiye na dhambi)--- elewa faida hii !" Kwa maelezo hayo,inatuwia waziwazi kuwa Mawlana Ali Akbar Mawdudi anamchukua Imam al- Mahdi al-Maw-ud a.s. kuwa ni Qutb wa zama baada ya Imam Hasan al-Askary a.s. na vile vile alikuwa akitikadi kuwa alikuwa Maasum (asiye na madhambi) na vile vile alikuwa akisema daima kuwa Imam Mahdi Sahib az-Zamaan a.s.alikuwa haonekani kwa wote illa wale walio makhsusi tu ndio walioweza kumwona.

(3). Mulla Jamiy r.a.
Huyu ni Aalim mashuhuri katika Ahli Sunna na iwapo mtu atataka kumsifu yeye basi ni sawa na kutaka kuumulika jua kwa taa zetu,huyo anaeleweka kwa kuwa ni kitovu cha ilimu ya dhahiri na batini.Yeye ameandika katika tasnif yake mashuhuri Shawahid Nubuwwah kuwa al-Imam Mahdi a.s. ni Imam wa kumi na mbili na ameandika sura moja ndefu sana ambamo ameandika juu ya kiujiza na karama kabla ya kuzaliwa kwa Imam Mahdi Sahib az-Zamaan a.s. na wakati wa kuandika matukio yote .Vile vile ameandika kuwa mimba ya Imam a.s. ilikuwa haionekani na kuzaliwa kwake tu alisujudu na kusoma aya za Qurani Tukufu.

Naye alizaliwa akiwa amekwishakaa jando na hakuwa na ngozi ya utosini na katika bega lake kulikuwa kumeandikwa jaal haq wa zahaqal baatil,innal batila kana zahuqa na pale alipokula chfya alisema alhamdulillahi rabbil aalamiin. Ameandika habari hizi na kama hizi kwa mapana na marefu sana na kwa kutoa maelezo marefu na baadaye ameandika hivi:
"Rawi (mwenye kuripoti) amesema kuwa mimi nilikuwa pamoja na Imam Hasan al-Askary a.s. na nilimwambia "Ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ! Je ni nani atakayekuwa Imam au Khalifa baada yako ?" Basi Imam a.s. alikwenda ndani na alirejea akiwa na mtoto mikononi mwake. Mtoto huyo alikwa mfano wa mbalamwezi --- akipendeza na alijawa nuru---na umri wake ulikuwa kama miaka mitatu hivi.

Hapo akasema " Ewe Fulani ! Iwapo wewe usingalikuwa daraja la juu mbele ya Allah swt,basi mimi nisingalikuonyesha kamwe huyu mtoto.Jina lake ni jina la Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na kuniyah yake ni ile ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.. Na huyu ni yule ambaye atakayeijaza dunia kwa uadilifu na haki kama vile itakavyokuwa imejaa kwa dhuluma na ufIssadi." Vivyo hivyo ipo riwaya nyingine isemayo Wakati Imam Hasan al-Askari a.s. alipomwonyesha mtoto wake na kusema: "Huyu ndiye Imam wenu !" na hapo Imam Mahdi a.s. aliteremka kutoka mapajani mwa Imam Hasan al-Askary a.s.. Abu Mohammad a.s. alimwambia mwanae "Ewe mwana ! Uwe mafichoni (ghaibu) hadi wakati maalum" hivyo aliingia ndani ya chumba huku mimi nikimwona. Hapo Imam Hasan al-Askary a.s. aliniambia "inuka na ukamtafute huyo mtoto" .Nami nilikwenda kumtafuta huyo mtoto chumbani,lakini sikumwona mtu yeyote !

(4). Khwaja Muhammad Parsa
"Ilikuwa ni jambo lafuraha mno kwa masheikh na maulamaa kwa kukutana naye",anaandika katika kitabu chake Faslul Khitab : Na wakati Abdullah Jaafer,mwana wa Imam Ali an-Naqi a.s. alipozusha habari kuwa ndugu yake Imam Hasan al-Askari a.s. alikuwa hana mtoto yeyote na hivyo yeye akiwa kama ndugu yake,basi uimamu ulikuwa umepatiwa yeye. Kwa hakika alikuja kuwa mashuhuri kwa jina la kadhib (mwongo) ....... Na mtoto wa Imam Hasan al-Askary a.s. ni Mohammad al-Mahdi a.s. na watu makhsusi walijua na wanajua.

