UKWELI WA USHIA

 
KUZURU MAKABURIJAMIIL:
Ni zogo gani hili mnalo jisababishi nyinyi Mashia bila ya sababu yoyote?
JAWAD:
Ni zogo lipi hilo?
JAMIIL:
Kulizuru kwenu kaburi la Mtume (s.a.w) na makaburi ya maimam na watu wema.
JAWAD:
Je kunatatizo lolote kufanya hivyo?
JAMIIL:
Hakika tendo hilo ni haram na kufanya hivyo ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu.
JAWAD:
Je wewe Jamiil ni punguwani.. mpiga kelele na kila apigae kelele, na mwenye kufuata upepo kama bendela? Kwa hakika mimi sikuwa nikitarajia jambo kama hili kwa mtu kama wewe-mtu mwenye elimu na mwenye kuelewa mambo- unafuata mambo kutokana na asabia bila ya kuwa na dalili wala uthibitisho, nilikuwa nikikuona mtu wa maana sana-hadi hivi sasa- kutokana na hamasa ya kufanya utafiti uliyo nayo na kuufuatilia ukweli na kwenda sambamba na haki kokote uikutako.


JAMIIL:
Je maneno yangu haya yanatokana na msukumo wa asabaia za madhehebu yangu?
JAWAD:
Ndio..si kinyume na hivyo.
JAMIIL:
Unasema ziara ya wapi?
JAWAD:
Hebu tuyazungumzie maudhui haya hivi sasa-kuzuru makaburi- na tuyaweke kwenye meza ya mazungumzo ili tuweze kuona nani yuko kwenye haki, na nani yuko katika upotovu?

JAMIIL:
Kwa hakika mimi niko tayari, kwa sababu mimi ninafahamu ya kuwa kuzuru makaburi ni shirki.
JAWAD:
Utasemaje ya kuwa kuzuru makaburi ni shirki?
JAMIIL:
Kwa sababu kitendo hicho kinafanana na namna washirikina walivyo kuwa wakiyatembelea Masanam wakati wote na kuto acha kuyazuru masanamu yao.


JAWAAD:
Kwa sababu hiyo imekuwa shirki?
JAMIIL:
Ndio..kwani kuyazuru makaburi ni sawa na kuyatembelea makaburi wakati wote, kama vile washirikina wanavyo yatembelea masanamu yao na kuto acha kufanya hivyo.
JAWAD:
Je kuwa wakati wote kwenye makaburi ndiko kuliko ifanya ziara kuwa ni shirki?
JAMIIL:
Ndio.
JAWAD:
Kwa maana hiyo, waislaam wote- bila kubagua- ni washikina, na hakuna mtu yoyote katika dunia asie kuwa mshirikina, na wewe pia ni katika washirikina!
JAMIIL:
Kivipi ?
JAWAD:
Je umefanikiwa kwenda hija?
JAMIIL:
Ndio, ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa hilo.
JAWAD:
Je ulifanikiwa kusali ndani ya masjidul-haram (msikiti mtukufu wa makka)?
JAMIIL:
Ndio. Ninamshukuru Allah.
JAWAD:
Je uliwaonaje waislaam-wakati wa sala-wakiizunguuka na kukaa pembezoni mwa kaaba kwa ajili ya sala, kwa mfano alie simama upande wa magharibi huupa mgongo upande wa magharibi na kuielekea kaabah, na alie simama upande wa kusini huupa mgongo upande wa kusini na kuielekea kaabah, na alie simama upande wa kaskazini mgongo wake huuelekeza upande wa kaskazini na kuielekea kaabah, na kila mmoja upande wowote atakapo kuwa huuelekeza mgongo wake upande ule na kuielekea kaabah kwa ajili ya sala rukuu na sijda, na mengineyo, je hayo uliyaona?


JAMIIL:
Ndio yote hayo niliyaona na kuyashuhudia, na mimi nilikuwa nikifanya hivyo hivyo wakati wa sala, upande wowote wa msikiti niliko kuwa nilikuwa nikiuelekeza mgongo wangu huko na kuelekea kibla, kwa sababu sala bila kuelekea kibla ni batili.

