TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA SABA

 TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA SABA


Haki ya kunaikli imehifadhiwa na:
AL-ITRAH FOUNDATION
ISBN: 9987-665-39-X
Kimeandikwa na:
Sheikh Muhammad Jawad Mughniyya
Kimetafsiriwa na:
Sheikh Hasan Mwalupa
S.L.P. 88290, Mombasa / Kenya.
Email:mwalupa@hotmail.com
Kimehaririwa na:
Ustadh Abdallah Mohamed:
S.L.P. 1017, Dar-es-Salaam.
Email:info@alitrah.org
Kupangwa katika Kompyuta na:
Ukht Pili Rajabu.
Toleo la kwanza: Februari 2003
Nakala: 5000
Toleo la Pili: Septemba 2004
Nakala: 2000
Kimetolewa na kuchapishwa na:
Alitrah Foundation
P.O.Box 1017
Dar es Salaam, Tanzania
Simu: +255 22 2110640
Fax: +255 22 2126757
Email: alitrah@daiichicorp.com
Website: www.alitrah.orgSURATU AL-MAAIDA {SURA YA TANO}
YALIYOMO
Aya 83 - 86: Uadui wa Mayahudi na urafiki wa
Wakristo............................................................3
Ni nani walio karibu na waislamu
kimapenzi......................................................... 4
Aya 87-88: Msiharamishe vizuri....................................... 9
Aya 89: Viapo vya Upuuzi.......................................... 11
Aya 90-92: Pombe na Kamari............................................14
Aya 93: Wenye Takua na kuamini................................16
Aya 94-96: Hakuna kuwinda katika Haram wala pamoja na
Ihram..............................................................19
Maana ya kujaribu kwa Mwenyezi Mungu....20
Aya 97-99: Nyumba takatifu.............................................24
Aya 100: Wingi wa Mwovu...........................................27
Je riziki ni bahati au majaaliwa......................28
Aya 101-102: Msiulizeulize mambo..................................... 32
Aya 103-105: Hakuna bahira wala saiba...............................36
Aya 106-108: Kuthibitisha wasia.........................................39
Aya 109-111: Mitume na siku ya kukusanywa .................. 44
Isa na Utume wa utoto................................... 46
Aya 112-115: Chakula kutoka mbinguni..............................50
Wanafunzi wa Muhammad (s.a.w) na
wa Isa (a.s).....................................................51
Aya 116-118: Issa na watu.....................................................55
Aya 119-120: Ukweli wa wakweli........................................58
AL -AN'AM { Sura ya 6}
Aya 1-3: Kuumba mbingu na ardhi....................................... 60
Aya 4-6: Kukana hoja za Mwenyezi Mungu........................63
Hakuna udikteta ardhini wala mbinguni................64
Aya 7-11: Lau tungelikuteremshia karatasi............................ 68
Aya 12-16: Amejilazimishia Rehema ........................................72
Aya 17-19: Hakuna mwondoaji madhara ila
Mwenyezi Mungu....................................................77
Aya 20-24: Wanamfahamu kama wanavyo wafahamu
wanawao..................................................................82
Aya 25-26: Nyoyo zao zina pazia...............................................87
Aya 27-32: Watakaposimamishwa motoni.................................91
Aya 33-37: Tunajua kuwa yanakuhuzunisha.............................97
Aya 38-39: Wanyama na ndege ni umma ................................102
Aya 40-45: Sema niambieni.....................................................106
Mwenyezi Mungu na maumbile............................107
Aya 46-49: Akichukua Mwenyezi Mungu kusikia na
Kuona ....................................................................111
Aya 50-55: Sifuati ila ninayopewa...........................................115
Assalamu Alaykum wa Rahmatullah.....................119
Aya 56-58: Sifuati hawa zenu...................................................122
Aya 59-62: Hazina ya siri iko kwake.......................................125
Aya 63-67: Ni nani anayewaokoa...........................................130
Aya 68-70: Mpaka waingie katika mazungumzo mengine.......134
Aya 71-73: Je, tuwaabudu wasiokuwa Mwenyezi Mungu.....138
Masufi....................................................................140
Aya 74-79: Ibrahim na Baba yake na watu wake.....................142
Aya 80-83: Je, Mnanihoji juu ya Mwenyezi Mungu................147
Aya 84-90: Na tukampa Is-haq na Yaq'ub ..............................152
Hasan na Husein ni wana wa Mtume (s.a.w)........153
Aya 91-92: Hawamheshimu Mwenyezi Mungu kama inavy
otakiwa................................................................. 158
Mitume wa Mwenyezi Mungu na wanasayansi...161
Aya 93-94: Kumzulia uwongo Mwenyezi Mungu...................166
Aya 95-99: Hutoa aliye hai katika maiti...................................171
Uhai umetoka wapi?..............................................171
Aya 100-107: Wamemfanyia Mwenyezi Mungu washirika........178
Aya 108-109: Msiwatukane.........................................................184


Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu
UTANGULIZI WA MCHAPISHAJI
Kitabu hiki kilichoko mikononi mwako hivi sasa ni juhudi ya miaka mingi sana ya watu waliojitolea kuona kazi hii imefanikiwa bila ya kumsahau Marhum Abu Muhammad wa London. Kama lilivyo jina la Tafsiri yenyewe ndivyo ilivyo Tafsiri yenyewe ambayo mwanachuoni huyu mahiri kabisa aliyeifafanua ni mtu aliyebobea katika fani zote ambazo mfasiri (Mfafanuzi) anatakiwa awe nazo. Sheikh Muhammad Jawad Mughniyya ameonesha cheche zake katika vitabu vingi alivyoviandika katika maudhui mbali mbalimbali na hivyo kujipatia wasomaji wengi sana.


