UKWELI WA USHIA
 
WAOKOENI WATU KUTOKANA NA UJINGA UPOTOVU NA DHULMA KAMA IMAM HUSEIN (A.S) ALIVYO WAOKOA [5]MANENO YA MHESHIMIWA AYA TULLAHIL-UDHMAA IMAM SAYYID SWADIQ SHIRAZIY (Mungu amzidishie umri) ALIYO YATOA KWA MNASABA WA KUMBUKUMBU ZA ASHURA SIKU ALIYO UWAWA SHAHIDI SAYYID SHUHADAA IMAM HUSEIN (A.S)
Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma mwenye kurehemu. Sifa zote njema na himidi ni za Mola wa viumbe wote na sala na salam ziwe juu ya Mtume wake alie muaminifu Muhammad (s.a.w) na Aali zake watwaharifu na laana iwe juu ya maadui zao wote. Ama baada, hakika Mwenyezi Mungu alie takasika alitaka kwa kufa shahidi Imam Hussein (a.s) kuweka mazingatio, kilio, ibra na kigezo kizuri, si kwa kizazi kilicho fuatia baada yake pekee, bali hata kwa Mitume na Manabii (a.s) ambao Imam Hussein alikuja baada yao (a.s).


Ama kuhusu mazingatio na kilio, kwa hakika alianza kutekeleza mambo hayo Muumba wa viumbe pale alipo muumba Adam (a.s) kwani Jibrilu alimtajia (a.s) watwaharifu watano ambao ni Muhammad, Ali, Fatima, Hassan, Hussein (a.s) na Adam akamwambia: Nina nini mimi kila ninapo mkumbuka Hussein macho yangu hutokwa na machozi, kisha kuamsha huzuni na majonzi yangu, na Mwenyezi Mungu mtukufu akamuambatanisha pamoja na manabii katika visa vyao kupita kwao katika ardhi tukufu ya Karbalaa na matatizo waliyo kumbana nayo katika ardhi hiyo, na hali hiyo ikaendelea katika muda wote mpaka Imam Hussein aliposema (a.s)
أنا قتيل العبرة لا يذ كرني مؤمن إلا بكي

(Mimi ni muuliwa mwenye Ibra (mazingatio) hanikumbuki muumini yeyote isipokuwa hulia). Ama kuwa kwake ni mazingatio na kigezo, kwa hakika Imam Swadiq (a.s) aliashiria katika ziyara yake aliyo msomea babu yake Hussein (a.s) siku ya kumbukumbu ya Arobaini ya Imam Hussein huku akimzungumzia Mwenyezi Mungu mtukufu kwa kumuashiria Hussein (a.s): Na akajitolea damu yake katika njia yako ili awaokoe waja wako kutoka katika ujinga na utata wa upotovu (njia ya upotovu).


Na waja hapa: Haimaanishi kikundi fulani, au umma fulani, au kizazi fulani. Na Kuokoa: Ni kuashiria kwenye mambo waliyo tihaniwa nayo watu wale. Na bado mtihani huo upo. Kama kutumbukia katika mabalaa ya aina tofauti na mambo ya kila aina ambayo msingi wake ni ujinga na upotovu. Na Kubabaika: Ambako kumewakumba watu wengi katika mwendo mzima wa maisha yao na mwisho wao (yaani akhera yao). Hizi ndio nukta ambazo zinaunda sehemu fulani kati ya malengo ya Imam Hussein (a.s) katika kauli zake na matendo yake katika historia ya Ashura.


Ni uzuri ulioje kwa waumini kila mahala walipo na kila mmoja wao kusimama na kutekekeza jambo hilo la kheri katika nyanja mbali mbali. Na kufanya awezalo kulifanya kama kufanya maandalizi ya kuwafikishia walimwengu wote habari zihusianazo na upande wa kufanya mazingatio na kulia kwa ajili ya Imam, kwa kufanya majlisi ya kumbukumbu za kufa shahidi kwa Imam Husein na kudhihirisha alama na shiari za Imam Hussein ambazo ndio kitu cha kuendeleza na kudhihirisha alama na shiari za Mwenyezi Mungu alie takasika, na kwa hakika Qur'an tukufu amelisifia jambo hili kuwa ni katika uchaji wa Mwenyezi Mungu
(من تقوي القلوب).

Na haya ndio ambayo yaliifanya hali ya kulia kwa mfazaiko kusiko kwa kisheria na kuliko kemewa kisheria katika misiba yote, liwe ni jambo lenye kusifika na kuamrishwa kulifanya na kupewa malipo juu ya jambo hilo ikiwa litafanyika kwa ajili ya Ashura, na katika njia ya bwana wa mashahidi Imam Husein (a.s).