JAWAD:
Kwa hivyo waislaam wote ni washirikina, na pia wewe ni mshirikina.
JAMIIL:
Kwa nini?
JAWAD:
Kwani kuelekea kwako kwenye kaaba ukiwa katika ibada kunafanana na waabudu masanamu wayaelekeavyo masanamu wakati wakiyaabudu masanamu yao hayo, kwani tunakuta kwamba waabudu masanamu huyaelekea masanamu waliyo yatengeneza kwa mikono yao-wakati wakiabudu, na wewe unaelekea kwenye nyumba yenye kuta ndefu na iliyo jengwa kwa mawe wakati unapo Sali.

JAMIIL:
Lakini kunatofauti kubwa kati ya kuielekea kaaba, na kati ya waabudu masanamu wayaelekeavyo masanamu yao.
JAWAD:
Ni tofauti ipi hiyo?
JAMIIL:
Kwa hakika mimi wakati ninapo elekea kwenye kaaba-katika sala-siizingatii kaaba kuwa ni Mungu ninae muabudu kinyume cha Mwenyezi Mungu-ninajikinga na Mwenyezi Mungu-hivyo hivyo waislaam wengine, hawaielekei kaaba katika sala zao kama Mungu, bali tunaelekea kibla kwa sababu Mwenyezi Mungu ametuamuru hivyo, na waabudu masanamu huyaelekea masanamu yao- katika ibada zao-wakiyafanya masanamu hayo kuwa ni miungu yenye kuabudiwa kinyume cha Mwenyezi Mungu alie takasika, kwani wao huyaelekea masanamu yao wakati wa ibada kwa nyoyo zao, na sisi wakati wa sala huelekeza nyoyo zetu kwa Mwenyezi Mungu mtukufu, na tendo lao hilo ni shirki ya wazi kabisa!


Lakini nitofauti iliyoje kati ya matendo hayo, na kuelekea kwetu kwenye kaaba wakati wa sala? Kati ya mambo mawili hayo kunatofauti kubwa kama tofauti iliyopo kati ya mbingu na ardhi!!

JAWAAD:
Kwa hivyo basi kufanana kwake sio sababu ya shirki, laa sivyo matendo yako nayo yange kuwa ni shirki kwa kufanana kwake na matendo ya wenye kuabudu masanamu, na kitu ambacho kimeyafanya matendo ya wenye kuabudu masanamu kuwa ni shirki ni nia yao ya kuyakusudia kwao masanamu, si yale matendo pekee. Na jambo ambalo liliitoa hali yako ya kuelekea kwenye kaaba kusiwe shirki ni kuto kusudia kwako kuiabudu kaaba kwa kuielekea kwako.


JAMIIL:
Ndio.
JAWAD:
Na sisi Mashia, pia waislaam wengine, katika ziara tuzifanyazo hatukusudii kamwe kumuabudu Mtume Imam au kumuabudu maiti yule alie mwema.. na kufanana kwa ziara hiyo na matendo ya washirikina ikiwa hilo ni sahihi, kwa hakika kufanana huko hakuifanyi ziara hiyo iwe ni jambo la haram na shirki ikiwa mwenye kufanya ziara hakukusudia kuabudu kwa ziara yake hiyo.

Kwa mfano imepokelewa katika hadithi tukufu:
(إنما الأعمال بالنيات )1
Kwani yawezekana amali na tendo moja likawa ni shirki ikiwa atamkusudia kumuabudu asie kuwa Mwenyezi Mungu kwa tendo hilo, na linaweza kuwa tendo hilo linajuzu kulifanya ikiwa hakukusudia kumuabudu asie kuwa Mwenyezi Mungu. Kwa mfano: Ikiwa utasimama sehemu kwa ajili ya sala na mbele yako kuna sanamu limewekwa, ikiwa katika sala yako utakusudia kuliabudu sanamu hilo utakuwa ni mshirikina kwa sala yako hiyo, na ikiwa utakusudia kwa sala yako hiyo kumuabudu Mwenyezi Mungu mtukufu bila ya kukusudia kulielekea sanamu kwa moyo wako sala yako itakuwa ni sahihi na tendo hilo litakuwa ni tendo linalo juzu au linalo faa na kwa kufanya kwako hivyo huwi ni mshirikina.


JAMIIL:
Baada ya kufikiria sana.. yote hayo ni sahihi. Nina muomba Mwenyezi Mungu mtukufu akuhifandhi ukiwa ni nguzo yetu tuitegemeayo, kwani umenifahamisha mambo muhimu sana, mambo ambayo asabia ilinizuia kuweza kuyaelewa. Lakini nataka kufaidika zaidi kwa kuuliza swali moja.

