UKWELI WA USHIA

 
KUYAJENGEA MAKABURI (KUJENGA JUU YA MAKABURI)FUADI:
Ewe Jaafar, je unaniruhusu nikuulize kuhusiana na maudhui ya Shia na Sunni? [1]
JAAFAR:
Uliza kwani nina penda sana kila mtu awe ni mwenye kufahamu mambo, mwenye elimu na anae fahamu mambo kutokana na utafiti na kwa kupata yakini na hawi ni mwenye msimamo legelege na mwenye kufuata kila akisikiacho na kipepeacho angani, au kila sauti ijitokezayo na kutangaa angani bila ya kufahamu usahihi wake na ubatilifu wake au ufisadi wake.

FUADI:
Je maneno yangu utayaamini ikithibitika kuwa sisi (Ahli sunna) ndio wenye haki?
JAAFAR:
Kwa hakika mimi niko msitari wa mbele kati ya wale wenye kuamini mambo ya kweli haraka pale wanapo yafahamu, na mimi sikushikamana na ushia isipokuwa ni baada ya kuuona kuwa ni haki na wewe unafahamu ya kuwa baba yangu na mama yangu na ndugu zangu na watu wa kabila langu .. wote ni masunni na kati yao hakuna Shia hata mmoja, na mimi sikufuata Ushia isipokuwa ni kwa ajili ya ukweli nilio uona na kuukuta ndani ya madhehebu hayo.. na lau nitafahamu usahihi wa maneno yako mimi ni wa mwanzo kuyaamini.


FUAD:
Nyie Mashia mnayajengea makaburi ya Manabii, Maimamu, Maulamaa na watu wema majengo makubwa, mnasali kwenye makaburi, wakati jambo hilo ni shirki, kama washirikina wanavyo abudu masanamu nanyi Mashia mnaaabudu majengo ya makaburi ya mawalii.

JAAFAR:
Ni wajibu sisi tuwe wakweli na tunao kwenda sambamba na uhakika wa mambo, tusiwe ni watu wachukuao maganda na kuacha kiini, tusiangalie yasemwayo na fulani au fulani, bali tuangalie ukweli ulio wazi katika kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Mtume wake (s.a.w), na mwenendo wa watu wema walio tangulia.

FUAD:
Ndio, nami ni hivyo hivyo, ninapenda kufahamu ukweli wa mambo kupitia njia za kielimu na ufahamu sahihi, si kufuata mambo ufuataji wa kipofu.
JAAFAR:
Kwanza kabisa: Sio sisi Mashia pekee tuhusikao na suala la kuyajengea makaburi, kwani waislaam wote wanayajengea makaburi ya Manabii na Maimam na wanazuoni wakubwa au viongozi wao, na ifuatayo ni mifano juu ya hayo: Kaburi la Mtume (s.a.w) na makaburi ya makhalifa wawili bado hadi hivi sasa yamejengewa kwa jengo kubwa na yenye kuba kubwa na ya hali ya juu kabisa.


Makaburi ya Mitume kadhaa, kama vile kaburi la Nabii Ibrahim (a.s) lililoko Jodan katika mji wa (Al-khaliil) makaburi hayo yana dharihi (yamejengewa) na juu yake kuna kuba na majengo makubwa. Kaburi la Nabi Mussa (a.s) lililoko Jodan kati ya mji wa (Qudsi) na (Omman) lina jengo kubwa. Kaburi la Abi Hanifa lililoko Baghdad hadi leo bado limejengewa kwa jengo kubwa, na juu yake kuna kuba. Kaburi la Abi Hurairah katika (Misri) hufanyiwa ziara na limejengewa na juu yake kuna kuba. Kaburi la Abdul-qaadir lililoko (Baghdaad) kaburi hilo lina uwanja mkubwa na dharihi na juu yake kuna kuba.

Na makaburi mengine ya Mitume, na makaburi ya Maimamu na wanazuoni wakubwa wa madhehebu, yote hayo yana majengo na juu yake kuna kuba, na yana waqfu maalum ambapo waqfu hizo faida zake hutumika kuyaimarisha na kuyakarabati makaburi hayo na kuyalinda yasiharibike. Na Miji ya kiislaam imejawa na majengo kama hayo.. na Waislaam wote pamoja na tofauti za madhehebu yao tangu siku ya kwanza hadi leo huyapenda mambo hayo, na huwaamrisha watu kuyatekeleza hayo, na hawakukataza kufanya hivyo hata siku moja, kwa hivyo si sisi Mashia pekee tuhusikao na hukumu hii, bali wanakubaliana nasi na kuwafikiana nasi Waislaam wengine wote, na wao pia huyajengea makaburi ya maimamu wao na wakati wote huyatembelea.

