BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

                                                                                                                                            

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

 

IMEANDIKWA NA NDUGU ZETU WA KIISLAMU

 

QUR_ANI KATIKA MTIZAMO WA KIMAGHARIBI

Kuna vitabu vingi vilivyoandikwa na wataalamu waliokuwa sio waislamu, wataalamu hao katika vitabu vyao hivyo wameelezea na wameukubali utukufu wa kitabu hicho kitukufu, vile vile katika vitabu hivyo mmetajwa majina ya watu ambao wameukubali utukufu wa Qur-ani.

Katika kipengele hiki tutasoma kwa ufupi majina ya wataalamu hao:

- Carlituwn- As- kun ni Doctor wa ufumbuzi wa mwanaadamu anayeishi Amerika, anasema:-

Moja katika jambo kubwa na tukufu linaloonekana katika kitabu kitukufu cha Qur-ani ni balagha iliyomo katika kitabu hicho, pindi itakapokuwa Qur-ani inasomwa kwa usahihi hapana shaka kwamba msikilizaji wa Qur-ani akiwa anaielewa lugha ya kiarabu au haielewi, anafahamu au haifahamu, itamletea athari kubwa na athari hizo zitabakia katika akili yake, basi hapana shaka kwamba balagha iliyomo katika Qur-ani haiwezi kutarjumiwa.

- Ameyl Durmiyngom ni Mfaransa, yeye anasema:-

Dalili bora inayothibitisha utume wa hadharati Muhammad (s.a.w.w) ni muujiza wa Qur-ani, hakuna shaka kwamba sio wanaadamu wala majini hawajaweza wala hawatoweza kuleta au kuvumbua kitabu kama cha Qur-ani.

Hata itakapokuwa kila aya moja ilioyomo katika Qur-ani inaelezea kuhusu maisha ya Nabii Muhammad (s.a.w.w), aya hizo zimeelezewa kwa utaalamu kabisa kiasi ya kwamba mwanaadamu anaposoma aya hizo na kuzifahamu humletea athari kubwa moyoni mwake, kwa hiyo muujiza wa Qur-ani unaleta athari zaidi ukilinganisha na miujiza mengine ya kiakili.

Kiynst Gric kutoka London,ni mwalimu wa university (chuo kikuu) wa Comboriyj yeye anasema:-

Kitabu cha Nabii Isaa (a.s) hakikuandikwa katika zama za uhae wake, kwa upande mwengine kitabu cha Qur-ani kimeandikwa katika zama zake nabii Muhammad (s.a.w.w) na waandishi wake. Ama baada ya miaka 2000 hadi sasa baina ya Maulamaa wa dini ya Masihi (cristian) kuna hitilafu (wanahitilafiana) kuhusiana na mtu wa mwanzo alieandika kitabu cha Injili. Qur-ani inafahamu kauli (ibara) zote za lugha ya kiarabu na kama tukizingatia kiwango cha elimu katika nchi za Kiarabu tutagunduwa kwamba watu wengi wameihifadhi wanaifahamu na lugha ya Kiarabu kwa undani kabisa, ijapokuwa hakuna nchi yoyote iliyoweza kufikia kiwango cha elimu ya balagha iliyomo ndani ya Qur-ani.

Njia na mlolongo uliotumiwa katika Qur-ani unaonesha kwamba ndani ya Qur-ani mna maneno ya balagha nay a fasihi yanayoonekana kwa uwazi kabisa, lakini vile vile maneno hayo yamekusanya maana ya ndani kabisa.

Kiynst Gric anaendelea kwa kusema:-

“ Ama kwa upande wetu sisi watu wa London lugha iliyokuwa ikizungumzwa karne kumi na nne zilizopita katika nchi ya Britania na katika visiwa vyingi vya London sasa hivi haifahamiwi, na wataalamu wa Kifaransa ambao wanajulikana kuwa ni walimu wa lugha hawawezi kuifahamu lugha ya kifaransa iliyokuwa ikizungumzwa karne kumi na nne zilizopita”.

Bibi Lawra, Waakisa, waalgiyriy kutoka Italia ni Profesa mtaalamu wa lugha wa nchi za kimagharibi, ni mwalimu wa elimu ya tarehe na tamaduni za kiislamu, katika chuo kikuu cha Napil Italia. Yeye anasema:-

Qur-ani ambacho ni kitabu cha kiislamu ni moja miongoni mwa miujiza ya Mwenyeezi Mungu.

Moja miongoni mwa mambo muhimu yaliyoelezewa katika Qur-ani ni matokeo yatakayotokea katika zama zinazofuata, katika Qur-ani tunasoma matokeo ambayo yametokea baada ya kuteremshwa Qur-ani. Ndani ya kitabu cha Qur-ani mna elimu ya hali ya juu kabisa, elimu ambayo hata wataalamu wakubwa ambao ni mahodari waliobobea katika elimu, kwa mfano Mafilosofi (philosophy), wanasiasa na… wameshindwa kuitambuwa elimu ya undani iliyomo katika kitabu hicho.

Dalili zote hizo zinathibitisha kwamba Qur-ani sio kitabu kilichotungwa na mtaalamu wa kielimu duniani, mtaalamu ambaye ameutumia muda wake wote katika kutafuta elimu ikiwa katika sehemu maalumu au nchi yoyote ile duniani, bali Qur-ani ni kitabu kitukufu cha Mwenyeezi Mungu Mola ambaye ni mwenye elimu ya vitu vyote duniani.

 

MWISHO