WAULIZE WANAOFAHAMU

 
Kauli ya Ahlu-dhikri kuhusu Mtume (s.a.w.).
Imam Ali (a.s.) anasema: "Mpaka karama za Mwenyezi Mungu zikamfikia Muhammad (s.a.w.), akamtoa kutoka kwenye maoteo yenye asili bora, na mahala penye mapandio yenye nasaba tukufu, (akamtoa) kutoka katika mti ambao Mitume wake wametokana nao, na kutokana na mti huo (Mwenyezi Mungu) ameteua wawakilishi wake, kizazi cha Mtume ndiyo bora kuliko vizazi vyote, na ukoo wake ndiyo bora kuliko koo zote, na mti wake ndiyo bora kuliko miti yote, umeota mahala patakatifu na ukachanua mahala pema, una matawi marefu na matunda yasiyodhurika kwa chochote kile. Basi yeye Mtume ndiyo kiongozi wa yeyote anayemcha Mungu, naye ndiye jicho la mwenye kuongoka, ni taa ing'arayo mwanga wake na ni miali ambayo nuru yake imechomoza, yeye ni mwenge ambao mng'ao wake ni wenye kumeta, mwendo wake ni wenye msimamo na Sunna yake ni uongofu, maneno yake ndiyo upambanuzi na hukumu yake ni yenye uadilifu. Mwenyezi Mungu alimtuma akiwa ni miongoni mwa Mitume katika muda muafaka kwani ulikuwa ni wakati wa upotofu na matendo ya kijinga miongoni mwa watu. Mtume akatoa nasaha kikamilifu, akapita katika njia (ya haki) na akalingania (watu) kwa hekima na mawaidha mazuri ... Makazi yake ni makazi bora na chimbuko lake ni chimbuko tukufu lililomo ndani ya asili bora na makazi ya amani. Kwa hakika nyoyo za (watu) wema zimegeuziwa upande wake na macho yamemwelekea. Kwa sababu yake Mtume, chuki baina ya watu zimezimwa na uadui nao umeangamizwa, na kwa ajili yake udugu (Kiislamu) umeunganika na ukabomolewa uhusiano (na kufru). Kupitia kwa Mtume mnyonge ameheshimika na amedhalilishwa mwenye kiburi, maneno yake ndiyo ubainifu na ukimya wake ni usemi (tosha). (Mwenyezi Mungu) amemtuma kwa hoja zilizokamilika, na mawaidha yenye kuponya, na wito ulio mzuri, kwa Mtume amezidhihirisha sheria zilizokuwa zimesahaulika na kwake yeye amekemea uzushi uliokuwa umeingizwa (katika dini) na kwake akazibainisha hukumu kwa ufafanuzi. Alimtuma pamoja na mwangaza, na akamtanguliza kwa kumtukuza kwake yeye Mtume, akaondosha maovu na akawashinda wenye kuipinga haki, na akayawepesisha yaliyo mazito na akazidhalilisha itikadi mbaya mpaka akautenga mbali upotovu kutokana na njia ya haki.MLANGO WA TATU
YANAYOWAHUSU WATU WA NYUMBA YA MTUME (S.A.W.W.)
Swali la Tatu: Ahlul-Bait (Watu wa Nyumba ya Mtume) ni kina nani? Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: (Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu enyi (watu) wa nyumba (ya Mtume) (Qar'an, 33:33). Ahlu-Sunna Wal-Jamaa, wanasema kwamba aya hii ilishuka kwa ajili ya wake za Mtume (s.a.w.w.), na wanatolea ushahidi wa madai hayo kulingana na mfumo wa aya zilizo itangulia aya hii na zinazoifuatia. Kwa mujibu wa madai yao ni kwamba Mwenyezi Mungu amewaondolea uchafu wakeze Mtume na amewatakasa kikamilifu. Na miongoni mwa hao Ahli-Sunnah wapo wanaowaongeza juu ya wakeze Mtume (s.a.w.w) Imam Ali, Fatma, Hassan na Husein (a.s.). Lakini ukweli ulivyo na kama ulivyonukuliwa, kadhalika akili na historia vinaikataa tafsiri hii, kwani Ahlu-Sunnah haohao wanazo riwaya ndani ya vitabu vyao (zisemazo) kwamba aya hii ilishuka kuwahusu watu watano tu nao ni: Mtume Muhammad (s.a.w.w.), Ali, Fatma, Hasan na Husein (a.s.), na kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) ndiye aliyewahusisha hao na nafsi yake tukufu kwenye aya hii pale alipomuingiza Ali, Fatma, Hasan na Hussein pamoja na yeye mwenyewe ndani ya kisaa (shuka) na akasema: "Ewe Mwenyezi Mungu hawa ndiyo watu wangu basi waondolee uchafu na uwatakase kikamilifu." (Tafsiri) hiyo wameiandika wanachuoni wengi wa Kisunni, mimi nitawataja baadhi yao tu: 1) Muslim ndani ya Sahihi yake katika mlango waFadhail-Ahlil-Bait Juz. ya 2 uk. 368.
