UKWELI WA USHIA

 
KUPAMBWA KWA MAKABURI YA MAIMAMKHALID:
Salaamun alaykum.
BAAQIR:
Wa alaykumus-salaam warahmatullahi wabarakatuhu.
KHALID:
Umefanya vizuri umekuja lini?
BAAQIR:
Nimekuja kumtembelea mtoto wa ami yangu anaishi hapa.
KHALID:
Nakuomba leo hii ukaribie nyumbani kwetu.

BAAQIR:
Kwa hakika ninakazi nyingi nilizo ziacha kwa ajili ya kuwatembelea ndugu (kuunga udugu) na kuomba unisamehe sana kwa wito huo.
KHALID:
Haiwezekani..marafiki wawili baada ya kutengana kwa muda wa miaka kumi wanakutana kisha wasibakie na kufuatana walau kwa muda wa saa moja. Hakika mimi -pia nina haki ya udugu wa kiislaam. Kisha kulitokea mazungumzo kati yangu na ndugu yangu mmoja muumini kuhusiana na maudhui ya Shia na Sunna na kutokana na kuwa mimi ninamatumaini na imani na wewe ninataka na ninakusudia kufanya mazungumzo na wewe kuhusu maudhui hayo ili niweze kuelewa ukweli na uhaki katika maudhui hayo.


BAAQIR:
Hakuna shaka. Walifuatana pamoja hadi nyumbani kwa Khalid, na kufika nyumbani kwake, na kila mmoja akaketi pembezoni mwa mwenziwe. Na baada ya kuzungumza kuhusiana na mambo yanayo wahusu na yaliyo maalum kwa ajili yao wawili, Baaqir akamuwahi mwenzie kwa kumuuliza swali na kusema: Ni mazungumzo gani yaliyo fanyika kati yenu?

KHALID:
Mazungumzo yalikuwa yakihusiana na kuyapamba makaburi ya Manabii, maimam, maulamaa, waumini na watu wema na mfano wa hao, kwa Dhahabu na Fedha na mapambo mengineyo.
BAAQIR:
Ni tatizo gani lililopo kuhusiana na jambo hilo?
KHALID:
Je kufanya hivyo si haram?
BAAQIR:
Kwanini iwe haram?
KHALID: Je maiti anafaidika na mapambo hayo?

BAAQIR:
Hapana, hafaidiki nayo.
KHALID:
Kwa hivyo, hayo yote ni Israfu na matumizi mabaya, na Mwenyezi Mungu anasema
ولا تبذر تبذ يرا * إن المبذ رين كانوا إخوان الشياطين
Wala usitawanye (mali yako) kwa ubadhirifu. Hakika watumiao kwa ubadhirifu ni ndugu za mashetani. suratul- israai aya 26-27.

BAAQIR:
Unasemaje kuhusiana na nguo ifunikwayo juu ya Kaaba na mapambo yake, na Dhahabu Fedha na vitu ambavyo vipo juu ya Kaaba na ndani ya Kaabah?
KHALID:
Sijui.
BAAQIR:
Ndio, Kaaba ina nguo ambayo hufunikwa juu yake, na kuna Dhahabu nyingi, ambayo watu huitoa zawadi kwa ajili ya Kaaba kutoka sehemu tofauti za Dunia tangu zama za ujahilia hadi katika zama zetu hizi. Ibnu Khaladuni [1] anasema katika utangulizi wa kitabu chake:[2] Kwa hakika tangu zama za Ujahilia kaumu mbali mbali walikuwa wakiitukuza Kaaba, na wafalme walikuwa wakituma mali na vitu vya thamani kwenye nyumba hiyo kama vile Kisraa na wengineo, Na kisa cha mapanga na nguo zilizo fumwa kwa dhahabu, vitu ambavyo Abdulmutwalib alivikuta chini alipo chimba kisima cha Zamzam ni maarufu sana).


Na Mtume (s.a.w) alipo ikomboa Makka alikuta katika kisima kirefu kukiwa na Awqiyah sabini elfu za Dhahabu vitu ambavyo wafalme walikuwa wakizitoa zawadi kwa ajili ya nyumba ya Allah. Na kulikuwa na dinari milioni moja, yaani zenye uzito wa Kintwari milioni mbili. Na Ali (a.s) alisema kumwambia Mtume: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu unaonaje ukitumia mali hii ikakusaidia katika vita vyako? Mtume hakufanya hivyo. Kisha akamwambia Abubakar nae hakuzitoa. (hadi akasema)

(Amesema Abu waail): Niliketi kwa Shaibah bin Othuman nae akasema Aliketi kwa Omar bin Khattab, akasema: Niliazimia nisibakishe katika nyumba hiyo chembe yoyote ya Dhahabu wala Fedha isipokuwa nitaigawa kati ya Waislaam. Nikasema Hutafanya hivyo?
Akasema: Kwanini nisifanye hivyo?
Nikasema: Sahiba wako hakufanya hivyo.

