FADHILA ZA SAYYIDNA ALI (A.S)

 

HADITHI YA THELATHINI NA TATU
uMalaika wameumbwa kwa nuru ya Ali"
Omar (R.A.) amesema kuwa: Mtume (s.a.w.w.) amesema, "Hakika Mwenyezi Mungu ameumba Malaika katika nuru ya uso wa Ali Bin Abi Talib, wanahimidi, kusifu na kumwadhamisha (Mwenyezi Mungu) na kuwaandikia thawabu za hiyo kazi yao wenye kumpenda (Ali) na wenye kupenda kizazi chake."

Hii ni hadithi nyingine aliyoipokea Omar (R.A.) kuhusu ubora wa Ameerul Mumeneen (Ali A.S.) mbali na ile iliyotangulia; na hadithi hii wameipokea Maulama wengi wa Kisunni, na miongoni mwao ni Al-Khateeb Ahmad Khwarizmi Hanafiy katika kitabu chake maarufu Taareekh Maqtalul Husein (A.S.) juzu ya kwanza kilichopigwa chapa Najaf (Iraq). Hakika yeye ameinakili hadithi hiyo kwa kuirejesha kwa Abi Bakar bin Abdillahi bin Abdir-Rahmaan ambaye amesema, "Nimemsikia Uthmani bin Affani akisema nimemsikia Omar bin Khattab, akisema nimesikia Abu Bakari Bin Abi Qahafa, akisema nimesikia Mtume (s.a.w.w.) akisema, "Kwa hakika Mwenyezi Mungu ameumba katika nuru ya uso wa Ali Bin Abi Taalib Malaika ambao wanamhimidi Mweneyzi Mungu na kumtukuza, nao huwaandikia thawabu za hiyo (kazi yao) wenye kumpenda Ali (A.S.) na wenye kuwapenda kizazi chake."

HADITHI YA THELATHINI NA NNE
"Hasan na Husein ni Mabwana wa watu wa Peponi na Ali ni bora kuliko wao"
Katika Kifaayatu-Taalib, imenakiliwa hadithi kutoka kwa Naafii ikitokana kwa Ibnu Omar kuwa Mtume (s.a.w.w.) amesema, "Hasani na Husein ndio mabwana wawili wa vijana wa watu wa peponi, na baba yao ndiye bora kuliko wao wawili. Kisha akasema hadithi hii ni kweli, thabiti; Mwenyezi Mung ametujaalia kuipata na tunamshukuru. Na ameendelea kusema, "Imaamu wa wanazuoni wa hadithi Abulqasim Tabrani katika kitabu chake kiitwacho Muujam Al-Kabeer katika sura kuhusu Hasan bin Ali (A.S.) anaeleza hadithi zinazotoka kwa masahaba na miongoni mwao ni Omari bin Khattab, na Ali Bin Abi Talib na Hudhayfah, nazo ni kama hivi: Imepokewa hadithi kutoka kwa Zari ikitoka kwa Hudhayfah ikisema kuwa, "Tuliona furaha kuu usoni mwa Mtume (s.a.w.w.) siku moja. Tukasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tumeona katika uso wako bishara nyingi za furaha. Mtume (s.a.w.w.) akasema, "Namna gani nisifurahi! Na hali Jibrilu amenijia na amenibashiria kuwa hakika Hasan na Husein ndio mabwana wawili wa vijana wa watu wa Peponi, na Baba yao ndiye bora kuliko wao wawili." Kisha El-Ganji akasema, "Kukusanyika (kufungamana) hizi habari kwa pamoja ni thibitisho na dalili ya ukweli wake."


Mtungaji amesema: Kwa kauli ya Tabraani iliyo katika Al-Muujamil Kabir hadithi itakuwa miohgoni mwa hadithi alizozipokea Omar bin Khattabi kuhusu ubora wa Ameerul Mumineen, Ali Bin Abi Talib (A.S.); na hadithi hii wameitoa wanazuoni (Maulama) wengi wa Kisunni; miongoni mwao ni Al-Ganji Ash-Shafiiy, na Attabrani, na Muhibud-Deen Tabari Shafiiy katika kitabu chake 4Dhakhairul-Uqba' chini ya anwani kuwa (hao wawili Hasani na Husein ni mabwana wa vijana wa Peponi) amesema kuwa hadithi kutoka kwa Hudhayfah imesema. "Nilimwendea Mtume (s.a.w.w.) na nikasali pamoja nave. akaendelea kusali mpaka akasali sala ya Insha. Kisha akaondoka. nami nikamfuata aliposikia sauti yangu, alisema, "Nani huyu? Ni Hudahayfah?" Nikasema "ndiyo". Mtume (s.a.w.w.) akasema, "Hakika huyu ni Malaika. Hakupata kuteremka kabisa katika ardhi kabla ya leo, amemtaka idhini Mola wake ili anisalimie mimi, na anipe bishara kuwa, kwa hakika Fatimah ndiyo Bibi wa wanawake wa watu wa Peponi; na hakika Hasan na Husein ndiyo mabwana wawili wa vijana na watu wa Peponi."

Hadithi hiyo imenakiliwa na Ahmad bin Hanbal na Tirmidhi Abu Haatim amenakili hadithi yenyewe inayosema, "Tumeuona uso mtukufu wa Mtume (s.a.w.w.) unatoa bishara za furaha; Mtume akasema, "Kwa nini nisifurahi na hali imenijia Jibrilu na akanibahiria kuwa hakika Hasan na Husein ndio mabwana wawili wa vijana wa watu wa Peponi na Baba yao ndiye bora kuliko wao wawili." Na Abu-Ali Bin Shaadhani vile vile ameieleza hadithi hiyo kutoka kwa Ibni Omar na Ali Al-Mattaqi ameinakili hadithi hiyo katika Kanzul Ummal Jalada 6, uk. 222.