JAWAD:
Uliza hakuna taabu yeyote.
JAMIIL:
Nimefahamu ya kuwa kuzuru makaburi si jambo la haram bali ni jambo linalo faa (linalo juzu), lakini ni siri gani iliyoko katika kuendelea kwenu na kuyatilia umuhimu mkubwa makaburi hayo, na ni sababu gani iwafanyayo kufanya hivyo?
JAWAD:
Kwa sababu ni sunna muakkadah (iliyo tiliwa mkazo).
JAMIIL:
Ni sunna kufanya hivyo?
JAWAD:
Ndio..na sunna hiyo imetiliwa mkazo sana.
JAMIIL:
Je kuna hadithi inayo julisha kuwa kuzuru kaburi la Mtume na makaburi ya waumini wema (s.a.w) ni sunna?
JAWAD:
Ndio..kuna hadithi nyingi sana, ukiongezea matendo ya Mtume (s.a.w) mwenyewe, na sira (mwenendo) wa waislaam tangu mwanzoni mwa kuja Uislaam hadi hivi leo.
JAMIIL:
Tafadhali nitajie baadhi ya mifano hai juu ya hilo.
JAWAD:
1-Imepokelewa katika hadithi sahihi [2] ya kuwa Mtume (s.a.w) aliwazuru mashahidi walio kufa katika vita vya Uhudi.
2-Imepkelewa pia ya kuwa Mtume (s.a.w) alikwenda kuyazuru makaburi ya Baqii'i.
3-Imepokelewa katika (Sunanun-nasaiy) na (Sunanu ibnu Majah) na (Ihyaaul-uluum) cha Ghazaliy kutoka kwa Abi Hurairah
amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu:
(زوروا القبور فإنها تذ كركم بالآخرة ) 3
Yatembeleeni (yazuruni) makaburi kwani yana kukumbusheni Akhera).
4- Imepokelewa katika kitabu hicho hicho kutoka kwa Abi Hurairah amesema: Mtume (s.a.w) alizuru na kulitembelea kaburi la mama yake na kulia na kuwaliza walio kuwa pembezoni mwake, na akasema:
(فزوروا القبور فإنها تذ كركم بالآخرة)
Basi yatembeleeni (yazuruni) makaburi kwani makaburi ni yenye kuku kumbusheni Akhera.[4]


5-Na mlango wa hadithi zilizo pokelewa kuhusiana na jinsi na namna ya kuwazuru walio fariki umejawa na hadithi nyingi katika vitabu vyote vya hadithi, kama vile vitabu vya Sahihi na Sunanu. Na kati ya hadithi hizo ni kuwa: Mwenye kuyazuru makaburi anapotoka na kwenda kwenye Baqii'i inabidi aseme:
السلا م عليكم أهل الد يار من المؤمنين والمسلمين
(Salam iwe juu yanu enyi watu mlioko makaburini kati ya waumini na waislaam).[5] Hizi ni zile hadithi zihusianazo na sunna ya kuzuru makaburi ya waja wema na waumini, na namna inavyo sisitizwa na kuhimizwa kufanya hivyo.Ama zihusianazo na kulizuru kaburi la Mtume (s.a.w) ni nyingi sana, na tutataja baadhi ya hadithi hizo:


1-Imepokelewa na Daru Qutniy [6] na Ghazaliy [7] na Baihaqiy [8] na wengineo ya kuwa Mtume (s.a.w) alisema:
(من زارني وجبت له شفاعتي )
(Atakae nizuru na kulitembea kaburi langu basi itakuwa ni wajibu kupata shafaa yangu). 2-Na imepokelewa ya kuwa Mtume (s.a.w) alisema:
من زارني بالمد ينة محتسبا كنت له شفيعا وشهيدا يوم القيامة
Mwenye kunizuru katika mji wa Madina akitaraji thawabu za Mwenyezi Mungu basi nitakuwa ni muombezi wake na mwenye kumshuhudia siku ya kiama) [9]. 3- Imepokelewa kutoka kwa Naafiu, kutoka kwa Ibnu Omar, kutoka kwa Mtume (s.aw) amesema:
(من حج ولم يزرني فقد جفاني)
(Mwenye kwenda hija na asinizuru hakika atakuwa maenitelekeza na kuniacha nikiwa mpweke.[10]


