FADHILA ZA SAYYIDNA ALI (A.S)

 

HADITHI YA AROBAINI NA TANO
"Mtume asisitiza kumpenda Ali na Ahli Bayti"
Katika Kanzul Ummaal (J. 6, Uk. 155) imenakiliwa kutoka AL-MUUJAMUL KABEER cha Tabarani, hadithi nyingine zilizo sahihi kutoka kwa wanazuoni wa hadithi. Miongoni mwa hadithi hizo ni hadithi aliyoikariri kutoka kwa IBNU UMAR, kuwa Mtume (s.a.w.w.) amesema kumwambia Ali, "Ewe Ali, nikuridhishe na ufurahi? Wewe ni ndugu yangu na waziri wangu, utalipa deni langu, utatekeleza ahadi yangu, na utaniondolea jukumu langu. Basi atakayekupenda katika uhai wangu hakika ametekeleza wajibu wake, na atakayekupenda katika uhai wako baada yangu Mwenyezi Mungu atamfanya awe na mwisho (hatima) mwema, yenye Imani. Na atakayekupenda baada yangu bila kupata kukuona, Mwenyezi Mungu atamfanya awe na mwisho (hatima) mwema, na atamlinda siku ya kutisha (Qiyama). Ewe Ali! Na atakayekufa na hali anakubughudhi (basi) atakufa kifo cha ujinga (ukafiri). Mwenyezi Mungu atamchukulia hisabu kwa yale aliyoyafanya katika UISLAM.


Hadithi hii ni sahihi, maana imetangazwa na TABARANI na wengineo, katika AL-MUUJAMUL KABEER. Hadithi hii imechukuliwa katika vitabu vya wanazuoni wa Kisunni, Shafiiy na Hanafiiy. Miongoni mwao ni Abu Naeem Al-Isfahani katika HILYATUL-AW-LIYAA (J. 1, Uk. 86) Ali Al-Muttaqi Al-Hanafiy katika KANZUL-UMMAAL (J. 6, Uk. 155) ambaye ameyachukua kutoka katika AL-MUSTADRAK cha Saheehaini Bukhari na Muslim na kutoka kitabu cha Fadhailu-Sahaba cha Abi Naeem Al-Isfahani. Maneno yenyewe ya hadithi hiyo ni: "Kutoka kwa Zaidi bin Arqa ambaye amesema kuwa Mtume (s.a.w.w.) amesema, "Atakayependa kuishi (kama) maisha yangu na kufa kifo changu na kukaa katika Pepo ya milele, aliyoniahidi Mola wangu, hakika Mola wangu Mtukufu ameotesha miti (Peponi) kwa Qudra yake, basi AMPENDE Ali Bin Abi Talib, hakika yeye (Ali) hatawatoeni kutoka uongofu, na hatawatieni katika upotevu.

Ali Al-Muttaqi Al-Hanafiiy amekariri hadithi nyingine katika KanzuI-Ummaal (J. 6, Uk. 155) yenye maana ya hadithi iliyotajwa (pamoja na tofauti ndogo katika baadhi ya matamko yake) kutoka vitabu vingi kutokana na Mutayri, na Bawardi na Ibn Shaahin, na Ibnu Mundah, na Ziyaad bin Miitraf. Maelezo yake ni kuwa amesema Mtume (s.a.w.w.) "Atakayependa kuishi (kama) maisha yangu na kufa (kama) kifo changu na kuingia katika Pepo, ambayo ameniahidi Mola wangu, miti katika rq$iti yake ameipanda kwa Qudra yake Mola, nayo ni ile Pepo ya milele, basi AMPENDE ALI na dhuria zake baada yake; hakika wao hawatawatoeni kutoka mlango wa uongofu, na hawatawatieni katika mlango wa upotevu".


Sayyid Muhammad Saleh Al-Hanafiy amenakili hadithi katika kitabu chake: "La-Kaw-Kabud-Dur-Riy" (Uk. Ill) kutoka katika "Khulaasatul Manaaquib" kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) kuwa amesema, "Atakayependa kuishi (kama) maisha yangu na kufa (kama) kifo changu na kuingia katika Pepo ambayo ameniahidi Mola wangu, basi amfanye Ali Bin Abi Talib na dhuria zake viongozi wake watakatifu (awakubali) Maimamu wa uongofu. na taa za kiza baada yake (Ali); hakika wao hawatakutoeni kutoka mlango wa uongofu (na hawatakutieni) katika mlango potevu.

Ali Al-Muttaqi Al-Hanafiy ameeleza hadithi katika Kanzul Ummaal (J. 6, Uk. 117) yenye maana ile ile, kutoka kwa Ibnu Abbasi, na humo mna ziada nyingi zilizo muhimu. Naye amenakili kutoka katika AL-MUUJAMUL KABEER cha Tabarani kuwa Mtume (s.a.w.w.) amesema, "Atakayefurahika kuishi maisha yangu, na kufa kifo changu, na kukaa mwenye Pepo ya milele ameipanda (miti) Mola wagu, basi ampende Ali baada yangu. na ampende anayempenda, na awafuate Ahli-Baiti zangu baada yangu. Hakika wao ni dhuria zangu, wameumbwa kutokana na udongo wangu, na wameruzukiwa fahamu zangu na elimu zangu. Basi adhabu iliyo (kali) kwa wanaokanusha utukufu wao katika umati wangu, wanaokata kwao udugu (sila) wangu: Mwenyezi Mungu hatawapa (watu hao) Shafaa."


Hakika Mtume (s.a.w.w.) katika hadithi hii tukufu, ameongeza (amezidisha) amri yake (kwa Umma) juu ya kuwapenda Ahlul-Bait zake na anawaamrisha Umati zake kuwafuata katika mambo ya ulimwengu wao na dini yao, na anataja sababu ya (man; yake kuhusu jambo hilo, (wameruzukiwa fahamu zangu na elimu yangu). Basi anathibitisha Mtume (s.a.w.w.) kuwa hakika wao (a.s.) ndiyo wanaofaa kuwafuata kwa vile wao wamebarikiwa na wanazo fahamu za Mtume (s.a.w.w.) na elimu Łake si kwa sababu wao ni jamaa za Mtume (s.a.w.w.). Basi hadithi hii ni kama zile hadithi zinazojulikana kwa majina ya Hadithi ya Thaqalain na Hadithi ya Safina ambamo Mtume (s.a.w.w.) amesema wazi kwamba, hakika uongofu katika mambo yanayohilikisha hapa duniani na akhera unategemea na kushikamana nao, na kupanda jahazi (Safina) ya uongofu kwa kuwafuata wao.


