UTAMBUE UKADIANI

 
UTAMBUE UKADIANI

BISMILLAHIR RAHMANIR RAHIIM
Anti Ahmadiyya Movement in Islam
Jinsi Mirza Ghulam wa Qadiyyan anavyojikanganya
katika maandishi yake
[Na Dk Rashid]
Watukufu waislamu Asalamu Aleykum
Doublethink-Dhana dufu ni mtindo wa kujidanganya kiakili [George Orwel]. Dahan dufu ni dhana inayojengwa kwa ntu kukubaliana na upogotenge na urongo hasa hasa pale unapotumika kama nyenzo ya kupandikizia fikra Fulani [kamusi ya America heritage,toleo la 3]. Mirza Ghulam Qadiyan ndiye muanzilishi wa harakati za dini ya Ahmadiyya.yeye alidai kuwa ni mjumbe mpya wa uislamu na nabii wa Mungu na pia Masih aliyeahidiwa pamoja na madai mengine mengi.Enzi za uhai wake aliandika takriban vitabu 80 ambavyo ndio vitatubainishia wasifu wake. Katika makala haya nitaibainisha mikanganyko katika maandiko yake yeye mwenyewe Mirza Ghulam Qadiyyan hata hivyo kabla ya kufanya ningependa kuwaomba wasomaji msome kwa makini nukuu mbalimbali zifuatazo toka katika vitabu vya Mirza Qadiyyan ambazo ndio zitatusaidia kumtia kitanzi Mirza wa Qadiyyani na kumnyongelea mbali kwa kutumia maandishi yake mwenyewe.


Fatwa ya Mirza juu ya mikanganyiko ya maandiko
Mirza Ghulam Qadiyyani alitoa Fatwa kadhaa kuhusu mtu mwenye kujipinga pinga ya mwenye kujikanganya mirza anaandika 'Maandiko ya mtu mrongo lazima yawe na mikanganyiko[migongano] Tazama zamima Barahiin Ahmadiya sehemu ya 5,Roohan Khazain juz.21uk 275 Mirza anaendelea kuandika "Maandiko ya mtu mkweli na ya mtu mwenye akili timamu hayawi na migongano yoyote naam kama mtu ni punguani na majununi na mnafiki bila shaka maandiko yake yatakuwa na kujikanganya [kujipinga] Tazama sat bachan,Roohan khazain juzu.10uk132 "Mtu yeyote mwenye akili timamu na busara katu hawezi kuwa na imani mbili tofauti' Tazama Roohana Khazain juzu.3uk220 sasa hebu tuangalie mifano ya mikanganyiko katika maandiko ya MirzaMaadili ya Mirza
Mirza anaandika kwa kujitukuza "Mungu ni mmoja ambaye amemtuma Mtume wake,naye ndio mimi mtu muungwana mwenye mwenendo na maadili mema ' Tazama Roohan Khazain juzu.17uk426 "Sijawahi hata siku moja kumjibu mtu kwa lugha ya matusi" tazama Roohan Khazain juz19uk336 kuhusiana na mtu kumlaani mwingine Mirza anaandika "kulaani sio sifa ya SIDDIQ[mtu mkweli]muumini wa kweli hawezi kuvurumisha laana kwa wengine"tazama Roohan khazain juzu.3uk456 nadhani wasomaji mmeona nukuu hizo zilizotanguliaMirza akitoa fatwa kupinga kulaani,matusi nk sasa tazameni Mirza anavyojikanganya kuhusu misimamo hiyo anasema nini na anafanya nini sasa soma nukuu zifuatazo Mirza hapo mwanzo alisema kuwa hajawahi kumjibu mtu kwa kwa lugha ya matusi sasa someni anaandika kwa hamaki na matusi na kulaani akijibu wapinzani wake Mirza anajibu kwa kuandika hivi;


