SHAHADA YA SAYYIDAT FATIMA (A.S)

 

SEHEMU YA SITA
KISA KINACHOONYESHA FADHILA ZA FIDH-DHA ALIYEKUWA MHUDUMU WA SAYYIDAT FATIMA (A.S).
Abul Qaasim Al-qash-ariy katika kitabu chake amenukuu kauli hii au kisa hiki kutoka katika kauli za baadhi ya watu wenye kufuatilia fisa na mikasa, ambapo amesema namna hii:
Wamesema baadhi yao;{Kuhusiana na alivyosimulia msimulizi mwenyewe wa kisa hiki}:Nilitengana {au niliachana} na msafara wangu {niliokuwa pamoja nao} kijijini, {Nikiwa kwenye kipando-yaani Farasi} nikakutana na Mwanamke {ambaye naye alikuwa na msafara,lakini msafara huo ukamuacha na hatimaye akapotea njia}, nikamuuliza:

Wewe ni nani? ,Yule Mwanamke akasema:
*وقل سلام فسوف يعلمون*

*Na uwambie maneno ya amani (yaani salam):Hivi karibuni watajua*. Nikamsalimia kisha nikamuuliza:Unafanya nini hapa? Yule Mwanamke akasema:
*من ?هدي الله فلا له من مضلٍّ*

*Na ambaye Mwenyeezi Mungu anamuongoza hakuna awezaye kumpoteza.* Nikamuuliza;wewe ni katika Majini au ni katika wanaadam?

Yule Mwanamke akasema:
*?ا بني آدم خذوا ز?نتکم*

*Enyi Wanaadam! Chukueni pambo lenu* Nikamuuliza,umetokea sehemu gani? Yule Mwanamke akasema:
*?ُنادَونَ مِن مَکانٍ بَع?د*

"Wanaitwa kutoka mahala pa mbali." Nikamuuliza:Unakusudia sehemu gani?

Yule Mwanamke akasema:
*ولله عل? الناسِ حجّ الب?ت*

*Na ni haki ya Mwenyeezi Mungu juu ya watu kuhiji Nyumba hiyo* Nikamuuliza:Nilini umeachana na msafara wako? Yule Mwanamke akasema:
*ولقد خلقنا السماوات والأرض وما ب?نهما في ستة أ?ام*

*Na bila shaka tumeziumba mbingu na Aradhi na vilivyomo kati yake kwa muda wa siku sita* Nikasema:Unahitajia chakula? Yule Mwanamke akasema:
*وَمَا جَعلنَاهُم جَسَداً لا يَأکُُلونَ الطعَام*

*Wala hatukuwafanya miili isiyokula chakula*, Nikampatia chakula (akawa akila chakula ile huku tukiedelea na mwendo).Kisha nikasema:Tembea kwa haraka na ufanye haraka.

Yule mwanamke akasema:
*لا ?ُکلِِّف الله نفساً إلا وُسعَها*
*Mwenyeezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote (katika jambo loloye) ispokuwa lile iliwezalo* Nikamuuliza:Nikupandishe (pia juu ya farasi)? Yule Mwanamke akasema:
*لو کان ف?هما آلهة ٌ إلا الله لفسدتا*

*Lau kama wangelikuwako humo (Mbinguni na Ardhini) waungu wengine ispokuwa Mwenyeezi Mungu,lazima zingeliharibika* Nikashuka na kumpandisha yeye,kisha akasema yule Mwanamke:
*سبحان الذي سَخَّرَ لنا هذا*

*Atukuzwe yeye aliyetutiisha haya* Hapa Mwanamke huyo alikusudia mnyama yule aliyempada kwamba:Kwa uwezo wa Mwenyeezi Mungu (s.w) mnyama yule (na viumbe wengine mfano wake ) kamfanya awe ni mwenye kumtii Mwanaadam,kutokana na hilo Mwenyeezi Mungu (s.w) anastahiki kutukuzwa sana maana yeye ndiye aliyetutiisha haya na lau kama si yeye basi tusingeliweza kutenda haya au tusingeliweza kuwafanya wanyama hao sisi wenyewe wawe ni wenye kututii.Na ndio maana Mwanamke huyo baada ya kupandishwa juu ya kipando kile au farasi yule,alisema kauli hii:

*Atukuzwe yeye aliyetutiisha haya* Baada ya kuufikia Msafara wa Mwanamke huyo,nikamuuliza mwanamke huyo: Kuna mtu yeyote katika msafara huu unayemfahamu? Yule mwanamke akasema:
*?ا داود إنا جعلناک خل?فة في الأرض*
*Ewe Daudi! Hakika (sisi) tumekujaaliya kuwa khalifa katika Ardhi*
*وما محمد إلا رسول*
*Na hakuwa Muhammad ila ni Mtume*
*و?ا ?حي خذ الکتاب*

*Ewe Yahya! Shika Kitabu kwa nguvu*
*?ا موس? إنَّني أنا الله*
*Ewe Musa! Kwa hakika mimi ndiye Mwenyeezi Mungu* (Yule Mwanamke ) Akaita majina haya,mara ghafla nikaona vijana wanne wakimuelekea mwanamke huyo,nikamuuliza (Mwanamke huyo):Hawa ni akina nani kwako?

Yule Mwanamke akajibu:
*المال والبنون ز?نة الح?اة الدنيا*

*Mali na watoto ni pambo la maisha ya dunia* Baada ya vijana wale kumfikia Mama yao,Mama yao (yaani ni Mwanamke yule) akasema:
*?ا أبَتِ استأجِرهُ إن خ?رَ مَنِ استأجرتَ القويُّ الأم?ن*

*Ewe baba!Muajiri hakika mbora uwezaje kumuajiri ni yule mwenye nguvu,mwaminifu* Mara wale vijana wakanipa baadhi ya vitu (ikiwa ni sehemu ya ujira ya kumuongoza njia Mwanamke huyo). Kisha yule Mwanamke akasema (baada ya kuwa nimeisha pokea vitu vile):
*وَ اللهَ ?ضائف لمن ?شاء*

*Na Mwenyeezi Mungu humzidishia amtakae* Vijana (wale) wakaniongezea,kisha nikawauliza vijana wale kuhusiana na mwanamke yule:wakasema: "Huyu ni mama yetu,FIDH-DHA,mtumishi wa Fatimatuz-Zahraa (a.s),hajawahi kuzungumza kwa muda wa miaka ishirini ispokuwa kwa Qur'an tu."

Huyu ndiye alikuwa mtumishi wa Fatima (a.s),ambaye kuzungumza kwake ilikuwa ni Qur'an tupu,swali: Ikiwa Mtumishi anaijua Qur'an namna hii kiasi kwamba kila ukimuuliza swali anakupatia jibu kutoka ndani ya Qur'an Tukufu kwa haraka hakara kama radi vile,je itakuwa kwa Fatima (a.s) kuhusiana na Qur'an Tukufu ambaye ndiye mmiliki wa Mtumishi huyo?

Jawabu lake ni kwamba Fatima (a.s) alikuwa akiijua Qur'an Tukufu kuliko Mtu yeyote yule maana Qur'an hii imeshuka katika Nyumba ya Mtume (s.a.w) na Fatima (a.s) ni mmoja kati ya watu nyumba ya Mtume (s.a.w), hivyo (watu wa Nyumba ya Mtume -s.a.w-) Ahlul Bayt (a.s) ndio wanaoijua Qur'an Tukufu kwa maana ya kuijua, na yeyote anayejikurubisha au anayekaa karibu na Ahlul-bayt (a.s) au anaye bahatika kuipata Elimu ya Ahlul-bayt (a.s),au anayewafuata Ahlul-bayt (a.s) na kujifunza kila kitu kutoka kwao,kwa bara ya watu hawa wema waliotwaharishwa,na waliozama zaidi katika elimu,na wanaolijua jina kubwa la Mwenyeezi Mungu (s.a.w),mtu huyo atakuwa na elimu iliyo sahihi katika kila kitu,mfano mzuri ni FIDH-DHA aliyekuwa mtumishi wa Bi Fatima (a.s).