2) At-Tirmidhi ndani ya Sahih yake Juzuu ya 5 uk. 30.
3) Musnadul-Imam Ahmad ibn Hanbal Juzuu 1 uk. 330.
4) Mustad-rak-Al-Hakim Juzuu 3 uk. 123.
5) Khasaisul-Imamin-Nasai uk. 49.
6) Tal-Khisud-dhahabi Juzuu 2 uk. 150.
7) Mu'ujamut-Tabrani Juzuu 1 uk. 65.
8) Shawahidut-Tanzil ya Al-Hakimul-Haskani Juz.2 uk.ll
9) Bukhari ndani ya Tarikhul-Kabir Juz. 1 uk. 69
10) Al-Isabah ya ibn Hajar Al-Asqalani Juzuu 2 uk. 502.
11) Tadh-Kiratul-Khawas ya ibn Al-jauzi uk. 233.
12) Tafsirul-Fakhrir-Razi Juz. 2 uk. 700.
13) Yanabiul-Mawaddah ya Al-Qanduzi Al-Hanafi
uk. 107.
14) Manaqibul-Khawar-Zami uk. 23.
15) As-siratul-Halabiyyah Juz.3 uk. 213.
16) As-siratud-dah-laniyyah Juz. 3 uk. 329.
17) Usudul-ghabah ya ibnul-Athir Juz. 2 uk. 12. jl8) Tafsirut-Tabari Juz. 22 uk.6.
19) Ad-durul-Manthur ya Suyuti Juz. 5 uk. 198.
20) Tarikhu ibn A'sakir Juz. 1 uk. 185.
21) Tafsirul-Kashaf ya Az-Zamakhshari Juz. 1 uk.193
22) Ah-kamul-Qur'an ya ibn Arabi Juz. 2 uk. 166.
23) Tafsirul-qur-Tubi Juz. 14 uk. 182.
24) As-sawaiqul-Muhriqah ya ibn Hajar uk. 85.
25) Al-Istiiabu ya ibn Abdibarri Juz. 3 uk. 37.
26)Al-Iqdul-Farid ya ibn Abd rabih Juz. 4 uk. 311.
27) Muntakhabu Kanzil-Ummal Juz. 5 uk. 96.
28)Masabihus-Sunnah ya Al-baghwi Juz. 2 uk. 278.
29)As-babun-nuzul ya Al-wahidi uk. 203.
30)Tafsiru ibn Kathir Juz. 3 uk. 483.