HADITHI YA THELATHINI NA TANO
"Ali ni bora kuliko wote baada ya Mtume (s.a.w.w.)"
Katika "Yanabiul-Mawaddah" imepokewa hadithi kwa Sayyid All Hamdaniy Shafiiy, kutoka kwa Ibnu Omar ambaye anaeleza kwamba Mtume (s.a.w.w.) amesema, "Bora wa wanaume wenu ni Ali Bin Abi Talib, na bora wa vijana wenu ni Hasan na Husein na bora wa wanawake wenu ni Fatimah binti Muhammad (s.a.w.w.)"

Wanazuoni wa Kisunni wamekariri hadithi hii au yenye maana kama hii katika vitabu vyao vingi kama vile Ali Al-Muttaqi Al-Hanafii katika Kanzul-Ummal (juzu ya 6), ya kutoka kwa Ibnu Abbas akisema kuwa, Mtume (s.a.w.w.) amesema "Ali ni bora miongoni mwa watu wote." Al-Ganji Shafiiy katika Kifaayatu-Taalib, alikariri hadithi kutokana na Jaabir Bin Abdillah, kuwa amesema, "Tulikuwa kwa Mtume (s.a.w.w.) akasema, basi mara Ali Bin Abi Talib akaja; Mtume (s.a.w.w.) akasema, "Hakika amekujieni ndugu yangu." Kisha akageuka kuelekea upande wa El-Kaaba akaipiga kwa mkono wake, na akasema, utNaapa kwa yule ambaye nafasi yangu ipo mikononi mwake, hakika huyu (Ali) na wafuasi wake, ndio wenye kufaulu siku ya Kiyama.

" Kisha akasema, "Hakika yeye ndiye wa mwanzo wenu kuamini, na ndiye mtekelezaji wenu zaidi wa ahadi ya Mwenyezi Mungu, na ndiye mwadilifu wenu zaidi kati ya raia, na ndiye mgawaji wenu zaidi wa usawa, na ndiye mkubwa wenu zaidi wa daraja mbele ya Mwenyezi Mungu." Na (Jaabir) amesema hapo ndipo ilipoteremka aya hii isemayo: "Hakika wale walioamini na wakatenda mambo mema basi hao ni wabora wa viumbe." (98:7) Na (Jaabir) amesema, "Sahaba wa Mtume Muhammad (s.a.w.w.) wakimwona Ali bin Abi Talib anakuja walikuwa wakisema, "Hakika amekuja aliye bora wa viumbe." El-Ganji amesema kuwa hivyo ndivyo alivyopokea mwanazuoni wa hadithi wa nchi ya Shamu aitwaye Ibnu Asaakir katika kitabu chake kinachojulikana sana kwa (jina) la Taarikh Ibn Asaakir, na mwanazuoni wa hadithi wa nchi ya Iraq amepata hadithi hiyo kutoka kwa Zar, ikitoka kwa Ali Bin Abi Talib (A.S.) kuwa amesema kwamba Mtume (s.a.w.w.) amesema.

"Mtu yeyote asiyesema kuwa (Ali) ndiye bora wa watu basi amekufuru," na katika hadithi nyingine iliyotokana na Hudhayfa amesema, "Nimemsikia Mtume (s.a.w.w.) akisema, "Ali ndiye bora wa watu', yeyote atakayekataa na kukanusha. basi amekufuru." Hivyo ndivyo alivyopokea El-Haafidh Ad-Dimishqi katika kitabu chake At-Taarikh kutoka kwa Al-Khatiib Al-Haafidh, na katika riwaya iliyotokana na Jaabir, amezidisha kusema: Mtume (s.a.w.w.) amesema "Ali ndiye bora wa watu, basi yeyote atakayekataa, hakika amekufuru."

Na katika riwayah ya mwanazuoni wa Shaami imeelezwa kuwa "Hawezi kumchukia (Ali) ila Kafir." Na katika riwaya ya Bibi Aisha ikitokana na Ata, amesema, "Nilimwuliza (Bibi) Aisha kuhusu Ali naye basi alisema, "Huyo ndiye bora wa watu, haoni shaka juu ya jambo hili ila Kafir." Kisha akasema, hivyo ndivyo alivyotaja Al-Haafidh Ibn Asaakir kuhusu Ali (A.S.) katika Tarehe yake, juzu ya hamsini. (Kitabu hiki kina majuzu mia tatu katika hayo ni za Ali (A.S.).

Na miongoni mwa hayo ni "Dhakhasirul Uqba", katika kitabu cha "Yanaabiul Mawadda" imenakiliwa hadithi ya (Bibi) Aisha iliyotangulia na hadithi ya Ali (A.S.) na hadithi ya Hudhayfa kuwa Mtume (s.a.w.w.) amesema: "Ali ndiye bora wa watu, na yeyote atakayekataa, basi hakika amekufuru. Vile vile zimeelezwa hadithi nyingi nyingine zenye maudhui ya hadithi hii zilizotokana na Jabir. Katika hadithi hizo ni zile ambazo zimo katika kitabu cha Kanzul Haqaaiq kilichopigwa chapa pembezoni mwa kitabu cha "Jamii Sagheer" Juzu 2, na zile zilizomo mwenye Musnad ya Ahmad Bin Hambal, Juzu ya tano, na katika Nuzhatul Majaalis ya (Sheikh) Assafuriyu Ash-Shaffly, Jalada 2, kilichopigwa chapa Misri mwaka 1320 A.H.
Katika Manaaqib ya (Sheikh) Al-Khwarazmi, imenakiliwa hadithi sahihi iliyotokana na Mtume (s.a.w.w.) kuwa kwa hakika amesema, "Bora wa waliopo juu ya ardhi baada yangu ni Ali Bin Abi Talib."