"Enyi makabwela! Mafedhuli!maadui wa Allahna mtume!mmefanya hila ya kiyahudi katika bishara hii ili muujiza huu mkubwa usionekane duniani…urongo wenu umebainika Enyi magalasa nyie…kwa msamiati gani hawa wapumbavu walizielewa maana hizi?Enyi majuha! Vipofu nyie..!msio na haya hasahasa huyu kinara wa madajal Abul Haq Ghaznavi na wafuasi wake Malapa ya Laaana za mungu yakuangukieni mara laki moja ….Enyi madajal Wachafu!utabiri umetimia lakini chuki imekutieni upofu'Tazama Zamima anjam-e-Atham,Roohan khazain juz 11 uk 330 Haya wasomaji mwajionea wenyewe Mirza Ghulam Qadiyyan anaanza kujikanganya katika maandishi mwanzo anadai hajawahi na hawezi kumjibu mtu kwa lugha za matusi hapa mwajionea wenyewe anavyotukana akiendelea zaidi na matusi anaendelea hapa sasa anamjibu kwa matusi mpinzani wake mwingine Hazrat Mehr Ally Shah. Mirza anajibu kwa matusi haya "Bazaz,Fedhuli,…Nge! Laana ya mungu ikushukie ,wewe umelaanika kwa sababu ya mtu aliyelaanika' tazama Roohan Khazain Juzu.18 mirza anaendelea na matusi zaidi sasa hapa anatukana waisalmu wasiokubali utume wake anasema "Maadui [yaani waislamu] wamekuwa kama nguruwe pori kwenye mbuga na wanawake wao wamekuwa wachafu kuliko Malaya" Tazama Roohan Khazain Juzu.14 uk 53 Juu ya mpinzani wake Maulvi Saadullah Ludhianvi. Mirza kaandika kwa kumtukana Hivi "kinyamkela,fisadi,Ibilisi,kizazi cha laana cha mtu muovu,fedhuli,fatani na toto Nuksi la Malaya" Tazama Roohan Khazain Roohan khazain Juzu.14uk53
Baada ya Mirza kuwamiminia wapinzani wasiomkubali laana na matusi mazito sasa jikumbushe soma tena maneno haya ya Mirza "Mimi sijawahi hata siku moja kumjibu mtu yeyote kwa lugha ya matusi"Roohan Khazain Juzu.19uk.236 "Mungu ni mmoja ambaye amemtuma Mtume wake ambaye ni mimi mtu muungwana ,mwenye khulka na tabia njema" Roohan KhazainJuz17 uk426 "kulaani laani sio sifa yaSIDIQ[mtu mkweli]muumini havurumishi matusi Tazama Roohan Khazain Juz3 uk 456 Haya wasomaji sisi hatuna mengi mmeona wenyewe Mirza navyojikanganya huku anasema hivi kule anasema vile mara yeyehajawahi kujibu kwa matusi lakini mmeona anajibu watu kwa matusi mara anasema kulaani sio vizuri mara yeye mwenyewe Mirza anageuka na kulaani.Mirza Ghulam-ukweli dhidi ya urongo
Tukiendelea zaidi na uchambuzi wetu juu ya kujikanganya Mirza Ghulam Qadiyyan katika maandishi yake tazameni tena anavyojipinga yeye mwenyewe hapa anasema hana mwalimu! Anasema "Mahd si mwanafunzi wa mtu yeyote yule Naapa kuwa huu ndio wasifu wangu hasa.hakuna mtu yeyote anayeweza kuthibitisha kuwa kuna mtu Fulani ambaye amenifundisha mimi Qur 'an" Tazama Roohan Khazain Juz 14 uk.394 wasomaji mmeona hapo Mirza Ghulam Qadiyyan anadai hajapata kuwa na mwalimu aliyemfundisha Qur'an sasa soma hapa anajikanganya anataja walimu wake waliomfunza Qur'an Mirza anasema "Nilipotimiza umri wa miaka 10 mwalimu mmoja wa kiarabu akateuliwa kunifundisha jina lake fazal Ahmed … na nilipokuwa na umri wa miaka 17-18nikafundishwa na mwalimu mwingine[Moulvi saheb] ambaye jinalake ni Gul Ally Shah huyu aliajiriwa na Baba yangu kwa kazi ya kunifundisha Kule Qadiyyan Tazama Roohan Khazain Juzu.13uk180 Mirza anaendelea kukiri kuwa anao walimu waliomfundisha anasema,; "Nilipokuwa mtoto wa miaka 6-7 mwalimu wa kiajemi aliajiriwa kunifundisha Qur'an tukufu….jina la mwalimu huyo ni Fazal Illah" Tazama Roohan Khazain Juz 13 uk 180Mirza asema yeye sio Nabii