Kwa sababu wao (a.s.) ndiyo hazina ya elimu yake, na ndiyo warithi wa upole wake na ndiyo waongozi wa (mambo) yanayo hitaji Ukhalifa na uongozi. Basi Mtume (s.a.w.w.) amewabainishia na kuwaeleza Masahaba zake, ili wawabainishie Waislamu katika njia ya uongofu na kufuzu mema. (Pia) amewabainishia yanayofaa (katika) mambo yao ya Kiislamu na yanayotia nguvu Uislamu wao kwa maelezo mbali mbali. Miongoni mwa maelezo hayo ni yale yaliyotangulia, nay^ale aliyoyatoa Ali Al-Muttaqui Al-Hanafiy, katika Kanzul Ummaal (J. 6 Uk. 218) kwa kunakili kutoka kitabu cha Tarehe cha (mwanazuoni wa hadithi ya mji wa Shaam) IBNU ASAAKIR. Sasa nakuletea^yaliyomo katika Kanzul Ummaal (J. 6, Uk. 218). Hakika yeye ameipata kwa "njia kutoka kwa Ali (a.s.) kuwa amesema, kuwa Mtume (s.a.w.w.) amesema: "Ewe Ali! Hakika Uislamu uko uchi, nguo yake kumcha Mungu (Taqwa) na nywele zake uongofu, na kipambo chake ni haya, na nguzo yake utawa, na nguvu zake ni amali njema na msingi wa Kiislam ni kunipenda mimi na kuwapenda Ahli Baiti zangu.


HADITHI YA AROBAINI NA SITA
"Ali ni Bwana wa Waarabu"
Katika "As-Sawaaiqul Muhriqa" cha Ibnu Hajar Al-Haytami Ash-Shafii (Uk. 75) na katika "Kanzul Ummaal" cha Ali Al-Muttaqui Al-Hanafi (J. 1, Uk. 157) na katika "Kifaayatut-Taalib" cha Al-Kanji Ash-Shafii (Uk. 91), na katika Yanaa-biul-Mawadah cha Sheikh Sulaiman Al-Kanduzi Al-Hanafii (Uk. 274) o kutokana na maneno ya Ali Muttaqi amepokea hadithi ilioelezwa na Bi. Aisha amesema kuwa Mtume (s.a.w.w.) amesema, "Ewe Aisha! Ukiwa wafurahishwa kumwangalia bwana wa Waarabu. basi mwangalie Ali Bin Abi Talib. (Aisha) akasema, nikasema, "Ewe Mtume (s.a.w.w.) wewe ni bwana wa Waarabu? Mtume (s.a.w.w.) akajibu, "Mimi ni Imamu wa Waislamu na ni bwana wa wacha Mungu.


Hakika hadithi hii wameipokea kundi la Masahaba kwa maneno mbali mbali. Miongoni mwa hadithi hizo ni ile aliyoipokea Al-Kanji Ash-Shafiiy katika Kifaayatut-Taalib (Uk. 91) kutoka kwa Hasan bin Ali, kuwa Mtume (s.a.w.w.) amesema, "Ewe Anas! Nenda ukaniitie bwana wa Waarabu. (Anakusudia Ali Bin Abi Talib) Aisha akasema: "Wewe si Bwana wa Waarabu?

(Mtume) akasema: "Mimi ni Bwana wa watoto wa Adam, na Ali ni Bwana wa Waarabu. (Anas) akasema, Ali alipokuja Mtume (s.a.w.w.) akampeleka (mtu) kwa Ansari (kuwaita); wakaja; Mtume (s.a.w.w.) akawaambia: "Enyi Ansari! Mwaonaje nikujulisheni jambo ambalo mkishikamana nalo hamtapotea baada yake? (Ansari) wakasema: Ndiyo ya Rasulal-Laahi (tujulishe); akasema: "Huyo Ali mpendeni kwa ajili ya kunipenda, na mhishimuni kwa ajili ya heshima yangu; hakika Jibrili ameniamrisha (kuyasema) hayo niliyokuambieni yametoka kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka. Kisha Al-Kanji akasema "Nasema hadithi hii imethibti na ni sahihi, alivyoithibitisha Imam wa hadithi Sulaiman bin Ahmad Tabarani katika kitabu chake Mujamul Kabeer kwa maelezo hayo hayo tulivyotoa.

Kisha akatoa hadithi nyingine yenye maana hiyo hiyo kutoka kwa Ibnu Abi Layla (kutoka kwa Husein Bin Ali (a.s.) kuwa amesema kuwa Mtume (s.a.w.w.) amesema, "Ewe Anas! Hakika Ali ni Bwana wa Waarabu"; wakasema, wewe siyo Bwana wa Waarabu? (Inaendelea kama ilivyotangulia hadithi iliyonakiliwa kutoka kwa Imam Hasan Bin Ali (a.s.). Kisha al-Kanji akascma: Hadithi hii ni mashuhuri. Na katika Kanzul Ummaal (j. 6, Uk. 400) amenakili hadithi Aitoka kwa Bi. Aisha kuwa amesema: Nilisema "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, wewe ndiyo Bwana wa Waarabu? Akasema mimi ni Bwana wa watoto wa Adam (a.s.) na Ali ni Bwana wa Waarabu. Na katika kitabu hicho hicho amekariri hadithi iliyopita kutoka kwa Hasan bin Ali (a.s.) na katika kitabu cha Hilyatul Awliyaa cha Abi Nairn Isfahan!, maneno yake ni sawa na maneno ya Al-Kanji Ash-Shafliy ila yeye amesema Mtume (s.a.w.w.) amesema hivi: mwaonaje niwajulisheni jambo ambalo mkishikamana nalo hamtapotea baada yake abadan? Wakasema (Ansari); Ndiyo tujulishe. Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Mtume (s.a.w.w.) akasema, "Huyu Ali mpendeni kwa mapenzi yangu (mpaka mwisho wa hadithi).


