BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

 

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

 

IMEANDIKWA NA NDUGU ZETU WA KIISLAMU.

 

MASHARTI YA KUWA MUISLAMU WA KWELI

Kila Muislamu anatakiwa muwa na masharti hata yafuatayo:-

1. Ayashughulikie mambo ya wenzake kama anavyoyashughulikia yake.

2. na awapendelee anayoyapendelea.

3. Awafanyie anayopenda wamfanyie, mambo kikowa ukifanya utafanyiwa.

na anayewafanyia wenziwe hayo mema, na yeye afanyiwe ili azidi kuendelea na asije akavunjika moyo akayawachia, akasikitika kama alivyosikitika mtu huyu aliyesema:-

Nami nilitaahadi kichango kuwa ni changu

Haona hapana budi ni machezo na wenzangu

Haya sikuyafanidi kukosa heshima yangu.

Na asije akawavunja watu moyo wasifanye mema kama aliyewavunja nyoyo huyu aliyesema:

Zema zinapandwa wapi Hazipaliliye

Ninunue na madoo Maji nitiliye.

Kama zema zinalipwa Ningelipwa miye.

Na katika aya nyengine, Allah (s.w) anasema:-

[1]

Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa Watu wa Kitabu nao wameamini ingeli kuwa bora kwao. Wapo miongoni mwao waumini, lakini wengi wao wapotovu.

Maelezo kuhusiana na Aya ya 110 ya Surat Al-Imrani.

Hapa inatajwa sababu ya kuwa bora umma huu, basi natushikamane nayi, au hatutakuwa hivyo, zingatia Aya ya 143 ya Suratul-Baqarah. Aya ambayo tayari tumeshaitolea maelezo yake.

 

ٰ ٰ ٰ ٰ [2]

Na vivyo hivyo tumekufanyeni muwe Umma wa wasitani, ili muwe mashahidi juu ya watu, na Mtume awe ni shahidi juu yenu. Na hatukukifanya kibla ulicho kuwa nacho ila tupate kumjua yule anaye mfuata Mtume na yule anaye geuka akarejea nyuma. Na kwa yakini hilo lilikuwa jambo gumu isipo kuwa kwa wale alio waongoa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu hakuwa mwenye kuipoteza Imani yenu. Kwani Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa watu na Mwenye kuwarehemu.

Na katika Aya ya 78-79 ya Surat Maaidah Mola (s.w) anabainisha hivi:-

ٰ ٰ
[3]

Walilaaniwa walio kufuru miongoni mwa Wana wa Israili kwa ulimi wa Daud na wa Isa mwana wa Maryamu. Hayo ni kwa sababu waliasi na wakawa wanapindukia mipaka.

Maelezo kuhusiana na Aya ya 78-79 Almaidah

Unatajwa hapa ubaya wa:-

a)Kutoamrisha mema, b)Kutokataza mabaya, kwa mkono wake, kama hawezi basi akataze kwa ulimi wake, hata hili ikiwa anaogopa ndiyo achukie kwa moyo wake, lakini hii ni daraja ndogo kabisa ya Uislamu- unaogopa hata kusema!

wametia Makadiyani ukafiri wao tena katika aya hii waliyoifanya kuwa ni ya 79 wakaandika hivi:-

Yesu alipigiliwa msalabani, ukafiri wao huo wa kumpinga Mwenyeezi Mungu wakasema kama Manasara, kuwa Nabii issa amesulubiwa na hali ya kuwa Mwenyeezi Mungu anasema wamaa salabuhu (hawakumsulubu).

Watu hao walikuwa hawakatazani maovu waliyo kuwa wakiyafanya. Hakika ni maovu yalioje mambo waliyo kuwa wakiyafanya!.

Kwa hiyo, watu pekee watakaokuwa na idhini ya kuzungumza siku ya Kiyama, idhini ambayo watapewa na Mwenyeezi Mungu, ni wale watakaozungumza mazungumzo ya haki.

[4]

Siku atakapo simama Roho na Malaika kwa safu. Hawatasema ila Mwingi wa rehema aliye mruhusu, na atasema yaliyo sawa tu.

 

Maelezo kwa ufupi kuhusiana na makala iliyopita.

* Walimwengu wote siku ya Kiyama watapitia hatua tatu, kuhudhuria katika uwanja wa siku ya Kiyama, kuhesabiwa amali na matendo yao, na kupata malipo kulingana na yale mema na mabaya waliyoyatenda.

* Makafiri na waovu watahudhuria katika uwanja wa hesabu wakiwa na hofu na woga mkubwa kutokana na mabaya waliyoyatenda, na siku hiyo hawatapata idhini ya kuzungumza chochole ila kwa idhini ya Mola wao.

* Waumini na wacha Mungu watahudhuria katika uwanja wa hesabu wakiwa na nyoyo tulivu zilizotulia kwa furaha, hii ni kutokana na yale mema waliyoyatenda, na Mola atawapa waja wake hao malipo mema mazuri.

 

 

  Masuali.

1. Siku ya Kiyama kuna idadi ngapi ya visimamo, na kila kisimamo kinachukua muda gani?

2. Kwa kutumia mabainisho ya Aya za Qur-ani Elezea hatua tatu za siku ya Kiyama .

3. Kwa mtazamo wa qur-ani, ni watu wa aina gani watakuwa katika amani na salama ya Mwenyeezi Mungu?.

4. Siku ya Kiyama ni vitu gani vitakavyotoa shahada ya amali za watu waovu?.

5. Kuna tofauti gani iliyopo katika kuhudhuria katika uwanja wa siku ya Kiyama baina ya waumini na waovu?.

  

 

 

 

[1] Surat Al-Imrani aya ya 110

[2] Suratul-Baqarah Aya ya 143.

[3] Suratul-Maidah Aya ya 78-79

[4] Suratun-Nabaa Aya ya 38.


 

 

MWISHO