Wako wengine wasiokuwa hawa miongoni mwa wanachuoni wa Ahlul-sunnah Wal-jamaa, wengi tu hatukuwataja lakini tumetosheka na idadi hii. Sasa basi ikiwa wanachuoni wote hawa wanakiri kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu ndiye aliyebainisha makusudio ya aya hii, je zina nafasi gani kauli za wengine wasiokuwa Mtume miongoni mwa Masahaba na Tabiina au wafasiri ambao wanataka kuipeleka maana ya aya hiyo kinyume na vile atakavyo Mwenyezi Mungu na Mtume wake eti kwa lengo la kutaka kumridhisha Muawiyah na kutumainia (mali) aliyonayo? Kama ambavyo Mtume (s.a.w.w.) amepata kuwaashiria watu nyumba yake kwa mara nyingine na akawahusisha kwamba wao ndio Ahlul-bait na siyo wengine wasiokuwa wao, napo ni pale iliposhuka kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu isemayo: "Basi waambie njooni tuwaite wanetu na wanenu, na wanawake wetu na wanawake wenu na sisi wenyewe na ninyi wenyewe, kisha tuapizane na tuombe laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo" (Qur'an, 3:61). Bwana Mtume alimwita Ali, Fatma, Hassan na Husein na akasema "Hawa ndiyo wanetu na sisi wenyewe na wanawake wetu, basi njooni ninyi wenyewe na wanenu na wanawake zenu." Na katika riwaya ya Muslim amesema, "Ewe Mwenyezi Mungu hawa ndiyo watu wangu.'[34] Na wale wanachuoni wa Ahli-Sunna Wal-Jamaa ambao nimewataja katika rejea zilizotangulia vile vile wote wanakiri kuwa aya hii (Qur'an, 3:61) ilishuka kuwahusu watu watano hawa waliotajwa, rehma na amani za Mwenyezi Mungu ziwashukie wote. Ifahamike kwamba, wakeze Mtume (s.a.w.w.) waliyafahamu makusudio ya aya hiyo tukufu, (Qur'an, 33:33). Na ndiyo maana hakuna mmoja wao aliyedai kwamba yeye ni miongoni mwa Ahlul-Bayt (a.s.) na hasa hasa wakitanguliwa na Ummu Salamah na mwana Aisha, kwani kila mmoja wao (wawili hawa) ameleta riwaya (isemayo) kwamba aya hii inamuhusu Mtume wa Mwenyezi Mungu, Ali, Fatma, Hassan na Husein (a.s.), na wameandika juu ya kukiri kwa wake za Mtume kuhusu aya hiyo, Muslim, Tir-midhi, Al-Hakim, Tabari, Suyuti na Ibnul- Athir na wengineo.Zaidi ya yote hayo ni kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) aliondoa utatanishi na mush-keli huu, kwani yeye alifahamu kwamba Waislamu wataisoma Qur'an na kuwafahamu Ahlul-Bait kutokana na mtiririko wa aya zilizotangulia na zinazofuatia ambazo zinawaonya wake wa Mtume, hivyo akawahi kuufundisha umma (wake) makusudio ya aya ya kuwaondolea uchafu na kuwatakasa (watu wa nyumba ya Mtume) pale alipodumu kwa mfululizo wa muda wa miezi sita (baada ya kushuka aya hii) kwa kupita kwenye mlango wa (nyumba ya) Ali, Fatma, Hasan na Hussein kabla ya kuanza kusali kwa kusema: (Bila shaka Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu enyi watu wa nyumba ya Mtume na kukutakaseni sana sana, basi amkeni mkasali Mwenyezi Mungu akurehemuni. Suala la Bwana Mtume kuwahi kuufundisha umma wake ni jambo aliloliandika Tir-midhi katika Sahih yake Juz. 5 uk. 31, Al-hakim katika Mustad-rak Juz. 3 uk. 158, Ad-dhahabi ndani ya Tal-khisi yake, Ahmad ibn Hanbal ndani ya Musnad yake Juz. 3 uk. 259, Ibnul-athir ndani ya Usudul-ghabah Juz. 5 uk. 521 na Al-Has-Kani katika Shawahidut-tanzil Juz. 2 uk. 11, As-suyutti ndani ya Ad-durul-manthur Juz. 5. uk. 199, Tabari katika tafsiri yake Juz. 22 uk. 6, Al-baladhuri ndani ya Ansabul-Ash-raf Juz. 2 uk. 104, ibn Kathir katika tafsiri yake Juz. 3 uk. 483 na Haithami katika Majmauz- zawaid Juz. 9 uk. 168 na wengineo.Zaidi ya hawa wanachuoni wa Kisunni tukiwaongeza