4-Imepokelewa kutoka kwa Abi Hurairah, kutoka kwa Mtume (s.a.w) amesema:
(من زارني بعد موتي فكأنما زارني حيا )11
(Mwenye kunizuru baada ya kufariki kwangu ni kana kwamba amenizuru nikiwa hai). 5-Imepokelewa kutoka kwa Ibnu Abbas, kutoka kwa Mtume (s.a.w) amesema:
(من حج وقصد ني في مسجدي كانت له حجتان مبرورتان)
(Mwenye kufanya hija na akanikusudia kwa kunifanyia ziara katika msikiti wangu atakuwa na hija yenye kukubaliwa).[12] Na kuna hadithi zingine nyingi zisizo kuwa hizi zinazo julisha na kusisitiza juu ya kuwa sunna kwa tendo hili na kwamba ni sunna iliyo tiliwa mkazo kulizuru kaburi la Mtume (s.a.w) na kuyazuru makaburi ya waja wema kati ya waumi.


Je kauli ya Mtume (s.a.w) isemayo (hakika amenitelekeza) [13] haitujulishi ya kuwa ni sunna iliyo sisitizwa kumzuru? Je kauli yake (s.a.w) isemayo: Mwenye kunizuru atawajibikiwa na shafaa yangu) haijulishi ya kuwa kuna sunna kubwa katika tendo hilo.[14] Je kauli yake (s.a.w) isemayo: Yatembeleeni (yazuruni) makaburi kwani yanawakumbusheni akhera) [15] haitujulishi ya kuwa imeamuriwa kuyafanyia ziara, na amri hapa ikiwa haikutujulisha kuwa tendo hilo ni wajibu je kuna shaka yoyote ya kuwa amri hiyo katika hadithi hiyo ni ya sunna?


JAMIIL:
Hadithi hizi zimetajwa wapi na katika kitabu gani?
JAWAAD:
Vitabu vya hadithi vimejawa na hadithi kama hizi na mfano wa hizi, wewe rejea kwenye vitabu hivyo na usome utaona hadithi nyingi sana.
JAMIIL:
Kwa hakika mimi hadi sasa sijaona , wala sijasikia hadithi hata moja kati ya hadithi hizi.
JAWAD:
Je umesoma sahihi Bukhariy? [16]
JAMIIL:
Kwa bahati mbaya hatuna kitabu hicho?
JAWAD:
Je umesoma sahihi Muslim? [17]
JAMIIL:
Babu yangu alikuwa nacho lakini alipo fariki baba yangu mdogo akakichukua.
JAWAD:
Je umefanikiwa kusoma Sunanu Nasaiy?[18]
JAMIIL:
Ni ipi hiyo?
JAWAD:
Ni kitabu cha hadithi.
JAMIIL:
Hapana ..sijawahi kukiona kitabu hicho.
JAWAD:
Sasa ni hadith zipi ulizo zisoma?
JAMIIL:
Samahani kwa hakika mimi ni mwanafunzi katika chuo cha udaktari, na bado ninafanya juhudi na kuhudhuria shuleni kwangu ili niweze kufaulu katika masomo yangu, na sina muda wala fursa ya kusoma hadithi pamoja na kuwa ninapenda sana kuzisoma.
JAWAD:
Ikiwa hujawahi kusoma hadithi yoyote, na huja angalia kitabu chochote cha hadithi inakuwaje unakuwa na ushupavu na ujasiri wa kupinga kumzuru Mtume (s.a.w) na maimam (a.s), bila kuwa na maarifa yoyote ya hadithi? Je maarifa yako ya kwamba kuzuru makaburi ni shirki hayakuwa ni yenye kujitegemeza kwenye dalili yoyote?


JAMIIL:
Kila nililo lisikia kwa baba yangu, babu yangu na marafiki zangu..kuhusiana na zira halikuwa ni jambo jingine, bali ilikuwa ni kupinga na kukemea jambo hilo, na hakuna hata siku moja niliyo sikia hadithi hizi ulizo zitaja na kuzinukuu hapa.
JAWAD:
Ni wajibu kwa kila mtu kufanya uchunguzi kuhusu ukweli ili aweze kuufikia ukweli huo na asibakie akishikamana na kauli azisikiazo kwenye mazingira na jamii anayo ishi, huenda wao walikuwa kwenye makosa kwenye itikadi hizo, basi ni wajibu ayafanyie uchunguzi yeye mwenyewe, na yeye mwenyewe afuatilie kwa karibu zaidi ukweli huo na asome vitabu mbali mbali, mpaka afike kwenye hatua ya kuishi kiitikadi na katika matendo yake na kauli zake kama atakavyo Mwenyezi Mungu mtukufu.