HADITHI YA THELATHINI NA SITA
Katika Yanabeul Mawaddah kutokana na kitabu "Mawad-datul-Qurba" cha Sayyid Ali El-Hamdaany Shafiiy imeelezwa hadithi kutoka kwa Abi Waail, iliyotokana na Ibn Omar ambaye amesema: Abu-Bakar, Omar, Othman basi mtu mmoja akasema:' "Ewe baba wa Abdir-Rahmani! Ali si katika masahaba wake'? Akasema: "Ali ni katika Ahli-Bayt, hakisiwi na yeyote; yeye yuko pamoja na Mtume (s.a.w.w.) katika daraja yake; hakika Mwenyezi Mungu anasema (katika Qur'ani tukufu), "Ambao waliamini na wakafuatwa na dhuria zao kwa kuamini, tutawakutanisha nao dhuria zao" (52:22) Basi Bibi Fatima (A.S.) yu pamoja na Mtume (s.a.w.w.) katika daraja yake na Ali (A.S.) yu pamoja nao.


Kwa hakika, kauli ya Ibnu Omar kuwa "Ali ni katika Ahli-Bayti, hakisiwi na yeyote," ni ushuhuda na uthibitisho wa kutosha. Kauli hiyo imekaririwa katika Dhakaairul-Uqba cha Muhib buddin Attabari Ash-Shafiiy; ambaye amesema chini ya maudhui kuwa (hakika wao hawakisiwi na yeyote) kutokana na Anas, ambaye amesema kuwa Mtume (s.a.w.w.) amesema, "Sisi ni Ahlul-Bayti, hakisiwi nasi yeyote". Na hakika hadithi hii imenakiliwa na Ubaydullah El-Haafiiy katika kitabu chake Ar-Jahul Mataalib kutokana na "Dhakaairul Uqba" isipokuwa amesema kuwa hadithi hiyo imeelezwa na Ibnu Marduwayhi katika El-Manaaqib, ambamo pia amesema kuwa Ali (a.s.) alisema juu ya mimbari kuwa, "Sisi ni katika watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w.), hatukisiwi na yeyote". Hadithi hiyo imenakiliwa na Day-amiy katika Firdawsil Akhbar. Na katika Yanaabiiul-Mawaddah baada ya kueleza ile hadithi iliyonakiliwa kutoka kwa Ibnu Omar, amesema kuwa "Abdallah bin Ahmad bin Hambal alimwuliza baba yake kunako "Ubora" naye akasema, "Abu Bakar, Umar, Uthman." Tena akanyamaza. Abdallah bin Ahmad akasema, "Ewe baba yangu, yuko wapi Ali Bin Abi Talib?" Akasema: Yeye ni katika watu wa nyumba (ya Mtume S.A.W.W) hakisiwi na hawa." Na Ali Al-Muttaq El-Hanafiiy amenakili hadithi hii katika 'Kanzul Ummal' Juzu ya 6, kutokana na Firdawsul Akhbar ya Daylamiy, ambayo imesema, "Sisi ni katika Ahlul-Bayti, hakisiwi nasi yeyote."


HADITHI YA THALATHINI NA SABA
"Ali ni bwana wa mwumini baada yangu"
Katika Yanaabiiul-Mawaddatul Qurba imeelezwa hadithi ya Ibnu Omar kuwa amesema, "Tulikuwa tukiswali pamqja na Mtume (s.a.w.w.) basi akatupa jicho kwetu na akasema, "Enyi watu! Huyu ndiye mpenzi wenu baada yangu, duniani na akhera; basi muhifadhini (yaani, anamkusudia Ali a.s.)".

Hadithi hii au yenye maana kama hiyo imenakiliwa na kundi la wanazuoni wa Kishafiy, Hambali na Imaamiyah (Shia) katika vitabu vyao vinavyo zingatiwa sana; na katika jumla ya wanazuoni wa Kisunni waliopokea hadithi hii ni Ibnu Kathiri katika kitabu chake Al-Bidaya Wan-Nihaya, Juzu 7. Yeye ameinakili kwa Imraani bin Hasiini, ambaye amesema, w'Baadhi ya Masahaba walimshitaki Ali (a.s.) kwa Mtume (s.a.w.w.). Basi Mtume (s.a.w.w.) aliwaendea hali uso wake umebadilika kwa ghadhabu na akasema "Mwacheni Ali, mwacheni Ali, mwacheni Ali, hakika Ali ni katika mimi na mimi ni katika yeye, naye bwana wa kila mwenye kuamini baada yangu."


Kwa ufupi hadithi hiyo imemalizikia hapa. Na katika kitabu hicho hicho cha Al-Badaaya Wannihaya juzu ya saba, imekaririwa hadithi kwa mapokeo ikitoka kwa Wahab bin Hamza naye amesema kwa ufupi, "Nilisafiri pamoja na Ali basi niliporejea nikakutana na Mtume (s.a.w.w.) ambaye mara akamkumbuka Ali (a.s.). Mimi nilimsema Ali kwa maneno mabaya, basi Mtume (s.a.w.w.) akaniambia, "Usimseme Ali kabisa (maneno mabaya kama haya); kwani Ali ndiye bwana iwen baada yangu." Na Muhibbud Deen Tabari amenakili hadithi hiyo katika Dhakhaairul Uqba na Tirmidhi katika Saheeh yake, juzu ya pili, kwa mapokeo ya hadithi iliyotoka kwa Mtume (s.a.w.w.) ambaye kuhusu habari za Ali (a.s.) amesema kuwa, "Hakika yeye ndiye bwana wa kila mwenye kuamini baada yangu."