Akiendelea kujikanganya sasa hapa anadai yeye sio Nabii Mirza anasema "Hivi inawezekanaje mimi nidai unabii na nitoke katika uislamu na kujiunga na chama cha makafiri " Tazama Humamatul Bushra,Roohan Khazain juz27 uk297 Mirza anaendelea kusema "Enyi watu msiwe wapinzani wa qur'an na baada ya kukoma kwa unabii[khatamun nabiyyin]msianzishe silsila nyingine na wahyi wa kinabii"Tazama Asmani Faisla,Roohan Khazain Juzu.4uk335 "Je huyo mzushi mwovu anaedai kuwa yeye ni nabii na Mtume anaamini kweli Qur 'an, na mtu mwenye kuamini Qur an na kuamini aya isemayo walakin Rasulullah wakhataman Nabiyyin kuwa ni maneno ya allah anawezaje kusema mimi pia ni mtume na nabii baada ya Nabii[s.a.w]" Tazama Anjane ,Athan,Roohan Khazain juzu.11uk297 "Mimi simdai wa unabii wala sikanushi miujiza ,malaika,usiku wenye cheo na baada ya sayidna na muhamad[s'a'w] namuhesanu mtu yeyote anayedai unabii na utume kuwa ni mrongo na kafiri"Tazama Tabligh Risalatjuzu.2uk.22 collection of Advertisements Juzu 1uk 230 wasomaji nadhani mmeona hapo mirza anakataa yeye hawezi kudai unabii na pia anamuhesabu atakayedai unabii kuwa ni kafiri na adui mkubwa. Sasa soma tena maneno yake anajikanganya tena na kudai eti yeye ni nabii Mirza Qadiyyan anasema " Naapa kwa yule ambaye mikono mwake upo uhai wangu yeye amenituma mimi ameniita mimi nabii na amenitaja mimi kama ndiye masih aliyeahidiwa'Tazama Haqiqatulwahyi,Roohan Khazain Juzu.2uk503"Mungu wa kweli ni yule aliyemtuma Nabii wake kule Qadiyyan"Tazama Dafal bala uk 11Roohan Khazain Juzu 18 uk 231 Tukiendelea zaidi na uchambuzi wetu kuhusu kujikanganya kwa Mirza wa Qadiyyan Hapa sasa mirza anakataa yeye sio Masih aliyeahidiwa Mirza GhulamQadiyyan anasema "Kamwe sijawahi kudai kuwa mimi niMasih aliyeahidiwa Issa BinMariyyam na yule anayenizushia jambo hilo huyo ni muongo na mzushi kabisa kabisa" Tazama Izala -E-Auham,Roohan Khazain Juzu.3uk192 "Mtu huyu muungwana yeye amejiita masiil masihi ambapo majitu majinga yakafikiri eti ni msihi aliyeahidiwa"Tazama Roohan KhazainJuzu.3uk192 watukufu wasomaji mmeoana hapo Mirza Ghulam Qadiyyan anakataa kuwa yeye sio masih aliyeahidiwa sasa tazamezi anajikanganya tena sasa anasema yeye kuwa ndio masih aliyeahidiwa Mirza anasema "Natangaza kuwa mimi ndiye masih mwenyewe aliyeahidiwa ambaye vitabu vyote vitukufu vimebashiri kuwa atatokea katika siku za mwisho" Tazama RohanKhazain juzu.17 uk 295"Naapa kwa yule mungu ambaye kutunga urongo juu yake ni kazi ya wale waliolaaniwa yeye amenituma mimi kama masih aliyeahidiwa" Tazama Collection of Advertisiment of mirza ghulam juzu 3 uk 435 Mirza alalama haelewi lugha ya ufunuo tukiendendelea zaidi na uchambuzi wetu kuhusu Mirza Ghulam Qadiyyan sasa wasomaji tazameni huyu Mirza anajiita Mtume na kuwa anapata ufunuo toka kwa mungu lakini sasa analalama kuwa ufunuo huo anaoshushiwa haulewi kwa kuwa unakuja katika lugha asiyoijua yaani inashangaza tangu lini mungu anatuma Mtume alafu anamshushia wahyi katika lugha asiyoijua Mirza alalama anasema "Huu ni uchwara mtupu ni jambo lisilo na mantiki kabisa kwamba lugh asili aya mtu ni nyingine na ufunuo unashushwa kwa lugha nyingine ambayo hawezi kuielewa hata kidogo kwa sababu kuna utata mwingi ndani yake na ni nini basi manufaa ya wahyi huo ambao uko nje ya ufahamu wa mwanadamu" Tazama chashma -e-ma'arifa uk 209 Roohan khazain juzu.23uk218 Mirza aendelea kulalama kuhusu kutoelewawahyi anaoshushiwa Anasema