JAMIIL:
Hivi sasa nimeamini ya kuwa kulitembelea kaburi la Mtume (s.a.w) ni sunna iliyo tiliwa mkazo na iliyo sisitizwa, vile vile kuzuru makaburi ya maimam na makaburi ya waumini na watu wema kati ya waja wa Mwenyezi Mungu.
JAWAD:
Nina ombi moja kwako.
JAMIIL:
hakuna tatizo sema tu.
JAWAD:
Kwa hakika mimi ninasisitiza ombi langu kwako ya kuwa usiwe mtu mjinga mwenye kufuata kila sauti uisikiayo na kila muitaji aitae, na wala usifuate itikadi zilizoko kwenye jamii unayo ishi isipokuwa baada ya kuzifahamu kupitia njia za kielimu na kuzifanyia utafiti, kwani ikiwa utafanya hivyo utakuwa umefaulu.

JAMIIL:
Na hili ndilo nilikusudialo kulifanya siku za mbeleni, kwani baada ya kuwa nilikuwa nikiitakidi ya kuwa kuzuru makaburi ni shirki nimefahamu kupitia njia ya Uislaam ya kuwa ni sunna iliyo sisitizwa, na nimefahamu ya kuwa ninacho takiwa kukifanya ni kufanya uchunguzi katika maudhui tofauti. Na kuhusu jambo hili kwanza kabisa nitakwenda kufanya mazungumzo na baba yangu , -kabla ya jambo lolote lile-baba ambae ndie aliekuwa ni sababu pekee ya mimi kuitakidi maudhui haya, huenda nikajaaliwa kumuongoza.


JAWAD:
Ninakushukuru.
JAMIIL:
Nami ninakushukuru kwa kuniongoa.


________________________________________

[1]- Rejea Sahihul-bukhary juzu ya 1\ 1-3, mlango wa 1 Kayfa kana bad'ul-wahyi ila rasuuli llahi (s.a.w) min kitabi bad'il-wahyi, Pia tafsirul-kabiir ya Fakhrur-raziy juzu ya 4\ 5 mas'alatur-raabiah min tafsiri aya 112 ya suratul Baqarah, Tahdhiibul-ahkaam 1\ 83\ 67 mlango wa 4\ sifatul-wudhuu min kitabut-twaharah, na juzu ya 4\ 186\ mlango wa 44 Niyatus-swiyaam

[2]- Rejea Sahihi Muslim juzu ya 2\ 63, na Sunanun-nasaiy juzu ya 3\76.


[3]- Sunanu Ibnu Majah juzu ya 1\ 500-1569, mlango wa 4\ Maa jaa'a fii ziyaaratil-qubuur: Tudhakkirukumu bil-aakhirah, na Ihyaaul-uluumid-din juzu ya 4\ 490, ufafanuzi kuhusi kuyazuru makaburi na kumuombea maiti na yahusianayo na ziara hiyo, na katika mlango huo kuna hadithi hii:
( زر القبور تذ كر بها الآخرة )
Yatembelee makaburi na ujikumbushe Akhera kwa kufanya hivyo.

[4]- Sunanu Ibnu Majah juzu ya 1\ 501\ 1572, mlango usemao: Maa jaa'a fii ziyaaratil-qubuuril-mushrikiina, na katika mlango huo kuna hadithi ifuatayo:
فإنها تذ كركم الموت
( Kwa hakika makaburi yanakukumbusheni kifo).


[5]- Sunanu Ibnu Majah juzu ya 1\ 494\ 1547, mlango wa 36 Maa jaa'a fiimaa yuqalu idha dakhalal-maqaabir. Sahihi Musliim juzu ya 2\ 365\ 104, mlango wa 35 Maa yuqaal inda dukhuulil-qubuur wad-duaa'a liahliha. Muntakhab Kanzul-ummal fii haamish Musnad Ahmad juzu ya 2\ 89, na katika mlango huo kuna hadithi ifuatayo: Kati ya waumini wa kiume na waumini wa kike…

[6]- -Ali bin Omar Daru Qutniy katika Sunani yake juzu ya 2\ 278\ 194, babul-mawaqiitr, na katika mlango huo kuna maneno yafuatayo:
من زار قبري وجبت له شفاعتي
(Mwenye kulizuru kaburi langu atawajibikiwa na Shafaa yangu).

