MOTO NA PEPO

 
NAFSI YA KUKARIPIA - LAUMU (al-Nafs al- Lawwama).

Inawezekana wakati mwingine kuwa hivyo kwa vyovyote vile na kiasi chochote kile cha madhambi ayafanyayo, mtu hajisikii chochote cha kutenda kosa, wala hasikitiki, wala hajilaumu mwenyewe. Nafsi kama hiyo ni ile iliyoshindikana. Hata hivyo, ile nafsi baada ya kuanguka na kutenda madhambi na itajikaripia yenyewe na kujishutumu yenyewe, kabla ya yeyote yule kufanya hivyo, basi imeingia katika sharti tukufu mojawapo la nafsi itakiwavyo kuwa. Qur'ani Tukufu inatuelezea:
"Naapa kwa siku ya Kiama. Tena naapa kwa nafsi inayojilaumu; (kuwa mtafufuliwa na mtalipwa)". (75:1-2).
Ni dhahiri kuwa iwapo Mwenyezi Mungu akiapia kwa vitu, basi kuna utukufu wake humo. Nayo pia ni wazi kuwa yeyote yule aifunzae nafsi yake vyema hadi ule wakati wa kutenda madhambi, yenyewe (nafsi) hujaa masikitiko na kujilaumu, basi imefikia mojawapo ya vina vya utakatifu.

NAFSI ILIYOFUNGULIWA HERI (al-Nafs al-Mulham):

Sharti lingine la nafsi ni kuongozwa na Mungu. Twaambiwa kaika Qur'ani:
" Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake" (91:8)
Maongozi haya ni kutia moyo kwa nafsi wakati itapokuwa katika hali ya kutakasika- 'Nafsi halisi si' ambayo tumeishaizumgumzia. Ni lazima iwapo nafsi itaelekezwa kwa mujibu wa madhambi basi muongozo na kufunguliwa kwa heri kutoka kwa Allah (swt) yatafikia kikomo chake.
Kwa kupingana na sifa na masharti ya nafsi ambazo ni sababu ya furaha ya milele na utakatifu, baadhi ambazo zimekwisha tajwa hapo awali, pia hapo hapo kuna sifa na masharti yanayosababisha maovu ya nafsi, sasa tuziangalie.

NAFSI YENYE MADHAMBI (al-Nafs al-Athima):

Iwapo roho au nafsi ya mtu ikiwa na tabia ya kutenda madhambi, basi huitwa yeye madhambi. Qur'ani inazungumzia kulipa kwa amana:
"Na atakaeficha basi hakika moyo moyo wake ni wenye kuingia
dhambini."(2:283)
Hii inathibitisha kuwa nafsi ya yeyote yule ambaye ameshajizoelesha madhambi ni nzito na ni wazi na tayari kwa kutenda madhambi wakati wowote ule.

NAFSI ILIYO SINZIA (al-Nafsal-Ghafil)

Sababu mojawapo ya kushidwa na kufifia kwa nafsi ni kulegea au kusinzia au kuwa zembe. Kwa kutenda mambo maovu na kwa kuendelea kutenda madhambi ndiko kunakosababisha nafsi kuelekea palipo paovu na kutomsikia Allah (swt). Anaelezea Mwenyezi Mungu katika Qur'ani Tukufu
"Wala usiwatii wale ambao tumezighafilisha nyoyo zao wakafuata
matamanio yao..." (18:28)

NAFSI ZILIZOTIWA MUHURI (al-Nafs al- Matbu)

Hapa inamaanisha kufungwa muhuri juu yake na hivyo ndivyo hatua ya mwisho ya kungwa, inatuambia:
"Na watakaokuwa na uzani khafifu, basi hao ndio waliozitia hasarani nafsi zao kwasababu ya kuzifanyia ujeuri Aya zetu."
Popote pale mtu anapokuwa fidhuli au juvi kuelekea Allhah (swt) hadi kudharau na kutokubali ujumbe wake na maamrisho ya Allah ambayo Mwenyezi Mungu ambazo amewekea mbele yake, au , iwapo yeye atazikubalia, anazipa umuhimu kidogo na kuwa na kosa la upinzani basi hapo moyo wake unaingia katika hatua ile ambayo ni sawa na kama tahadhari, maamrisho Matukufu na yale yaliyo haramishwa hayatakuwa na athali yoyote ile kwake yeye. Na hii ni hatua mojawapo ya kudidimiza kwa nafsi na kushindwa kwake.

NAFSI ILIYO POFUKA ( al-Nafs al- Amya):

Hali nyingine ya Nafsi ni kupofuka. Qur'ani inatuambia kuwa:
"Kwa hakika macho hayapofuki, lakini nyonyo ambazo zimo vifuani ndizo zinapofuka. (22:46)
Nyoyo hizi zinaona vingine mbali na Allah (swt) na hazimwoni Mwenyezi Mungu. Nyoyo za aina hizi huona yale tu yatakayo yenyewe bila ya kuyazingatia yale maamrisho ya Allah (swt) na kwa hakika ndizo zilivyo kama vile vimepofuka tu.

