SHAHADA YA SAYYIDAT FATIMA (A.S)

 

SEHEMU YA NANE:
USIA WA SAYYIDAT FATIMA (A.S) KWA MUMEWE ALI (A.S).
Imepokewa kutoka kwa Raudhat Al-waaidhiina na wengine, kwamba: Sayyidat Fatima (a.s) aliumwa maradhi makali sana,na alibaki muda wa siku arobaini (40 tu) katika maradhi yake mpaka alipokufa (a.s).Baada ya kujihisi kuwa hawezi kupona kutokana na maumivu makali yaliyotokana na maradhi hayo, akamuita Ummu Ayman,na Asmaau bint Amiysi wakakaa karibu naye,na Imam Ali (a.s) akiwa kando ya mkewe Fatima (a.s),kisha Fatima (a.s) akasema:

Ewe Mtoto wa Ami yangu! Kwa hakika Nafsi yangu imesha pata tangazo la kifo (Death announcement), na hakika mimi sioni mbele yangu kilichobaki ila (karibuni hivi) nitakutana na Baba yangu saa baada ya saa, na mimi nakuusia (Mume wangu) mambo kadhaa kutoka katika Roho yangu; Imam Ali (a.s) akamwambia:

"Niusie chochote kile utakachokitaka Ewe Bint ya Mtume (s.a.w)", akakaa karibu sana na Kichwa cha Bi Fatima (a.s),kisha akawatoa wote waliokuwa mahala pale katika nyumba ile,wakabaki wawili tu,kisha Faatima (a.s) akaanza kumuusia Mumewe Imam Ali (a.s) namna hii:

Ewe Mtoto wa Ami yangu! Hujanihaidi kitu chochote ukiwa ni mwenye kusema uongo au kunifanyia khiyana,na sijawahi kukukhaalif u au kwenda kinyume na kauli yako tangu tuanze kuishi pamoja;Imam Ali (a.s)akasema:Najikinga kwa Mwenyeezi Mungu,wewe ni mjuzi zaidi wa kumjua Mwenyeezi Mungu,na ni Mchamungu,Mkarimu pia na mnyenyekevu,na wewe ni mwenye Kumuogopa sana Mwenyeezi Mungu kiasi kwamba siwezi kuthubutu hata sekunde kukushakia kwamba kuna siku ulikwenda kinyume na kauli yangu (na kunikhaalif),ninasikitika sana kutengana na wewe,ispokuwa ni jambo ambalo lazima liwe,na Mwenyeezi Mungu (s.w) kaufanya msiba wa Mtume (s.a.w) kuwa mpya,na kifo chako na kutenga na wewe ni pigo kubwa sana kwangu,kwa hakika sisi wote ni wa Mwenyeezi Mungu (s.w) na sisi kwake yeye tutarejea,ni msiba mkubwa ulioje na wenye kusikitisha zaidi,Wallah! Msiba huu ni msiba usiokuwa na fanaka (yaani kitulizo au liwazo),na ni masaibu yasiyokuwa na mfano wake,kisha wote wawili wakalia kwa muda wa saa zima hivi,Kisha Imam Ali (a.s) akakichkua kichwa cha Sayyidat Fatima (a.s) na kukikumbatia katika kifua chake,kisha akasema:


Niusie chochote kile utakachokitaka, kwa hakika utanikuta ni mwenye kutekeleza yote kama ulivyoniamrisha nifanye,na nitachagua jambo lako kuliko jambo langu,kisha Fatima (a.s) akasema: Mwenyeezi Mungu (s.w) akulipe kheri ya malipo Ewe Mtoto wa Ami yangu.

Kisha akamuusia amuoe baada yake Amaama ambaye ni binti ya Dada yake Zainab,na amuandalie jeneza.na kwamba ahakikishe hashuhudii yeyote yule miongoni mwa wale waliomdhulumu na kuchukua haki yake,na ahakikishe pia hamsalii mtu yeyote miongoni mwao wala yule ambaye ni miongoni mwa wafuasi wao,na kwamba amzike usiku macho yatakapo pumzika na kulala.