Baadaye mwandishi anaendelea kuelezea kuwa ilipofika tarehe 15 Sha'aban mwaka 255,usiku huo Bi.Hakimah Khatun alikuja nyumbani mwa Imam Hasan al-askary a.s. naye hakumruhusu kuondoka na kulipokaribia wakati wa alfajiri,alizaliwa Imam Mahdi a.s. na baada ya hapo,mwandishi anaendelea kuandika:
"Hakimah Khatun anaelezea:
"Nilipomwijia Imam Hasan al-askary a.s. nilimwona mtoto aliyezaliwa na kuviringishwa katika kitambaa cha rangi ya kijani na us wake ulikuwa umejaa kwa nuru na furaha hadi kunifanya mimi nijiwe na mapenzi yake moyoni mwagu. Mimi nilimwambia Imam Hasan al-Askary a.s. 'Ewe Imam wangu ! Iwapo unayo ilimu yoyote kuhusu huyu mwana mpenzi,basi naoma nami uniambie machache.'

Imam a.s. aliniambia,"Ewe dada yangu! Huyu ndiye yule Imam asubiriwaye ambaye tulikuwa tumeshakwishapata ubashiri wake." Bi.Hakimah Khatun anasema kuwa 'mimi papo hapo nilifanya sujuda ya kumshukuru Allah swt.Na nilikuwa nikienda daima nyumbani mwa Imam Hasan al-Askary a.s..Lakini siku moja nilikuwa sikumwona huyo mwana na papo hapo nilimwuliza Imam Hasan al-Askari a.s. 'Ewe Imam wangu ! Je umemfanya nini Imam wetu al-Muntadhir (aliyengojewa) ?"

Imam a.s. alinijibu, "Mimi nimeshampa katika hifadhi ya Allah swt ambaye alikadhibiwa Mtume Musa na mama yake katika hifadhi Yake (i.e.Allah swt). " Ibara hii imekuwa ikitoa hidaya lakini vile vile imetuongezea uhakika kuwa Khwaja Muhammad Parsa pia ni muumin wa Imam al-Asr (Imam Mahdi a.s.) na vile vile juu ya ghaiba na pia alikuwa akiitikadi kuwa pale atakapotaka Allah swt ndipo atakapodhihiri,hapo ndipo itakapotimia ubashiri wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.

Vile vile katika kitabu hiki Khwaja Muhammad Parsa ameandika dalili za kudhihiri kwa Imam al- Muntadhar a.s.:
Na zipo Hadith nyingi mno zisizokadirika kuhusiana na maswala haya,na Imam Mahdi radhiyallahu Anhu (Imam-i-Zamana -- ambaye haonekani machoni mwa watu na ambaye yupo katika kila zama) anaelezewa mambo mengi mno yaliyo mema kabisa na vile vile zipo Hadith zinazooana kuhusiana na swala la kudhihiri kwake na kusambaa kwa nuru yake. Yeye ataimarisha sharia ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.na atafanya jihad kwa ajili ya Allah swt .Ataitakasisha kwa kutokomesha najisi na maonevu juu ya ardhi ya Allah swt kutokea ncha moja hadi ya pili,zama zake zitakuwa ni zama za muttaqiina (wacha Mungu),masahaba wake hawatakuwa na mashaka au udanganyifu wa aina yoyote ile na vile hawatakuwa na aibu za aina zozote zile na watakuwa wakimfuata Imam wa zama na kutanda kwa mujibu wa hidaya zake na Allah swt atawajaalia maarifa ya Imam Mahdi Sahib az- Zamaan a.s. Imam Mahdi Sahib az-Zamaan a.s.ndiye atakaye khitimisha Ukhalifa na Uimamu na kwamba yeye yu Imam kuanzia siku ile ambayo baba yake (Imam Hasan al- Askary a.s.) alipokuwa shahidi."

(5). Sibt ibn Jawzi
Huyu pia ni miongoni mwa Maulamaa wakubwa wa Ahli Sunna,naye katika kitabu chake mashuhuri Tadhkirt khawas al-ummah fi ma'arifat il-Aimmah anaandika kuhusiana na Imam al-Mahdi a.s.: Yeye ni mwana wake Imam Hasan al-Askary a.s. na kuniyyah yake ni Abu Abdillah na Abul Qassim. Naye ni i Khalifa hujjat, Imam wa zama hizi,ni Qaim na Muntadhar na baqi na yeye tu ndiye Imam-i-zamana (Imamu wa zama).