NAFSI YENYE MARADHI (al-Nafs al-Maridha):

"Nyoyoni mwao mna maradhi, na Mwenyezi Mungu amewazidishia maradhi."(2:10)
Ugonjwa wa aina hii inawezekana kuonekana mioyoni mwetu kwa sababu ya yale madhambi tuyafanyayo sisi siku hadi siku. Kama vile mtu mgojwa huwa hana hamu ya vyakula wala madawa ambavyo ni vyenye manufaa kwake na vile vile vyakula vizuri havitakuwa na ladha yoyote kwake, ndivyo vivyo hivyo kuhusu NAFSI iliyougua, kwani inapatikana kuonywa ( na Mwenyezi Mungu) na kukaribia kwa upole kwa mapendo na matakwa yake ya humu ulimwenguni na akhera kuwa yenye adhabu kali sana na yenye kutisha mno. Kilicho zaidi ni kwamba mtu aliyeugua hivyo ni yule mwenye, kuipendelea kwa ajili ya nafsi yake yale yote yaliyo mabaya na maovu, kwani huwa avutiwa navyo kama kambwa ndivyo vyenye kumfaa yeye. Kwa hakika hii ndiyo ile nafsi ilikwisha ugua; kama vile ilivyo kifo kwa mtu hatakayetibiwa magonjwa yake na hivyo ndivyo vinaweza kutokea kwa ajili ya aina hii ya nafsi iwapo haitoweza kutibiwa kabla ya ugonjwa kuenea pote na hatimaye mtu aweza kuangamia.
Popote pale mtu aonapo kuwa yeye hatamani chochote kile atakiwacho kukifanya yaani kumkumbuka Mwenyezi Mungu katika sala na kutii Sheria Tukufu za Dini ambazo hazimfai na ambazo ni chungu kwake, kwa hivyo ni wazi kabisa kuwa atambua kuwa huo moyo wake umeshaanza kuugua maradhi, na bila ya kisita inambidi afanye kila hila awezayo ili ajielekeze kwa mujibu wa aya za Qur'rani Tukufu, kwa watawa na walio waumini halisi na wale walio hodari katika elimu na ujuzi huu: waganga waa moyo, i.e.., wanavyuoni waelewao na wafuatao mienendo ya Mtume Mtukufu (s.a.w.w.), ili waweze kuitibu nafsi ya aina hiyo iliyopatwa na maradhi.

NAFSI INAYOKWENDA UPANDE (al-Nafs al-Za'igha):

Moyo au Nafsi pia inaweza kusemwa kuwa inakwenda upande au inapotoka. Aina hii ya Nafsi ni ile ichaguayo upotofu wakati ipatiwapo chaguo katika hali mbili ya wema na uovu.
Kama mategemeo yote ya maisha, katika sehemu zote za Imani, maadili na matendo, mambo yake yote yaliyo dhahiri na yale yote yaliyo batili mwake, mwanadamu daima anakubwa na mgawanyiko wa njia mbili mbele yake , mtu ambaye amefaulu na kufurahika ni yule ambaye daima anachagua njia ile aitakayo Mwenyezi Mungu. I.e njia iliyo nyooka (Sirat al-Mustaqeem) ya dini katika kila hali. Hata hivyo, mtu ambaye moyo wake unampotosha, huwa daima ndiye achanguaye njia ya upotofu
Katika Qur'ani, kuzungumzia mifano na mafumbo ya aya na kwa kuelezea wazi wazi, Mwenyezi Mungu anatuambia:
"Wale ambao nyoyoni mwao mna upotofu wanafuata zile zinazobabaisha kwa kutaka kuwaharibu watu kutaka na kujua hakika yake vipi........"(3:7)
Hivi kwa kuchagua mfano (mutashabih au allegorical) wa aya za Qur'ani ili kuitumia Qur'ani kwa kuhakikisha matakwa ya mtu binafsi ni sampuli ya ile nafsi iliyopotoka.

NAFSI YA MOYO MGUMU (al-Nafs al-Qasiya)

Sharti lingine la nafsi kuwa hivyo ni kutokana na moyo mgumu na katili.
"...........Na tukazifanye nyoyo zao kuwa ngumu" (5:13)
"...........Kwa hivi nyoyo zao zikiwa ngumu" (57:16)
Hali kama hii inaelezewa katika aya zinginezo pia. Nyoyo kama hizi zina sifa kama zile za jiwe na chuma, kuwa hakuna chochote kile kiwezacho kuathiri au kuacha alama yoyote juu yake ila kwa mshindo mkali tu moto. Hadi kufikia hali ya moyo kuwa mgumu kiasi hiki ni dhahiri ikionekana vile maovu yalivyo mteka huyo mtu hadi akawa mtumwa wa matakwa na maovu yake. Kwa hakika imepotoka!

NAFSI WASIWASI (al-Nafs al-Murtaba):

Nafsi ya aina hii imo katika hali hii ya wasiwasi kuhusu vile vitu iipasavyo kuvijua na kuviamini. Shaka kuhusu mizizi ya dini ya Islam kama vile kushuka kuwapo kwa Allah (swt), akhera, Unabuwa na vile vile Uimamu (a.s.), na kushuku matawi ya Dini kama vile sala, saumu na mema na mengineyo mengi.
"Nyoyo zao zina shaka; kwahivyo wanasitasita kwa ajili ya shaka yao." (9:45)
Hii ni mojawapo ya sababu ya upotofu wa Nafsi na ni fardhi kwa watu wale walio katika hali kama hii kujielekeza hadi aya za Quarani na hadithi Tufuku za Mtume (s.a.w.w.) na ma -Imam (a.s.) na kwa wanavyuoni wa dini ili kuweza kutokomeza hali hii kabla ya kutanda juu ya Nafsi nzima undani mwake. Ama sivyo, iwapo hali kama hii haitashughulikiwa na badala yake ikapuuzwa na kubakia Nafsini, basi itamwelekeza mtu katika hali ya kukatiza na kukataliwa (kupuuzwa na kudhoofika).