"Hili ni jambo la ajabu kabisa kwamba aya zinazoshushwa kwangu katika lugha ambazo mimi sizielewi kabisaa!!!kama vile kiingereza,kisanskrit,kiebrania n.k"Tazama Nuzuul- el-masih uk 57Roohan Khazain juzu.18uk435 'Tokea wiki hii ianze maneno kadhaa wa kadha yamefunuliwa kwangu kwa lugha ya kiingereza na kadhalika na japo kuwa baadhi yake yametafsiriwa na kijana wa kihindu lakini hiyo haotohi na baadhi ya aya zilitafsiriwa kwa na Mungu katika lugha na baadhiya maneno yapo katika lugha ya kiibrania yote hayo lazima yatafitiwena kupambanuliwa.... ebu jaribuni kupata ufafanuzi wake haraka iwezekanavyo nitaarifuni kwa mwandiko mzuri unaosomeka kirahisi"rejea barua ya Mirza Ghulam kwa Mir Abbas Shah,maktabat-e-Ahmadiyya ,collection of letters of Mirza Ghulam juzu.1uk68 subhanallah !jamani waislamu vioja hivi yaani mtu aliyeteuliwa na mungu haelewi lugha anayoshushiwa na mungu yaani mungu anamshushia aya nabii wake katika lugha asizoelewa mpaka analazimika kutafuata msaada toka kwa vijana wa kihindu!!! Mir Abbas Saheb alikuwa ni muridi wa kwanza wa Mirza Ghulam Qadiyyan baada ya kuona ubabaishaji wa anama hii toka kwa kiongozim wake Mirza hatimaye akamkana Mirza na kuingia katika uislamu kwa maelezo zaidi kumuhusu huyu bwana alivyomkana Mirza soma habari hii katika Kwa kumalizia nakukumbusha tena soma tena maneno haya ya Mirza ili umuhukumu vizuri "maandiko ya mtu mrongo lazima yatakuwa na mapingano'Zamima Braheen ahmadiyya sehemu ya 5,RoohanKhazain juzu.21uk275"Maandiko ya mtu mkweli mwenye akili timamu katu hayawezi kuwa na migongano naam kama mtu punguani na majununi au ni manafiki ambaye ni mtu wa kukubali tu mambo kwa lengo lwa kuvikwa kilemba cha ukoka maandiko yake bila shaka yatagongana gongana 'Rejea Sat Bachan Roohan khazain juzu.10uk132 'Mtu yeyote mwenye busara hawezi kuwa na imani mbili tofauti"Rejea Rohan khazainjuzu 3 uk 220


HITIMISHO
Tunawaomba wasomaji wenyewe mchukue fursa hiyo kumuhukumu Mirza Ghulam alikuwa ni punguani?,murongo?,mwendawazimu?au kikaragosi sisi tumetaja vit6abu ambamo mikanganyiko hiyo imo tumetaja ukurasa na jalada lake kama kuna kadiyyani yeyote mwenye kutaka kujua haki basi fursa ndio hiyo akarejee vitabu hivyo ajionee mwenyewe mikanganyiko ya Mirza wala asikalie ushabiki bali kama ana nia njema ya kutafuta kujua haki iko wapi tunaomba kwa moyo mkunjufu Makadiyyani wakasome vitabu hivyo tulivyorea InshaAllah ataiona haki na kurejea katika uislamu Amani iwe juu ya yule anayefuata uongofu Dk syed Rashid Ali P.O.Box 1156 Dibba Al-Fujaira United Arab Emirates rasyed@emirates.net.ae http://alhafeez.org/rashid/


Bismillah Al-Rehman Al-Raheem
Anti Ahmadiyya Movement in Islam
Safari yangu ya kutoka kwenye Urongo kwenda kwenye ukweli halisi.