Na Ubaydullaah El-Hanafiy ameeleza hadithi hii katika kitabu chake Ar-Jahul Mataalib kwa mapokeo ikitokana na Imraan bin Hasiin ambaye amesema kuwa Mtume (s.a.w.w.) alipeleka jeshi, na Ali Bin Abi Talib alikuwa pamoja nao, basi akaenda na kikosi hicho, na (huko) akapata mjakazi wakamchukua masahaba wane (katika wao) wakafanya shauri yao na wakasema, "Tukimkuta Mtume (s.a.w.w.) tutamshitakia na (utamwambia namna alivyofanya (Ali)" Na Waislamu walipokuwa wanarejea safari zao, kwanza huenda kwa Mtume (s.a.w.w.) kumsalimu, kisha ndipo huenda zao makwao.

Basi kilipofika kile kikosi walimsalimu Mtume (s.a.w.w.); (kisha) mmoja wa wale watu wane akasimama na akasema "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Je. hukumwona Ali amefanya hivi na hivi?" Basi Mtume (s.a.w.w.) akanyamaza kisha akasimama wa pili na akasema kama yule wa mwanzo na akasimama wa tatu na wane na wakasema kama vile walivyosema wenzao. Hapo Mtume (s.a.w.w.) akawakabili kwa uso wa ghadhabu na akasema, "Mnataka nini nyinyi kwa Ali?" Na alisema hivyo mara tatu, na akaendelea kusema kuwa: "Hakika Ali ni katima mimi na mimi ni katika yeye; na yeye ndiye Bwana wenu (mwenye mamlaka) baada yangu." Amenakili hadithi hiyo Abu-Daud At-Tayalisi katika kitabu chake "Sanaun" (J.H.). Vile vile Ahmad bin Hambal amenakili katika kitabu chake "Musnad" (J.H. uk 460) kwa kusema kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimwambia Buraydah, "Ewe Buraydah! Usimseme Ali kwani yeye anatokana nami, na mimi natokana naye, na yeye ni bwana wenu na mwenye mamlaka juu yenu baada yangu."


HADITHI YA THELATHINI NA NANE
"Ali ni Nduguye Mtume (s.a.w.w.)"
Katika Dhakhairul Uqba imenakiliwa hadithi ya Ibnu Omar kuwa Mtume (s.a.w.w.) alifanya udugu kati ya masahaba wake; basi Ali alikuja na akasema, "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, umefanya udugu kati ya masahaba wako, na wala hukufanya udugu kati yangu na kati ya mwingine yeyote?" Mtume (s.a.w.w.) akasema, "Wewe ndiye ndugu yangu katika dunia na akhera.

Hadithi hii imepokewa kutoka kwa Omari bin Khattab (r.a.) na kwa Abdalla bin Omar. Na hadithi aliyopokea Ibnu Omari imenakiliwa na mabingwa wa wanazuoni wa Kisunni; miongoni mwao Tirmidhiy katika Saheeh yake, juzu 2, uk. 461 na amesema (kuwa) hadithi hii ni hasa (kweli). Kadhalika El-Baghawi, katika Masaabiihus-Sunnah (juzu 2, uk. 202), Ibnu Kathiiri katika El-Bidaaya Wannihaya, juzu 7, uk. 335, Ali El-Muttaq El-Hanafiy katika KanzuI-Ummal, juzu 6. uk. 122, 152, 153. 159, 390, 394, 399, 400, 402 na 404. Na mahali pengine pengi kama vile Ibnu-Athiir El-Jazary katika Usdul Ghaba Juzu 4 uk. 16 na Al-Muwaffaq bin Ahmad El-Hanafiy katika El-Manaaqib, uk. 82,83,91 na95.

Vile vile Ahmad bin Hambal katika Musnad yake mahali chungu nzima ametaja, k.v. katika juzu 1, uk. 230, Ibrahim bin Muhammad Al-Hamwiniy Ash Shafiy katika Faraidus-Simtain, j. 1, babu 21, mahala aliponakili hadithi ya "Al-Muaa-khaat" (udugu) Al-Mannawi katika Kanzul Haqaaiq iliyoandikwa pembezoni mwa kitabu, Al-Jaamul Sagheer cha Suyuti Shafiiy (j. 2. uk. 70) na wanazuoni wengi wa Kisunni waliopokea hadithi hii minghairi ya hawa. Na vitabu mahsusi vimetungwa vya hadithi hii ya uMua-khaat". Angali kitabu cha Ghas-yatul Maraam cha Allama Al-Mujja As-Sayyid Hashim Al-Bahrani, kilichopigwa chapa Iran.


HADITHI YA THELATHINI NA TISA
"Anayefarakana na Ali anafarakana na Mtume"
Katika Manaaqib ya Al-Khateeb Al-Muwaffaq bin Ahmad Al-Khwarizmi Al-Hanafi uk. 62, imo hadithi iliyotokana na Ibnu Omar kuwa Mtume (s.a.w.w.) amesema. Mtu yeyote atakayefarakana (Kujitenga) na Ali ndiyo amefarakana na mimi na yeyote atakayefarakana na mimi ndiyo amefarakana na Mwenyezi Mungu.

Hadithi hii na hadithi yenye maudhuui kama haya imeelezwa na kikundi cha wanazuoni wa Kisunni katika vitabu vyao. Miongoni mwao ni Ali Al-Muttaqi Al-Hanafiy katika Kanzul Ummal (j. 9 uk. 156) kwa matamko mbalimbali kutokana na vitabu vingi, k.v. Al-Muu-jam Al-Kabeer ya Tabarani kutokana na Ibnu Omar kuwa Mtume amesema, wCMtu yeyote atakayefarakana na Ali ndiye amefarakana na Mwenyezi Mungu." Tena humo humo katika Al-Muu-jam Al-Kabeer, Ibnu Omar amesema kuwa Mtume (s.a.w.w.) amesema, "Yeyeote atakayefarakana nawe ewe Ali! Basi hakika ndiyo amefarakana na mimi, na yeyote atakayefarakana na mimi, basi hakika ndiye amefarakana na Mwenyezi Mungu." Na ameinakili tena katika "Al-Mus-tad-rak ya Saheehain (sahihi mbili) cha Al-Haakim Nisa-puri kutoka kwa Abu-Dhar; na tamko lake na tamko la Tabraani katika Al-Muu-jami ni sawa sawa.