HADITHI YA AROBAINI NA SABA
"Ali na Fatima walikuwa wakipendwa sana na Mtume"
Katika Kifaayatut-Taalib (Uk. 119) cha Al-Kanji Ash-Shafiy imenakiliwa hadithi kutoka kwa Ataa kuwa amesema kuwa: "Nilimuuliza Aisha kuhusu Ali Bin Abi Talib, akasema: "Yeye (huyo) ni mbora wa viumbe, hamtilii shaka ila kafiri". Hadithi hii pia ameitaja Hafidhi Bin Asaakir katika habari ya maisha ya Ali (a.s.) katika kitabu chake cha Taareekhul-Kabeer.

Hadithi hii imeikuta katika Tareekhul Kabeer cha Ibnu Asakir (kilichopo katika Maktaba ya Ameerul Monnineen (a.s.) katika Najaf-Iraq) na hadithi hii ya Aisha ameikariri Sheikh Sulaiman Al-Kanduzi Al-Hanafiiy katika Yanaabiul Mawaddah (Uk. 246). Al-Kanji Shafiy katika Kifaayatut-Taalib ameikariri hadithi hiyo kwa njia mbali mbali na kutoka Masahaba wengi mbali na Aisha. Katika Tiao ni Ameerul Momineen Ali Bin Abi Talib (a.s.) na Jaabir .na Hudhaifa na wengine. Maneno yao katika hadithi yatofautiana. Maneno ya Ameer (a.s.) ni hivi: "Asiyesema kuwa Ali ni Mbora wa viumbe, basi hakika amekufuru." Na kwa maelezo ya Hudhaifa ni hivi: "Nimemsikia Mtume (s.a.w.w.) anasema, "Ali ni Mbora wa viumbe, atakayekataa basi hakika amekufuru. Na riwaya ya Jabir ni sawa na ya Hudhaifa ila neno moja tu ni "Fe" iliyoko kabla ya Man). Maneno ya Jabir kutokana na upokezi wa Muhaddithu Shaami Ibnu Asakir, kutoka kwa Jabir kuwa: "Huyo (Ali) ni Mbora wa viumbe, hamchukii mtu yeyote ila Kafiri.


Sheikh Manawi ametoa hadithi hii katika kitabu chake Kanzul Haqaaiq, kilichopigwa chapa pembezoni mwa kitabu cha Al-Jaamius-Sagheer cha Suyuti (J. 2, Uk. 20, 21) kutoka kitabu cha Sunan Abi Yaal kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) kuwa hakika yeye (Mtume s.a.w.w.) amesema, "Ali ni Mbora wa viumbe, atakayetia shaka (katika jambo hilo) amekufuru." Hadithi hiyo hiyo imekaririwa katika Tareekh Al-Khateeb na Al-Baghdadi kuwa: "Ali ni mbora wa viumbe atakaye kataa basi hakika amekufuru." Ali Al-Muttaqi ameeleza hadithi hiyo katika Kanzul Ummaal (J. 6, Uk. 159) kutoka kwa Ali Bin Abi Talib na Ibnu Abbasi na Ibnu Mas-udi, na Jabir. Lakini maelezo ya hadithi kutoka kwa Jabir ni sawa na tuliyoyakuta katika Kanzul Haqaiqi cha Manawi. Na maneno na maelezo ya Ameerul Momineen (a.s.) na Ibn Masudi na Ibn Abbasi ni sawa na tuliyonakili kutoka Kifaayatut-Taalib. Kwa hakika baadhi ya (Ulamaa) wanazuoni wa Kishia.... Maneno ya hadithi hii katika kitabu maalum kiitwacho Nawaadirul Athar fee Aliyin Kharil Bashar kilichopigwa chapa Tehran (Iran) mwaka 1369 A.H.


HADITHI YA AROBAINI NA NANE
"Bi Aisha athibitisha mapenzi ya Mtume kwa Ali na Fatima"
Katika Kifaayatut-Taalib (Uk. 184) imeelezwa hadithi kutoka kwa Shuraih bin Hani, kutoka kwa baba yake kutoka kwa Aisha kuwa amesema, Mwenyezi Mungu hakuumba kiumbe aliyekuwa mpenzi mno kwa Mtume (s.a.w.w.) kuliko Ali Bin Abi Talib. Kisha akasema hadithi hii ni hasan (Sahihi) ambayo imepokewa na Ibnu Jareer katika kitabu chake cha Manaaqib na Ibnu Asakir ameinakili hadithi hiyo katika maelezo ya maisha ya Ali (a.s.).

Al-Hakim An-Nishapuri katika kitabu chake Mustadrak As-Sahee-hain (J. 3, Uk. 154) amekariri hadithi yenye maana ile ile lakini humo mna maneno zaidi, na hayo ndiyo aliyoyapata kutoka kwa Jamii bin Ibnu Umair ambaye amesema: Niliingia na mama yangu kwa Aisha, nikamsikia kwa nje ya pazia (nyuma) anaulizwa kuhusu Ali. Akasema, unaniuliza (habari za) mwanamume, Wallahi simjui mtu (mwanamume) yeyote aliyekuwa mpenzi mno kwa Mtume (s.a.w.w.) kuliko Ali na (simjui) katika ardhi mwaamke aliyekuwa mpenzi mno kwa Mtume (s.a.w.w.) kuliko mkewe Ali, Fatima (a.s.). Kisha akasema hadithi hii ni sahihi yenye uthibitisho kamili (lakini) kina Bukhari na Muslim hawakuinakili.