Maimamu wa nyumba ya Mtume na wanachuoni wa Kishia ambao hawana shaka juu ya kuhusika kwa Mtume, Ali, Fatma Hassan na Husein katika aya hii tukufu, basi hakuna nafasi yoyote ya kujitetea watakayokuwa nayo wapinzani miongoni mwa maadui wa Ahlul-Bait na wafuasi wa Muawiyah na Banu Umayyah ambao wanataka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa kutumia vinywa vyao na Mwenyezi Mungu (bila shaka) ataitimiza nuru yake (ing'ae) japokuwa makafiri watachukia. Kwa hakika wamedhihirisha wazi hao wanaofasiri aya hizo kinyume cha tafsiri ya Mtume (s.a.w.w.) kwamba, wao ni miongoni mwa wanaojipendekeza kwa watawala wa Banu Umayyah na Bani Abbas hapo zamani mpaka sasa, kwani (wafasiri) hao ni miongoni mwa watu wenye chuki ambao hawampendi Ali japo watajificha kwa mavazi ya Uanachuoni na Ufaqihi. Tunasema hivi kwa sababu akili peke yake tu inatosha kupata uamuzi wa kutokuwaingiza katika aya hii yaani (kuondolewa uchafu na kuwatakasa) wakeze Mtume (s.a.w.w.).1) Kwa mfano tukimchukua Ummul-Muuminina Aisha ambaye yeye anadai kuwa ni kipenzi mno kwa Mtume kuliko wakeze wengine na ni wa karibu mno kwa Mtume kiasi kwamba wake wengine wa Mtume walimuonea wivu na wakamtumia ujumbe (Mtume) wa kumtaka awe muadilifu kwa sababu ya binti Abi Quhafah, kama tulivyotangulia (kueleza) hakuthubutu na wala hakuna aliyethubutu miongoni mwa watetezi wake na wampendao si miongoni mwa waliopita wala wale waliofuatia (hakuna aliyethubutu) kusema kuwa Bibi Aisha alikuwa ndani ya Kisaa siku iliposhuka aya hiyo. Basi ni utukufu ulioje wa Muhammad (s.a.w.w.) katika maneno yake na vitendo vyake na ni utukufu ulioje wa hekima yake pale alipowafunika ndani ya Kisaa mpaka Ummul-Muuminina Ummu Salamah ambaye ni mke wa Mtume alitaka kuingia pamoja nao ndani ya Kisaa na akamuomba mumewe ambaye ndiye Mtume wa Mwenyezi Mungu (naye aingie), lakini Mtume akamzuwia kuingia na akamwambia, "Wewe uko kwenye kheri". 2) Kisha aya hii kwa maf-humu yake makh'sus na ile ya jumla inajulisha juu ya "Isma" (ambayo ni kuhifadhika kutokana na kila aina ya madhambi), kwani kuondolewa uchafu kunakusanya kila aina ya dhambi, maasi na uovu, madogo na makubwa, na hasa itakapoongezewa utakaso huo kuwa unatoka kwa Mola Mtukufu mwenye nguvu.


3) Na iwapo Waislamu hujitoharisha kwa maji na udongo tahara ya kimwili ambayo haivuki zaidi ya nje ya miwili, basi Mwenyezi Mungu amewatakasa Ahlul-Bait kwa tahara ya kiroho iliyosafisha akili na moyo, na haukuachiwa nafasi yoyote ushawishi wa shetani wala kutenda maovu. Kwa hiyo nyoyo zao (Ahlul-Bait) ni safi, zimetakasika, zenye ukweli wa dhati kwa Muumba wao katika kila harakati zao na utuvu wao. 4) Kwa yote hayo watu hawa wamekuwa kiigizo kwa watu wote katika ucha Mungu, ukweli, elimu, upole, ushujaa, utu, utakasifu, kuipa nyongo dunia na kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na historia haikupata kuandika maasi au dhambi ya yeyote miongoni mwao muda wote wa uhai wao. Na kama mambo yako kama hivyo, hebu na turejee kwenye mfano wa kwanza unaohusu wakeze Mtume (s.a.w.) na (tumuone) Mwanaisha ambaye amefikia daraja tukufu na cheo cha juu na umaarufu mkubwa ambao hakuna mke yeyote wa Mtume (s.a.w.) aliyeufikia. Haiwezekani kabisa kuzifikia sifa kemkem za bibi Aisha binti Abubakr hata kama sifa zao (wake wengine wa Mtume) zitakusanywa pamoja, na hivi ndivyo wasemavyo Ahlus-Sunnah kuhusu sifa za Mwanaisha pia Ahlus-Sunnah wanaamini kwamba nusu ya dini inatokana kwake (Bibi Aisha) peke yake.