HADITHI YA ARUBAINI
"Ali ni miongoni mwa wa mwanzo kuingia Peponi."
Katika Kanzul Ummal (j. 6, uk. 391) Ali Al-Muttaqi Al-Hanafiy amenakili hadithi hii kutokana na Ib un-Najjari katika tarehe yake, na kutoka kwa Ibnu Omar kuwa hakika Mtume (s.a.w.w.) alimwambia binamu yake Ali Bin Abi Talib (a.s.) kuwa. "Ewe Ali, wewe (utaingia) Peponi."

Zimepokewa hadithi nyingi katika vitabu vya wanazuoni wa Kisunni ambazo zinawaflkiana na hadithi hii katika maneno (yake) na kwa maana pia kwa matamshi mbali mbali zikitokana na Ibnu Omar na wengineo. Katika hadithi hizo ni ile ambayo iliyomo ndani ya Tarikh ya Ibnu Asaakir (J. 4, uk. 318) kuwa Ali (a.s.) amesema, "Nilimshitakia Mtume (s.a.w.w.) husuda za watu (wanazonifanyia mimi)" Mtume (s.a.w.w.) akasema, "Ewe Ali! Hakika watu wanne wa mwanzo watakaoingia Peponi ni mimi, na wewe, na Hassan, na Husain, na dhuria zetu watakuwa nyuma yetu, na wake zetu watakuwa nyuma ya dhuria zetu" Ali (a.s.) akauliza, "Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, watakuwa wapi wafuasi (Shia) wetu? Mtume (s.a.w.w.) akajibu, "Wafuasi (Shia) wenu watakuwa nyuma yenu."

Na katika hadithi hizo ni zile ambazo zimo ndani ya "AS-SAWA-IQUL MUHRIQA" uk. 98. Yeye amenakili hadithi ambayo ilinakiliwa na IBN ASKARI na amezidisha mwisho wa hadithi hiyo kuwa "Na wafuasi (Shia) wetu watakuwa upande wetu wa kulia na wa kushoto". Vilevile hadithi hii imo katika kitabu cha Tafsiri cha Nishaapuri ambacho kimepigwa chapa pembezoni mwa Tafsiri ya Tabari, (juzu 25, uk. 31).

Kadhalika, Ibrahim Bin Muhammad Al-Mamuuniy Ash-shafiiy katika kitabu chake, Faraidus-Simtayn, (]. 2, Mlango 9), Ali Al-Muttaqi katika Kanzul Ummal (J. 6 uk. 212), Sheikh Sulaymaan Al-Qanduuzi Al-Hanafy, katika Yanaabeeul-Mawaddah (Uk. 269), kwa hakika yeye ameikariri hadithi kutokana na Ali (a.s.) kutoka kwa Ibn Masud na kwa Abii Raafii (R.A.). Ama tamko la Ameerul-Momineen Ali Bin Abi Talib (a.s.) ni kuwa Ali (K.W.) amesema hivi, "Nilimshitakia Mtume (s.a.w.w.) husuda ya watu (wanayonifanyia) mimi; basi Mtume (s.a.w.w.) akasema kuniambia mimi; Je, huridhii kuwa wa nne katika (watu) wane? - Wa mwanzo atakayeingia peponi ni mimi, wewe, Hasan, na Husein; na wake zetu watakuwa upande wetu wa kulia, na wafuasi (Shia) wetu watakuwa upande wetu wa kushoto". Na dhuria zetu watakuwa nyuma ya wake zetu. Aidha ameitoa hivyo Ath-Thaalabiy, na Ahmad ameieleza katika Al-Manaaquib, na Sibtu Jawzi. ameelezea vivyo hivyo.


Na tamko la Ibnu Masud linasema hivi: Mtume (s.a.w.w.) alimwambia Ali (a.s.) "Je, huridhii kuwa hakika wewe utaingia peponi na mimi na Hassan na Hussein; na dhuria zetu, watakua nyuma ya migongo yetu na wake zetu watakuwa nyuma ya dhuria zetu; na wafuasi wetu watakuwa katika upande wetu wa kulia na wa kushoto. Hadithi hii imo katika Al-Manaqib. Ama tamko la Abbii Raafii ni kuwa Mtume (s.a.w.w.) amesema, "Ewe Ali! Hakika watu wane na mwanzo watakaoingia peponi ni mimi na wewe na Hassan na Husein, na dhuria zetu watakuwa nyuma ya migongo yetu, na wake zetu watakuwa nyuma ya dhuria zetu. na wafuasi wetu watakuwa upande wetu wa kulia, na wa kushoto". Tabarani katika "Al-Muujamul Kabeer"


HADITHI YA AROBAINI NA MOJA
"Imani ya Ali ni nzito kuliko ardhi na mbingu."
Katika Kanzul Ummal (J. 6 uk. 156) imo hadithi iliyopokewa na Ibnu Umar kuwa Mtume (s.a.w.w.) amesema, wwlwapo kama mbingu na ardhi zingewekwa katika kitanga kimoja (cha mizani) na Imani ya Ali Bin Abi Talib katika kitanga kingine, bila shaka Imani ya Ali ingalizidi." Angalia Daylami katika kitabu chake Firdawsul Akhbaar. Hadithi hii ilikwishatangulia iliyotokana na Umar Bin Khattab. ... kwa sababu ya hitilafu za mpokeaji na maneno tumekariri hadithi hii mara ya pili, kwa ajili ya kuthibitisha vile ilivyotakikana.


