TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA SITA

 TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA SITA


Haki ya kunaikli imehifadhiwa na:
AL-ITRAH FOUNDATION
ISBN: 9987-665-39-X
Kimeandikwa na:
Sheikh Muhammad Jawad Mughniyya
Kimetafsiriwa na:
Sheikh Hasan Mwalupa
S.L.P. 88290, Mombasa / Kenya.
Email:mwalupa@hotmail.com
Kimehaririwa na:
Ustadh Abdallah Mohamed:
S.L.P. 1017, Dar-es-Salaam.
Email:info@alitrah.org
Kupangwa katika Kompyuta na:
Ukht Pili Rajabu.
Toleo la kwanza: Februari 2003
Nakala: 5000
Toleo la Pili: Septemba 2004
Nakala: 2000
Kimetolewa na kuchapishwa na:
Alitrah Foundation
P.O.Box 1017
Dar es Salaam, Tanzania
Simu: +255 22 2110640
Fax: +255 22 2126757
Email: alitrah@daiichicorp.com
Website: www.alitrah.orgSURATU AN - NISAA { Sura ya 4 }
YALIYOMO
Aya: 148-149: Dhalimu haheshimiwi......................................................2

Aya: 150-152: Wanaamini baadhi na kukanusha baadhi.......................6

Aya: 153-154: Walisema tuonyeshe Mwenyezi Mungu waziwazi............8

Aya: 155-159: Kuvunja kwao ahadi........................................................11

Aya: 160-162: Dhulma ya Mayahudi......................................................17

Irabu................................................................................17

Aya: 163-166: Tumekuletea Wahyi........................................................22

Je Mitume wote ni wa mashariki?..................................24

Aya: 167-170: Walikufuru na kuzuilia.....................................................32

Aya 171-173: Msipetuke mipaka katika dini yenu.................................35

Qur'an na wanaohubiri Utatu..........................................36

Aya 174-175: Imewafikia Hoja kutoka kwa Mola wenu........................42

Aya: 176: Mwenyezi Mungu anawapa fatwa juu ya mkiwa............45

AL - MAIDAH { Sura ya 5 }

Aya 1-2: Tekelezeni mapatano......................................................48

Mapinduzi na kupinga mapinduzi..................................51

Aya: 3: Mmeharamishiwa Mfu....................................................53

Kukamilishwa dini na kutimizwa neema.........................56

Aya: 4 Na mlichowafunza wanyama wa mawindo.....................60

Aya: 5: Utwahara wa watu wa Kitabu.........................................62

Aya:6-7: Udhu natayammam........................................................69

Irabu................................................................................69

Aya: 8-10: Uadilifu ndio Unayokurubisha kwenye Takua.................75

Aya: 11: Kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu........................77

Aya: 12-14: Kufanya agano na Waisrail.............................................80

Aya: 15-16: Imekwishawafikia Nuru...................................................85

Uislamu na wapigania amani.........................................87

Aya: 17-19: Walisema Mwenyezi Mungu ni Masih............................91

Ashaira na Wakristo.......................................................92

Aya: 20-26: Musa na watwake...........................................................97

Aya: 27-31: Qabil na Habil...............................................................102

Aya: 32: Mmoja na wengi...........................................................104

Aya: 33-34: Malipo ya ufisadi...........................................................107

Aya: 35-37: Tafuteni njia ya kumfikia...............................................110

Aya: 38-40: Mwizi mwanamume na mwanamke..............................113

Irabu..............................................................................113

Aya: 41-43: Wasikilizao sana uwongo..............................................117

Aya: 44: Usiwaogope watu.........................................................122

Aya: 45-47: Mtu kwa Mtu.................................................................125

Ukafiri, Ufasiki na Dhuluma..........................................127

Aya: 48-50: Kila uma na sharia yake...............................................131

Aya: 51-53: Msiwafanye kuwa marafiki mayahudi na wakristo......137

Petroli na mayahudi na wakristo..................................139

Aya: 54: Wanyenyekevu kwa waumini wenye nguvu kwa

makafiri.........................................................................143

Mapatano ya maadili....................................................147

Aya: 55-56: Hutoa zaka wakiwa wamerukui....................................150

Aya: 57-59: Dini yenu wameifanyia mzaha na mchezo...................153

Aya: 60-63: Akuwafanya wengine manyani na nguruwe.................158

Aya: 64-66: Mayahudi walisema mkono wa Mwenyezi Mungu

umefumba....................................................................161

Mayahudi na moto wa vita............................................165

Riziki na Ufisadi............................................................168

Aya: 67: Fikisha uliyoteremshiwa...............................................171

Mwenye al-manar na Ahlubayt.....................................173

Aya:68-69: Kusimamisha Tawrat na Injil.........................................175

Aya: 70-71: Agano la wana wa Israil...............................................176