Tukishikamana na ukweli bila ya chuki wala kupendelea, hivi kweli inaingia akilini kwamba Mwanaisha ametakasika hana madhambi wala maasi? Au tuseme kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu alimuondolea Mwanaisha hifadhi na kizuwizi (cha kutofanya dhambi) baada ya kifo cha mumewe (ambaye) ni Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.)? Basi hebu na tuuangalie kwa pamoja ukweli halisi ulivyo. Bibi Aisha katika zama za uhai wa Mtume (s.a.w.w.) Tunapoyafanyia uchunguzi maisha yake na mumewe, tunayakuta madhambi na maasi mengi (aliyoyatenda). Mara nyingi alikuwa akifanva njama yeye na bibi Hafsa dhidi ya Mtume (s.a.w.) mpaka akamlazimisha Mtume kujinyima kitu alichohalalishiwa na Mwenyezi Mungu. Maelezo ya jambo hilo yamo ndani ya Bukhari na Muslim, na wawili hao walisaidiana dhidi ya Mtume (s.a.w.) kama zilivyolithibitisha jambo hilo sihah na tafsiri zote, na Mwenyezi Mungu ameyataja matukio yote mawili ndani ya kitabu chake kitukufu.


Vile vile ni kama ilivyokuwa wivu ukitawala moyo na akili zake na akawa hana heshima wala adabu mbele ya Mtume (s.a.w.), kuna wakati alimwambia Mtume (s.a.w.) pale Mtume alipomtaja bibi Khadija mbele yake, (bibi Aisha akasema) "Kuna uhusiano gani kati yangu na Khadija, hakika yeye alikuwa bibi Kizee mwenye midomo myekundu na Mwenyezi Mungu amekubadilishia (mke) bora kuliko yeye." Na kwa ajili hii Mtume wa Mwenyezi Mungu alikasirika mpaka nywele zake zikatikisika.[35] Kuna wakati fulani mmoja kati ya wakeze Mtume (s.a.w.) alimpelekea Mtume sahani ambayo ndani yake mlikuwa na chakula ambacho Mtume alikuwa akikipenda, bibi Aisha (kwa wivu aliokuwa nao) akaivunja sahani hiyo na chakula chake mbele ya Mtume (s.a.w.).[36]


Kuna mara nyingine tena bibi Aisha alimwambia Mtume, "Hivi wewe ndiye unayedai kuwa ni Mtume wa Mwenyezi Mungu? [37] Pia ipo siku ambayo Mama Aisha alikasirika mbele ya Mtume na akamwambia Mtume, "Fanya uadilifu." Baba yake[38] alikuwepo mahala hapo akampiga mpaka damu zikamtiririka. Na kutokana na wingi wa wivu (aliokuwa nao) alimdanganya Asmaa binti Nu'uman alipokuwa bi harusi nyumbani kwa Mtume akamwambia, "Mtume humfurahia sana mwanamke ambaye akiingia kwake amwambie, "Najilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana nawe". Lengo la Mama Aisha ilikiwa kinyume cha hivyo, bali ni alitaka mwanamke huyo asiye na kosa aachike, na Mtume alimuacha kwa sababu ya maneno haya.[39] Kutokana na adabu yake mbaya mbele ya Mtume (s.a.w.w.), ilifikia mahali ambapo Mtume alikuwa akiswali naye bibi Aisha amenyoosha miguu yake kwenye Qibla, na Mtume akisujudu huisogeza pembeni ndipo (bibi Aisha) huikunja, Mtume akisimama yeye huionyoosha miguu yake kwenye Qibla yake.[40] Kuna kipindi fulani walikula njama yeye na Mama Hafsa dhidi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) ikapelekea (njama hiyo kumfanya Mtume) ajitenge na wakeze kwa sababu ya njama hiyo kwa muda wa mwezi mmoja kamili Mtume analala kwenye jamvi.[41] Iliposhuka kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu isemayo: "Na umuahirishe umtakaye miongoni mwao na umsogeze umtakaye" (Qur 33:51). Aisha alimwambia Mtume bila hata aibu "Simuoni Mola wako isipokuwa anaweka mbele matamanio yako".[42]