HADITHI YA AROBAINI NA MBILI
"Mambo matatu ni mahsusi kwa Ali (a.s.) tu"
Katika Manaaquib ya Al-Khateeh Al-Muwaffaq Bin Ahmad Al-Khwarazmi Al-Hanafi, (Uk. 187) imeelezwa hadithi kutoka kwa Abdalla Bin Umar kuwa Omar bin Khattab. Alisema Ali anayo mambo matatu na nilitamani kuwa na moja miongoni mwa (mambo) hayo, ingalikuwa bora zaidi kwangu kuliko kupewa ngamia wekundu: (1) kuozwa na Bibi Fatima (a.s.) (2) Kupewa bendera siku ya (vita ya) Khaybar (3) kutenda kama ilivyoamrishwa kwa mujibu wa aya ya NAJWA.

Imeshatangulia hadithi kuhusu mambo mawili; na lile jambo la tatu (yaani) lile la tokea la "Najwa" ni mashuhuri sana, tena ni katika mambo yanayomhusu Imam Ali (a.s.) peke yake. wala hashirikiani katika sifa hii na yeyote katika Masahaba. Na wanazuoni wa hadithi na Tafsiri zote wanawaflkiana katika jambo hilo. Basi katika "Kifaayatu-Taalib cha Al-Kanji Shafiiy, (uk. 52) mlango wa ishirini na tisa, imesemwa kuwa "Hakika aya ya "AN-NAJWA" ilifuata kitendo cha Ali (a.s.) tu wala si sahaba yeyote mwingine. Kisha aya hiyo ikanasikhishwa (kuondolewa na hakupata kuitenda mtu yeyote ila Ali a.s.)".

Kisha ameipokea hadithi kwa umadhubuti kwa Ali bin Alqama Al-Anmaary ikitokana na Ali bin Abi Talib (a.s.) kuwa amesema, "Iliposhuka aya (58:12) Enyi mlioamini: Mnapomsemeza Mtume kwa siri toeni sadaka kabla ya kumsemeza Mtume (s.a.w.w.) akaniita, na akaniambia: "Je, unaonaje dinari moja? Nikasema hawaiwezi. Mtume (s.a.w.w.) akasema ngapi basi? Nikasema, dhahabu yenye uzito wa kipimo cha punje au shayiri moja, Mtume akasema, "Hakika wewe ni mtawa! Basi ndipo ilipoteremka aya hii, "Oh! Mnaona taabu kutanguliza hiyo sadaka kabla ya kumsemeza kwenu? (58:13). Basi Ali (a.s.) akasema "Kwa sababu yangu Mwenyezi Mungu amefanya wepesi kwa umma huu, na wala haikupata kuteremka (yah hii) kwa yeyote kabla yangu, wala haikuteremka kwa yeyote baada yangu, wala hakuifuata aya hii mtu yeyote ila mimi tu".


Ibnu Umar amesema: "Ali bin Abi Talib alikuwa na mambo matatu. Laiti ningekuwa na moja tu miongoni mwa hayo, ingalikuwa inanipendeza mno kwangu kuliko (kitu kingine chochote) duniani. (1) Kuozwa Bibi Fatima (a.s.) (2) Kupewa bendera (3) kuteremka aya ya "AN NAJWA". Mujaahid amesema, "Masahaba walikatazwa kuonana faraghani na Mtume (s.a.w.w.) hadi watoe sadaka. "Basi ikawa hakuonana naye faraghani isipokuwa Ali bin Abi Talib (a.s.) (yeye) alikwenda na dinari moja, basi akaitoa sadaka, kisha ndipo ilipoteremka ruhusa. Kwa hiyo sadaka ilikuwa ni faradhi itokayo kwa Mwenyezi Mungu wakati wa maonano ya faragha. Basi aya hii iliyo katika kitabu cha Mwenyezi Mungu (Qurani) hakuifuata na kuitenda mtu mwingine isipokuwa Ali bin Abi Talib (a.s.). Kisha Al-Kanji amesema. "Katika jambo na tendo hilo kuna fadhila na utukufu usiokuwa na mfano, na wanafahamu na kujua wale wenye akili! Na kule kuenea kwake (kisa hiki) kwa mabingwa (waongozi) wa hadithi, kunatosheleza maneno na maelezo yake mwenye Ibn Jarir At-Tabary ambaye .amesema hivi: "Wamewafikiana mabingwa wa Tafsiri wote kuwa hakika hakufuata na kutenda juu ya aya hiyo yeyote isipokuwa Ali tu."