Na haya ndio mazingatio na kilio vitu viwili ambavyo vimekuwa mutawaatir na mashuhuri na kupokelewa kwa wingi kutoka kwa Watu wa nyumba ya utume na ujumbe wa Allah (a.s) hadi macho yao yakapatwa na vidonda, na kuhusiana na hilo Imam Ridhaa (a.s) amesema katika hadithi iliyo pokelewa kutoka kwake na Rayyaan bin Shabiib ya kuwa:
(إن يوم الحسين أقرح جفوننا )

(Hakika siku ya Husein Imeyatia vidonda macho yetu).[6] Na haya ndio yaliyo sababisha kutokwa machozi macho yale matwaharifu ya walii mtukufu wa Mwenyezi Mungu Imam Mahdi mwenye kusubiriwa (rehma za Mwenyezi Mungu zowe juu yake na Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake na faraja yake tukufu) kama ilivyo pokelewa katika ziara ya (An-nahiyatul-muqaddasa):
(ولأبكين عليك بد ل الد موع د ما )
(Na kwa hakika nitakulili damu badala ya machozi). Na kuhusu mazingatio na kigezo, mambo ambayo Imam Husein (a.s) aliyatangaza na kuyadhihirisha mara kadhaa wa kadhaa tangu alipotoka katika mjiwa wa babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu na kuyarudia katika mji mtukufu wa Makka, na katika muda wote alipokuwa njiani akielekea Karbalaa tukufu, na katika Karbalaa, na katika Usiku wa Ashura, na siku ya Ashura, katika hotuba yake barua zake na maneno yake mbali mbali, na kupitia muamala wake katika mwendo huu wa ushindi, na mazingatio yale ni kusimama kidete kwa kufanya juhudi kubwa kwa ajili ya kuwatenga pia kuwaepusha watu wote na ujinga na upotovu.


Na haliwezi kuthibitika hilo isipokuwa kwa kufanya juhudi kubwa na kuwa na ikhlaas kwa ajili ya Mwenyezi Mungu alie takasika. Na kujitolea muhanga kwa kiwango kikubwa na cha hali ya juu katika njia ya kuwaelimisha watu na waja wa Mwenyezi Mungu mtukufu, na kuieneza nuru ya Ahlul bayti (a.s) kila upande na kila mahala na katika kila mji na kijiji, na katika kila nyumba na vibanda vya makuti, na kuifikisha kwa kila mtu wanamume kwa wanamke, mabinti kwa vijana.


Na kutekeleza mfumo na mwenendo wa Imam Husein (a.s) katika kuitumia Ashura kwa ajili ya kuwaokoa waja wa Mwenyezi Mungu mtukufu kutokana na dhuluma na mauaji yaliyopo katika zama hizi, umwagaji wa damu, na kuonekana kuwa ni kikundi kidogo chenye kufuata batili na kuadhibiwa, na kudharauliwa kwa mambo matukufu ambayo watu wengi katika siku hizi wamekuwa wakiyavunjia heshima yake, na hasa hasa waislaam katika sehemu tofauti za Ardhi hii.

Na kwa ajili ya kueneza misingi ya Uislaam na matawi yake. Kupitia vyombo vyote vya habari na tabligh. Katika nyanja mbali mbali za maisha. Na Mwenyezi Mungu ndie mwenye kuombwa msaada awawafikishe wote kupata mazingatio haya na kigezo hiki, na awawafikishe kupata mazingatio pia kutokwa na machozi, nae ndie mwenye kutegemewa.

________________________________________
[1] Moja kati ya hotuba zake aliyo itoa mheshimiwa Swadiq kwa wanafunzi wa Hawzah ya kielimu watokao katika nchi ya India, na alisisitiza katika hutuba hiyo juu ya majukumu wayabebayo katika kuutumikia Uislaam na kueneza itikadi ya Ahlul baiti (a.s) mwaka 1423.
[2]- suratun-nahli aya 96.
[3]- Al-kafiy juzu ya 5 \ mlango wa Ad-dua ilal-islaam kablal-qitaal, ukurasa wa 36 \ hadithi namba 10.
[4]- Ar-rawdhatu minal-kafiy juzu ya 8 \ hadithi ya Rayyaah \ 93 hadithi ya 66.
[5]- Muharramul-haram mwaka 1423 hijiria.
[6] -Buharul-anwaar juzu ya 44\ mlango wa 34\ hadithi ya 17\ ukurasa wa 283.