Muhibbuddeen At-Tabari ameikariri hadithi katika Dhakhairul Uqba (Uk. 35) na maelezo yake kutoka kwa Aisha kwamba yeye aliulizwa ni mtu gani aliye mpenzi mno wa Mtume (s.a.w.w.)? Akasema, "Fatima; akaulizwa tena, katika wanaume Je? Akasema, "Mumewe; nilivyojua ni mwingi wa kufunga na kuswali. Ameyaeleza Tirmidhi katika Saheeh yake (J. 2, Uk. 475). Ibnu Ubaid ameinakili hadithi hiyo hiyo na baada ya mwingi wa kuswali amezidisha maneno mwenye kauli ya kweli Buraydah amesema kuwa Fatima alikuwa kipenzi mno wa wanawake kwa Mtume (s.a.w.w.) na kwa waaume ni Ali. Hadithi hiyo ameikariri Abu Umar huo ndio mwisho wa maelezo ya Tabari katika (Dhakhair).


Al-Haakim ameeleza hadithi hii katika Mustadrak Saheehain (tazama J. 3, Uk. 157), Ibnu Atheer katika Ussdul Ghaba (J. 3 Uk. 522), Ibnu Abdil Bar katika Istlaab (J. 2, Uk. 772) Tirmidhi katika Saheeh yake (J. 2, Uk. 471), katika babu kuhusu sifa za Usama; na Khawarazmi Al-Hanafiiy katika Maqtal Al-Husein (a.s.) (J. 1, Uk. 57). Ali-Muttaqi Al-hanafi, katika Kanzul Ummaal (J. 6, Uk. 450). Hadithi hiyo imechukuliwa kutoka katika vitabu vya wanazuoni wa Kisunni.


HADITHI YA AROBAINI NA TISA
"Ali alikuwa mtu wa mwisho kuonana na Mtume (s.a.w.w.)"
Katika Kifaayatut Taalib (Uk. 133) imeelezwa hadithi kwa Aisha kuwa Mtume (s.a.w.w.) alisema (wakati) Mtume (s.a.w.w.) alipokuwepo nyumbani mwaka (Aisha) ilipomkaribia mauti): Niitieni mpenzi wangu. Nikamwita Aba Bakri, akamwangalia (kisha) akarudisha (akaweka) kichwa chake. Kisha akasema: Niitieni kipenzi changu, nikamwitia Umar, alipomwangalia tu akarudisha kichwa chake. Kisha alisema: Niitieni niitieni kipenzi changu. (Mimi nikasema: upotovu wenu, niitieni Ali, naapa kwa Mwenyezi Mungu hamkusudii (mtu) mwingine ila Ali. Basi (akaitwa) Ali, alipomwona Ali, Mtume akafunua nguo ambayo ilikuwa juu yake (aliyojifunika), kisha akamtia (Ali) katika ile nguo; akawa amemkumbatia mpaka ikachukuliwa roho yake, na mkono wake (Mtume) uko juu yake Ali."


Hadithi hii ameikariri Al-Kanji, ili kuthibitisha kwamba hakika Ali alikuwa karibu mno kuliko mtu yeyote kwa Mtume (s.a.w.w.) wakati alipofariki dunia. Kisha akasema Al-Kanju nina jambo linalo ..... ni kuwa hakika Ali alikuwa karibu mno kuliko wote kwa Mtume (s.a.w.w.) wakati Mtume (s.a.w.w.) alipofariki. Hadithi hii imetajwa na Abu Yaala Al-Moosali katika Musnad yake, na Imam Ahmad bin Hanbal katika Musnad Mtume (s.a.w.w.) yake. (Kisha akaeleza) hadithi hii kutoka kwa Ummu-Salama ambaye amesema: 'Naapa kwa Mwenyezi Mungu (kuwa) Ali alikuwa mtu wa mwisho aliyeonana na Mtume (s.a.w.w.) katika uhai wake (Mtume s.a.w.w.). Akasema, Mtume (s.a.w.w.) alikuwa anasema, Ali amekuja? Ali amekuja? Mara kwa mara.


Fatima amesema: (Mtume s.a.w.w.) alikuwa amempeleka (Ali) akaulize mahitaji yake. Baada ya muda akaja Ali; nikadhani kwamba yeye (Mtume) anamhitaji Ali, basi tukatoka nje ya nyumba, na tukakaa mlangoni, nikawa karibu nao kutoka mlango, nikamwona Ali akamwangukia (Mtume) akawa anasema nayc kwa siri mpaka Mtume (s.a.w.w.) alipofariki siku hiyo. Basi akawa ndiye wa mwisho kuzungumza na Mtume (s.a.w.w.). Al-Kanji amesema: "Nasema, hadithi hii ameikariri Ahmad bin Hambal katika Musnda yake (J. 6, Uk. 300) Al-Moosali katika Musnad yake amesema kuwa Mtume (s.a.w.w.) alimwangukia Ali. Na Muhibbu Tabary amekariri katika Dhakhairul Uqba (Uk. 72) hadithi ya Ummu-Salama na Aisha na akasema kuwa hadithi hiyo amenakili Ahmad bin Hanbal katika Musnad yake, na maneno ya Muhib Attabari na Al-Kanji ni sawa ila katika baadhi ya sehemu.

HADITHI YA KHAMSINI
"Kuangalia Uso wa Ali ni Ibada"
Katika Kanzul-Ummaal (J. 6, Uk. 152) imekaririwa hadithi kutoka katika kitabu cha Firdausul-Akhabaar cha Daylami, kuwa Aisha amesema kuwa Mtume (s.a.w.w.) amesema: "Kuangalia uso wa Ali ni ibada".

Hadithi hii imekwishatangulia katika hadithi ya pili; nayo ni ile aliyoipokea ABU BAKR kuwa hakika Mtume (s.a.w.w.) amesema: "Kuangalia uso wa Ali ni ibada" Hadithi hii tumeichukua kutoka kitabu cha Al-Bidaya-Wan-Nihaya (J. 7, Uk. 357) na tumetaja kuwa hakika Ibnu Katheer amesema kuwa "Hadithi hii imepokewa na Masahaba wengi." Akawahisabu na kuwataja, kisha, akasema: Katika hao ni Aisha binti Abi Bakr, Jalaalud-Deen As-Suyooti Ashafiiy katika Tareekhul Khulafaa (J. 1, Uk. 96) amekariri hadithi hii inayosema: "Kuangalia uso wa Ali ni ibada." Ibnu Asaakir amekariri hadithi hii inayosema: "Kuangalia uso wa Ali ni ibada." Ibnu Asaakir amekariri hadithi hiyo hiyo iliyoelezwa na Abu Bakr na Uthmani bin Affan, na Maadhi bin Jabal, na Anasi na Thaubani, na Jabir bin Abdullahi, na Aisha.