Tumekwishaeleza kwa ufupi tafisiri na maana ya aya AN NAJWA. Hapa tunakuelezea baadhi ya wale ambao wameandika kisa hiki katika vitabu vyao, katika wanazuoni wa Kihanafi na Shafiiy. Miongoni mwao ni Allaamah Jaral-Laah Mohmood bin Umar Al-Hanafy katika kitabu chake kiitwacho Al-Kash-Shaf (J. 2, Uk. 443) kilichopigwa chapa Misri mwaka 1308 A.H., Abu Jaffer At-Tabary mwenye Kitabu kiitwacho "Tafseer At-Tabary" (J. 28, Uk. 14) kilichopigwa chapa Misri mwaka 1321 A.II.. Muhammad bin Saib Al-Kalbi, katika tafsiri yake, (J. 4:105) iliyopigwa chapa Misri mwaka 1355 A.H., AsSuyooti Ash-Shalli, katika tafsiri yake maarufu AD-DURRUL MAN-THOOR (J. 6, Uk. 185), ALAA-UD-DEEN anayejulikana sana kwa jina la AL-KHAAZIM, katika tafsiri yake maarufu Tafsirul Khazin, au Lubabut-Taaweel wa Maani - Tanzeel (J. 4, Uk. 242), Ibrahim bin Maaqal An-Nasafi Al-Hanafi, katika kitabu chake kiitwacho Madaarikut Tanzeel wa Haqaaiqut-Taaweel kilichopigwa chapa pembezoni mwa kitabu cha tafsiri cha Al-Khazin (J. 4, Uk. 242). Na katika tafsiri hii hasa ametaja kwa urefu kisa cha aya ya "AN-NAJWA" na ameeleza kiasi alichotoa sadaka Ameerul-Mumineen Ali bin Abi Talib (a.s.) alipokwenda kuongea siri na Mtume (s.a.w.w.) baada ya kushuka aya yenyewe na ameeleza maswali kumi aliyouliza Ali kwa Mtume (s.a.w.w.) nayo ni mambo kumi muhimu na maelezo yake yameshatangulia.

Na mwisho wa maneno yake humo amesema hivi. "Alipokwishamaliza Ameerul Momineen Ali bin Abi Talib (a.s.) maswali yake (kwa Mtume (s.a.w.w.) ndipo iliteremshwa aya kufuta (Naskh) amri ya aya hiyo"

HADITHI YA AROBAINI NA TATU
"Kuwapenda Aali Muhammad (s.a.w.w.) ni bora kuliko Ibada"
Katika kitabu cha MANAA-QIB cha Al-Khateeb Al-Muwaffaq bin Ahmad Al-Khawarazmi Al-Hanafi, Uk. 43; imeelezwa hadithi kutoka kwa Naafii ikitokana na Ibn Umar kuwa Mtume (s.a.w.w.) amesema, "Yeyote atakayempenda Ali, Mwenyezi Mungu hukubali swala yake, na saumu yake, msimamo wake (ndani ya swala), humkubalia Dua lake, na yeyote atakayempenda Ali Mwenyezi Mungu atampa kwa kila mshipa ulio ndani ya mwili wake mji katika Pepo (Akhera). Fahamuni! Na yeyote atakayewapenda Aali Muhammad (Ahlul Bait a.s.) atasalimika katika Hesabu na Mizani na Sirati (huko Akhera): Fahamu! Na yeyote atakayekufa katika (hali) ya kuwapenda Aali Muhammad, basi mimi ninamdhaminia kuingia Peponi pamoja na Mitume; Fahamuni! Na yeyote atakayewachukia Aali Muhammad. atakuja siku ya Kiyama hali imeandikwa katika ya macho yake (kuwa) ni mwenye kukupuka) kukata tamaa katika rehema ya Mwenyezi Mungu."


"Hatuna haja ya kutaka kuthibitisha kupendwa kwa Ali (a.s.) au Aali Muhammad (s.a.w.w.) baada ya kuwa Mwenyezi Mungu kishawajibisha na kufaridhisha mapenzi yao juu ya watu wote katika Qurani tukufu, kama alivyosema Subhanahu Wataala, "Waambiye sikutakini malipo yoyote kwenu ila kuwapenda jamaa zangu. Basi jambo linalofaa kutajwa ni kubainisha dalili na thibitisho za kuwapenda na kuwabughudhi kwa hadithi zilizopokewa kutoka kwa Mtume mtukufu (s.a.w.w.)- Miongoni mwa hizo ni ile hadithi iliyotangulia aliyoinakili Al-Khwarazmi Al-Nanafy. Hakika zimepokelewa hadithi nyingi zenye madhumuni ya hadithi hii. Miongoni mwa hadithi hizo ni ile hadithi iliyotangulia tuliyonakili katika hadithi ya thelathini na mbili (32). Na hadithi hiyo na ile iliyonakiliwa mwanzo zatosha.

Hadithi iliyo nzuri mno ni ile hadithi fupi ya Mtume (s.a.w.w.) ambamo amebainisha faida ya kuwapenda jamaa za Mtume (Aali Muhammad s.a.w.w.) katika dunia na akhera. Nayo ni ile hadithi aliyoinakili mwanazuoni Al-Allama Ubaidullaah Al-Hanaty katika kitabu chake Ar-jahul-Mataalib (Uk. 319). Amesema, "Imepokewa hadithi kutoka kwa Ibnu Mas-udi kwamba Mtume (s.a.w.w.) amesema: "Kuwapenda Aali Mohammad (Jamaa za Mtume) siku moja ni bora kuliko kufanya Ibada kwa mwaka mmoja na atakayekufa na katika hali ya kutowapenda hawataingia Peponi."

HADITHI YA AROBAINI NA NNE
"Mtume Muhammad (s.a.w.w.) na Ali (a.s.) wameumbwa kwa Nuru moja"
Katika Manaaqibul Khateeb, Al-Muwaffaq bin Ahmad Al-Khwarazmi Al-Hanafiy (Uk. 47) na katika kitabu chake kingine kijulikanacho kwa jina la MAQ-TALUL Husein (a.s.) J. 1, Uk. 42) kilichopigwa chapa AN-NAJAAFUL ASHRAF amenakili hadithi kutoka kwa Abdullah Bin Umar kuwa amesema "Nimemsikia Mtume (s.a.w.w.) akiulizwa kwamba lugha (sauti) gani alisema naye Mola wako usiku wa Miraji? (Mtume s.a.w.w.) akasema, "Amenisemjga kwa lugha ya Ali Bin Abi Talib. Akanitia moyoni (mpaka) niKasema "Ewe Mola wangu! Wewe ndiye uliyenisemeza au Ali?" Mwenyezi Mungu akasema, "Pwe Ahmad! Mimi niko (lakini kuweko kwangu) si kama vitu vilivyopo, sifananishiwi na watu wala sisifiwi kwa vitu, nimekuumba kutokana na nuru yangu na nimemwuumba Ali kutokana na nuru yako. Basi nikatazama katika siri za roho yako nisimkute (mtu) umpendaye zaidi kuliko AJi Bin Abi Talib, basi nikakusemeza kwa lugha (sauti) ya Ali upate tulizo la roho yako."