>
NAFSI ILIYOPATA KUTU (al-Nafs-al-Ra'ina):

'KUTU' ni shida nyingineyo ambayo nafsi inaweza kupatwa kwani ni sawa na ule mfano wa kioo cha kujitazamia, iwapo ile poda itabanduka basi hutaweza kujitamazama kiooni. Basi kioo cha moyo ambavyo ni sehemu ya umuhimu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu utukufu wa ukamilifu wake, fadhila zake zitamorudishwa kwake, hazitoweza rudishwa iwepo itashika kutu, na hatimaye itaweza kupoteza ile nguvu ya kupeleka ujumbe wako kwa Mwenyezi Mungu.
Ingawaje mwanadamu hawezi kumtazama Mwenyezi Mungu kwa macho yake, lakini anao uwezo wa kumwona Mwenyezi Mungu, Utukufu wake na Ukuu wake kwa kupitia NURU iliyomo katika Nafsi yake. Nafsi ile ambayo imeshakwisha shikwa na kutu ambamo sasa hakuna uwezo wa kurudishia (reflect ) kutoka na kwa Mwenyezi Mungu, basi bila shaka itatapatapa huko na huko ikimtafuta sheitani na hasa kwa mujibu wa matilaba yake. Qurani ikiwa inatumbusha kuwa:
"Sivyo hivyo! Bali yametia juu ya nyoyo zao (maovu) waliokuwa wakiyachuma." (83:14)
Katika 'aya hii twaelezewa vyema kabisa kuwa chanzo cha kupatwa kwa kutu kwa Nafsi ni kule kutenda madhambi. Kwa hivyo kila dhambi itatupia uzito (itatanda kiza juu ya moyo; na ifikiapo hali kama hii, inambidi mtu afanye Tawba mara moja kwa ajili ya kuyasafisha hayo matendo maovu na atende matendo mema ili kuzuia kupotea kwa nuru iliyotunukiwa Nafsi yake. Vile vile, twaambiwa katika hadithi Tukufu kuwa: "Mtu mwenye furaha kuu katika siku ya Kiama ni yule atakaye yaona maneno aliyokuwa akiyatamka 'naomba msamaha wa Mwenyezi Mungu' chini ya kila dhambi alilolitenda. Kwa Hivyo inambidi kila Mwislam mmoja wetu apige msasa kila ovu alilolitenda ama sivyo, Mwenyezi Mungu azitowazo onyo zake za upole zitabadilika na kuwa ghadhabu kubwa sana.

NAFSI AMURU (al-Nafs al- Ammara):

Nafsi isiyofunzwa hasa wakati wa ujana wa mtu, huamuru kutendwa kwa matnedo ya madhambi bila kiasi. Katika Qurani, kuhusu kisa cha Mtume Yussuf, Nafsi inasemwa:
"Nami sijitasi Nafsi yangu; kwa hakika (kila) Nafsi ni yenye kuamrisha sana maovu (12:53)
Sentensi hiyo inaonyesha kuwa ilitamkwa na Zuleikha aliyekuwa amependa Nabii Yussuf. Pale alipotoa ushahidi, alithibitisha kuwa ndiye chanzo cha uovu huo. Kwani Yussuf alikuwa hayupo wakati huo wa ushahid, lakini kwa kuwa Zuleikha alikuwa hana hila yoyote ile zidi ya Yussuf. Pia kuna uwezekano kuwa hayo yametamkwa na Yussuf au ni wote vyovyote vile, Qur'an inatuambia kuwa "Nafsi ni yenye kuamrisha sana maovu. (12:53)
Nafsi yoyote ile isiyokuwa imeongozwa kwa mujibu wa mfano ya Islam, huwa daima inavutwa popote pale penye madhambi na ma'asiyah kwani yote hayo yako yamedhalilishwa kabisa. Mfano wa Nafsi hii ni sawa na mtoto mchanga atakaye kila kitu kuchezea bila kutazama ubora wake, faida au hasara zake, iliramdi yeye apate kuchezea tu, Nafsi ya yule aliye na utamaduni mzuri, aliyekomaa na kubaleghe inavutika pale penye mema na hujiepusha na matilaba yake; na ile nafsi elimishwa na inavutika pale penye maovu ya kila aina na kwa hivyo lazima ifunzwe vyema, itasaidia kutakasisha hiyo Nafsi.
HATIMAYE: Kile kilichoelezwa hapo kinasema kuwa Nafsi inaweza kuwa bora kabisa ama mbovu kabisa au vinazidiana katika vina na ngazi. Kuna nafsi zifikiapo kuitwa 'Nafsi halisi na 'Nafsi ridhika' n.k. na vile vile kuna zinapofifia hadi kufikia hali mbaya kabisa na matokeo yake ni majanga, majonzi na maovu na kufikia ile sifa ya "kupigwa mihuri" au 'zilizopofuka' na 'zenye maradhi' zikiwa ni kama mifano.
Hali hii inadhihiridha kuwa Nafsi zinapangwa na kila mtu anayo Nafsi moja tu.

JE UMEJING'AMUA UNA NAFSI YA AINA GANI UNDANI MWAKO??


(JITAHADHARISHE)!