Msomi huyu, mwenye fikra huru na anayetetea kile anachokiamini, ni mtu mwenye mawazo mapana na kuyaangalia mambo kwa undani sana, kipaumbele chake ni katika maslahi ya umma huu na amejaribu sana kwenda na wakati.


Sifa kubwa pekee ya mwanachuoni huyu ni kuwa yeye hakujihusisha sana na kung'ang'ania madhehebu fulani tu, labda hii yatokana na wadhifa wake wa ukadhi aliokuwa nao katika nchi ya Lebanon ambayo ina madhehebu mengi, ambapo sula la madhehebu ni nyeti nchini humo, hata hivyo yeye aliweza kuamua matatizo ya watu kwenye ofisi yake kulingana na madhehebu yao pale walipomwendea, hiyo ilimsaidia sana hata kuweza kutoa kitabu kitwacho 'Al-Fiqh a'laa madhaahabil-khamsah' (Fikhi ya madhehebu matano) yaani ya Hanafi, Maaliki, Shafi, Hambali na Shia (ambacho twataraji kitatoka hivi karibuni Inshaallah).


Jambo lililotupa msukumo wa kukifasiri kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili ni zile faida nyingi atakazozipata msomaji na kujua mambo mengi na ya ajabu yaliyo mapya kwake ambayo si rahisi kuyapata kwa wafasiri wengine.


Msomaji atapata faida katika fani za Sayansi, Siasa, Historia, Mashairi, visa vizuri, na Saikolojia miongoni mwa mengine; ndiyo maana msomaji atashangaa kidogo anapoisoma Tafsiri hii atakapoona mwandishi amewataja na kuwanukuu watu kama kina Mfalme Edward, wanasyansi kama kina Enstein, Charlie Champlin (Mchekeshaji maarufu), na wengineo,vile vile kutaja nchi mbalimbali zikiwemo za Afrika; kama vile Afrika ya kusini, Zimbabwe nk, hali inayoifanya tafsiri hii kuwa ni ya kipekee kabisa. Mtindo alioutumia mwandishi ni sahali uliokusudiwa watu wa tabaka mbalimbali, wanavyuoni na watu wa kawaida.


Nia yetu ni kukigawanya kitabu hiki bure lakini tumelazimika kukiuza kwa bei nafuu ili kurudisha gharama za uchapishaji. Mwisho: Shukrani kubwa iwaendee bila ya kuwataja watu waliojitolea usiku na mchana, jopo la wafasiri, wahariri, wachapaji, waliotupa moyo na kutoa maoni yao na walioisimamia ili kuhakikisha kwamba kitabu kimemfikia msomaji.


Makosa ya Chapa.
Sikumbuki kama nimewahi kusoma kitabu kilichotoka kupigwa chapa, cha zamani au cha sasa, bila ya kukuta makosa ya chapa. Nafikiri sitasoma kitabu kisichokuwa hivyo. Nimejaribu sana kuliepuka hilo katika tungo zangu, lakini sikufanikiwa. Nilikuwa sifikirii kama ninaweza kuona makosa haya katika maandishi ya msahafu mtukufu, kama yale yaliyo katika baadhi ya chapa; kwa mfano neno yabswutu kwa swad, badala ya yabsutu kwa sin, na katika chapa ya Tafsir Arrazi ya Misr ya mwaka 1935, Sura ya (2:146). Imeandikwa La Ya'alamuun, (hawajui) badala ya Ya'alamuun (wanajua). Mfano wa makosa haya hausameheki.


Katika Tafsir Al-Manar, chapa ya Pili, sura (5:212), imeandikwa "Fawqahum ila yawmil qiyama" badala ya "Fawqahum yawamal qiyama". Hatuwezi kusema kosa hili ni kubwa zaidi kuliko lile. Lakini mkosaji atatuletea udhuru kwa msemo mashuhuri huko kwetu jabal amail 'Makosa ya chapa.' Katika Tafsiri Majmau chapa ya Urfan, Sura (46:15), imeandikwa: " Hatta idha balagha arbai' na sanah badala ya: Hattaidha balagha ashuddahu arbai ' na sanah"


Kusema hivi sio kama ninajitetea kutokana na makosa ya chapa atakayoyakuta msomaji katika kitabu hiki, ijapokuwa naomba msamaha kama litatokea hili, lakini makusudio yangu hasa ni kumwambia yule atakayefungua macho yake kwenye makosa ya matamko na kuufungia macho uzuri wa maana. Vilevile ninamwambia yule ambaye siku moja aliniambia: "Vitabu vyako vimejaa makosa ya chapa, kama kwamba hakuna kitu chochote katika vitabu hivyo isipokuwa makosa ya chapa tu. Wote hao ninawaambia: Mungu awasamehe na aniongoze mimi na nyinyi.

Vyovyote iwavyo, mimi ninaomba msamaha kutokana na makosa ya kifikra na ya chapa. Anasema Amirul Muminiin (a.s): "Watu wote ni wapungufu wenye kuchanganyikiwa, isipokuwa yule aliyehifadhiwa na Mwenyezi Mungu." Na Mwenyezi Mungu (s.w.t) ndiye mwenye jukumu la kunikubaliayale niliyoyapatia na kunisamehe niliyakosea, kwa jaha ya Mtume na kizazi chake, ziwashukie rehema na amani (Amin). MUHAMMAD JAWAD MUGHNIYYAH