Je kunaweza kubakia chochote katika kuelezea kubakia hai na kuwapo kwa Imam Mahdi a.s.? (6).Abu Abdillah Muhammad ibn Yusuf bin Muhammad Ghibhi Shafi'i Utunzi wake upo mashuhuri wa kifayat il-taalib na vile vile ameandika kitabu kingine albayan ambacho ameandika khususa juu ya hali ya Imam Zamana a.s. kuzungumzia Uimamu,kuwapo kwake,umri wake mrefu na akiandika na kutoa maelezo juu ya kuwapo kwake Imam al-Mahdi al- Maw-ud a.s.,anaandika:
Kuanzia ghaibat ya Imam Mahdi a.s. kuwapo hai kwake hadi leo kuna dalili moja ya kwamba si muhali kwake kubakia kwake hadi leo. Katika Maawliya Allah wapo Mtume Issa bin Maryam a.s. na Mtume Khizr a.s. na Ilyas a.s. na hao wapo hai na katika maadui wake Allah swt wapo Dajjal na mal-un Iblis nao wote pia wapo hai. Na kubakia kwao hai na maisha yao yanaelezea katika Quran na Hadith na vinathibitishwa hivyo. (Iwapo Allah swt anawaweka hai na baki shakhsiyyah zingine,jee itashindwa nini kumweka hai na baki Imam Mahdi a.s.?)

(7). Sheikh Nurdin ibn Sibagh al-Malik
Sheikh mashuhuri na mwenye kuheshimiwa katika Ahli Sunna,anaandika kwa marefu juu ya kuwapo kwa Imam Mahdi a.s. katika kitabu chake Al-Fusul ul-muhimmah kama yafuatavyo: ' Sura ya kumi na mbili: Katika kuzungumzia mwana wa Imam Hasan al-Askary a.s. aitwaye Abul Qasim Muhammad hujjat Khalaf Saleh,naye ambaye ni Imam wa kumi na mbili,na kuelezea historia yake ya kuzaliwa na Uimamu wake na katika dalili zake na hali yake na ghaibat na muda wa kuwapo kwa autawala wake na katika kuelezea nasabu yake,kuniyyat na laqab yake. '

Katika sura hii kuna habari nyingine ielezewavyo,lakini tunanakili badhi ya habari kama ifuatavyo: Mwana wa Imam Hasan al-Askary a.s. aliyeitwa Abul Qasim alizaliwa tarehe 15 mwezi wa Sha'aban katika mwaka 255 Hijriyyah,katika mji wa Samarrah huko Iraq ....... Na hali hii inatudalilisha juu ya mtoto huyo aliyezaliwa ni Imam wa kumi na mbili na ambavyo ipo imebashiriwa na Maimamu watukufu a.s. Zipo riwaya nyingi kuhusu yeye na Hadith nyingi zipo mashuhuri,nasi bila ya kufikiria tumefupisha maelezo yote yale na kuyaacha na muhaddithiin wanaziandika Hadith zile ambazo zimetolewa na wanatutaka sisi tuzikusanye hizo Hadith ....

Maulamaa wa Hadith wamesema kuwa Mahdi ni yule yule ambaye ni qaim al-Muntadhar na kuhusu kudhihiri kwake riwaya zote zipo zinaoana na kuhusu nuru yake pia wanaafikiana na vile vile dhuluma zote zitaangamia kwa kuja kwake,na kwa kuja kwake hapatakuwa na kiza cha aina yoyote illa mng'aro kama vile usiku unavyobadilika katika siku, na ni karibu tu yeye atajitokeza kutoka ghaibu na nyoyo zote zitajawa kwa furaha tele.

(8). Shah Waliullah Dehlavi
Ahli Sunna wanamwita khatimil Aarifiin,Sayyidil Muhaddithiin,sanadil Mutakallimiin,Hujjatulahi ala-Aalamiin anaelezea kwa marefu mno katika tasnif yake Fadhlul Mubiin juu ya Imam wa zama na kuwapo kwake na pia amekuwa mwenye kuamini juu ya Uimamu.Hivyo anaandika kwa kunakili Hadith moja:
Mimi nimesema kuwa Ibn Akilah ameniruhusu kwa mdomo mambo yote ambayo riwaya zilikuwa zinaruhusiwa kwa ajili yake.Nami katika mfululizo wa Hadith niliikuta Hadith moja mfululizo ambayo kila sehemu yake ilikuwa ikichukua upeke wa aina yake na ilikuwa na sifa adhimu ya watu wakuu,nayo ni kwamba Ibn Aqila alisema kuwa mimi niliarifiwa na Sheikh mkuu pekee wa aina yake katika zama zote Sheikh Hasan Ibn Ali Ajmiy,naye aliarifiwa na hafidh wa nyakati zake Bwana Jamalud-Din Babli aliarifiwa na mnakili na mtoa mawaidha,Bwana Muhammad Hajjazi naye aliarifiwa na Sufi wa wakati huo Sheikh Abdul Wahab Shu'arani,naye aliarifiwa na Mujtahid wa zama zake Jalaludin as-Suyuti,naye aliarifiwa na zahid wa zama Imam Jamaluddin ibn Muhammad ibn Muhammad al-Jamal,naye amearifiwa na aliyekuwa Muhaddith wa nchi za Uajemi Imam Muhammad ibn Mas'ud,naye amearifiwa na Sheikh mkuu wa zama zake Sheikh Isma'il bin Mudhaffar Shirazi,naye aliarifiwa na Muhaddath wa nyakati zake Abdus-Salaam bin Abu ar-Rabi'i Hanafi,naye amearifiwa na Sheikh wa zama zake Abu Bakar Abdullah bin Muhammad Shaabur al-Kalamsi,naye amearifiwa na Imam wa wakati wake Abdul Aziz ibn Muhammad Adami,naye amearifiwa na aliyekuwa mtu wa nadra wa zama zake Suleiman bin Ibrahim bin Muhammad bin Suleiman naye amearifu kuwa amemwarifu Ahmad bin Hashim Biadhuri ambaye amebainisha kuwa aliyekuwa hafidh wa zam zake aliambiwa na Imam al-Asr a.s.

