UKWELI WA USHIA

 
KUENEZA ITIKADI YA USHIA NI FURSA YA THAMANI SANA KATIKA UMRI WA MTU

YAPANGENI VEMA MAMBO YENU NA WALA MSIYAACHE HORERA [1]
Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma mwenye kurehemu. Sifa zote njema zinamstahiki Mola wa viumbe wote na sala na salam ziwe juu ya bwana wetu Muhammad na Aali zake walio watwaharifu, na laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu ya maadui zao wote hadi kitakapo simama kiama.
(Mlivyonavyo vitakwisha na vilivyoko kwa Mwenyeezi Mungu ndivyo vitakavyo bakia) [2]

Aya hii ni miongoni mwa aya nyingi za kitabu kitukufu cha Allah na maana yake ni kuwa kila mlicho nacho ni chenye kutoweka na kumalizika bila shaka yoyote, na yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ni yenye kubakia milele. Kwa hakika katika usiku huu mmetekeleza na kusali sala mbili Maghribi na Isha, na Shekh Tusy (Radhi za Allah ziwe juu yake) alifariki na kuiaga dunia kabla ya zaidi y miaka elfu moja iliyo pita, lakini sehemu fulani ya thawabu za sala ya Magharibi na Isha mlizo zisali na kuzitekeleza ataandikiwa yeye, kwa sababu yeye alikuwa ni sababu ya kusaliwa sala hizi, kwani mas'ala mengi, pia Hadithi nyingi zilizo tufikia sisi zimetufikia kupitia kwake na kutokana na juhudi zake,
Na mwenye kuwaongoza watu kwenye kheri ni kama mfanyaji wa kheri hiyo (katika thawabu)Ni watu wangapi walio fanikiwa kusali katika usiku huu wa leo?! Bila shaka yoyote ni mamilioni kadhaa, sasa angalieni kiasi cha thawabu ambazo atazipata Shekh Swaduq kutokana na sala hizi pekee. Si vibaya kueleza kuwa Marhum Shekh Tusy alikuwa na ndugu ambae alifahamika kwa wema wake na kwamba alikuwa ni mtu alie shikamana na dini vema, lakini ndugu yake huyo hakutuachia athari yoyote, (kumbukumbu yoyote) na wote wawili walikuwa ni watoto wa baba mmoja na wakiishi wakati mmoja, lakini mamilioni haya ya thawabu yanamfikia Shekh Tusy kila siku wakati ambapo ndugu yake hapati thawabu hizo, kwa sababu hakuacha athari wala chembe yeyote katika dunia kama alizo ziacha ndugu yake wa tumbo moja.

Na jaribuni kuangalia (fanyeni Taswawwur) ya kuwa baada ya miaka elfu moja tokea sasa ni nani utajo wake utabakia na nani atasahaulika na kuto kumbukwa kabisa, kwa hivyo basi nyinyi mnaweza hivi sasa kufanya mambo au matendo ambayo yatakuwa ndio sababu ya kubakia utajo wenu na mkawa ni wenye kukumbukwa kwa muda wa maelfu kadhaa ya miaka na mkajipatia thawabu zisizo koma na kumalizika na zenye kuendelea milele na bila kukatika.


Kwa hakika Mwenyezi Mungu alikadiria kuwa nchi ya India ibadilike na yote kugeuka na kuwa nchi ya Kiislaam, (yaani watu wake wote wabadilike na kuwa Waislaam), katika siku za usoni, na vizazi vyote vijavyo visilimu, vizazi vitokanavyo na waabudu masanamu, kama vile wenye kuabudu Ng'ombe, panya na wenye kuabudu jua. Kwa mfano kabla ya miaka mia moja iliyopita nchi ya Iran yote ilikuwa ni nchi ya kikafiri na baada ya miaka mia moja ili badilika yote na wakazi wake wote wakawa ni Waislaam wa madhehebu ya sunni, kisha wananchi wake wakaongoka na wengi wao au asilimia kubwa kati yao hivi leo wakawa ni wafuasi wa Madhehebu ya Ahlul-bayti (a.s), na haya ndio yatakayo tokea katika nchi ya India vilevile, kwa utashi wake Allah.


Na hapa linajitokeza swali moja nalo ni kuwa: Baada ya miaka kadhaa, ni ipi nafasi yenu na dauru lenu katika mabadiliko hayo yatakayo tokea?! Inasemekana kuwa katika nchi ya India kuna zaidi ya watu milioni 600 wenye kuabudu masanamu, sasa ikiwa mmoja wenu atachukua jukumu la kusoma vizuri kitabu kitukufu cha watu wenye kuabudu masanamu kisha baada ya kufanya hivyo akachukua jukumu la kukusanya vijana na mabarobaro ambao ni watoto wa wenye kuabudu masanamu katika nchi ya India na akawafafanulia yaliyomo kwenye kitabu chao kitukufu na akawatolea mihadhara, pia akawakusanya wanafunzi wa vyuo vikuu na walimu, pia wasomi, wabunge, mawaziri na watawala kwa kutumia mantiki ya akili na akasema: Je nyinyi mmekinaika na mafundisho haya yaliyomo kwenye kitabu chenu kitakasifu?!

