TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA PILI

 TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA PILIHaki ya kunakili imehifadhiwa na:

AL-ITRAH FOUNDATION

ISBN: 9987 665 34 - 9

Kimeandikwa na:

Sheikh Muhammad Jawad Mughniyya

Kimetafsiriwa na:

Sheikh Hasan Mwalupa

P.O. Box 1017, Dar es Salaam/Tanzania.

Email:mwalupa@hotmail.com

Kimehaririwa na:

Dr.M.S. Kanju.

S.L.P 1017, Dar es Salaam.

Email: drmkanju@yahoo.com

Website: www.dartabligh.org

Kupangwa katika kompyuta na:

Ukhti Pili Rajabu.

Toleo la kwanza: Februari 2004

Nakala:5000

Kimetolewa na kuchapishwa na:

Alitrah Foundation

P.O. Box 1017

Dar es Salaam, Tanzania

Simu:+255 22 2110640

Fax: +255 22 2126757

Email: alitrah@daiichicorp.com

Website: www.alitrah.orgYALIYOMO
AL- BAQARAH –(Sura ya pili)
Aya 142: Nini kilichowageuza kutoka Qibla chao . . . . . . . . . . .2
Kwa nini kuswali upande maalum . . . . . . . . . . . . . . .2
Aya 143: Tumewafanya kuwa ni Umma wa wastani . . . . . . . . .4
Ukamilifu na uwiano katika Uislamu . . . . . . . . . . . . .6
Aya 144-145: Hakika tunakuona unavyogeuza uso wako................10
Ni wakati gani unapasa kuelekea Qibla......................14
Watu wa Qibla.............................................................14
Uislamu na watu wenye upendeleo na dini zao 16
Aya 146-147: Wanamjua kama wanavyowajua watoto wao . . . . . . . .
18
Mimi na Mhubiri . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
18
Aya 148-152: Kila Umma ulikuwa na Qibla chake . . . . . . . . . . . . . .
20
Katiba ya Uislamu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
24
Kumshukuru Mneemeshaji . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
26
Aya 153-157: Jisaidieni kwa Subira . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
26
Thamani ya Pepo . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
30
Aina ya malipo ya wanaosubiri . . . . . . . . . . . . . . . . .
32
Aya 158: Swafa na Marwa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
34
Aya 159-162: Wanaoficha yaliyoteremshwa . . . . . . . . . . . . . . . . . .
36
Ubaya wa adhabu bila ya ubainifu . . . . . . . . . . . . . . .
38
Hukumu ya laana katika sharia . . . . . . . . . . . . . . . .
40
Aya 163-164: Na Mungu wenu ni Mungu Mmoja . . . . . . . . . . . . . . .
42
Mbingu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
42
Ardhi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
42
Kuwapo Mungu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
44
Upi uliotangulia Usiku au Mchana . . . . . . . . . . . . . . .
46
Aya 165-167: Wanafanya waungu asiyekuwa
Mwenyezi Mungu (s.w.t.) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
46
Taqlid na Maimamu Wanne . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
50
Aya 168-170: Kuleni vilivyomo katika Ardhi . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
50
Kufuata na msingi wa itikadi . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
54
Aya 171: Mfano wa anayeita asiyesikia . . . . . . . . . . . . . . . . . .
58
Aya 172-173: Kuleni Vizuri . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
60
Mwenye dharura na hukumu yake . . . . . . . . . . . . . .
62
Aya 174-176: Wafichao aliyoyateremsha
Mwenyezi Mungu (s.w.t.) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
62
Mvutano kati ya Haki na Batili . . . . . . . . . . . . . . . . . .
66
Aya 177: Anatoa mali akiwa aipenda . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
68
Wema katika ufahamu wa Ki-Qur’an . . . . . . . . . . . . .
74
Aya 178-179: Kisasi cha waliouawa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
74
Aya 180-182: Wasia kwa wazazi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
80
Kuwausia warithi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
82
Aya 183-185: Mmelazimishwa kufunga . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
84
Aya 186: Naitikia maombi ya mwombaji . . . . . . . . . . . . . . . . . .
88
Aya 187: Mmehalalishiwa Usiku wa Saumu . . . . . . . . . . . . . .
90
Aya 188: Kula mali kwa Batili . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
92 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
Hukumu ya kadhi fasiki . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu.
UTANGULIZI WA MCHAPISHAJI
Kitabu hiki kilichoko mikononi mwako hivi sasa ni juhudi ya miaka mingi sana ya watu waliojitolea kuona kazi hii imefanikiwa bila ya kumsahau Marhum Abu Muhammad wa London. Kama lilivyo jina la Tafsiri yenyewe ndivyo ilivyo Tafsiri yenyewe ambayo mwanachuoni huyu mahiri kabisa aliyeifafanua ni mtu aliyebobea katika fani zote ambazo mfasiri (Mfafanuzi) anatakiwa awe nazo. Sheikh Muhammad Jawad Mughniyya ameonesha cheche zake katika vitabu vingi alivyoviandika katika maudhui mbali mbalimbali na hivyo kujipatia wasomaji wengi sana.