Mama Aisha alipokuwa akikasirika (na ni mara nyingi alikuwa akikasirika) huacha jina la Mtume (s.a.w.w.) na hutaja jina la Muhammad na hupata akasema: "Ewe Mlezi wa Ibrahim.[43] (Kwa kweli) Aisha alimuudhi Mtume wa Mwenyezi Mungu mara nyingi na kumpa taabu, lakini Mtume (s.a.w.w.) ni mpole mwenye huruma, na tabia yake ni tukufu na subira yake ni kubwa, mara nyingi alikuwa akimwambia Aisha, "Ewe Aisha shetani wako kisha kukuvaa" na mara nyingi alikuwa akisikitika kutokana na makemeo ya Mwenyezi Mungu kwake Aisha na Hafsa binti Umar, na ni mara nyingi Qur'an ilishuka kwa sababu yake, Mwenyezi Mungu amesema kuwaambia Aisha na Hafsa: "Iwapo mtatubia kwa Mwenyezi Mungu itakuwa kheri kwenu kwa hakika nyoyo zenu zimepotoka" (Qur'an 66:4). Aya hii inamaanisha kwamba amepotoka na kuiacha haki [44] na amesema tena Mwenyezi Mungu: "Na kama mtasaidiana dhidi ya (Mtume) basi Mwenyezi Mungu ndiye msaidizi wake na Jibril na Waislamu wema, na zaidi ya hayo Malaikapia watasaidia". (Qur'an, 66:4) Ni onyo la wazi kutoka kwa Mola Mtukufu (kuwaonya) Mama Aisha na Hafsa ambaye mara nyingi alikuwa akimfuata Aisha na kutekeleza anayomuamrisha. Na amesema tena Mwenyezi Mungu kuwaambia wawili hawa "Mtume akikupeni talaka Mola wake atampa badala yenu wanawake wengine walio bora kuliko ninyi Waislamu tena waumini." (Qur'an, 66:5).Aya hizi zilishuka kumuhusu Mama Aisha na Hafsa kwa ushahidi wa Umar ibn Khatab kama ilivyokuja katika Bukhari.[45] Basi aya hii pekee inajulisha kuwa, kuna wanawake waumini miongoni mwa Waislamu ambao ni bora kuliko Aisha. Kuna wakati fulani Mtume (s.a.w.) alimtuma Aisha pale Mtume alipotaka kumposa dada wa kiongozi wa kabila la Kalbi, Mtume akamtaka Aisha aende akamtazame mwanamke huyo, na aliporudi wivu ulikuwa umeusonga moyo wake, Bwana Mtume (s.a.w.) akamuuliza, "Umemuonaje ewe Aisha? Aisha akasema "Sikuona uzuri wowote." Mtume (s.a.w.) akamwambia Aisha, "Hakika umeona uzuri, hapana shaka umemuona msichana bora na umesisimka ukamuogopa." Basi Aisha akasema; "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu kwako wewe hapana siri na ni nani mwenye kukuficha."[46] Yote aliyoyafanya Aisha kumfanyia Mtume (s.a.w.) miongoni mwa njama (mbali mbali) mara nyingi alikuwa akimshirikisha Hafsa binti Umar, na la kushangaza ni kwamba tunakuta kuwa maelewano na mtiririko kamili kati ya wanawake wawili Aisha na Hafsah ni kama ulivyo mtiririko (wa ushirikiano) na maelewano baina ya baba zao Abubakr na Umar, isipokuwa kwa wanawake Aisha mara nyingi alikuwa na nguvu na hana woga na ndiye mwenye kuharakia (mambo), na yeye Aisha ndiye aliyekuwa akimkokota Hafsah nyuma yake katika kila kitu, wakati huo huo baba yake (Aisha) Abubakr alikuwa dhaifu mbele ya Umar, ambapo Umar alikuwa na nguvu na hana woga na ndiye mwenye kuchukua hatua ya mwanzo katika kila kitu.Kwa hakika tumeona katika maelezo yaliyopita kwamba (Abubakr) hata katika ukhalifa wake, Umar ndiye aliyekuwa mtawala mtendaji. Wanahistoria wamesimulia ya kwamba, Aisha alipokusudia kutoka kwenda Basra kumpiga Imam Ali (a.s.) katika vita ambayo iliitwa vita ya Jamal, aliwapelekea ujumbe wakeze Mtume (s.a.w.) akiwataka watoke pamoja naye, basi hakuna aliyekubali mwito huo miongoni mwao isipokuwa Hafsa bint Umar ambaye alijiandaa na akaazimia kutoka, lakini kaka yake Bwana Abdallah ibn Umar akamkataza na akaenda kumwita ndipo akavunja safari yake.