Na je mnafahamu ya kuwa mambo haya ya kutunga ni sehemu moja wapo ya itikadi yenu ya dini?! Niswadikisheni ya kuwa mmoja wenu anaweza kwa kufanya hivi kuziyumbisha Imani za maelfu miongoni mwao. Nitakutajieni baadhi ya mifano hai kati ya mambo yaliyomo kwenye kitabu chao kitakatifu, na kati ya hayo ni kuwa:Ikiwa mwanamume ataoa mwanamke na baada ya muda mrefu mwanamke yule asifanikiwe kuzaa au asimzalie mtoto na baada ya kuonana na madaktari na kumsisitizia au kumthibitishia ya kuwa mwanamume hana kizazi yaani ni tasa, inajuzu kwa mwanamke yule kulala na ndugu wa kiume wa mumewe ili aweze kupata mtoto mmoja tu na si zaidi, na mtoto yule hunasibishwa na kuambatanishwa na mumewe! Na jambo hili ni lenye kupingwa na nafsi ya kila kiumbe na ghera (wivu) inapinga kitu kama hicho, pia elimu inapinga kitu kama hicho.


Na katika mahala pengine kitabu hicho kitakatifu kina sema: Wakati mwingine hutokea mwanadamu kubadilika na kuwa Mungu kiasi kwamba yeye mwenyewe hahisii hivyo au bila ya yeye kuhisia! Na jambo hili ni jambo la batili na lisilo na maana yoyote kwa kiwango kikubwa.

Hakika kitabu chao hiki kimejawa na mambo ya kutunga na ya batili na ngano zisizo na maana, na anaweza mmoja wenu kuyafuatilia kwa karibu zaidi na kujua idadi yake na kuyaeleza wazi wazi bila kutumia matusi na kejeli. Kwa hivyo basi mas'ala muhimu kabisa katika dunia ni kuwaongoza viumbe, na Mtume (s.a.w) alimwambia Imam Amiril-muuminiin (a.s): Ewe Ali ikiwa Mwenyezi Mungu alie takasika atamuongoza mtu mmoja kupitia kwako ni bora kwako (ni kheri kwako) kuliko vitu vyote vichomozewavyo na jua (vipatavyo mwanga wa jua).[3]


Na ninakunukulieni kisa kingine, Imepokelewa katika moja wapo kati ya kitabu cha historia nacho ni (Atharul-bilaad wa Akhbaarul-ibaad) ya kuwa mtawala mmoja wa kisunni aliekuwa akitawala Iran alitengeneza muhuri wa chuma na akachonga kwenye muhuri huo Ibara hii (Abubakar wa Omar) na alikuwa akiwaonea na kuwadhulumu Mashia na akiwatawala kwa mabavu pia alikuwa akiwapiga muhuri huo kwenye mapaji ya nyuso zao baada ya kuuchemsha kwa moto, na kitabu hicho kinasimulia ya kuwa baadhi ya Mashia ambao walipigwa mhuri huo kwenye mapaji ya nyuso zao walikuwa hawatoki majumbani mwao kwa muda wote wa maisha yao na hawakutoka wala kuyahama majumba yao kutokana na aibu ya ibara hiyo kwa ndugu zao waumini ambao ni Mashia, na wakihofia masunni wasijekoge kupitia kwao.

Hebu jaribuni kuangalia na kuifikiria hali na mazingira magumu kama hayo wakati huo, lakini pamoja na yote hayo na mazingira hayo magumu na maonevu kama hayo, ugumu wa mazingira kama huu wa hali ya juu, Mashia walikuwa wakisindikiza majeneza ya masunni, hadi hivi leo Iran ikawa ni yenye itikadi ya Ushia, kwani mateso na maonevu yale hayakuwazuia kutekeleza majukumu yao bali waliendelea na juhudi za kuwaongoza waja na likathibiti na kuwa lile walilo litaka.