Muhammad ibn al-Hasan ibn Ali (aliye katika hali ya ghaibu kuwa mimi (Imam Mahdi) niliambiwa na Baba yangu Imam Hassan al-Askary a.s., naye aliambiwa na Baba yake Imam Ali an-Naqi a.s. naye aliambiwa na Baba yake Imam Muhanmadtaqi a.s. naye aliambiwa na Baba yake Imam Musa al-Kadhim a.s. naye aliambiwa na Baba yake Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. naye aliambiwa na Baba yake Imam Muhammad al-Kadhim a.s. naye Imam Zainul Aabediin a.s. naye aliambiwa na Baba yake Imam Syyidus-Shuhadaa, al-Husein ibn Ali ibn Abi Talib a.s. naye aliambiwa na Baba yake Sayyidil Awliya'a Ali ibn Abi Talib a.s. naye aliambiwa na Sayyidil Ambiya Mtume Mtukufu s.a.w.w. naye aliambiwa na Sayyidil Malaika Jibraili naye amesema kuwa Allah swt amesema "Mimi ni Allah na wala hakuna mwingine wa kuabudiwa ila ni mimi tu. Yeyote yule atakaye kubali na kusadiki upweke wangu basi atakuwa ameshaingia katika ngome yangu na yeyote yule atakaye kuwa ameingia katika ngome yangu, basi ameepukana na adhabu zangu."

Katika riwaya hii tumeonyeshwa kuwa si Shah Waliullah Dehlavi tu bali Maulamaa kumi na sita wa Ahli Sunna ambao walikuwa na sifa pekee katika zama zao... ambao walikuwa akiamini juu ya Imam Mahdi Akhiruz-zamaan a.s. kuhusu jina lake na ukoo wake na hali yake ya ghaibat na kuwapo kwake akiwa Imam wa zama zetu kwani asingelileta riwaya kama hiyo iwapo mmoja wa waarifu wake angelikuwa hajulikani kwa utukufu wake mbele yake, hivyo aliwaheshimu wote waliotajwa kwa pamoja.

(9) Sheikh Abdul Haq Dahlavi
Ni miongoni mwa wale walio mashuhuri katika sunan, naye ameandika katika risala yake Munaqib wa ahwaal Aimma at-haar kuwa: Na mwana wa Hasan al-Askary a.s. aliyeitwa Muhammad al-Mahdi a.s. alikuwa akijulikana na Sahaba makhsusi na kundi lililokuwa likiaminika tu. Ipo riwaya kuwa Bi. Hakimah Khatun binti Imam Muhammad Taqi a.s. ambaye alikuwa ni dada wa baba yake Imam Mahdi a.s. na alikuwa akiomba mno kwa Alah swt amjaalie mtoto Imam Hasan al-Askary a.s. ili aweze kumwona kwa macho yake katika uhai wake. Na Imam Hasan al- Askary a.s. alikuwa amemchagua Bi. Nargis Khatun kwa ajili ya ndoa. Ilipofika tarehe 15 ya mwezi Sha'aban mwaka 255 Hijriyyah, Imam Hasan al-Askary a.s. alimwambia Bi.

Hakimah Khatun abakie nyumbani kwake usiku ule kwani kulikuwa na jambo moja mbele yao usiku ule.Basi kwa mujibu wa ombi la Imam Hasan al-Askari a.s. Bi. Hakimah alibakia nyumbani mwa Imam a.s. Ilipokaribia wakati wa alfajiri, hali ya Bi. Nargis Khatun ilianza kubadilika. Naye Bi. Hakimah alimkaribia ili kumsaidia lakini alimkuta anaye mtoto mzuri mno aliyezaliwa na akiwa amekwisha tahiriwa na kuogeshwa, nk. Alimchukua mtoto huyo na kumleta kwa Imam a.s. naye alimpapasa kwa mkono juu ya bega lake na macho yake na aliuweka ulimi wake mdomoni mwa mtoto huyo, na aliisema Adhaan katika sikio lake la kulia na aliisema Iqamah katika sikio la kushoto na baadaye alimwambia:"Ewe Bibi! Mchukue huyu mtoto kwa mama yake" Na hivyo Bi. Hakimah Khatun alimpeleka mtoto kwa mama yake.