Akasema: Hao wawili ndio ambao hufuatwa nyendo zao. [3]
Je Kaabah ilikuwa ikifaidika na Dhahabu na Fedha hizo ewe Khalid?
Au -Mwenyezi Mungu -ametakasika na hili- alikuwa akifaidika na vitu hivyo viwili?

KHALID:
Hapana.
BAAQIR:
Pamoja na hayo Mtume (s.a.w) hakuunyoosha mkono wake kwenye mali hiyo iliyo kuwa imelimbikizana, wala hakutumia hata chembe moja ya mali hiyo, pamoja na kuwa wakati ule Uislaam ulikuwa ukihitajia sana mali na pesa nyingi wakati ambapo hazina ilikuwa imejaa, kwa ajili ya kuimarisha nguzo zake katika miji na nchi mbali mbali. Kwa nini hakufanya hivyo? Ni kwa sababu mali hiyo nyingi ilikuwa ni mali ya Kaabah na huiongezea Kaabah utukufu na heba yake machoni mwa watu, japokuwa utukufu na daraja yake ya kweli iko kwa Mwenyezi Mungu mtukufu, utukufu ambao haupungui wala kuongezeka, sawa iwe na mali zote za dunia, au isiwe na chochote.


Na maneno ni hayo hayo kuhusiana na makuba ya Dhahabu, na milango ya Dhahabu na Fedha, na nguo ifunikwayo juu yake na mapambo yatolewayo zawadi na kupambwa nayo makaburi ya mawalii wa Mwenyezi Mungu mtukufu kama vile: Amirul-muuminiin, Imam hasan na Imam Husein, Imam Ridhaa na wengineo juu yao rehma na amani. Watu hawa cheo na daraja yao ya kweli waliyo pewa na Mwenyezi Mungu haipungui wala kuzidi kwa kuwepo madini hayo ya thamani kwenye makaburi yao, na wala haipungui ikiwa hayakuwepo, kwa mfano Imam Hasan bin Ali (a.s) ni bora kuliko nduguye Husein (a.s) japokuwa kaburi la Imam Hasan (a.s) hupigwa na jua katika jangwa la Bakii'i likiwa halikujengewa juu yake au juu yake kukiwa hakuna jengo lolote, na likiwa halikupambwa na pambo la aina yoyote, na kaburi la Imam Husein (a.s) lilikuwa na majengo makubwa makubwa ya dhahabu halisi iangazayo angani na kuyaondoa mawingu.Lakini tumeyafanya hayo kwa ajili yao, na kutoa zawadi ya mapambo ya Dhahabu kwenye makaburi yao, na makuba ya makaburi yao kuyatia dhahabu na mengineyo, yote hayo kwa ajili ya kuwaenzi na kuwatukuza wao.

KHALID:
Je vitu hivi vinawapatia hawa utukufu katika macho ya watu?
BAAQIR:
Ndio. Na hivi sasa nitakufanya ukiri jambo hilo. Kwa mfano ukienda kwa Mayahudi na kuyaona makaburi ya maulamaa wao yakiwa yameharibika, yakipigwa na jua, hakuna kizuizi chochote juu yake au chumba ambacho mwenye kuyatembelea anaweza kujikinga jua kwenye kivuli chake. Kisha ukenda kwa Wakiristo, na ukakuta makaburi ya maulamaa wao yakiwa yamejengewa vizuri na kuhifadhika, yakiwa yamejengewa makuba na yakiwa yamepambwa kwa dhahabu na fedha, na mapambo mengine ya madini mbali mbali. Je ni maulamaa gani utakao waona kuwa ni wenye utukufu, ni maulamaa wa Mayahudi au Wakiristo, pamoja na kuwa unafahamu ya kuwa wewe ni Muislaam na unafahamu ya kuwa wote wawili wako kwenye batili?