3. DHULUMA ZA AINA TATU


Makala haya yametarjumiwa na:
Amiraly M.H.Datoo P.O.Box 838 Bukoba - Tanzania
Amesema al-Imam Muhammad al-Baquir a.s. : Al-Kafi, j. 2, uk.330
"Zipo aina tatu za dhuluma: "Aina ya kwanza ni ile ambayo Allah swt anatoa msamaha na ya pili ni ile ambayo haitolei msamaha na aina ya tatu ni ile ambayo yeye haipuuzi."
Ama dhuluma ambayo anaisamehe ni ile ambayo mtu huitenda baina yake binafsi na Allah swt. Na dhuluma ambayo Allah swt haisamehe ni kukufuru na dhuluma ambayo haipuuzii ni ile ambayo inatendewa dhidi ya haki za watu."
Ufafanuzi:
Aina ya tatu ya dhuluma ni ile ambayo mtu hukiuka na kuvunja haki za watu. Njia saheli ya kutaka kusamehewa ni kwanza kumridhisha yule ambaye haki zake zimekiukwa na kuvunjwa. Iwapo mtu huyo atamsamehe yule aliyemvunjia haki zake, basi hapo dhuluma hiyo itageuka kuwa dhuluma dhidi yake binafsi. Na hapo ndipo ataweza kuwa mstahiki wa kuomba msamaha wa Allah swt.