Hilo (nililolitoa hapo juu) ndio tamko la Khwarazmi katika Manaqib. Ama tamko lake lililomo katika tarekh kinachojulikana kwa Maqtalul Husein (a.s.) linasema hivi, "Imetokana na AbduJlah Bin Umar kuwa amesema, "Nimemsikia Mtume (s.a.w.w.) wakati alimwuliza: kwa Lugha (sauti) gani aliyosema nawe Mola wako? Mtume (s.a.w.w.) akasema, "Amenisemeza kwa lugha (sauti) ya Ali Bin Abi Talib. Nikaingiwa na hamu (mpaka) nikasema, Ewe Mola (ni we we) uliyenisemeza au Ali? Mwenyezi Mungu akasema "Ewe Ahmad! Mimi niko (lakini kuweko kwangu) si kama viumbe; sifananishwi na watu, na sisifiwi na vyenye kufanana. nimekuumba kutokana na nuru yangu, nikamwumba Ali kutokana na nuru yako; basi nikaangalia katika siri za roho yako. basi sikukuta rohoni mwako mpenzi mno kuliko Ali, basi nikakusemeza kwa lugha (sauti) yake ili upate tulizo la roho yako."


Kwa kuangalia sana matamko hayo mawili, utajua tofauti zilizopo kati yao. Na kuhusu habari zilizopokewa kuwa hakika wao Mtume (s.a.w.w.) na Ali (a.s.) wameumbwa kwa nuru ya Mwenyezi Mungu na hakika nuru yao ni moja, zipo hadithi nyingi sana; wamezikariri wanazuoni wa ki-Sunni, Shafii, na Hanafi na wanazuoni wa Ki-Shia (radhi za Mwenyezi Mungu ziwaendee wote). Miongoni mwao ni mwaazuoni mkubwa Al-Allama Ubaidullah Al-Hanafi katika kitabu chake, "ARJAHUL-MATALIB" (Uk. 459) ambaye ametafsiri hadithi kutoka kwa Husin Bin Ali Bin Abi Talib (a.s.) kutoka kwa baba yake kuwa Mtume (s.a.w.w.) amesema, "Mimi na Ali tulikuwa kwa Mwenyezi Mungu kabla ya kuumbwa Adam (a.s.) kwa miaka elfu kumi na nne. Mwenyezi Mungu alipomwumba Adam (a.s.) akapitisha nuru ile katika mgongo wake. Ikawa Mwenyezi Mungu anaihamisha (ile nuru) kutoka mgongo mmoja hadi mgongo wa pili hadi ikafika mgongo wa Abdul Muttalib, baadaye akaigawa nuru mara mbili. Nusu moja (akaitia) katika mgongo wa Abdullah, na nusu ya pili (akaitia) katika mgongo wa Abi Talib.


Basi Ali ametokana nami na mimi natokana naye; nyama yake ni nyama yangu na damu yake ni damu yangu. Basi atakayempenda (Ali) ndio mpenzi wangu (na mimi) nitampenda. na atakaycmchukia (Ali) ndiye adui yangu (na mimi) nitamchukia." Hadithi hiyo imeelezwa na Ibnu Marduwaihi katika "manaaquib" na vilevile Khwarazmi, Shihabuddini Ahmad, Al-Matarrizi, na Aasimy. Pia katika kitabu hicho hicho UK. 459, amesema: tuKatika riwaya (hadithi) ya Abd-Fathi Muhammad bin Ali bin Ibrahim An-Naseeri (iliyomo) katika Khasaisul-Alawiya" kutoka kwa Salmani kuwa amesema: Nimemsikia Mtume (s.a.w.w.) akisema, "Mimi na Ali tumeumbwa kutokana na nuru iliyo upande wa kulia wa Arshi. Tunamtukuza Mwenyezi Mungu kabla hajamwumba Adam kwa miaka kumi na nne elfu. Mwenyezi Mungu alipomwumba Adam, akatuhamisha miongonrmwa wanaume na matumbo ya wanawakc watukufu hadi kufika katika mgongo wa Abdul-Muttalib. Akatugawa (katika mgongo huo) nusu mbili. Basi nusu moja akaitia katika mgongo wa Abdul-Laahi na ile nusu nyingine akaijalia katika mgongo wa Abi Talib.


Basi kwa nusu ile (iliyoingia kwa Abdallah) nikaumbwa mimi, na Ali akaumbwa kwa ile nusu ya pili (iliyoingia kwa Abi Talib). Akatupatia (Mwenyezi Mungu) majina kutoka majina yake matukufu, basi Mwenezi Mungu ni Mahmud na mimi ni Muhammad, Mwenyezi Mungu ni AL-AALAA na ndugu yangu ni Ali, Mwenyezi. Mungu ni Faatir na binti yangu ni Fatima, Mwenyezi Mungu ni Muhsin na wajukuu zangu ni Hasan na Husein. Basi jina langu likawa katika Utume, na jina lake (Ali) likawa katika ukhalifa na ushujaa. Basi mimi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Ali ni upanga wa Mwenyezi Mungu.

Katika kitabu chetu cha ALI-WAL-WASIYYAH tumcnakili hadithi nyingi zinazohusu Nuru ambayo Mtume (s.a.w.w.) na Binamu Wake Ali (a.s.) wameumbwa nayo.