Pili: Sisi- Mashia- au waislaam wengine wakati tunapo Sali pembezoni mwa makaburi ya mawali, hatusali kwa ajili ya mawalii hao bali tunasali kwa ajili ya Mwenyezi Mungu pekee. Na liwezalo kukujulisha hilo ni kuwa sisi tunapokuwa katika sala huelekea kibla na wala hatuyaelekei makaburi hayo, na lau kama tunge kuwa tukiyasalia makaburi yale, na kuelekea kwenye ibada zatu kwenye dharihi zile (majengo yale ya makaburi), ingewajibika kuyaelekea, na tusinge elekea kwenye kibla.

FUAD:
Kwa nini mnasali nyuma ya makaburi hayo, mpaka mkayafanya kuwa ni kibla chenu?
JAAFAR:
Hakika sisi wakati tunapo Sali nyuma ya makaburi, tunaelekea kibla na wala hatuyaelekei makaburi, bali makaburi yale-imetokea tu- yakawa mbele yetu, bila ya sisi kukusudia kuyaelekea.


Na hili halitokei isipokuwa kwa mtu anae Sali akiwa ameelekea kibla katika sehemu fulani na ikatokea kwa mfano kukawa na jengo kubwa mbele yake, je kusali katika sehemu hiyo kunamaanisha kuwa mwenye kusali anaabudu jengo hilo?! Na zaidi ya hayo Maulamaa wote wa Waislaam wanasema kuwa: Inajuzu kusalia katika majumba ya ibada za washirikina hali ya kuwa umeelekea kibla hata kama mbele ya mwenye kusali kutakuwa na sanamu lenye kuabudiwa kinyume cha Mwenyezi Mungu, Kwani mwenye kusali humuelekea Mwenyezi Mungu na wala halielekei sanamu. Je hii inamaana kuwa mwenye kusali analiabudu sanamu lile?


FUAD:
Ikiwa kuyajengea makaburi si shirki- kama unavyo sema- na waislam wote wanasema ya kuwa inajuzu kufanya hivyo, ilikuwaje wakavunja madharihi (majengo ya makaburi) na makuba yaliyo jengwa juu ya makaburi ya maimamu na wengineo, kwa hoja ya kuwa kufanya hivyo ni shirki na ni kumuabudu asie kuwa Mwenyezi Mungu, na maulamaa wa Hijazi wakatoa fat'wa ya kufanya hivyo?

JAAFAR:
Kwa hakika ni baadhi tu walio toa fat'wa kama hiyo kati ya maulamaa wa Hijazi katika zama zile, kwani kuna baadhi ya Mashekhe waishio katika mji wa Madina walio nihadithia na kunisimulia kwa kusema: Kwa hakika wakati huo walipo toa amri ya kubomoa makuba na majengo ya makaburi, maulamaa wenyewe wa Hijazi walipinga amri hiyo, wakitoa hoja kuwa hilo si shirki bali vitu kama hivyo ni sunna katika sheria ya kiislaam, kutokana na kauli yake Mwenyezi Mungu mtukufu:
( )
jambo lililo pelekea kufukuzwa kwa maulamaa wale, na kuwauzulu wengine katika nyadhifa zao na kuwatenga. Kwa hivyo basi: Fat'wa hiyo haikutolewa isipokuwa na baadhi tu ya maulamaa wa Hijaz.

FUAD:
Kwa hakika mimi nilikuwa nikifikiria na kujiuliza ya kuwa: Ikiwa kujenga madharihi na makuba ni haram na shirki, kwa nini maulamaa wa Waislaam hawakuzinduka na kuliona hilo tangu zama za Mtume (s.a.w) hadi leo, na kwanini hawakuzuwia kufanya hivyo? Na ilikuwaje Waislaam wasilifahamu hilo kwa muda wa karne kumi na tatu?


JAAFAR:
Nitakuongezea elimu na maarifa: Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) alikiri na kukubali kujengea makaburi, madharihi na makuba na hakukataza kufanya hivyo. Kwa mfano hili ni jengo la hijri Ismail mahala alipo zikwa Nabi (Ismail) na sehemu alipo zikiwa mama yake Haajar. Na haya hapa makaburi ya Manabii wengine-kama Ibrahim Musa na wengineo- walio zikiwa pembezoni mwa baytul-maqdas, yalikuwa ni yenye majengo makubwa katika zama za Mtume (s.a.w) na hadi zama zetu hizi, na wala hakuzuwia yeyote si Mtume Mwenyewe (s.a.w) wala mmoja wapo kati ya makhalifa wake.