Bi Hakimah Khatun anasema kuwa:"Baadaye nilimwona mtoto akiwa mikononi mwa baba yake akiwa amevishwa nguo za rangi ya kijani na akitokwa na nuru hadi mimi nilijawa na maenzi yake hadi hapo yalinitoka:'Ewe Imam wangu!Je kuna chochote unachokielewa kuhusu huyu mtoto aliyezaliwa ili uweze kuniambia?"

Imam Hasan al-Askary a.s. alisema:"Ewe dada yangu! Huyu mtoto ni yule ambaye alikuwa akisubiriwa (al-Muntadhar) na ubashiri wake tulikuwa tumeshaupata." Bi Hakimah Khatun anasema:"Mimi nilifanya sujuda juu ya ardhi kwa kutoa shukrani zangu kwa Allah swt. Na daima nilikuwa nikija nyumbani kwa Imam Hasan al-Askary a.s. Na siku moja nilipokuja sikumwona huyo mtoto, basi sikusita kuuliza,"Ewe Imam wetu!Je imemwia nini Sayyidil Muntadhar wetu?"

Hapo Imam Hasan al-Askari a.s. alinijibu kuwa alikuwa ameshamkabidhi yule ambaye alikabidhiwa na mama yake Mtume Musa a.s. Na vile vile inapatikana riwaya isemayo kuwa aliulizwa jina la Qaim wao litakuwa nini, alijibu kuwa:"Sisi tumehukumiwa kutotamka jina lake kabla ya kuzaliwa kwake." Je dalili zote hizo hazitoshelezi kuthibisha kuwapo kwa Imam Mahdi a.s?

(10) Muhaddith Jamalud- Din
Huyu bwana anahesabiwa miongoni mwa walio mabingwa katika ilimu ya Hadith na vitabu vyake vinatazamwa kwa heshima kubwa. Yeye anadhihirisha itikadi yake katika kitabu chake mashuhuri kiitwacho Rawdhatil Ahbaab hivi:
Mazungumzo katika bayani ya Imam wa kumi na mbili:
Mu'tamin Muhammad bin Hasan katika riwaya nyingi mno zinazooana zinaelezea juu ya kuzaliwa kwa Imam al-Mahdi a.s. ilikuwa ni tarehe 15 Sha'aba 255 Hijriyyah mjini Samarrah na mama yake alikuwa ni mtumwa aliyeitwa Sakil au Susan au Nargis. Majina ya Imam a.s. yalikuwa yakifanana na yale ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na vile vile al-Mahdi al- Muntadhar na Khalafi Saleh na Sahibu az-Zamaan. Kwa mujibu wa riwaya katika kzama za Baba yake (ambaye ni karibu na usahihi) alikuwa na umri wa miaka mitano na pengine labda ni miaka miwili ambapo Allah swt alipomjaalia hekima na alipatiwa daraja la juu la Uimamu kama Mitume Yahya a.s. Zakariyyah a.s. Imam wa zama a.s. katika kipindi cha Khalifa Mu'atamad na katika mwaka 265 au 266 Hijriyyah, inasadikiwa kuwa katika mji wa Samarrah, alikuwa ghaibu."

(11) Allamah Muhiddin bin' Arabi
Kwa sasa tunawaleteeni ushahidi wa Allamah huyu wa Kisunni na ambavyo kauli yake hadi leo ipo mashuhuri kuwa: Hussein a.s. aliuawa kwa upanga wa Babu yake (Mtumes.a.w.w.) kwa sababu Bay'a ya Yazid ilikuwa imefanyika na Hussein a.s. alimwasi (huyu Yazid aliyekuwa imam wa haki). (Je ni nani aliyekuwa juu ya haki: Hussein au Yazid)?

Ni dhahiri kuwa iwapo Sheik mwenye msimamo mkali kama huo (kwani amethubutu kumwita Yazid kuwa ni Imam wa haki na kwamba Imam Hussein a.s. kuwa ni mwasi)! Akianza kuelezea kuwa Imam Mahdi a.s. ameshazaliwa na yupo ghaibu na kufikia karibu na Qiyama atadhihiri na vile vile ni maasum na pia ameelezea kwa kinaga ubwaga sifa njema za Imam al-Mahdi a.s. na kumsifu katika kila hali, basi inathibitisha waziwazi kuwa haki daima huwa juu ya kila kitu. Naye katika kitabu chake mashuhuri kiitwacho Futuhaati Makkiyyah katika sura ya 386 anaelezea kwa kirefu juu ya habari zinazomhusu Imam zamana na ametumia karatasi nyingi mno katika hayo, nanakuleteeni baadhi ya habari hizo juu ya kudhihiri kwa Imam Mahdi a.s., zama zake na haki na mwanzoni mwake au zile zinazozungumzia sifa zake au kuhusiana kiilhamu au kiwahii na kuimarisha Din kwa mara ya pili na bayani ya uharifu wake, nk.