4. MAKUNDI MANNE YA WATU

Imenakiliwa kutoka Jaafer ibn Muhammad naye kutokea Baba, naye kutokea kwa Babu yake naye kutokea kwa Imam Ali ibn Abi Talib a.s. kwamba Mtume s.a.w.w. alisema katika wasia wake.
Alisema Mtume s.a.w.w. " Ewe Ali ! Kuna makundi manne ambamo watu wanapatikana wamegawanyika kwa mujibu wa matendo yao humu duniani.[3]
A. Kupanda daraja
1. Kutawadha wudhuu katika baridi
Kwa hakika ni jambo gumu mno kuamka na kujiweka tayari kwa ajili ya ibada za Allah swt hasa kama utakuwapo kazita sehemu ambazo kuna baridi kali ambapo hata kunakuwa na hatari ya watu wengine kuathirika kwa baridi kali. Wakati huyo unakuwa ndio wakati mzuri wa kujipatia usingizi mnono na nguvu za Shaitani zinakuwa zikitushawishi sisi tutoe visingizio mbalimbali ili mradi tusiamke na kufanya ibada za sala hususan za Alfajiri.
2. Kusubiri sala baada ya sala .
Mumin wa kweli kwa hakika anakuwa akiusubiri wakati wa sala kuwadia kwa ajili ya kutaka kusali sala kwa mara nyingine. Fursa hii anaisubiri kwa hamu kwa sababu anapata fursa kwa mara nyingine kumwabudu na kumshukuru Allah swt na ni wakati mwema kwa ajili ya kuomba Tawba ya madhambi yake na vile vile ni wakati mwingine wa kujipatia neema na baraka za Allah swt. Kwa kifupi mumin huyoo amabye anausubiri wakati wa sala uwadie anakuwa na hamu ya kujipatia bahati ya kuweza kujiweka mbele ya Allah swt.
Tukiangalia mfano wa kidunia, iwapo mimi nitaambiwa kuwa nimepewa kibali cha kumzuru Raisi wa nchi yetu nyakati fulani fulani kwa siku. Hivyo mimi baada ya kumzuru mara ya kwanza kwa siku, nitakuwa na hamu na shauku ya kuwadia kwa muda wa mara pili na hivyo hivyo kwa mara zote. Kwa hakika nitaiona saa ikienda pole pole mno.
Na hivyo ndivyo inavyokuwa hali ya Mumin kwa ajili ya kutaka kuwa mbele ya Allah swt kwa nyakati angalau mara tano kwa siku.
3. Kutembea usiku na mchana kwa miguu kuelekea Jamaa'
Mumin kwa hakika daima hupenda kujumuika pamoja na jama'a yake katika mambo yote ya jumuiya yake na sala za jama'a .
Mtume s.a.w.w. amesema:
"Kwa hakika Allah swt hawakutanishi Ummah wangu katika upotofu, na mkono Wake uko pamoja na Ummah huo, kwa hakika atakayejitoa humo basi atambue kuwa amejitoa kwa ajili ya Jahannamů." Mizan al - Hikmah.
B. Kaffarah ya madhambi.
1. Kutoa na kupokea salaam kwa unyenyekevu.
Mumin huwa daima mwepesi wa kutoa salaam na kujibu salaam anazotolewa. Kamwe hawi mtu mwenye dharau wala kutegea kutolewa salaam au mwenye kiburi.
Allah swt anatuambia katika Quran kuwa tutolewapo salaamu ni faradhi kuijibu ama kwa kurejea salaam hiyo hiyo au kuijibu kwa ubora zaidi.
Mtume s.a.w.w. alikuwa akiviziwa na ma Sahaba wake kwa kujificha kiasi kwamba wapate fursa ya kutangulia kutoa salaam kwa sababu Mtume s.a.w.w. alikuwa ndiyo daima mtu wa kutoa salaa kwa mara ya kwanza. Sasa sisi tunayo kiburi cha nini ? Kwa hakika Allah swt anatuambia kuwa Salaam ni kauli itokayo Kwake.
2. Kuwalisha chakula wale wanaohitaji.
Mumin kwa hakika huwa na moyo wa huruma kiasi kwamba hawezi kula peke yake huku watu wengine wakiwa katika hali ya kubakia katika njaa. Na si hayo tu bali huwa na moyo wa kutaka kuwasaidia binadamu wenzake katika kila hali awezayo yeye.
Yeye huwa karimu na kamwe hawi bakhili ambaye yeye mwenyewe hula bila ya kuwapa wenzake.
3. Kusali sala za Tahajjud ( salat al - Layl au usiku wa manane ).
Mumin huwa anasali sala za usiku wa manane (Tahajjud ) wakati ambapo watu wanapokuwa wamelala usingizi mnono. Na husali kwa kutaka ridhaa ya Allah swt na wala si kwa kujionyesha kwa watu.
Kwa hakika sala hii huwa ikisaliwa na Mitume a.s. na Ma-Imamu a.s. kila siku bila ya kukosa. Hii ni ibada ambayo mtu huwa anamnyenyekea Allah swt wakati ambapo anakuwa ametulia kiroho na kiakili. Huwa hana mawazo au mambo yanayomsumbua huku na huko. Hivyo inamaanisha kuwa ibada hii inafanyika kwa roho khalisi na mtu hukubaliwa ibada zake haraka zaidi katika sala hizi.
Imam Hussain a.s. siku ya Aashura alimwusia dada yake Bi. Zainab binti Ali ibn Albi Talib a.s. kuwa : "Ewe dada yangu Zainab ! Naomba usinisahau katika sala zako za usiku i.e. Salat al-Layl."
C. Waangamio
1. Tabia mbovu
Wale watu wote wanaoingia katika kikundi hiki cha wenye tabia mbovu kwa hakika mwisho hao hujikuta kuwa wameangamia na kupoteza maisha yao. Yaani maji yameshakwisha mwagiga hayazoeleki tena. Tabia kama hizi zinamwigiza katika upotofu na kiburi na kujiona kuwa wao ndio watu waliostaarabika lakini kumbe ni kinyume na hali hiyo kwani Allah swt hawapendi wale wanaojifakharisha na kutakabari.
2. Kutii nafsi zao
Iwapo mtu ataitii nafsi yake katika kumpotosha basi atakuwa kwa hakika amepotoka na kuangamia humu duniani na Aakhera kwa pamoja.
Amesema Mtume Mtukufu s.a.w.w.: "Yeyote yule atakayeitambua nafsi yake (mwenyewe) basi hakika amemtambua Allah swt."
Vile vile amesema kuwa : " Kwa hakika hodari kabisa ni yule ambaye ameighalibu nafsi yake." Yaani nafsi yake haimpotoshi katika mambo mengi mno kama vile ulafi, uchoyo, ubakhili, uasherati, ukafiri, maasi n.k.
Iwapo mtu atatawaliwa na nafsi yake basi atakuwa mtumwa wa nafsi yake.
Msomaji anaombwa kusoma makala niliyoyatoa katika Sauti ya Bilal , P.O.Box 20033 DSM juu ya maudhui Maadili ya Kiislamu - sura izungumziayo juu ya sifa 18 za nafsi,Juzuu XXXI, Na. 5, Rabiul Aakhar 1418, Septemba 1997. (Iliyochapwa katika sehemu mbili.)
3. Kujifakharisha
Kwa hakika mtu anapoambukizwa ugonjwa huu basi atambue kuwa ameangamia humu duniani na Aakhera kwa pamoja. Mtu anapenda kujionyesha kuwa yeye ndiye mtu bora zaidi kuliko wengine kwa sababu ya kupata kwa mali zaidi au ilimu au wadhifa. Vitu vyote hivi ambavyo sisi tunavijua kuwa ni vyote vyeneye kuangamia na kupotea na tutaviacha humu humu duniani.
Mtu katika sura hizi anaanza kukufuru kwani anaanza kuwasema na kuwaona watu wenzake kama wanyama na waovu kiasi cha kuthubutu kusema ati wanamsumbua na kumpotezea wakati wake. Inambidi yeye kutambua kuwa Allah swt amemwingiza katika mtihani hivyo inambidi afanye mema ili aweze kufuzu.
D. Uokovu
1. Hofu ya Allah swt katika hali ya dhahiri na batini
Iwapo mtu atataka kupata uokovu inambidi awe na khofu ya Allah swt wakati akiwa peke yake na vile vile anapokuwa mbele ya watu. Isiwe kwamba mtu anapokuwa peke yake anaruhusiwa kufanya madhambi na wakati anapokuwa mbele ya watu kujionyesha kuwa ni mtu ambaye ana khofu ya Allah swt kupita watu wengine. Kutenda madhambi katika hali yoyote yanayo adhabu kali.
2. Kusudio madhubuti katika umasikini na utajiri
Mtu inambidi awe na makusudio yake madhubuti bila ya kuyumbishwa katika hali ya umasikini na utajiri pia. Kwa sababu anapokuwa na moyo wa kuwasaidia watu wenzake katika ufukara asiupoteze katika hali awapo tajiri. Iwapo alikuwa msalihina awapo katika ufukara basi aendelee vile vile kwani asije akatoa kisingizio cha kukosa wakati katika utajiri na biashara zake.
Vile vile mtu anapokuwa katika umasikini inambidi awe madhubuti katika imani yake ili asije akakufuru na kushuku uadilifu wa Allah swt kwa shida azipatazo maishani mwake. Kila mtu anakumbana na misukosuko mbalimbali humu duniani hivyo inambidi kuimarisha imani yake.Huo pia huwa ni wakati wa mtihani kutoka kwa Allah swt, na inambidi ajaribu kufuzu.
3. Uadilifu katika shida na raha
Inambidi mtu awe daima katika mizani ya kauli yake asije akatamka maneno ambayo yatamkufurisha wakati anapokuwa katika shida au raha. Anapokuwa katika shida asije akasema kuwa Allah swt amemtupa au hamjali wala hazisikii duaa zake (Allah swt atuepushe na wakati huo) na pale anapokuwa katika utajiri na starehe asije akakufuru kuwa yeye hana shida ya kitu chochote au mtu yeyote kwani anacho kile anachokihitaji, hivyo kujifanya maghururi na mwenye takabbur. Kwa hakika Allah swt hawapendi watu kama hawa.
Kwa wale walio matajiri inawabidi wafanye mambo mema kwa kutoa misaada kwa misikiti,madrasa masikini na mahala pote pale penye kupata ridhaa za Allah swt na wale walio masikini na mafukara inawabidi wakinai kwa kile walichonacho na wamshukuru Allah swt kwa kile anachowajaalia.
Maneno yetu yawe yamepimwa vyema kabla ya kuyatamka kwani isije tukasema mambo ambayo yatatufanya sisi tuwe mustahiki wa adhabu za Allah swt. Na wala tusiwaseme watu vibaya kwani na hayo pia yatatufanya sisi tuwe mustahiki wa Adhabu za Allah swt.
Hadith hii imesomwa na Sheikh Akmal Hussain kutoka Moshi, Tanzania.
Hadith hii imeshereshwa na: Amiraly M.H.Datoo 8th May 1998