Na hapana shaka ya kuwa nyinyi nyote mmesikia jina la Allamah Al-majlisiy, kwa hakika alikuwa ni mwanazuoni mkubwa, na baba yake alikuwa ni miongoni mwa maulamaa wakubwa pia, na katika kizazi chake Allamah Al-majlisiy ambae tangu kufariki kwake hadi sasa kumepita miaka 300 walijitokeza wanazuoni na maulamaa wengi na marajiut- taqlidi na waandishi wa vitabu wakubwa na watoa mawaidha kwa watu, illa tunakuta kuwa babu wa juu kabisa wa Allamah alikuwa ni mfuasi wa madhehebu ya sunni, na vijana wa kishia wa Isfahani waliweza kumkinaisha na yeye kuamua kujiunga na madhehebu ya Shia, pamoja na kuwa zama zile zilikuwa na taasubi kubwa kabisa ya kimadhehebu, lakini ukweli ni kuwa vijana wale walikuwa na hima ya hali ya juu na wakaweza kuwafanya mashia vijana wengine wa kisunni. Nanyi ni juu yenu kufanya kama walivyo fanya waumini na wapigana jihadi hao, na ni wajibu juu yenu kwa ajili ya kulifikia na kulithibitisha lengo hilo au malengo hayo, kwanza kabisa mjifunze vema na muwe ni miongoni mwa maulamaa wakubwa ili muweze kufanya mahojiano na majadiliano na kuwakinaisha.


Na sikilizeni kisa hiki ambacho kilitokea kabla ya miaka arobaini iliyo pita. Wakati huo tulikuwa Karbalaa, jarida moja la wakati huo liliandika ya kuwa mwanazuini mmoja wa kisunni amekuwa Shia, na walipo muuliza kwa nini umebadilisha madhehebu yako? Akasema: Nimebadilisha kwa sababu ya herufi moja kati ya herufi za jarri iliyotajwa katika Qur'an tukufu! Wakamuuliza ni herufi ipi hiyo?


Akawajibu: Hakika mimi nimesoma Qur'ani mara nyingi sana na mara ya mwisho suratul-fatiha ikanifanya nisite na kusimama katika aya ya mwisho ya sura hiyo, na nilipo anza kusoma suratu (Inna fatahnaa laka fathan mubiinaa) hadi nikafika mwisho wa surat (Muhammad rasulullah walladhina maahu.) na ambayo inamaanisha maswahaba wa Mtume rehma na amani ziwe juu yake, na kuona ya kuwa sura inawazungumzia maswahaba wa Mtume na imewataja mara kumi kwa swigha ya jam'u (mfumo wa wingi) au kwa dhamiri za wingi ambazo dhamiri hizo zinawakusudia wao, lakini sura hiyo inapozungumzia ya kuwa malipo na jazaa zao walizo ahidiwa kuwa ni pepo na msamaha na malipo makubwa inasema:
( )
(Mwenyezi Mungu amewaahidi wale ambao wameamini na wakafanya amali njema miongoni mwao)


Kwa hivyo basi herufi ya (Mim) inamaana ya (Baadhi), na herufi hii ilinifanya nifikirie na kujiuliza: Kwa nini Maswahaba wote hawaingii peponi kama tulivyo fundishwa?

Nikajisemea moyoni mwangu: Niwajibu niende na kufanya utafiti na udadisi kuhusu suala hili, na jambo hilo likanipa picha ya kuwa inawezekana suala hili likawa ni miongoni mwa mifumo ya Qur'an, lakini mimi nimeiona aya hii na kuikuta ikiwa wazi kabisa kwani herufi hiyo inamaana ya (Baadhi) ya (Maswahaba) na (sio wote) laa sivyo hakika Qur'an imewataja wote katika aya nyingi tofauti na katika aya hii, kwa hivyo nadharia ya uadilifu wa Maswahaba ikiwa imetenguka kwangu, na utafiti wangu ukanifikisha katika natija hii ya kuwa hawa (Baadhi) ya walio tajwa ni wafuasi wa Ali bin Abi Twalib (a.s) na wale walio shikamana na wilaya (utawala) yake na kutokana na utafiti huo nikawa Shia.


Kwa hivyo basi ni juu yenu kuyaandaa vema mambo yenu, na fanyeni juhudi kubwa na wala msipoteze fursa hii ya umri wenu, na someni vizuri na mtwalii sana (someni sana vitabu mbali mbali) mpaka muwe ni miongoni mwa watu wenye elimu, kwani watu wa batili hawana elimu na kila walicho nacho ni njozi za mashetani.

Imam Swaadiq (a.s) amesema: Ni juu yako kuwa na vijana (wenye umri mdogo) hakika wao ni wepesi sana kuelekea kwenye kila la kheri .[4]
Na Al-ahdaath walo tajwa kwenye hadithi ni kizazi kipya, kwani vijana bado akili zao hazija oshwa, na wao ni wepesi zaidi katika kufanya kheri kuliko wengine. Kwa hivyo fanyeni harakati na nashati ili India na ulimwengu wote wawe ni Mashia watupu..insha allah.