Kisha alimuusia Imam Ali (a.s) awe ndiye mwenye kumuosha, na kumvisha sanda, na kumsalia, na kumshusha kabrini, na kumlaza kwenye Lahdi, Kisha akasema kumwambia Imam Ali (a.s):Na uweke udongo juu yangu,kisha ukae sehemu ya kichwa changu kuelekea uso wangu,kisha usome na uzidishe kusoma Qur'an Tukufu na Dua,hakika wakati huo ni saa {au ni muda ambao } ambayo Maiti anahitaji msaada kutoka kwa aliyekuwa hai,na mimi ninakuaga kwa Mwenyeezi Mungu (s.w) na ninakuusia kwa (watoto wangu) kizazi changu yaliyokuwa ya kheri.Kisha baada ya hapo Ummu Kulthuum akaja mahala pale alipokuwa Imam Ali (a.s) akaungana na Fatima (a.s) na baada ya Sayyidat Fatima (a.s) kuaga Dunia,Imam Ali (a.s) akafanya yote hayo aliyousiwa na Mkewe Fatima (a.s).

Pia kuna Riwaya nyingine imepokelwa kwamba: Pindi mauti yalipomfika Sayyidat Faatuma (a.s), akamwambia Imam Ali (a.s): Nitakapo kufa,basi asijue yeyote kuhusiana na kifo changu ispokuwa Ummu Salama,na Ummu Ayman,na Fidh-dha,na Wanangu,na Abbaas,na Abdullah bin Abbaas,…..,na Salmaan,na Ammaar,na Miqdaad,na Aba Dhar,na Hudhaiyfa,kisha akasema Bi Fatima (a.s):

Hakika Mimi nimekuhalalishia uweze kuniona baada ya mauti yangu, hivyo kuwa Na wanawake wale watakaoniosha, wala usinizike ispokuwa usiku na mtu yeyote asijue kabri langu" Kwa ufupi hivi ndivyo "Shahada" ya Sayyidat Fatima (s.a.w) ilivyokuwa, ambapo hakukaa muda mrefu mbora huyu baada ya kifo cha Baba yake (s.a.w) ispokuwa siku tisini na tano (95 tu).

Na siku ya kifo chake (a.s) ilikuwa ni siku ya tatu (3) ya mwezi wa Jamaadul-A'khir (yaani Jamaaduth-thaaniy), mwaka wa kumi na moja (11) baada ya Hijra.na sababu kuu ya kifo chake,ni yale mabaya walimfanyia siku ile wabaya walipoamua kuivamia nyumba yake ambapo Umar alimpiga kwa Mjeredi wake na kumbamiza kwa mlango,kisha Qanfadha aliyelaaniwa,naye akampiga kwa mjeredi wake na kumuumiza kwa amri ya Umar bin Khattaab,ambapo kutokana na masaibu hayo akapata bibi Fatima (a.s) Mimba yake ya Muhsini ikatoka na kuharibika,na akaumwa maradhi makubwa sana kuazia siku hiyo,maradhi ambayo baada ya muda mfupi mno yalipelekea Bi Fatima (a.s) kuiga dunia.Kwa hakika Bi Fatima (a.s) hakumruhusu mtu yeyote yule aliyeshiriki kumfanyia maudhi na kumdhuru aingine tena katika nyumba yake na hakuzungumza nao tena wote kuanzia siku hiyo waliomfanyia ubaya huo mpaka mwisho wa maisha yake ya hapa duniani.

Napenda kuchukua nafasi hii kuwapeni pole waislaam wote ulimwengu wenye kupemnda haki na kupinga batili,wale ambao ni maadui wa dhulma,wenye kuwapenda Ahlul-Bayt (a.s) kama Mwenyeezi Mungu (s.w) alivyotuamrisha tuwapende katika Kitabu chake Kitukufu.Hakika Msiba wa Fatima (a.s) ni msiba unaozigonga nyoyo za Waumini,ni msiba unaowafanya waumini kusikitika.Ni mazito alioyofanyiwa kiasi kwamba Baba yake (s.a.w) laiti angelikuwa hai siku ya tukio basi asingelikuwa radhi na watu hao waofu.Kwa hakika Mwenyeezi Mungu (s.w) ni Mwokozi na Mwenye kuwanusuru wale wenye kuonewa na kudhulumiwa katika Ardhi hii,na ni Mwenye Nguvu na nguvu zake zimeshinda kila kitu.Siku yaja wabaya hao watapata malipo ya mchezo wao mbaya na haramu walioucheza wa kumuua Binti na kipenzi wa mjumbe wake Muhammad (s.a.w).