Kwanza kabisa ningependa kujielezea kwa kifupi. Mimi ni msichana niliyezaliwa katika jamii ya Ahmadiyya, asili yangu ni Mpakistan, nimekulia Mashariki ya kati. Nilirejea katika Uislamu takriban miaka mitatu iliyopita. Ni hivi karibuni tu nimefunga ndowa. Namna mimi mwenyewe ninavyoutazama Uhmadiyya, nasema kamwe sikuwa Ahmaddiyya. Hebu sasa nielezee zaidi. Mara yangu ya kwanza kabisa kuujuwa Uhmadiyya ilikuwa pale nilipokuwa na umri wa miaka kumi. Wakati huo nilikuwa na kawaida ya kupitisha mapumziko ya kiangazi nyumbani kwa nyanya yangu. Huko nikawa nasoma vitabu fulani vya utenzi ambapo naukumbuka utenzi mmoja usemao, "Mariam Meray Zanoon Main, papo hapo mimi nikaona kuwa huu ni uongo. Heshima na hadhi ya Bi Mariam iko juu na haiwezi kutumika katika ubeti kama huo. Aidha nakumbuka, baada ya kuhudhuriya Muhadhara wa Ahmadiyya, binamu yangu mmoja aliwahi kusema kuwa Majini maana yake ni watu "watokeao mlimani." Naye Baba yangu akazungumza na binamu huyo juu ya jambo hilo, mimi hilo halikuniingia kabisa.Vile vile nakumbuka Baba alikuwa akisema kuwa Vitabu vya Mirza Ghulam Ahmadi vinatumia lugha ya matusi. Basi masiku yakaenda nami nikahitimu masomo. Kwa vile sisi hatukuwa ndani ya wigo wa jamii ya Ahmaddiyya, hatukuwa na uhusiano nao mkubwa. Hii ndiyo maana ya mii kusema kuwa kamwe sikuwa Ahmadiyya na wala sikuwa hata na ile itikadi ya kupandikizwa. Kuna vipindi vitatu ambao uhitaji dini, pale mtu anapozaliwa, anapoolewa na anapokufa. Wakati wa kutafuta mchumba wa kufaa ndio wakati ambapo familia nyingi za Ahmadiyya uhudhuria sala za Ijumaa au mikutano mingine katika vituo vilivyo karibu nao. Ni sababu hiyo hiyo iliyoifanya familiya yetu ijinasibishe na jamii ya Ahmadiyya. Kilichoitanza akili yangu ni kile kiapo wanachokula ambacho kinasema kuwa "Ukimshuhudia Allah kuwa shahidi, basi hapo kuna tamka kutumia uhai na mali zao kwaajili ya kuitumikia Jumuiya ya Ahmmadiyya. Kamwe mimi nisengeliweza kula kiapo hicho kwani naamini kuwa katika kiapo chochote cha kumshuhudisha Allah kama shahidi, ni heri wewe mwenyewe ukinuwiye.Mimi nikawa nasimama tu na kuinamisha uso chini bila kuapa. Likatokea jambo jingine lililotanza fikra zangu. Ahmadiyya kwa ujumla wao hawajitangazi kuwa wao ni Ahmadiyya na hata katika Pasipoti hawaandikishwi kwa jina hilo. Pale Baba yangu alipofanya mazungumzo na mwenzangu mmoja juu ya vitabu vya Ahmadiyya, alikitaja kitabu kimoja kiitwacho, Truth, Revelation $ Reality kilichoandikwa na Tahir Ahmadi. Kesho yake mwenzangu huyo akawaambia Wapakstan wenzetu kuwa mimi ni Ahmadiyya, na nilipokabiliwa, nikakataa. Hiyo ilkuwa ni mara ya kwanza katika maisha yangu ambapo nilijihisi niko hatiani na dhambini, unaingia hatiani kwa kosa lisilokuwa lako. Baadaye nilipoanza kutafakari mambo hayo, nikatanabahi kuwa kumbe hatupaswi kurithi dhambi za wazee wetu waliotangulia na kukirithisha kizazi