Na katika Dhakaairul Uqba (Uk. 95) amenakili hadithi kutoka kwa Aisha, na Ibnu Mas-udi na Amri bin Asi, na Jabir na Abi Huraysah. Kisha akasema: Hadithi ya Aisha ameikariri Ibnus Samani katika kitabu chake Al-Muwaafiqa. Na katika Dhkhaairul-Uqba (Uk. 95) pia imo hadithi hii chini ya maelezo kuhusii ibada) kutoka kwa Aisha (R.A.) ambaye amesema: "Nimemwona ABA BAKRI anamwangalia sana usoni Ali, nikasema Ewe baba, nimekuona unaangalia sana uso wa Ali? Akasema, Ewe mwanangu nimemsikia Mtume (s.a.w.w.) anasema. "Kuangalia uso wa Ali ni ibada" Hadithi hiyo ameinakili Ibnu Sammani katika kitabu chake Al-Muwafiqa. Humo amesema kuwa Ibnu Mas'ud amesema: "Kuangalia uso wa Ali ni Ibada." Hadithi hiyo imekariri na Abdul Hasan Al-Harbi kutoka kwa Amr Bin Asi ambaye amepokea kama hivyo (hapo juu). Vile vile Al Abhari. Jabir amesema kuwa Mtume (s.a.w.w.) alimwambia Ali, nenda ukamtazame Imraan bin Haseen kwani yeye ni mgonjwa. (Ali) akaenda (huko) alikuwako Maadhi na Abu Haraira; basi. Imrani akawa anamwangalia sana Ali. Maadh akamwuliza kwa nini wamwangalia sana (Ali)? Akasema: Nimesikia Mtume (s.a.w.w.) anasema "Kumwangalia Ali ni ibada." Maadh akasema: Na mimi pia nimesikia (hadithi hiyo) kwa Mtume (s.a.w.w.) na Abu Huraira akasema na mimi pia nimeisikia kwa Mtume (s.a.w.w.).


Hadithi hiyo ameieleza Ibnu Abil-Furat. Na katika "Taarekhul kabeer cha Ibnu Asakir, kilichoko katika Maktaba ya Imaam Ameerul-Mumineen (a.s.) huko An-Najaf Al-Ashraf (Iraq) katika (Uk. 19) amekariri kutoka kwa Ibn Abbas kuwa Uthmani bin Affuni alikwenda kwa Ali na akamtaka Ali aende kwake na Ali akaenda, basi akawa Uthman anamwangalia sana. Ali akamwambia una nini waniangalia mno? (Uthman) akasema: Nimesikia Mtume (s.a.w.w.) akisema: "Kumwangalia Ali ni ibada"


Tunamaliza mukhtasari huu kwa hadithi ya "Kumwangalia Ali (a.s.)" iliyopokewa na Masahaba wengi watukufu, mwanzo wao ni Ameerul- Mumineen Ali bin Abi Talib, tena Ibnu Abbas, tena Abu Bakr na Umar, Uthman, na Thauban, na Imran bin Haseen, na Amr bin Asi, na Anasi bin Malik, na Jabir bin Abdillahi, na Abu Dhari, na Abu Huraira, na Abud-Dardai, na Abu Saeed al Khudri, na Wathila bin Al Asqa, na Maadh bin Jabal na Abdalla bin Masudi na Aisha.


Mwisho tunaomba rehema na amani zimwendee Mtume wake Muhammad Mtukufu, Al-Mustafa (s.a.w.w.) na Aali zake waongofu na sahaba zake watakatifu, ambao wametuhifadhia mambo waliyosikia kwa Mtume (s.a.w.w.) na wakayafikisha kwa waliofuata (Taabi-ina) na wakafuta maamrisho yake na wakaacha makatazo yake, na hao ndiyo wenye kufuzu.

13lllMuharram, 1391

11 Machi, 1971

MWISHO


MAREJEO
1- Mlango 19, uk. 234
2- Uk. 17
3 -Uk. 222
12 Uk. 161
4-Juzu 1, Uk. 39
5 - Juzu 1, Mlango 54
6 -Juzu 2, uk. 173, 177 na 244
7 -Uk. 95, chapa ya Iraq
8 -Juz 3, uk. 161
9- Uk. 459
10- Uk. 36
11 -Uk. 15
12- Uk. 161
13 -Sawaiqul-Muhriqa Ibn Hajar uk. 108


14 -Riyadhun Nadhra J. 2 163/244.
15 -Kifaayatut-Taalib cha Al-Kanji Ash-Shafii uk. 127, Tarekh Ibn Asaakir, Arjahul-Mataalib cha Ubaidullaah Al-Hanafy uk. 309
16 - (a) Manaaqib cha Al-Khowarazmi, uk. 59
(b) -Maqtalil Husein cha Al-Khowarazmi, J. 1, uk. 45
(c) -Sawaiqul Muhriqa cha Ibnu Hajar, uk. 68/78
(d) -Suyooti Ash-Shafiy, Tareekhul Khulafaa J. 1, uk. 66
17 -Saheeh Bukhari J. 14, uk. 387 na J. 18, uk. 89, Saheeh Muslim J. 2, uk. 278 Jeme'a Tirmizi uk. 461. Isabah J. 4, uk. 270, Usdul-Ghaba J. 4, uk. 25 Izalatul-Khifa M. 2, uk. 260-261. Riadhun-Nadhra J. 2, uk. 188 na 203. Musnad I. Hambal J. 1 uk. 330. Sunan Ibne-Majah uk. 12 Mishkat J. 8, uk. 119. Jam'a Sagheer uk. 56 Mustadrak J. 2, uk. 337 na J. 3, uk. 19. Musnad Imaam Hambal J. 1, uk. 170, 173, 175, 179, 182, 184 na 331; na J. 3, uk. 32 na 338; na J. 6 uk. 369 na 438.
18 - (a) Kanzul-Ummal, J. 6 Uk. 393/395
(b) -Manaqib cha Kharazmi Uk. 32.
(c) -Ibnu Asakir katika Tarekh w. 16.