[47] Kwa ajili hiyo basi Mwenyezi Mungu alikuwa akiwaonya Aisha na Hafsa kwa pamoja katika kauli yake aliposema: "Na kama mtasaidiana dhidi yake (Mtume) basi Mwenyezi Mungu ndiye msaidizi wake na Jibril na Waislamu wema, na zaidi ya hayo Malaika pia watamsaidia." Na vile vile kauli yake aliposema: "Iwapo mtatubia kwa Mwenyezi Mungu (itakuwa kheri kwenu) kwa hakika nyoyo zenu zimepotoka." Kwa hakika Mwenyezi Mungu aliwapigia (Aisha na Hafsa) mfano wa hatari sana katika Surat-tahrim ili Mwenyezi Mungu awafahamishe Waislamu wengine ambao wanaamini kwamba Mama huyu wa waumini ataingia peponi bila ya hesabu wala adhabu, eti tu kwa kuwa ni mke wa Mtume (s.a.w.). Sivyo kabisa, Mwenyezi Mungu amewajulisha waja wake wanaume kwa wanawake kwamba hali ya kuoana hainufaishi wala haidhuru mbele ya Mwenyezi Mungu, bali ni matendo ya mtu mwenye we (ndiyo yatakayomsaidia).Mwenyezi Mungu anasema: "Mwenyezi Mungu amewapigia mfano wale waliokufuru kwa mkewe Nuhu na mkewe Lut, walikuwa chini ya waja wetu miongoni mwa waja wetu wema wawili hao (Nuh na Lut) basi (wanawake hao) wakawafanyia hiyana waume zao, hawakuweza kuwakinga kwa lolote (kutokana na adhabu) mbele ya Mwenyezi Mungu, na wakaambiwa ingieni motoni pamoja na wenye kuingia (humo). Surat-tah-riim, aya ya kumi. Mwenyezi Mungu amepiga mfano kwa wale walioamini (akamtaja) mke wa Firaun pale aliposema: "Ewe Mola wangu! nijengee nyumba peponi na uniokoe kutokana na Firaun na matendo yake (machafu) na uniokoe kutokana na watu madhalimu. Na Mariamu binti wa Imran aliyejihifadhi tupu yake, tukampulizia humo roho yetu (inayotoka kwetu) na akayasadikisha maneno ya Mola wake na vitabu vyake na alikuwa miongoni mwa (watu) wanyenyekevu." (Qur.66:ll-12).Kutokana na hali hii basi inabainika kwamba kuoana na urafiki japokuwa kuna ubora mwingi lakini hausaidii (chochote) kuepukana na adhabu ya Mwenyezi Mungu isipokuwa (kuoana huko na urafiki) kutakapo jitambulisha kwa matendo mema, vinginevyo basi adhabu itakuwa maradufu, kwani uadilifu wa Mwenyezi Mungu ni kutomuadhibu aliye mbali ambaye hakusikia wahyi (kwa kiwango) kama cha yule ambaye Qur'an inashuka nyumbani mwake, na haitakuwa sawa adhabu ya mtu aliyeifahamu haki kisha akaipinga aadhibiwe kama mjinga ambaye hakutambua haki. Ewe msomaji sasa hivi hebu angalia baadhi ya riwaya zenye ufafanuzi ili upate kumfahamu vyema mwanamke huyu aliyechukua nafasi kubwa ya kumtenga Imam Ali kutoka kwenye Ukhalifa na akampiga vita kwa kila aina ya nguvu na vitimbi. Vile vile ili upate kufahamu kwamba ile aya ya kuondolewa uchafu na kutakaswa haimhusishi kabisa Mama Aisha kwa umbali wa masafa ya mbingu na ardhi, na kwamba Ahlu-Sunnah wengi wao ni mateka wa uharibifu na uzushi (wa Banu Umayyah) na wanawafuata Banu Umayyah hali yakuwa wao hawafahamu.