Hivyo tunakuleteeni madondoo yanayozungumzia juu ya majina yake, unasaba wake, kuzaliwa kwake na vile vile ghaibat:
Na muelewe kuwa kudhihiri kwa Imam al-Mahdi a.s. ni dharuri, lakini yeye hatadhuhuri hadi dunia itakapokuwa imejaa kwa dhuluma na ufIssadi, basi atadhihiri kwa kuijaza dunia kwa uadilifu na haki na ikiwa hata kama itabakia siku moja katika umri wa dunia, basi Allah swt atairefusha siku hiyo hadi hapo huyu Khalifa atatawala naye atatokana na kizazi chake Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na atakuwa katika wana wa Fatimah az-Zahra a.s. na babu yake ni Hussein ibn Ali ibn Talib a.s. na Baba yake mzazi ni Imam Hassan al-Askari ibn Ali an-Naqi a.s. (aliendelea kuelezea nasaba nzima hadi kumfikia Imam Amiral Muuminii Ali ibn Abi Talib a.s.) ...Vile vile mjue kuwa jina lake litakuwa likiaafikiana na jina la Mtume Mtukufu s.a.w.w.

...Na pia mujue kuwa wakati Imam Mahdi Sahib az-Zamaan a.s. atakapodhihiri, Waislamu wote kwa pamoja na wale walio makhususi watafurahi mno...Na sasa kipindi chake kimeshafika na kipindi hicho ndicho kipindi mulichomo. Naye atadhihiri katika karne ya nne ambayo ni kabla ya karne tatu zilizopita (yaani wakati wa suluhu katika kipindi cha Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ndicho kipindi cha kwanza, kipindi cha pili ni kile kilichofuatiwa cha tabiin na kipindi cha tatu ni kile cha tabaa Tabiin kilipita kipindi fulani baada ya vipindi vitatu hivi na kulizuka matukio mapya mapya mawazo na matamanio ya nafsi yalIssambaa kote na umwagikwaji wa damu ulitokea naye huyo (al-Mahdi a.s.) alikuwa ghaibu kwa kipindi kirefu hadi 'utakapotokezea' wakati maalum wa kudhihiri.

12. Kamaluddin bin Talha Shafi'i
Huyu ni Aalim mmoja wapo miongoni mwa wale waliokuwa mashuhuri katika hali Sunna, na kauli yake inasadikiwa kuwa ni sahihi katika figh, Hadith na usul na katika kila fani, naye ametasnif kitabu kilichopo mashuhuri matalib il-usuul fi manaaqib Ali Rasuul humo katika sura ya kumi na mbili, Allamah huyu kubatilisha shaka za wazushi yaliyokuwa yakifanywa na wale waliokuwa dhidi yake. Tunawaleteeni baadhi ya habari kutoka kitabu chake, zinazozungumzia juu ya Imam Mahdi a.s. kuhusu jina lake, nasaba yake na kuzaliwa kwake na vile vile ghaibat n.k:
Sura ya kumi na mbili
Katika kuelezea juu ya Abul Qasim Muhammad Hujjat ibn Hassan Khalis (Askary) ibnAli Mutawakkil bin Muhammad (Taqi) Qania bin Ali ar-Ridha a.s. anaandika: ".....basi alizaliwa (al-Mahdi a.s.) tarehe 23 Ramadhaan 258 Hijryyah katika mji wa Samarrah. Lakini nasaba yake kwa upande wa Baba na mama yake ni Imam Hasan al-Askari a.s. (nasaba nzima hadi kufikia kwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s.) na habari yake kamili ipo imeelezwa mwanzoni, na mama yake alikuwa mtumwa, aliyeitwa Sakiil na vile vile Hakimah pia aliitwa Muhammad, pia anatambuliwa kwa majina ya Abul Qasim, al-Hujjat, Khalaf Saleh na Muntadhar."