[7]- Ihyaaul-uluum juzu ya 4\ 490-491, Ufafanuzi kuhusiana na kuzuru makaburi na kumuombea maiti na yahusianayo na kuzuru makaburi, kwa nassi ya Daru Qutniy.

[8]- Ahamd bin Husein Al-bayhaqiy fii sunanil-kubraa juzu ya 5\ 244, mlango wa Ziara qabrin-nabiiy (s.a.w), na katika mlango huo kuna hadithi ifuatayo:
من زار قبري, أو قال: من زارني كنت له شفيعا.
(Mwenye kulizuru kaburi langu, au alisema: Mwenye kunizuru nitakuwa ni muombezi wake).

[9]- Ihyaaul-uluum juzu ya 4\ 491, ufafanuzi kuhusiana na ziara ya makaburi na kumuombea maiti na yahusianayo na maiti. Muntakhab kanzul-ummal Haamish Musnad Ahmad juzu ya 2\392, na katika mlango huo kuna hadithi ifuatayo:
شهيدا و شفيعا
(nitakuwa shahidi na muombezi wake).

[10]- Kanzul-ummal, Haamish Musnad Ahmad juzu ya 2\ 392, na ndani yake kuna hadithi isemayo: Mwenye kuhiji nyumba ya Allah………….nk.

[11]-Kitabu hicho hicho kilicho tajwa hapo juu, na kuna hadithi isemayo: Ni kana kwamba amenizuru katika uhai wangu.

[12]- Kitabu hicho hicho, na kuna hadithi isemayo: Mwenye kuhiji makka kisha akanikusudia kunifanyia ziara katika msikiti wangu ataandikiwa hijja mbili zenye kukubaliwa.

[13]- Kitabu hicho hicho.

[14]-Ihyaau-uluumid-din juzu ya 4\ 490-491.

[15]- Sunan Ibnu Majah juzu ya 1\ 500-1569, mlango wa 47 Maa jaa'a fii ziyaaratil qubuur, na katika mlango huo kuna hadithi isemayo: kuzuru makaburi kuna kukumbusheni akhera.

[16]- Sahihi Bukhariy: Kitabu Sahihi cha Muhammad bin Ismail Al-bukhariy, Hafidh Al-akiliy amesema: Bukhariy alipo tunga kitabu Sahihi Bukhariy, alimuonyesha Ahmad bin Hanbali, na Yahya bin Muiin, na Ali bin Al-madiniy, na wengineo na wakasema kuwa ni katabu kizuri na kupendezewa na kitabu hicho, na wakatoa ushahidi wa usahihi wa kitabu hicho isipokuwa katika hadithi nne. Amesema -na kauli katika hadithi hizo ni kauli ya Bukhariy-nazo ni sahihi, na Nasaiy alisema kuhusiana na hadithi hizo: Yaliyoko kwenye vitabu hivi ni mazuri zaidi kuliko yaliyoko kwenye kitabu cha Muhammad bin Ismail, Al-haakim An-naisaburiy amesema: Mwenyezi Mungu amrehemu Imam Muhammad bin Ismail hakika yeye ndie ambae alie tunga na kuandika misingi na kuwajengea watu msingi, na kila alie fanya kazi baada yake katika uwanja huu, kwa hakika alichukua kutoka kwenye kitabu chake.


[17]- Sahihi Muslim: Sahihi Muslim binil-hajjaj Al-qushairiy An-naisaburiy, Haafidh Abu Ali An-naisaburiy Amesema: Hakuna chini ya mbingu kitabu kilicho sahihi kuliko kitabu cha Muslim bin Al-hajjaj katika elimu ya Hadithi.

[18]- Sunanun-nasaiy: Sunanu Ahmad bin Shuaibu An-nasaaiy, Ibnu Rushdi Al-fahriy amesema:Kitabu cha Nasaiy ni kitabu kizuri sana kati ya vitabu vilivyo andikwa katika Sunan na chenye mpangilio mzuri sana, na kitabu chake hicho kilikuwa kimekusanya kati ya njia mbili ya Bukhariy na Muslim pamoja na kuwa kina kasoro nyingi.