(d) -Askafi katika Naqdh Uthmaniyah al-Jashidh Uk. 21 kimepigwa chapa Misri.
19 - (a) Yanaabee-ul-Mawadah, J. 1 Uk. 249.
(b)- Khowarazmi, Al-Manaaqib, Uk. 18
(c) -Al-Kanji Ash-Shafiy, Kifaayatu Talib, Uk. 123.
20 - (a) -Suyootee katika Tareekh J. 1, Uk. 56.
(b) -Tirmizi Hanafy katika Al-Kaukabud-Durry, Uk. 131.
21 - (a) -Tabari katika Dhakaairul Uqba, Uk. 89/91
(b) -Al-Kanji katika Kifaayatut-Taalib, Uk. 76.
(c)-Ali Al-Muttaqi katika Kanzul-Ummal J. 6, Uk. 159.
(d) -Khowarazmi katika Manaaqib
(e)- Riyadhun-Nadhra J. 2, Uk. 211.
22 - As-Sawaa-qul-Muhriqa, Uk. 78
23 - Riyadhun Nadhra Juzu 2, uk. 98
24 -Tareekhul Khulafaa Juzu 1, Uk. 66
25 -Al-Ishaab, Juzu 2, Uk. 484
26 - Dhakhairul-Uqba, Uk. 82
27 - Tadh-kira Khawaa-Sul-umma (Chapa ya Iran) Uk. 87.
28 -Uk. 14, 118 na 127
29- Kifaa-Yatut-Taalib, Uk. 130.
32 -Juzu 2, Uk. 198
30 - Al-Fussoolul-Muhim-ma, Uk. 17
31 - Kifaa-yatut-Taalib, Uk. 140
32 -Juzu 2, Uk. 198


VITABU VILIVYOPOKEA HADITHI ZILIZONAKILIWA MWENYE KITABU HIKI
(1) Tafseer cha Thalabi; (430 A.H.)
(2) Tafseer Kash-shaaf; Zamakh-shari (528 A.H.)
(3) Tafseer cha Nishapuri
(4) Tafseer cha Muhammad bin Saaib Al-Kalbi
(5) Tafseer Libaabut Taaweet wa Maanil anzeel; Khazn
(6) Tafseer Madarikut Tanzeel wa Hakaaikut Taweel
(7) Tafseer Ad Darrul-Manthoor; Jalaalud-Deen Suyooti
(8) Saheeh Al-Bukhari
(9) Saheeh Muslim
(10) Sunan Ibnu Maajah Al-Qazwini
(11) Sunan Abi Yaala
(12) Sunan Ad-Daar Qutni


(13) Kanzul Ummal; Ali Muttaki Al Hanafi
(14) Mustadrak-Saheehain; Al-Hakim Nishapuri
(15) Muntakhab Kanzul Ummal; iliyoko pembezoni mwa kitabu cha Musnad cha Ahmad bin Hanbal
(16) Masabeehus-Sunna; Baghawi
(17) Musnad; Ahmed bin Hanbal
(18) Musnad; Abi Daud Al-Tayaalisi
(19) Musnad; Abi ya'laa Al-Moosali
(20) Al-Mujamul-Kabeer; Tabarani
(21) Usdul Ghabah fi Maarifatis Sahaba; Ibnul Atheer Ash-Shafii (630 A.H.)
(22) Is-aafur-Raaghibeen, Ibnu Sabbaan-Sahfii
(23) Al-Isteeab; Ibn Abdil-Bar Annamry; (463 A.H.)
(24) Al-Isaba fi Tamyeezis Sahaba; Ibnu Hajar Al-Askalani; (863 A.H.)
(25) Jaami Tirmiz


(26) Khasasi Ahmad bin Shueib Annasai Ash-Shafii; (303 A.H.)
(27) Tabakaat; Ibnu Saad
(28) Firdausul Akhbaar; Ad-Daylami
(29) Faraidus-Simtain; Ibrahim bin Muhammad Al-Hamwini Ash- Shafii
(30) Al-Fusoolul Muhimma; Ibnu Sabbagh-Al-Maliki
(31) Kunoozul Hakaik, Abdurrauuf Al-Manawi Ash-Shafii (1031 A.H.)
(32) Kifaayatut-Taalib, Al-Kanji Ash-Shafii
(33) Al-Kaukabud-Durri; Sayyid Muhammed Saleh Al-Tirmizi Al-Haanafi
(34) Al-Kuna; Al-Hakim
(35) Manaakib; Al-Muwaffak bin Ahmad Al-Khwarazmi Al-Hanafi (865 A.H.)
(36) Manaakib; Ibnu Maghazili Ash-Shafii (483 A.H.)
(37) Maktalul Husein (a.s.); Al-Muwaffak bin Ahmad Al-Khwarazmi Al-Hanafii
(38) Mawaddatul Kurba; Sayyid Ali Al-Hamdani Ash Shafii
(39) Al-Ikdul Fareed; Ibnu Abdi Rabbih


(40) Al-Gheelaaniyaat, Abi Bakr Ash-Shafii
(41) Arjahul Mataalib; Ubaidullah Amristary Al-Hanafii
(42) Al-Ithaaf Behubbil Ashraak Sheikh Abdullah Shabrawi As-Shafii
(43) Al-Alkaab; Ahmad bin Abdurrahman Shirazi
(44) Al-Bidaya Wannihaya; Ibnu Katheer Ad-damashki (774 A.H.)
(45) Tareekhul khulafa; Jalaalud-Deen Assuyooti; (911 A.H.)
(46) Tareekhul Kabeer; Ibnu Asaakir; (571 A.H.)
(47) Tareekhul Kaamil; Ibnu Atheer Aljuzary; (606 A.H.)
(48) Tareekh Baghdad; Al-khateeb Al-Baghdad
(49) Tareekh Baghdad; Ibnu Najjar