Na lau kama tendo hilo linge kuwa haram au linge kuwa ni shirki basi Mtume ange amuru kuvunjwa na kubomolewa kwa majengo na makuba hayo, na ange kataza kufanya hivyo. Na kutokana na ukweli kuwa hakufanya hivyo tunafahamu na kuwa na yakini ya kuwa mfano wa vitu kama hivyo au kufanya hivyo ni kitu kinacho juzu na kinafaa.

Hivyo hivyo baada ya kufariki Mtume (s.a.w), kwani Mtume wa Mwenyezi Mungu alipo chukuliwa roho yake alizikwa katika chumba chake, na mlango wa chumba kufungwa, na kaburi lake likawa katikati ya chumba kilicho jengewa kuta na dari, na lau kama sahaba yeyote ange sikia kutoka kwa Mtume (s.a.w) kuwa tendo kama hilo ni haram basi wasinge thubutu kumzika Mtume katika chumba hicho kilicho jengewa, na lau kama ingelazimika kumzika chumbani mwake basi ingekuwa wajibu kubomoa chumba hicho ili kaburi hilo lisiwe na jengo au lisiwe ni lenye kujengewa.

Na kutokana na kutofanya kwao hivyo, tukafahamu ya kuwa kujenga juu ya makaburi si haram, sasa vipi itakuwa ni shirki?.
FUAD:
Ninakushukuru kwa wema wako kwani umeniongoza kwenye ukweli (haki), na kunijulisha ya kuwa kujenga juu ya makaburi si haram wala shirki, na kwamba wale ambao wanaharamisha jambo hilo hawana dalili yoyote katika sheria wawezayo kuitegemeza kwayo kauli yao Na kwa hakika mimi nitakushukuru daima juu ya hili.

JAAFAR:
Nami ninakushukuru kwa kukubali kwako ukweli na haki baada ya kuifahamu, na kuufuata kwako uongofu pale ulipo uona, kwani wewe ni mwenye kufuata muongozo wa akili na mantiki sahihi, kwa hivyo basi ninapenda kukuzidishia maarifa zaidi kuhusiana na haki na ukweli, na kukupatia maarifa mbali mbali katika dini, je unawakati zaidi ili niweze kuzungumza na wewe?

FUAD:
Kwa hakika mimi ninapenda sana maneno ya kweli, zungumza ulitakalo, hakika mimi niko tayari kukusikiliza na kuyajaza masikio yangu kwa maarifa.
JAAFAR:
Kutokana na mazungumzo yetu yaliyo pita imethibiti kuwa kujenga juu ya makaburi ya mawalii wa Mwenyezi Mungu ni jambo linalo faa na inajuzu kufanya hivyo, na jambo hilo si haram.


FUAD:
Ndio.. nami niko pamoja nawe katika hilo.
JAAFAR:
Hivi sasa nataka kusema hivi: Hakika kujenga juu ya makaburi ya mawalii wa Mwenyezi Mungu na kuweka madharihi juu yake na kujenga makuba.. yote hayo ni sunna, hupewa thawabu mwenye kuyafanya hayo yote, si tu kwamba inajuzu.

FUAD:
Vipi inakuwa sunna?
JAAFAR:
Mwenyezi Mungu mtukufu amesema:
.
( Na anayeziheshimu alama za Mwenyeezi Mungu basi hayo ni katika unyenyekevu wa nyoyo). Kwa hivyo kila kitu ambacho huzingatiwa na kuhesabiwa kuwa ni katika shiari za Mwenyezi Mungu kukitukuza ni sunna katika Uislaam.

FUAD:
Ndio..lakini vipi itakuwa kujenga juu ya makaburi ya mawalii wa Mwenyezi Mungu ni katika shiari za Mwenyezi Mungu?
JAAFAR:
Shiari ni vitu ambavyo huitukuza dini katika mtizamo wa ulimwengu bila kuwepo dalili juu ya uharamu wake.
FUAD:
Je dini hutukuzwa kwa majengo na makuba hayo?
JAAFAR:
Ndio.
FUAD:
Ki vipi?
JAFAAR:
Kujengea makaburi ya maulamaa na viongozi watukufu wa kiislaam, na kujenga makuba juu yake, na kuyahifadhi yasiharibike na yasibomoke, ni kuwatukuza watukufu hao bila shaka yoyote. Kwa mfano: Akijitokeza mtu fulani na kupanda uwa waridi kwenye kaburi la mtu alie kufa, je mtu huyu haonekani kuwa amemtukuza maiti yule, na kuwa amemuenzi?