KHALID:
Bila shaka kutokana na mandhari ya makaburi ya pande mbili niliyo yaona nitachukua picha fulani ya utukufu wa maulamaa wa Wakiristo, na picha ya udhalili wa maulamaa wa Mayahudi.
BAAQIR:
Kwa hivyo basi wayafanyayo Mashia na Masunni kwa kujenga madharihi juu ya makaburi, na kujenga haram na makuba na mengineyo juu ya makaburi ya maimamu na Mitume.. ni kwa ajili ya kuwatukuza wao na kuwaenzi, kwa sababu hiyo huyapamba kwa Dhahabu Fedha na mapambo mengine ya madini mbali mbali.
KHALID:
Yote hayo ni sahihi lakini je jambo hilo linakitoa kitendo hicho kwenye sifa ya israfu na matumizi mabaya na yasiyo ya lazima?.
BAAQIR:
Ndio, na zaidi ya hapo. Ikiwa itathibiti kuwa matendo haya ni kuwatukuza mawalii wa Mwenyezi Mungu, wakati huohuo ni kuutukuza Uislaam, kwani kuwatukuza viongozi na watukufu wa Uislaam ni kuutukuza Uislaam, na kila kitu ambacho ndani yake kuna kuutukuza Uislaam basi kitu hicho ni katika shiari za Mwenyezi Mungu ambazo Mwenyezi Mungu amesema kuhusiana nazo:
( ومن يعظم شعا ئرالله فإنها من تقوي القلوب )
Kwa hivyo basi kuyapamba makaburi ya mawalii wa Mwenyezi Mungu ni katika shiari za Mwenyezi Mungu ambazo ni sunna kuzifanya na kufanya kazi kwa ajili yake, na mtu mwenye kufanya hivyo hupewa thawabu kwa matendo yake hayo.
KHALID:
Nakuomba samahani, kwa kuchukua kiasi hiki cha wakati wako lakini mbele ya Mwenyezi Mungu ni mwenye malipo, kwani umenitoa kwenye kiza cha ujinga na kuniweka kwenye nuru ya elimu na ufahamu, ni kwa kiasi gani nilikuwa nikifikiria kuhusiana na upambaji huu wa makaburi na nisielewe siri yake na faida yake na usahihi wake, kwa hakika hivi leo-wewe- umenitia nuru kwa elimu yako hii, na umenifikisha niliko kuwa nikipakusudia.
BAAQIR:
Sasa shaka yote uliyo kuwa nayo kuhusiana na kupamba makaburi imetoweka?
KHALID:
Ndio.. hakuna shaka yoyote niliyo bakia nayo kwani kufanya hivyo ni sunna na jambo lililo himizwa na Qur'ani tukufu kwa kauli yake Mwenyezi Mungu:
ومن يعظم شعا ئرالله فإنها من تقوي القلوب
BAAQIR:
Alaa ayyi hal (Kwa hali yoyote ele):Hakika mimi niko tayari kufahamiana nawe katika maudhui kama haya ili niweze kufaidika, au wewe pia ufaidike, na wote kwa pamoja tuwe ni wenye kuyafahamu mambo kwa ufahamu mzuri na wenye mazingatio.
KHALID:
Ninakushukuru sana sana, na ninamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu akuwafikishe kwa yale ayaridhiayo.

________________________________________

[1]- Ibnu Khaladun: Ni Abdur-rahman bin Muhammad bin Khaladun Al-khadhramiy, alizaliwa mwaka 732 Hijiria katika nchi ya Tunisia anatokana na asili ya familia ya Andalusi Ashbiliy, Ibn Khatib amemuelezea katika kitabu chake kiitwacho: Al-ihaatwah fii Akhbari gharnaatwah) amesema: Kwa hakika ni fakhari wa matumbo na vizazi vya Moroko-yaani Ubnu Khaladun- alisherehesha kitabu Al-mubarridah kwa sharh nzuri jambo lililo toa dalili juu ya umakini wa kuhifadhi kwake na akili yake na ufahamu wake wa fani mbali mbali, na kuandika mihutasari ya vitabu vingi sana vya ibnu Rushdi, na akaweka ufafanuzi wake kwenye kitabu Sultani Abi Saalim ufafanuzi ambao ulikuwa ni wenye faida katika elimu ya Mantiki. Alifariki katika nchi ya Misri mwaka 808 hijiria, na miongoni mwa vitabu vyake mashuhuri katika Historia (At-taarifu bi ibnu Khaladun wa rihlatihi sharqan wa gharban) na kitabu chake ( Al-ibaru wadiiwaanul-mabdau wal-khabaru fii taarikhil-arab wal-barbar wamin Aaswarahum min dhawi sha'anil-akbar wa huwa tariikh Ibnu Khaladun Al-maaruf) (Rejea juzu ya kwanza ya tarikh ibnu Khaladun).

[2]- Utangulizi wake: Nayo ni sehemu ya kwanza ya kitabu (At-tariikh) kilicho pangwa katika milango sita na fasli zake zilizo tofauti zilizoko kwenye kitabu cha kwanza fii twabiati umran fil-khalifah na ayaelezayo katika kitabu hicho kama vile bidaa utamaduni ushindi biashara maisha na viwanda na elimu mbali mbali na mfano wa hayo na yahusiana na hayo kati ya sababu na illa mbali mbali. \ juzu ya 1\ 303 chapa ya Daaru-ihyaait-turathil-arabiyah, Bairut. Lebanon.

[3]- Chanzo kilicho tangulia. Taarikh ibnu Khaladun juzu ya 1\ 353 mlango wa nne katika kitabu cha kwanza sehemu ya sita kuhusiana na misikiti na majumba makubwa ulimwenguni.