kijacho. Iwapo Uhamadiyya ni ukweli basi mimi napaswa kusimama kidete kuuteteya na napaswa niuonee fahari, lakini kama si ukweli basi niachane nao kabisa, nisijibebeshe tena dhambi hiyo katika maisha yangu yaliyosalia.Ndipo nikakutana na Mirza Tahiri Ahamadi mjini London. Kwa vile wazazi wangu walimueleza kuwa mimi nilikuwa bado sijaolewa yeye alipendekeza wachumba kadhaa. Alinisifu kwa kuniambia kuwa mimi ni mrembo. Sina budi kukiri kuwa kweli nilivimba kichwa. Baadaye nilipotafakari na kukutana na viongozi wengine wa Dini, niliona kuwa wao hushusha macho ya chini wanapozungumza na wanawake na hawaghafiliki kuthubutu kutamka maneno kama hayo. Basi ukafika wakati wa kufanya uchaguzi wa wachumba. Kulikuwa na mchumba mmoja kutoka Suni. Kwa dhati mimi nikamwambia Mama, kwanini mtu huyo asifikiriwe, yeye akaniambia kuwa sisi haturuhusiwi kuoana na mtu yeyote asiyekuwa Ahmadiyya. Na Yule anayefanya hivyo basi familiya yake yote hutengwa na jamii ya Ahmadiyya. Familiya hiyo huenguliwa Hazoor (Neno lenye maana ya viongozi. Mimi jambo hilo likanishangaza kwani Allah hamtowi yeyote yule katika jamii yake. Hapo ndipo mimi nilipochanganyikiwa. Nilipoanza kuyatafakari mambo yaliyonitatiza kichwani na kuanza kutafuta majibu: Nilijadiliana na mwenzangu mmoja juu ya mambo haya naye akanishauri kwamba niamuwe niwe nani kisha ndiyo nifikiriye kuolewa, kwani vinginevyo kutakuwa na tathira mbaya.


Kwa kweli ushauri huu ulinigusa sana na kwa mara ya kwanza sasa katika maisha yangu yote, nikaanza kuusoma Uahmadiyya. Nilisoma tovuti zilizopinga uahmadiyya, nikasoma tovuti zilizounga mkono uhamdiyya. Nikajadiliana na wenzangu ambao niliona wanajuwa mengi kuhusu Uislamu. Jambo la mwisho kabisa ambalo lilinileta katika Imani ya kweli, ilikuwa pale nilipopata vitabu halisi vilivyoandikwa na Mirza Ghulam Ahmadi katika lugha ya kihudu. Mimi naamini kabisa kuwa Ahmadiyya yeyote yule anayesoma vitabu hivyo sambamba na kusoma Qur'an, huku akiwa ameiweka huru akili yake ataachana kabisa na Ahmadiyya. Kuna mambo machache ambayo ni muhimu kuyataja, kama vile Mirza anavyojielezea kuwa yeye aligeuka kuwa Nabii Issa (Yesu)! Anaeleza katika kitabu chake kuwa, kwanza yeye alikuwa Bi Maryam, kisha akawa mjamzito kwa kipindi cha chini ya mwaka mmoja, kisha ndipo Yesu akazaliwa. Huu ni mzaha mtupu wa kuchezea aya ya Allah! Hitimisho langu juu ya kwanini Mirza Ghulam Ahmadi aliamuwa kupinga muujiza wowote uliotajwa katika Qur'an ni kwasababu yeye hakuweza kufanya muujiza wowote. Kwavile yeye hakuweza kufanya muujiza wowote ndio maana akakanusha miujiza yote ile iliyotokeya kwa uweza wa Allah (s.w). Hivyo pale mtu anapo thibitikiwa na ukweli, kuna njia mbili za kufuata, ama abakiye kuwa Ahmadiyya kwaajili ya kuwafurahisha watu au aachane kabisa na Ahmadiyya. Mtandao wa kijamii wa Ahamdiyya una nguvu sana na humfanya mtu aone vigumu kujitowa.