FUAD:
Ni sahihi.
JAAFAR:
Vipi ikiwa atajenga juu ya kaburi lake jengo kubwa na kuweka kuba juu yake, hakika kufanya hivyo ni kumtukuza na kumuenzi maiti huyo bila shaka yoyote. Na kuwatukuza viongozi na maulamaa wa kiislaam pia maimamu na mawalii.. ni kuutukuza Uislaam, na kuitukuza na kuienzi dini ambayo watu hawa walikuwa wakiilingania, na wakiwaelekeza watu kwenye dini hiyo. Je mtu fulani anapo mtukuza Raisi wa chama fulani, au walinganiaji wa itikadi za chama hicho huzingatiwa kuwa ni mwenye kukitukuza chama kile na itikadi ile au laa?

FUAD:
Ndio ni kama usemavyo.
JAAFAR:
Kwa hivyo basi kuyajengea makaburi ya mawalii wa Mwenyezi Mungu ni kuwatukuza wao na kumtukuza Mwenyezi Mungu, na ni kuuinua na kuutukuza Uislamm, na kila kitu ambacho kukifanya kutakuwa ni kumtukuza Mwenyezi Mungu na ndani yake kuna kuuinua Uislaam, kitu hicho ni katika shiari za Mwenyezi Mungu ambazo anahimiza kuzifanya, kwani anasema:
( )
Suratul- haji aya 32.
FUAD:
Kwa hivyo..kuvunja na kubomoa makaburi ya mawalii na Mitume na maimam, inakuwa ni kuidhalilisha dini, na kuutia dosari utukufu wa kiislaam.. kwani kuyabomoa ni kuwadharau viongozi wetu, na ni kuwahini wao.. na kuwahini wao ni kuihini dini, na kuutia dosari utukufu wao ni kuutia dosari utukufu wa Uisalaam.


JAAFAR:
Na mimi pia nimekuwa Shia, na nimefuata madhehebu ya Ahlil-bayti (a.s) na nimebadilisha jina kutoka jina la Waliid na kuwa Jaafarkwa sababu hii hii? Kwa hakika mimi wakati nilipo kuwa nikifuata rai za watu wengine sikuwa nikidhania ya kuwa hakuna alie kwenye haki kinyume changu mimi, lakini nimeitafuta haki na kuifuata hadi kuifikia. Na mtu wakati wote anapo acha nyuma na kuzitupilia mbali asabia za madhehebu, na kukifungua kifua chake kwa ajili ya kuikubali haki, na kuitafuta haki.. hapana budi ataifikia haki hiyo na kuipata.


FUAD:
Mimi, na baada ya msimamo na mawkifu haya, nitakuwa makini katika mambo mbali mbali, na nitakuwa ni mwenye kuitafuta haki, mpaka niweze kuifuata haki kokote nitako ikuta. Na kwa hakika nitakushukuru kwa muda wote.. Basi niruhusu nende zangu kwani nina ahadi na mtu fulani.

JAAFAR:
Nenda, Mwenyezi Mungu akulinde.
FUAD:
Fii amani llahi.
JAAFAR:
Uwe katika amani ya Mwenyezi Mungu.

________________________________________

[1]- Mashia kutokana na utambulisho wa maulamaa wa ahli Sunna: Ni wale ambao walimfuata Ali (a.s) pekee na waliitakidi kuwa ndie Imam na Khalifa wa Mtume (s.a.w) kwa Nassi (dalili) na kutokana na Usia wa Mtume (s.a.w), ima usia wa waziwazi au kwa njia ya siri, na wakaitakidi ya kuwa Uimam hautoki nje ya kizazi chake, na ikiwa utatoka basi ni kwa dhulma iliyo fanywa na yule alie uchukua, au kwa kufanya kwake taqiyyah (Rejea kitabu Al-milali wannahli cha Shahristaniy, juzu ya 1\ 147-147 sehemu ya sita). Na neno Shia ni wingi wa neno
( ),
na Shiatur-rajuli yaani ni marafiki zake na wasaidizi na answari wake. Na mwanzoni mwa uislaam lilitumika kwa yule mwenye kumtawalisha Ali na Ahli bayti wake, na hutumika jina hili kwa Mashia halisi katika mukabala wa Masunni, na watu wa karibu wa kila mtu yaani watu wa karibu, na baada ya matumizi yake kuwa mengi likawa ni jina maalum la wafuasi na wenye kumpenda Ali. Na jina la Mashia ni la tangu zamani.


Abu haatam Ar-raziy katika kitabu chake (Az-ziinah) anasema: Kwa hakika jina la kwanza lililo dhihiri katika zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu ni Shia, na jina hili ndilo lililo kuwa jina mashuhuri (Laqab) la masahaba wane nao ni: Abu Dharri Salman Miqdaad na Ammar.