Baadaye zinazungumziwa Hadith za Mtume Mtukufu s.a.w.w. juu ya Imam Mahdi a.s. zinazothibitisha kuwa sifa zote hizo (zilizopo katika Hadith) pamoja na majina yake zinapatikana katika Imam Hujjat a.s. kwa hivyo sasa inatubidi kuamini na kusadiki kuwa ni yeye tu al-Mahdi Maw-ud na kwamba atadhihiri pale patakapokuwa hukumu ya Allah swt Katika mazungumzo haya ameandika kurasa nyingi mno, na baadaye anaendelea kuandika kuwa:
Lakini umri wake unapohusika, ni kwamba yeye (al-Mahdi a.s.) alikuwa katika zama za Khalifa Mu'tamid Allah na alikuwa katika hali iliyojaa khofu na hapo ndipo alipokuwa ghaibu... Na kudra ya Allah swt ipo wasili (pana) na amewajaalia rehema zake waja wake na iwapo mashekhe wakubwa wakubwa watataka kujua na kuelewa sababu za kudura na uhakika wa yale ayatendayo (Allah swt), basi hao mashekhe hawataweza kamwe kufanikiwa na macho yao yatachoka na watarejea wakiwa katka hasara na ndimi zao zitasema na kuchoka kwani Allah swt anatuambia katika Qurani tukufu:Hamkupewa ilimu isipokuwa kidogo.

Na si jambo lenye kustaajabisha kuwa Allah swt kurefusha umri wa watu walio makhususi au kuwazidishia umri wao kwa ziada ya kipindi fulani.Je Allah swt hajawazidishia kundi moja umri wao ukawa mrefu.....na miongoni mwa maawliya na ma-asfiya na miongoni mwa waliokhilafuDin? Basi katika Maasfiyallah yupo Mtume Issa a.s. na pia humo yupo Imam al-Mahdi a.s. na katika Ambiya, wapo wengi ambao umri yao ipo mirefu hata kuzidi miaka elfu moja au wengineo wanaokaribia miaka elfu moja mfano Mtume Nuh a.s. na wengineo, na katika maadui wake Allah swt wapo Iblis na Dajjal3 na vile vile kuna wengineo kama qaum ya Add4 ambao walikuwapo watu waliokwisha fikisha miaka hata zaidi ya elfu moja, navyo vivyo hivyo yupo Bwana Luqman, na mifano yote hiyo inaletwa mbele yenu kwa kutaka kuwaonyesha kuwa ni uwezo wake Allah swt na ni amri yake kwa kutaka kwake anawazidishia umri mrefu wale awatakiao.Sasa itamwiaje vigumu kumrefushia umri mrefu al-Mahdi a.s. na je kuna ugumu au ukatazo wa aina gani kwa kufanya hivyo?

Iwapo ni Allah swt mwenyewe akihitaji kufanya hivyo? Basi hadi yeye (al-Mahdi a.s.)adhihiri, tunaendelea kutekeleza maamrisho yake Allah swt, na kwa kuwa kauli imeshafikia hadi hapa na kalamu imeshafikia mwishoni mwake, basi sisi twamaliza uandishi wa makala haya kwa kalimah ya Alhamdu-lillahi rabbil Aalamiin kwani hiyo ndiyo kalimah tukufu ya waendao katika Jannah kwa kuridhiwa na Allah swt kwani ndiyo dua ya mwisho ya waendao Jannah.