(50) Tareekh Attabari Al-Kabeer; Abi Jaafar Ibnu Jareer: (310 A.H.)
(51) Tadhkiratu Khawaasil Umma: Sibt Ibni Jauzi Al-Hanafi (654 A.H.)
(52) Hilyatul Awliyaa; Abi Naeem Al-Isfahani (530 A.H.)
(53) Khulaasatul Manaakib
(54) Dhakairul Ukba; Muhibbuddeen At-Tabari (695 A.H.)
(55) Ar-Riyaadhun Nadhra; Muhibbuddeen At-Tabari Ash-Shafii
(56) Rashfatus-Saadi; Sayyid Shahaabud-Deen Abi Bakr Ash-Shafii
(57) Assawaikul Muhrika; Ibnu Hajar Al-Haytami Ash-Shafii
(58) Al-Masheekhatul Baghdaadiya; Al-Hafidh As-Salafi
(59) Nuzhatul Majalis; As-Safoori Ash-Shafii
(60) Wafayaat-ul-Aayaan; Ibnu Khallikan Ash-Shafii
(61) Yanaabee-ul-Mawaddah Shaikh Suleina Al-Kanduzi Al-Hanafii (1294 A.H.)


FAHARASA YA MANENO YALIYONENWA NA MTUKUFU MTUME WETU (S.A.W.W.)
(1) Kauli ya Mtume (s.a.w.w.); hatavuka Sirati yeyote isipokuwa aliyeandikiwa ruhusa na Ali.
(2) Kauli yake (s.a.w.w.); Ali ni mgawaji wa Pepo na Moto
(3) Kauli yake (s.a.w.w.); kuangalia uso wa Ali ni Ibada
(4) Kauli yake (s.a.w.w.); mfano wa Ali katika Umma huu ni mfano wa Kaaba
(5) Kauli yake (s.a.w.w.); kumwangalia Ali ni Ibada
(6) Kauli yake (s.a.w.w.); Ali ni mlango wa elimu yangu na mwenye kuwaeleza umma wangu madhumuni ya kuletwa kwangu (duniani na Mungu).
(7) Kauli yake (s.a.w.w.); Kumwangalia Ali ni rehema, mapenzi na ibada
(8) Kauli yake (s.a.w.w.); Mwenyezi Mungu amemjalia ndugu yangu Ali kuwa sifa na vyeo visivyohisabika.
(9) Kauli yake (s.a.w.w.); Kumkumbuka na kumdhukuru Ali ni Ibada
(10) Kauli yake (s.a.w.w.); Ali kwangu ni kama nilivyokuwa mimi kwa Mwenyezi Mungu.
(11) Kauli yake (s.a.w.w.); kwamba Ali ni mpole kwa Umma na mwenye subira mno.
(12) Kauli yake (s.a.w.w.); kwamba Ali anapendwa zaidi naye kuliko mtu yeyote.
(13) Kauli yake (s.a.w.w.); gao langu na la Ali katika uadilifu ni sawa.
(14) Kauli yake (s.a.w.w.); Mimi niko katika suluhu na yule atakayekuwa na watu wa hema hii.
(15) Masahaba walikuwa na sifa kumi na nane na katika hizo Ali alikuwa na sifa kumi na tatu ya pekee na kashirkiana nao katika tano zilizobaki.
(16) Kauli yake (s.a.w.w.); wewe kwangu kama alivyokuwa Harooni kwa Musa.
(17) Kauli yake (s.a.w.w.); ya kuonekana imani ya Ali kuwa mbora zaidi kuliko watu wote wa mbinguni na ardhini.
(18) Kauli ya Umar kwamba Ali amepewa sifa tatu ambazo ningalipata walau mojawapo ingalikuwa kwangu bora kuliko ngamia wekundu.


(19) Kauli ya Mtume (s.a.w.w.); Lau bahari ingaligeuka wino na miti kuwa kalamu isingaliwezekana kuandika sifa zote za Ali Bin Abi Talib (a.s.)
(20) Kauli yake (s.a.w.w.); Ewe Ali mkono wako utakuwa katika mkono wangu utapoingia Peponi nami.
(21) Kauli yake (s.a.w.w.); Huyu Ali ni ndugu yangu hapa duniani na kesho akhera.
(22) Kauli yake (s.a.w.w.); Hakuchuma mchumaji wa aina yeyote kama alivyokuwa nayo sifa Ali (a.s.)
(23) Kauli yake (s.a.w.w.); Hakuna sahaba yeyote aliyekuwa na sifa kama za Ali (a.s.)
(24) Kauli yake (s.a.w.w.); Mwenyezi Mungu amewaumba Malaika kutokana na nuru ya Ali (a.s.).
(25) Kauli yake (s.a.w.w.); Mwenyezi Mungu katika mbingu ya nne amemwumba malaika katika sura na mfano wa Ali (a.s.)
(26) Kauli yake Umar (R.A.) Ali tu ndiye mwenye ujuzi wa kuhukumu.
(27) Kauli yake (s.a.w.w.); kwamba Ali ni mjuzi zaidi wa kuhukumu kuliko watu wa Madina.
(28) Alikuwa Umar (R.A.) akiomba kwa Mwenyezi Mungu amwepushe kwenye dhiki wakati ambapo Ali hayupo.
(29) Kauli ya Umar (R.A.) kusema Ewe Mola wangu usinishushie dhiki yoyote ila akiwapo Ali (a.s.).
(30) Kauli yake (s.a.w.w.); Ali ndiye mwamuzi asiokuwa mfano na anavyoamua yeye ndiyo sawa.
(31) Uthibitisho wa Al-Kanji As-Shafiiy kuwa Ali ni mwenye elimu kuliko wote.
(32) Maamuzi ya Ali (a.s.) kuhusu mabedui wawili.