Na Shekh Mohammad Husein Kaashiful-Ghitaa katika kitabu chake kiitwacho (Aslush-shia wa Usuuliha) anasema: Hakika mbegu ya mwanzo ya Ushia iliwekwa na kupandikizwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) tangu zama za mwanzo kuanza kueneza Uislaam bila ya kutofautisha kati ya vitu viwili hivyo na vikiwa sawa.


Na ushahidi ni hadithi zake tukufu si kupitia njia za Mashia na upokezi wa wapokezi wa Kishia Imamiyyah pekee bali ni hadithi za maulamaa wa kisunni na wanazuoni wao na kupitia njia zao wanazo ziamini ambazo hazidhaniwi kuwa zina chembe ya uongo, na katika hadithi hizo ni hadithi iliyo pokelewa na Suyuut katika kitabu chake (Ad-durrul-manthuur fii tafsiri kitabillahi bil-ma'athur) katika kuitafsiri kauli yake Mwenyezi Mungu mtukufu:
( )
(Hao ndio viumbe bora) (suratul bayyinah aya 7). Amesema: Ametoa hadithi Ibn Asakir kutoka kwa Jaabir bin Abdillahi amesema: Tulikuwa kwa Mtume (s.a.w) mara akatokea Ali na kuingia na Mtume (s.a.w) akasema: Nina apa kwa haki ya yule ambae nafsi yangu iko mikononi mwake hakika huyu na wafuasi (Mashia) wake ndio walio faulu na kufuzu siku ya kiama. Na hapo ikatelemka aya isemayo:
( )
(Hakika wale ambao waliamini na kufanya matendo mema hao ndio viumbe bora). (Suratul-bayyinah aya 7). Ibnu Hisham katika Siiratun-nabawiyyah anasema: Hakika umma wa kiarabu uligawanyika katika makundi mawili Masunni na Mashia tangu siku ya Sakifa.

Muhammad Abu Zuhra anasema katika kitabu chake kiitwacho Taarikhul-madhaahibil-islaamiyyah: (Ushia ni madhehebu ya kiislaam ya kisiasa ya tangu muda mrefu na Mashia walidhihiri na madhehbu yao hayo tangu mwishoni mwa zama za Uthuman na kukua na kupata nguvu katika zama za ukhalifa wa Ali, kwani kila alipo pata nafasi ya kuchanganyika na watu walizidi kupendezewa na kuvutiwa kutokana na kipawa chake na kutokana na nguvu ya Imani yake ya dini na elimu yake).


Ibnu Abil-hadiid anasema katika kitabu chake Sharhu Nahjul-balagha: (Hakika Mashia katika zama za dola na utawala wa Muawia walikuwa wakifadhilisha kuitwa Al-kitabiy na wasiitwe Shia. Kwani Ushia anwani yake na shiari yake ni kushikamana na Ahlul-bayti na kufuata elimu yao na kujiepusha na watu wa Bidaa (Uzushi) na kushikamana na kizazi kitwaharifu na kilicho pambika na tabia njema na bora kabisa) (Rejea kitabu Taarikhul-firaqil-islaamiyyah cha Shekh Muhammad Khaliil Az-zayni ukurasa wa 108-109).

Neno Sunnah: Lenye shadda, asili ya neno hilo ni njia, na neno hilo limepanuka maana yake katika makundi tofauti, na linapo tumika huwa lina maana ya aliyo yafanya Mtume (s.a.w) kama kauli vitendo au aliyo yakataza na kuyakemea, na hutumika katika maana hizo kupitia ndimi za wanazuoni na hadithi za Mtume (s.a.w). Na katika zama za hivi karibuni neno Sunnah limekuwa likitumika katika mukabala wa neno Shia, na Husemwa: As-sunnatu wal-jamaah katika mukabala wa watu maalum, na katika ufahamu wa Shekh wa madhehebu ya Hanbali Ibnu Taimiyyah: Neno Sunnah: lina maana ya kumpenda Ali Uthmani na kumtanguliza Abubakar na Omar kwa wawili hao walio tangulia.

Na madhehebu yalipokithiri na makundi kuwa mengi, baadhi wakashikamana na rai isemayo kuwa tamko Sunni lilikuwa likitumika kwa mtu ambae anafuata dini kwa kuwapenda na kuwatawalisha mashekhe wawili, (Abubakar na Omar), na ilikuwa ikisemwa Sunaatul-umariyyh) Rejea kitabu Tariikhul-firaqil-islaamiyyah ukurasa 44-45).