MWISHO
VITABU VILIVYOKUSANYWA NA KUTARJUMIWA NA AMIRALY M. H. DATOO
BUKOBA - TANZANIA
Anwani ya pepe: datooam@hotmail.com
Hazina kubwa ya elimu inapatikana katika mtandao :
o www.alitrah.org
o www.dartabligh.org
o www.al-islam.org/kiswahili
VITABU VILIVYOTAYARI
1. AHADITH 2500 ZA MTUME S.A.W.W. NA MA-IMAMU A.S.
2. BWANA ABU TALIB a.s. MADHULUMU WA HISTORIA
3. DALILI ZA QIYAMA NA KUDHIHIRI KWA IMAM MAHDI a.s.
4. DHAMBI KUU LA ISRAAF ( UFUJAJI )
5. DHAMBI KUU LA KHIANA
6. DHAMBI KUU LA KUFICHA UKWELI
7. DHAMBI KUU LA KULA VIAPO VYA UONGO
8. DHAMBI KUU LA KUTOA USHAHIDI WA UONGO
9. DHAMBI KUU LA KUTOKUTIMIZA AHADI
10. DHAMBI KUU LA UCHAWI
11. DHAMBI KUU LA ULAWITI
12. DHAMBI KUU LA ULEVI
13. DHAMBI KUU LA KUTOKULIPA ZAKA, KHUMS NA SADAQAH
14. ELIMU KWA MADRASSAH : KITABU CHA KWANZA
15. FUNGUO ZA PEPONI - DUA MBALIMBALI
16. HADITHI ZA WATOTO ( PAMOJA NA PICHA )
17. HISTORIA YA ISLAM
18. HUKUMU ZILIZOTOLEWA NA IMAM 'ALI IBN ABI TALIB a.s.
19. IMAM ALI IBN ABI TALIB a.s. : FADHAIL NA HUKUMU
20. JANNAT NA JAHANNAM
21. JE MAKHARIJI NI NANI ?
22. KANUNI ZA SAUM
23. KESI YA FADAK
24. SADAKA : KUTOA NA KUPOKEA
25. MAANDISHI YA NAWHA 200 ZA 14 MASUMIIN a.s. (KATIKA LUGHA YA URDU )
3 Katika sehemu ya kwanza ya kitabu hiki,kuna habari kwa marefu na mapana kuhusu huyu Dajjal kwani
anazungumziwa katika riwaya nyingi mno katika dalili mojawapo ya kuja kwa Imam Mahdi a.s.
4 Kuhusu kusoma vIssa katika Quran unaweza kupata vIssa na masimulizi mengi mno katika kitabu nilichokitayarisha
katika maudhui haya.
1 4
26. MAELEZO NA KANUNI YA HAJJ
27. MAFUNZO 150 YA MAISHA
28. MAKALA MCHANGANYIKO No. 1
29. MAKALA MCHANGANYIKO No. 2
30. MAKHALIFA 4 BAADA YA MTUME MUHAMMAD MUSTAFA S.A.W.W.
31. MASIMULIZI KUTOKA QUR'AN TUKUFU
32. MKUSANYIKO WA FAHIRISTI YA AYAH ZA QUR'AN
33. MSAFARA WA IMAM HUSAYN IBN Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. MADINA - KARBALA
34. MWONGOZO KATIKA KUTENGENEZA USIA.
35. NAWHA, MARTHIYYAH 3100 ZA 14 MASUMIIN a.s. (SAUTI KATIKA LUGHA YA URDU)
36. TADHWIN AL-HADITH
37. TAJWID ILIYORAHISISHWA
38. TAWBA
39. USAMEHEVU KATIKA ISLAM
40. UWAHHABI - ASILI NA KUENEA KWAKE
41. VITA VILIVYOPIGANWA KATIKA ISLAM
42. WAANDISHI MASHI'A KATIKA SAHIH NA SUNAN ZA AHL SUNNA
43. WANYAMA WALIOTAJWA KATIKA QUR'AN TUKUFU
VITABU VILIVYOCHAPWA
44. DHAMBI KUU LA KAMARI
45. DHAMBI KUU LA RIBA
46. DHAMBI KUU LA UWONGO (juzuu ya kwanza )
47. DHAMBI KUU LA UWONGO (juzuu ya pili )
48. HEKAYA ZA BAHLUL
49. KITABU CHA TAJWID
50. NDOA KATIKA ISLAM
VITABU VINAVYOTAYARISHWA
1. DHAMBI KUU LA KUDHULUMU HAKI ZA WENGINE AU KUTOZITIMIZA
2. DHAMBI KUU LA KUDHULUMU MALI YA MAYATIMA
3. DHAMBI KUU LA KUIBIA UZITO
4. DHAMBI KUU LA KUKWEPA JIHAD
5. DHAMBI KUU LA KURUDIA UKAFIRI BAADA YA KUSILIMU
6. DHAMBI KUU LA KUTOKUJALI ADHABU ZA ALLAH swt
7. DHAMBI KUU LA KUTOKUWATII WAZAZI
8. DHAMBI KUU LA KUVUNJA UHUSIANO NA NDUGU NA JAMAA
9. DHAMBI KUU LA KUWASAIDI MADHALIMU
10. DHAMBI KUU LA KUWATUHUMU WATU KWA ULAWITI
11. DHAMBI KUU LA MAUAJI
12. DHAMBI KUU LA MUZIKI
13. DHAMBI KUU LA SHIRK
14. DHAMBI KUU LA UTUMIAJI WA KILICHO HARAMISHWA
15. DHAMBI KUU LA UWIZI
16. DHAMBI KUU LA ZINAA
17. DHAMBI KUU LA KUTOWASAIDIA WANYONGE
18. HIARI NA SHURUTISHO KATIKA ISLAM
19. MADHAMBI MAKUBWA NA MADHAMBI MADOGO
20. MAJINA YA WATOTO WAISLAMU
21. MASWALI NA MAJIBU MBALIMBALI
22. QUNUT
23. QURBAA-MAPENZI YA WANANYUMBA YA MTUME MUHAMMAD MUSTAFA S.A.W.W.
24. TAFSIRI YA JUZUU' 'AMMA
25. TAFSIRI YA SURAH AL-YA-SIIN
26. TAQWA
27. TUSIUPOTEZE WAKATI
28. USINGIZI NA NDOTO
29. YAAS

MWISHO