(33) Kauli ya Umar (R.A.) Ali ni bwana wangu na bwana wa kila mwenye kuamini na anayo mamlaka juu yetu sote.
(34) Kutia adabu na Umar (R.A.); mwenye kumbugudhi Ali.
(35) Kauli yake (s.a.w.w.); Ali anatokana nami na mimi ninatokana na Ali.
(36) Kauli yake,(s.a.w.w.); kumwambia Buraydah usimbughudhi Ali (a.s.).
(37) Kauli yake (s.a.w.w.); Msimseme Ali.
(38) Kauli yake (s.a.w.w.); Ali ni (Bwana) mwenye mamlaka juu yenu baada yangu.
(39) Muhtasari wa kisa cha Ghadeer.
(40) Kauli ya Umar (R.A.): Nilimsikia Mtume (s.a.w.w.); akitaja sifa tatu za Ali (a.s.).
(41) Kisa cha kutekwa kwa Khaybar kwa mikono ya Ameerul Mumineen Ali (a.s.)
(42) Hadithi ya kisa cha Ghadeer kwa maelezo ya Umar (R.A.)
(43) Kauli yake (s.a.w.w.); kumwambia Ali (a.s.); wewe kwangu kama alivyokuwa Haruni kwa Musa.
(44) Kumwamrisha Ali kufikisha sura ya Bara-at kwa Makureshi wa Makka.
(45) Kisa cha kufungwa milango yote ifungukayo ndani ya Msikiti, na. ushindi wa Khaybar, na hadithi ya Ghadeer na hadithi ya Manzila.
(46) Kauli yake (s.a.w.w.); Laiti wangekusanyika watu wote kumpenda Ali (a.s.) asingaliumba Mwenyezi Mungu Moto (Jahanam).


(47) Kauli yake (s.a.w.w.); Ewe Ali, mwenye kukupenda wewe atakuwa pamoja na Mitume siku ya Qiyama.
(48) Mazungumzo ya Umar pamoja na Ibnu Abbasi kuhusu Khilafa (ukhalifa).
(49) Kauli ya Umar (R.A.) haukamiliki utukufu bila ya kumpenda Ali (a.s.).
(50) Kauli yake (s.a.w.w.); Mwenyezi Mungu amewaumba malaika kwa nuru ya uso wa Ali (a.s.).
(51) Kauli yake (s.a.w.w.); Hasan na Husain ni viongozi wa vijana wa Peponi.
(52) Kauli yake (s.a.w.w.); Mbora wa wanaume wenu ni Ali Bin Abi Talib.
(53) Kauli yake (s.a.w.w.); Ali ni mbora wa viumbe na mwenye kukataa hayo amekufuru.
(54) Kauli yake (s.a.w.w.); Mbora wa wote walio juu ya ardhi baada yangu ni Ali Bin Abi Talib (a.s.).
(55) Kauli ya Ibnu Umar, Ali ni katika Ahlu-Bait ambaye cheo chake hakikisiwi na mtu yeyote.
(56) Kauli yake (s.a.w.w.); Sisi Ahlul-Baiti hakisiwi mtu yeyote nasi.
(57) Kauli yake (s.a.w.w.); Huyu (anamkusudia Ali) ni Bwana (mwenye Mamlaka) wenu baada yangu humu duniani na Akhera.
(58) Kauli yake (s.a.w.w.); Hakika Ali anatokana nami na mimi ninatokana naye.
(59) Kauli yake (s.a.w.w.); kumwambia Ali, wewe ndugu yangu hapa duniani na kesho Akhera.
(60) Kauli yake (s.a.w.w.); mwenye kumwacha (asimfuata) Ali ameniacha mimi.
(61 ) Kauli yake (s.a.w.w.); Ali wewe utakwenda Peponi.
(62) Kuhusu wale wanne wataoingia Peponi.


(63) Imani ya Ali (a.s.) kuwa na uzito zaidi kuliko mbingu na ardhi.
(64) Kauli ya Abdullah bin Umar kusema; Ali anayo mambo matatu, ninatamani niwe nao mojawapo.
(65) Kuonana kwa siri Ali (a.s.) na Mtume (s.a.w.w.); na Ali kutoa sadaka alivyoamrisha Mwenyezi Mungu.
(66) Kauli yake (s.a.w.w.); Mwenye kumpenda Ali Mwenyezi Mungu atamkubalia swala na saumu yake.
(67) Kauli yake (s.a.w.w.); kuwapenda Aali Muhamad (dhuriya wa Mtume) siku moja tu ni bora kuliko ibada ya mwaka mmoja.
(68) Kuzungumza Mwenyezi Mungu na Mtume (s.a.w.w.) usiku wa Miraji kwa lugha (sauti) ya Ali.
(69) Kauli yake (s.a.w.w.); Nalikuwa Mimi na Ali mbele ya Mwenyezi Mungu kabla ya kumwumba Adam (a.s.).
(70) Kauli yake (s.a.w.w.); Kumwambia Ali, 'wewe ni ndugu na waziri wangu'.
(71) Kauli yake (s.a.w.w.); Mwenye kupenda aishi maisha yangu na kufa kwangu) basi ampende na kumfuata Ali.
(72) Kauli yake (s.a.w.w.); kumwambia Aisha kwamba Ali ni Bwana wa Waarabu.
(73) Kauli ya Aisha kwamba Ali ni bora wa viumbe hatilii shaka juu ya jambo hilo ila kafiri.
(74) Kauli yake (s.a.w.w.); Ali ni bora wa viumbe.
(75) Kauli ya Aisha, "Hakumwumba Mwenyezi Mungu aliye mpenzi zaidi kwa Mtume (s.a.w.w.) kuliko Ali (a.s.).
(76) Kauli ya Aisha kwamba: Ali alikuwa mpenzi mno wa Mtume kuliko watu wote.
(77) Kauli ya Aisha, "Kwamba Ali ni karibu zaidi katika huba kwa Mtume (s.a.w.w.) kuliko watu wote.
(78) Kauli yake (s.a.w.w.); kumwangalia uso wa Ali (a.s.) ni ibada.