Sehenu ya 2. Marejeo kuhusu Jannat na Jahannam

1. Qur'ani Tukufu
Jannat 11:35, 3:112, 3:113, 10:15, 10:13, 3:111, 10:14, 9:354, 14:119, 15:205, 17:315, 18;375, 18:129, 19:9, 19:123, 19:124, 19:137, 20:218, 20:213, 20:399, 14:83, 14:83, 14:84, 4:18, 4:20, 8:117, 8:123
Maana ya Jahiim j 5 uk. 256;
Jahannam : 11:20, 1:294, 14:357, 15:204, 17:232, 12:178, 18:130, 18:383, 19:141, 20:7, 20:412, 20:438, 8:350, 8:351, 8:352, 8:113, 8:114, 8:115, 20:9
(Namba inayotangulia ni ya Juzuu na inayofuata ni nambari za ukurasa.)
(Marejeo haya ni ya Al-Mizan fi tafsiril Qur'an, zipo juzuu 20. Chapa ya Intesharat Bayan, Teheran, Nasir khosru, Teheran. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran)
2. Nahjul Balagha
Hotuba: 16; 27; 28; 64; 66; 79; 83; 157; 171; 167; 160; 75; 109; 106; 119; 120; 124; 128; 12; 144; 152; 156; 193; 176; 165; 183; 192; 191; 193; 199;
Msemo: 199;
Barua: 17; 27; 31; 28; 41; 76;
Wasia: 24
Misemo ya hekima: 31; 368; 228; 349; 387; 429; 456; 131; 42
(Marejeo haya ni ya Chapa ya Sub-hi Salehe, Beirut. Libanon)
3.Sahifa-i-Sajjadiyah

NDOTO YA Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.