Mimi niliamini watu wanaweza kuwa na mitandao katika maisha yao, yawezekana ni kutokana na taaluma yako, yawezekana ni kutokana na tabiya zako au kwaajili ya maslahi. Msimamo wowote wa maisha ya mtu huwezekana iwapo tu utamuamini Mwenyezi Mungu. Nilisoma aya moja katika Qur'an ambayo inasema kuwa kama ukiona dhihaki inafanywa juu ya aya ya Mwenyezi Mungu basi usikae pamoja nao vinginevyo nawe utakuwa kama wao. Mimi naamini kuwa Ahmadiyya wanatumia hoja ya ujanja ujanja kuthibitisha Imani yao na ili kufanya hivyo, wachezee aya za Mwenyezi Mungu. Kwahiyo mimi nikaamuwa kutohudhuria Jalsa Salana ya Ahmadiyya. Hapo nikaelewa kwanini Ahmadiyya wanahesabiwa kuwa wako nje ya wigo wa Uislamu.Nikazungumza na maalim mmoja iwapo baada ya kuwa nimeachana na Ahmadiyya, je ningeweza kuolewa na Ahmadiyya, naye akanieleza kuwa hilo haliruhusiwi. Basi hatimaye ulipofika wakati, nikaamuwa kuolewa na Muislamu wa Sunni, nikakabiliwa na hatuwa ya kususwa kabisa na Ahmadiyya. Wazazi wangu walihudhuriya Arusi yangu lakini ndugu zangu hawakuhudhuriya. Yafaa hapa niitaje hatuwa ya mchumba wa dada yangu ambaye alitishiya kuvunja uchumba naye iwapo angehudhuriya harusi yangu kwani hilo lingemaanisha kuwa Dada yangu naye piya si Ahmadiyya na kwasababu hiyo yeye asingeweza kumuowa.Kwa kuwakosa ndugu zangu katika harusi yangu iliniuma kweli kweli. Upuuzi mwingine wa kutajwa hapa ni kuwa Baba yangu alimuuliza kaka yangu kuwa sheria inasemaje, Kaka yangu akajibu, "Iwapo Ahmadiyya anaolewa na mtu asiyekuwa Ahmdaiyya basi nyiye hamtakiwi kuhudhuriya harusi ya wa tu hao." Baba yangu akajibu kuwa sheria hiyo haifanyi kazi hapa kwani yeye (Dada yako) amekwishatangaza kuwa yeye si Ahmadiyya, kwahiyo hii ni harusi ya watu wawili wasiokuwa Ahmadiyya ambayo wewe unaweza kuhudhuriya. Kwa kauli hiyo kaka yangu akasema iwapo mtoto wa kiume ndiye anayeoa basi kuna fursa ya kuongeza idadi ya Ahamdiyya hivyo unaweza kuhudhuriya harusi yake, lakini kwa msichana ndiye anayeolewa haiwi hivyo. Basi ndugu zangu, na hao wanaoitwa wanajamii wenzangu wa Ahmadiyya na wengineo wote wakanisusa.Kwakweli mimi nawasikitikia wao kwa dhambi yao, kwani wanaamini kama wangehudhuriya harusi hiyo kiongozi wao angewatenga. Jamaa zangu wa Sunni walinisaidiya kikamilifu na wote walikuwepo kwaajili yangu. Mwisho namuomba Allah. Authubutishe msimamo wangu juu ya Uislamu na awaoneshe ukweli kuhusu Mirza Gulam wale Ahmadiyya waliopotea waukane Uahmadiya ili na wao waukatae uongo huu wa Mirza Ghulam Qadiyyan. Amiin Mwanamke aliyerejea katika Uislam Nitaandika makala yenye maelezo ya kina hivi karibuni.