Tazama: Bihaarul-Anwaar: Juzu ya 43: Ukurasa wa 10: Hadithi ya 1.
Kisha tazama: Dalaailul-Imaama: Ukurasa wa 10.
Tazama:Bihaarul-An-waar:Juzu ya 43:Ukurasa wa 218.
Tazama kisa hiki katika vitabu hivi:
1-Ruuhul-Maaniy:Juzu ya 3.Ukurasa wa 301.
2-Tafsirul-Kabiir:Juzu ya 8.Ukurasa wa 81.
3-Tafsiir Kurtubi:Juzu ya 4 .Ukurasa wa 104.
Tazama hadithi hii katika: Bihaarul-An-waar: Juzu ya 43: Ukurasa wa 23.Hadithi ya 17.
Rejea katika kitabu kiitwacho: Rabiul-Abraal: Cha Zamakhshariy utakuta habari hizi.
Tazama:Al-manaaqib:Juzu ya 3:Ukurasa wa 341.
Tazama:Ilalush-sharaayiu:Juzu ya 1.Ukurasa wa 182.
Kisha Tazama:Bihaarul-An-waar:Ukurasa wa 82.
Suuratuz-zukh-ruf:Aya ya 89.
Suuratuz-zumar:Aya ya 37.
Suuratul-Aa'raf:Aya ya 31.
Suurat Fusw-swilat(Haa Mym):Aya ya 44.
Suurat Aali Imraan:Aya ya 97.
Suuratul-Anbiyaa:Aya ya 8.
Suuratul Baqarah:Aya ya 286.
Suuratul-Anbiyaa:Aya ya 22.
Suuratuz-zukhruf:Aya ya 13.
SuuratuSwaad:Aya ya 26.
Suurat Aali Imraan:Aya ya 144.
Suurat Maryam:Aya ya 12.
Suurat Twaha:Aya ya 11 na 14.
Suuratul-Kahfi:Aya ya 46.
Suuratul-Qasas:Aya ya 26.
Suuratul-Baqarah:Aya ya 261.
Tazama Kisa hiki katika sehemu hii:
Al-manaaqib: Juzu ya 3.Ukurasa wa 343.
* Maasuudiy katika kitabu chake (ITHBAATUL-WASWIYYA) Ukurasa wa 123:Amesema:
Mara wakamvamia (yaani Imam Ali a.s), na wakauchoma moto mlango wake (mlango wa nyumba yake).*Na Sheikh Mufiid katika kitabu chake (AL-IKHTISWAASWU) Ukurasa wa 185 mpaka 186,amesema:
"Baada ya kufika (yaani Umar na watu wake waliokuwa wamebeba kuni wakielekea katika nyumba ya Bi Fatima -a.s-) mlangoni, Umar akaupiga mlango kwa mguu wake na kuuvunja….."


*Ukitaka kupata habari hizi za Kushambuliwa kwa nyumba ya Fatima na kuchomwa moto mlango wa nyumba yake na kumfanyia Binti ya Mtume (s.a.w) kila aina ya Maudhi soma kitabu hiki kiitwacho:
{KITABU SULEIMU BIN QAISI}: Ukurasa wa 83 mapaka ukurasa wa 84.

Kisha soma: {BIHAARUL-ANWAAR}:Juzu ya 28.Ukurasa wa 269.
* Tazama tukio hili katika kitabu hiki kiitwacho:
{AL-IYAASHIY}: Juzu ya 2.Ukurasa wa 67.*Pia tazama :{ BIHAARUL-ANWAAR}: Juzu ya 28: Ukurasa wa 227.
Tazama: Bihaarul-Anwaar: Juzu ya 43.Ukurasa wa 191.
Kisha tazama: Rawdhatul-waaidhiina: Juzu ya 1: Ukurasa wa 151.
Kisha tazama: Awaalimul-Uluumi: Juzu ya 6.Ukurasa wa 274.
Tazama: Bihaarul-Anwaar: Juzu ya 82: Ukurasa wa 27.
Tazama riwaya hii: Bihaarul-Anwaar: Juzu ya 43: Ukurasa wa 218.
Tazama: DALAAILUL-IMAAMA: Ukurasa wa 45.


*Mwandishi ni: Taqee Zacharia.

Anayekukaribisheni nyote katika website hii inayotumia lugha ya Kiswahili Sanifu: