MAHOJIANO BAINA YA MLAHIDI NA IMAMU JA'FAR SADIQ (A.S.)

 

MAHOJIANO BAINA YA MLAHIDI NA IMAMU JA'FAR SADIQ (A.S.)


Kimeandikwa na:
Sheikh Tabrisi


Kimetafsiriwa na:
Sayyid Muhammad Raza Mahdi Shushtary

Kimetangazwa na:
Bilal Muslim Mission of Tanzania,
S.L.P. 20033, Dar es Salaam,
TANZANIA.

Haki ya kunakili imehifadhiwa na:
Bilal Muslim Mission of TanzaniaISBN 9976 956 08 8

Toleo la Pili: 1990 Nakala 2500
Toleo la Tatu: 2007 Nakala 2500SHUKRANI

Hii ni tafsiri ya Kiswahili ya mahojiano baina ya Mlahidi mmoja na Imamu Ja'far Swadiq (a.s.) kama yalivyonakiliwa katika kitabu kiitwacho "IHTIJAJ" cha Sheikh Tabrisi na kutafsiriwa kutoka ukurasa wa 42-90 wa kitabu cha Kiingereza kiitwacho "BIOGRAPHY OF IMAM JA'FAR-E-SADIQ A.S)" kilichotolewa na Peer mahomed Ebrahim Trust, Karachi (Pakistan).

Safari moja Imamu Ja'far Swadiq (a.s.) aliwahi kuhojiana na Mlahidi mmoja, na mahojiano hayo yalikwenda kama ifuatavyo: -

MLAHIDI: Vipi viumbe wanaweza kumwabudu Mwenyeezi Mungu ambaye hawamwoni?