Siku moja Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliingia Msikitini na kuwaambia Ma-Sahaba, "Je niwasimulieni ndoto niliyoiota ?"
Ayah za Qur'an Tukufu zizungumziazo Jannat
Makala haya yemkusanywa na kutarjumiwa na
Amiraly M.H.Datoo - Bukoba Tanzania
Utaratibu ufuatao umetumika kuandika Surah na Ayah za Qur'an Tukufu : 5 : 119 hii ikimaanisha kuwa katika Surah ya 5 ya Qur'an Tukufu Ayah ya 119.
No. Maudhui inayozungumzwa Sura namba na Ayah namba
1 Afya bora katika Jannat 19 : 62
2 Ahadi na Jannat 25 : 16
3 Allah swt na Wakazi wa Jannat 35 : 34, 36 : 58
4 Amani ya Wakazi wa Jannat 52 : 20
5 Bahati za Wakazi wa Jannat 52 : 25
6 Baraka za Jannat 2:25, 2:36, 10:10, 15:46, 16:31, 22:23, 22:24, 25:10, 43:71, 43:73, 47:12, 47:15, 52:17, 52:18, 52:19, 52:22, 55:48, 55:50, 56:23, 56:33, 56:37, 57:12, 69:23, 69:24, 76:20, 76:22, 77:43, 82:13, 85:11, 87:8
7 Batili katika Jannat 19 : 62
8 Bi. Hawa katika Jannat 7:19, 7:20, 7:22
9 Bustani ya Jannat 13:23, 15:45, 16:31, 47:15, 61:12, 65:11, 66:8, 76:14, 85:11,98:7
10 Chakula cha Wakazi wa Jannat 8 : 74
11 Chakula cha watu wa Jannat 56:21
12 Chemichemi ya Tasnim katika Jannat 83:27, 83:28
13 Chemichemi za Jannat 15:45, 44:52,55:50, 76:17, 88:12
14 Daraja za Jannat 17:21, 46:19, 55:62
15 Familia ya Wakazi wa Jannat 52 : 21
16 Furaha ya Wakazi a Jannat 7:43, 88:9, 101:1
17 Furaha katika Jannat 37 : 58
18 Furaha za Wakazi wa Jannat 37 : 45
19 Habari njema za Jannat 50 : 35
20 Hali za Jannat 35:35, 76:29
21 Hariri iliyofumwa ya Jannat 76:21
22 Heshima katika Jannat 37 ; 42, 39 : 73
23 Heshima ya Wakazi wa Jannat 36 : 56
24 Hotuba za Wakazi wa Jannat 88 : 11
25 Hour al-'Ayn katika Jannat 37 : 48
26 Huruma za Wakazi wa Jannat 44:53, 56:16
27 Huzuni katika Jannat 35:34, 35:35, 36:48
28 Imani katika Jannat 36:55
29 Jannat katika maisha baada ya hapa ulimwenguni 2 : 25
30 Jannat kwa ajili ya wema 35: 33
31 Jannat Mlezi 37 : 42
32 Jannat na maisha ya baada ya hapa ulimwenguni 3 : 133
33 Jannat na wacha-mungu 50 : 31
34 Jannat ya wacha mungu 3 : 133
35 Jannat ya Wacha mungu 13:35
36 Jannat ya Wacha-mungu 38 : 49
37 Jinn katika Jannat 55:46
38 Kauli njema za wakazi wa Jannat 56 : 25
39 Kazi katika Jannat 36 : 55
40 Kinywaji cha Wakazi wa Jannat 37:45
41 Kitulizo cha Wakazi wa Jannat 18 : 31
42 Kituo cha karibu katika Jannat 83:28
43 Kuchekeshana kwa Wakazi wa Jannat 52:23
44 Kuelekea Jannat 5:119, 9:89
45 Kuingia katika Jannat 2:214, 3:185, 4:13,15:45, 15:46, 18:31, 1963, 36:26, 40:8
46 Kuishi katika Jannat 14:23, 15:47, 15:48, 76:16
47 Kuishi kifahari katika Jannat 35:34
48 Kuisifu Jannat 25 : 76
49 Kujamiiana katika Jannat 37 : 42
50 Kujamiiana kwa Wakazi wa Jannat 15 : 47
51 Kunyimwa kwa Jannat 5:72, 7:40, 38:77, 70:39
52 Kuridhika katika Jannat 92 : 21
53 Kuwastarehesha Wakazi wa Jannat 3 : 198
54 Lungilungi ( ua) la Jannat 56 : 28
55 Maamkiano katika Jannat 14:23, 19:62, 33:44, 36:58
56 Maamkizi ya Watu wa Jannat 13:23, 13:24, 14:23, 15:46, 56:26
57 Mafundisho ya Wakazi wa Jannat 7:43, 56:25, 78:35
58 Mahala ilipo Jannat 53 : 15
59 Mahala pa kupumzikia kwa ajili ya Wakazi wa Jannat 25 : 24
60 Maisha ya Wakazi wa Jannat 7 : 49
61 Majadiliano katika Jannat 37 : 54
62 Majeruhi katika Jannat 36 : 58
63 Makazi katika Jannat 9 : 72, 10 : 9
64 Makazi ya Jahannam na Jannat 7 : 50
65 Makazi ya Jannat na Jahannam 7 : 44, 7:54
66 Malaika wa Jannat 39 : 73
67 Malazi ya Wakazi wa Jannat 55:54
68 Malezi katika Jannat 36:57, 37:42
69 Malezi ya Wakazi wa Jannat 19 : 62
70 Malipo ya Jannat 2:25, 9:89, 9:11
71 Maneno katika Jannat 22:24
72 Manukato ya Jannat 83:26
73 Mapambo ya Wakazi wa Jannat 18 : 31
74 Mapenzi na usawa miongoni mwa Wakazi wa Jannat 10:23, 21:102, 21:103, 35:35, 50:34, 50:35, 52:23, 52:25, 55:54, 55:76, 56:12, 56:15, 56:20, 56:28, 56:31, 76:41, 88:15, 88:16
75 Mapokezi katika Jannat 25:75
76 Masharti ya Jannat 25 : 16
77 Mashujaa wa Imani katika Jannat 9:21, 9:98, 61:12
78 Matembezi katika Jannat 39 : 73
79 Matunda ya Jannat 44:55, 47:15, 55:52, 55:54, 55:68, 56:20, 56:28, 56:32, 69:23, 76:14
80 Mavazi ya Jannat 76 : 21
81 Mavazi ya Wakazi wa Jannat 18:31, 22:23, 44:53
82 Mazulia ya Jannat 88 : 16
83 Mazungumzo na Wakazi wa Jannat 37 : 50