Msomi huyu, mwenye fikra huru na anayetetea kile anachokiamini, ni mtu mwenye mawazo mapana na kuyaangalia mambo kwa undani sana, kipaumbele chake ni katika maslahi ya umma huu na amejaribu sana kwenda na wakati. Sifa kubwa pekee ya mwanachuoni huyu ni kuwa yeye hakujihusisha sana na kung’ang’ania madhehebu fulani tu, labda hii yatokana na wadhifa wake wa ukadhi aliokuwa nao katika nchi ya Lebanon ambayo ina madhehebu mengi, ambapo sula la madhehebu ni nyeti nchini humo, hata hivyo yeye aliweza kuamua matatizo ya watu kwenye ofisi yake kulingana na madhehebu yao pale walipomwendea, hiyo ilimsaidia sana hata kuweza kutoa kitabu kitwacho ‘Al-Fiqh a’laa madhaahabil-khamsah’ (Fikhi ya madhehebu matano) yaani ya Hanafi, Maaliki, Shafi, Hambali na Shia (ambacho twataraji kitatoka hivi karibuni Inshaallah).


Jambo lililotupa msukumo wa kukifasiri kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili ni zile faida nyingi atakazozipata msomaji na kujua mambo mengi na ya ajabu yaliyo mapya kwake ambayo si rahisi kuyapata kwa wafasiri wengine. Msomaji atapata faida katika fani za Sayansi, Siasa, Historia, Mashairi, visa vizuri, na Saikolojia miongoni mwa mengine; ndiyo maana msomaji atashangaa kidogo anapoisoma Tafsiri hii atakapoona mwandishi amewataja na kuwanukuu watu kama kina Mfalme Edward, wanasyansi kama kina Enstein, Charlie Champlin (Mchekeshaji maarufu), na wengineo, hali inayoifanya tafsiri hii kuwa ni ya kipekee kabisa. Mtindo alioutumia mwandishi ni sahali uliokusudiwa watu wa tabaka mbalimbali, wanavyuoni na watu wa kawaida.Nia yetu ni kukigawanya kitabu hiki bure lakini tumelazimika kukiuza kwa bei nafuu ili kurudisha gharama za uchapishaji. Mwisho: Shukrani kubwa iwaendee bila ya kuwataja watu waliojitolea usiku na mchana, jopo la wafasiri, wahariri, wachapaji, waliotupa moyo na kutoa maoni yao na walioisimamia ili kuhakikisha kwamba kitabu kimemfikia msomaji. Mchapishaji.


Makosa ya Chapa.
Sikumbuki kama nimewahi kusoma kitabu kilichotoka kupigwa chapa, cha zamani au cha sasa, bila ya kukuta makosa ya chapa. Nafikiri sitasoma kitabu kisichokuwa hivyo. Nimejaribu sana kuliepuka hilo katika tungo zangu, lakini sikufanikiwa. Nilikuwa sifikirii kama ninaweza kuona makosa haya katika maandishi ya Msahafu Mtukufu, kama yale yaliyo katika baadhi ya chapa; kwa mfano neno yabswatu kwa swad, badala ya yabsutu kwa sin, na katika chapa ya Tafsir Arrazi ya Misr ya mwaka 1935, Sura ya (2:146). Imeandikwa La Ya’alamuun, (hawajui) badala ya Ya’alamuun (wanajua). Mfano wa makosa haya hausameheki.Katika Tafsir Al-Manar, chapa ya Pili, sura (5:212), imeandikwa “Fawqahum ila yawmil qiyama badala ya Fawqahum yawamal qiyama”. Hatuwezi kusema kosa hili ni kubwa zaidi kuliko lile. Lakini mkosaji atatuletea udhuru kwa msemo mashuhuri huko kwetu jabal amail ‘Makosa ya chapa.’ Katika Tafsiri Majmau chapa ya Urfan, Sura (46:15), imeandikwa: “ Hatta idaha balagha arbai’ na sanah badala ya: Hattaidaha balagha ashuddahu arbai ‘ na sanah” Kusema hivi sio kama ninajitetea kutokana na makosa ya chapa atakayoyakuta msomaji katika kitabu hiki, ijapokuwa naomba msamaha kama litatokea hili, lakini makusudio yangu hasa ni kumwambia yule atakayefungua macho yake kwenye makosa ya matamko na kuufungia macho uzuri wa maana. Vilevile ninamwambia yule ambaye siku moja aliniambia: “Vitabu vyako vimejaa makosa ya chapa, kama kwamba hakuna kitu chochote katika vitabu hivyo isipokuwa makosa ya chapa tu. Wote hao ninawaambia: Mungu awasamehe na aniongoze mimi na nyinyi.Vyovyote iwavyo, mimi ninaomba msamaha kutokana na makosa ya kifikra na ya chapa. Anasema Amirul Muminiin (a.s): “Watu wote ni wapungufu wenye kuchanganyikiwa, isipokuwa yule aliyehifadhiwa na Mwenyezi Mungu.” Na Mwenyezi Mungu (s.w.t) ndiye mwenye jukumu la kunikubalia yale niliyoyapatia na kunisamehe niliyakosea, kwa jaha ya Mtume na kizazi chake, ziwashukie rehema na amani (Amin).
MUHAMMAD JAWAD MUGHNIYYAH