Aya: 72-75: Mwito wa masih kwa wana wa Israil............................180

Aya: 76-81: Hawawezi kuwadhuru wala kuwanufaisha...................184

Nahw.............................................................................184UTANGULIZI WA MCHAPISHAJI
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu.
Kitabu hiki kilichoko mikononi mwako hivi sasa ni juhudi ya miaka mingi sana ya watu waliojitolea kuona kazi hii imefanikiwa bila ya kumsahau Marhum Abu Muhammad wa London. Kama lilivyo jina la Tafsiri yenyewe ndivyo ilivyo Tafsiri yenyewe ambayo mwanachuoni huyu mahiri kabisa aliyeifafanua ni mtu aliyebobea katika fani zote ambazo mfasiri (Mfafanuzi) anatakiwa awe nazo. Sheikh Muhammad Jawad Mughniyya ameonesha cheche zake katika vitabu vingi alivyoviandika katika maudhui mbali mbalimbali na hivyo kujipatia wasomaji wengi sana.Msomi huyu, mwenye fikra huru na anayetetea kile anachokiamini, ni mtu mwenye mawazo mapana na kuyaangalia mambo kwa undani sana, kipaumbele chake ni katika maslahi ya umma huu na amejaribu sana kwenda na wakati. Sifa kubwa pekee ya mwanachuoni huyu ni kuwa yeye hakujihusisha sana na kung'ang'ania madhehebu fulani tu, labda hii yatokana na wadhifa wake wa ukadhi aliokuwa nao katika nchi ya Lebanon ambayo ina madhehebu mengi, ambapo sula la madhehebu ni nyeti nchini humo, hata hivyo yeye aliweza kuamua matatizo ya watu kwenye ofisi yake kulingana na madhehebu yao pale walipomwendea, hiyo ilimsaidia sana hata kuweza kutoa kitabu kitwacho Al-Fiqh a'laa madhaahabil-khamsah (Fikhi ya madhehebu matano) yaani ya Hanafi, Maaliki, Shafi, Hambali na Shia (ambacho twataraji kitatoka hivi karibuni Inshaallah).


Jambo lililotupa msukumo wa kukifasiri kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili ni zile faida nyingi atakazozipata msomaji na kujua mambo mengi na ya ajabu yaliyo mapya kwake ambayo si rahisi kuyapata kwa wafasiri wengine.


Msomaji atapata faida katika fani za Sayansi, Siasa, Historia, Mashairi, visa vizuri, na Saikolojia miongoni mwa mengine; ndiyo maana msomaji atashangaa kidogo anapoisoma Tafsiri hii atakapoona mwandishi amewataja na kuwanukuu watu kama kina Mfalme Edward, wanasyansi kama kina Enstein, Charlie Champlin (Mchekeshaji maarufu), na wengineo, hali inayoifanya tafsiri hii kuwa ni ya kipekee kabisa. Mtindo alioutumia mwandishi ni sahali uliokusudiwa watu wa tabaka mbalimbali, wanavyuoni na watu wa kawaida.


Nia yetu ni kukigawanya kitabu hiki bure lakini tumelazimika kukiuza kwa bei nafuu ili kurudisha gharama za uchapishaji. Mwisho: Shukrani kubwa iwaendee bila ya kuwataja watu waliojitolea usiku na mchana, jopo la wafasiri, wahariri, wachapaji, waliotupa moyo na kutoa maoni yao na walioisimamia ili kuhakikisha kwamba kitabu kimemfikia msomaji.


Makosa ya Chapa.
Sikumbuki kama nimewahi kusoma kitabu kilichotoka kupigwa chapa, cha zamani au cha sasa, bila ya kukuta makosa ya chapa. Nafikiri sitasoma kitabu kisichokuwa hivyo. Nimejaribu sana kuliepuka hilo katika tungo zangu, lakini sikufanikiwa. Nilikuwa sifikirii kama ninaweza kuona makosa haya katika maandishi ya msahafu mtukufu, kama yale yaliyo katika baadhi ya chapa; kwa mfano neno yabswutu kwa swad, badala ya yabsutu kwa sin, na katika chapa ya Tafsir Arrazi ya Misr ya mwaka 1935, Sura ya (2:146). Imeandikwa La Ya'alamuun, (hawajui) badala ya Ya'alamuun (wanajua). Mfano wa makosa haya hausameheki.


Katika Tafsir Al-Manar, chapa ya Pili, sura (5:212), imeandikwa Fawqahum ila yawmil qiyama badala ya Fawqahum yawamal qiyama. Hatuwezi kusema kosa hili ni kubwa zaidi kuliko lile. Lakini mkosaji atatuletea udhuru kwa msemo mashuhuri huko kwetu jabal amail 'Makosa ya chapa.' Katika Tafsiri Majmau chapa ya Urfan, Sura (46:15), imeandikwa: Hatta idha balagha arbai' na sanah badala ya: Hattaidha balagha ashuddahu arbai ' na sanah"


Kusema hivi sio kama ninajitetea kutokana na makosa ya chapa atakayoyakuta msomaji katika kitabu hiki, ijapokuwa naomba msamaha kama litatokea hili, lakini makusudio yangu hasa ni kumwambia yule atakayefungua macho yake kwenye makosa ya matamko na kuufungia macho uzuri wa maana. Vilevile ninamwambia yule ambaye siku moja aliniambia: "Vitabu vyako vimejaa makosa ya chapa, kama kwamba hakuna kitu chochote katika vitabu hivyo isipokuwa makosa ya chapa tu. Wote hao ninawaambia: Mungu awasamehe na aniongoze mimi na nyinyi.

Vyovyote iwavyo, mimi ninaomba msamaha kutokana na makosa ya kifikra na ya chapa. Anasema Amirul Muminiin (a.s): "Watu wote ni wapungufu wenye kuchanganyikiwa, isipokuwa yule aliyehifadhiwa na Mwenyezi Mungu." Na Mwenyezi Mungu (s.w.t) ndiye mwenye jukumu la kunikubalia.