84 Mazungumzo ya kipuuzi katika Jannat 19 : 62
85 Mikusanyiko katika Jannat 15 : 47
86 Miti ya Jannat 3:198, 4:57, 56:28, 56:29
87 Mito ya Jannat 88 : 15
88 Mito ya Jannat 2:25, 3:198, 4:57, 5:119, 7:43, 9:72, 9:89, 9:100,10:9, 58:22, 61:12, 65:11, 66:8, 98:7
89 Mtume Adam a.s. katika Jannat 2:35, 2:36, 7:19, 7:20, 7:22, 20:118
90 Mtume katika Jannat 9 : 89
91 Mwanamwali mzuri wa Jannat kwa ajili Wacha-mungu 38 : 49
92 Mwito kuelekea Jannat 2: 221
93 Neema za Wakazi wa Jannat 52:22, 52:23, 77:43
94 Ombi katika Jannat 36:57, 41:31, 44:55
95 Sababu za Jannat 19: 60, 57:21, 58:11, 58:22, 61:12, 66:8, 76:6, 76:12, 85:11
96 Shughuli za Wakazi wa Jannat 26:55, 83:25
97 Shukurani za Wakazi wa Jannat 7:43, 10:10, 35:35
98 Sifa kwa ajili ya Jannat 3:136, 3:142, 5:65, 14:23, 20:75, 25:15, 25:75
99 Starehe za Wakazi wa Jannat 36:56, 36:57, 52:18, 87:8, 89:26
100 Starehe za Wakazi wa Jannat 7:43, 15:47
101 Starehe za Wakazi wa Jannat 35:33, 36 :56, 37:58
102 Starehe zilizopo katika Jannat 37:42, 27:45, 37:48, 39:32
103 Tafrija za Wakazi wa Jannat 56 : 16
104 Uchovu katika Jannat 15:48, 35:35
105 Udugu wa Wakazi wa Jannat 10 : 10
106 Ufalme wa Jannat 18:31, 52:20, 55:76, 56:15, 83:35, 88:13
107 Uhalisi wa Wakazi wa Jannat 7 : 43
108 Uhuru katika Jannat 39:73
109 Uhuru wa Wakazi wa Jannat 56:33
110 Ukaribisho kwa Wakazi wa Jannat 50 : 34
111 Ukarimu wa Wakazi wa Jannat 37:42
112 Ukuu wa Wakazi wa Jannat 41 : 40
113 Ukweli katika Jannat 5 : 119
114 Ukweli wa Jannat 39 : 32
115 Ukweli wa Wakazi wa Jannat 15 : 47
116 Umilele katika Jannat 2:25, 2:82, 3:136, 3:198, 4:13, 4:57, 4:122, 5:85, 18:3, 19:61, 25:16, 25:76, 35:35, 37:58, 39:73
117 Umilele wa Jannat 43:71, 4:73, 44:56, 47:15, 48:5, 50:34, 56:33, 57:12, 64:9, 65:11, 76:11, 76:19, 98:8
118 Urafiki wa Wakazi wa Jannat 52:25
119 Uroho wa Jannat 70 : 36
120 Usahihi wa Wakazi wa Jannat 15 : 46
121 Usalama wa Wakazi wa Jannat 50:34, 52:18
122 Usalama wa Wakazi wa Jannat 15:46
123 Ushindani kwa ajili ya Jannat 3 : 133
124 Usumbufu katika Jannat 35 : 35
125 Utajiri wa Jannat 55 : 64
126 Utayari wa Jannat 3 : 133
127 Uthamini wa Jannat 9:89, 9:100, 13:24, 20:76, 44:57, 57:21
128 Utofauti katika Jannat 17:21
129 Uuwezo wa Jannat 12 3 : 133
130 Uwastani wa Jannat 76:13
131 Uwingi wa Jannat 55 : 62
132 Uzoefu wa Wakazi wa Jannat 44:53, 56:16
133 Vijana wa Wakazi wa Jannat 56: 17
134 Vinywaji vya Jannat 47:15, 56:18, 56:19, 76:16, 76:17, 83:26, 83:27, 88:14
135 Vito vya thamani katika Jannat 22:23, 35:33, 76:21
136 Vitu vya fahari vya Wakazi wa Jannat 7 : 50
137 Vyakula vya Jannat 83 : 26
138 Vyakula vya Jannat 7:50, 43:71, 47:15
139 Wafanya 'ibada katika Jannat 3:136, 16:31, 19:85, 38:49, 39:73, 44:55, 44:55, 47:15, 50:35, 52:17, 52:18, 52:19, 52:20, 52:21,54:54, 54:55, 78:32, 78:37
140 Wahamiaji katika Jannat 9:21, 9:22, 22:59
141 Wahudumu kwa ajili ya Wakazi wa Jannat 52:24, 76:15
142 Wahudumu wa Jannat 52:24, 56:17, 76:19
143 Wakazi wa Jannat katika Jannat 22 : 24
144 Wakazi wa Jannat katika Jannat 22 : 24
145 Wakazi wa Jannat na Hour al-'Ayn 37 : 48
146 Wakazi wa Jannat na marafiki zao 37 : 54
147 Wakazi wa Jannat na Wake zao 36 : 56
148 Walio okoka katika Jannat 76:6, 83:23, 88:10
149 Wanawake wa Jannat 56:36
150 Warithi wa Jannat 23 : 10
151 Washika Vikombe wa Jannat 76:15, 76:16, 83:23
152 Watenda mema katika Jannat 11:23
153 Watenda Usahihi katika Jannat 3:198, 10:9, 76:5, 77:44, 82:13, 83:23, 83:24
154 Watu wa Jannat 7:40, 7:43, 7:49, 25:15
155 Watu wa Vitabu na Jannat 2 : 111
156 Waumini katika Jannat 7:49, 9:22, 9:72, 9:100, 10:9, 11:23, 30:15, 40:81, 41:31, 43:70,48:5, 56:39, 57:12, 61:12, 64:9, 69:24, 70:35,76:22, 85:11, 98:8
157 Zawadi za Wakazi wa Jannat 18 : 3

________________________________________
[1] Nipo ninakitayarisha kitabu juu ya maudhui haya.
[2] Iwapo utapenda kusoma habari zaidi juu ya maudhui haya ya Tawbah, jipatie kitabu nilichokitafsiri cha Syed Dastaghib Sirazi
kinachozungumzia ka marefu na mapana kuhusu somo hili.
[3] Ninajaribu kutoa maelezo machache ili kuwezesha kueleweka vizuri ili nawe msomaji uweze kuchangia mawazo na kuweza kupanua ilimu yako. Hata hivyo itawabidi kufanya utafiti zaidi ili kujua mafhum ya usia huu vizuri zaidi.