MOTO NA PEPO

 
3. ADHABU ZA KABURINI

Sisi sote tunatambua kuwa kuwa kutakuwa na adhabu katika makaburi kwa ajili ya kila mmoja ikiwa ni Mwislamu au asiye Mwislamu. Lakini kunatofauti katika adhabu hizo baina ya makundi hayo mawili ya watu kwani makafiri, wanafiki na wasio wasio Waislamu itakuwa zaidi kuliko Waislamu. Lakini kuna baadhi ya Waislamu ambao wao wenyewe humu duniani wanapuuzia baadhi ya mambo na hivyo katika kituo cha kwanza cha safari ya Aakhera na ambacho ndicho baada ya dunia, watakumbana na magumu na mazito.
1. Sababu za adhabu za Kaburini
Ninapenda kuwaleteeni Hadith ya kwanza kutoka Bihar al-Anwar, J.6, uk. 222 inayomnakili Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s.
1 Kuchonganisha na kufitinisha
"Kwa hakika adhabu ya kaburi ni kali mno kwa yule mtu ambaye ni mchonganishi(mambo na maneno ya hapa anayapeleka huko na ya kule anayaleta huku na kufitinisha )
2. Kutojiepusha na vilivyo Najis
Sisi tunapuuzia mno na hatutilii muhimu Najis iwe katika katika hali yoyote ile kwa mafano mkojo, mavi ,damu na vitu vingi mno vinajulikana.
3. Kutowawia wema wananyumba yake
Mara nyingi tunaona kuwa mtu anakuwa mchungu na mkali kwa familia yake na hata wengine huwadhulumu wake na watoto wake na kuwaonea na kuwanyanyasa. Na hii ndiyo sababu moja kubwa ya adhabu kali za kaburini. Hivyo inambidi mtu awe mwema na mpole na mwenye mapenzi kwa mke na watoto wake na inambidi kuwalinda na kuwatimizia mahitaji yao na kuwalinda.
Sa'ad ibn Ma'adh alikuwa ni Sahabah wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na alikuwa mwzuri sana na kwamba sanda na mazishi yake yalikuwa yamesimamiwa na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. mwenyewe na hata kuteremka katika kaburi lake aliteremka Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na vile Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema kuwa Malaika wengi mno walikuwa wameshiriki katika mazishi yake.
Mama yake alipopata habari hizo, alisema kuwa Allah swt amjaalie Jannat na kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alijibu, "Bila shaka ! Lakini atakuwa na adhabu kali mno kaburini !" Kwa kusikia hayo Masahaba waliuliza, "Je itawezekanaje hivyo wakati bwana Sa'ad alikuwa ni mja na Sahaba mwema ?" Kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliwajibu, "Naam, alikuwa ni mtu mwema lakini alikuwa mkali kwa mke wake, na hivyo atapata adhabu kali humo kaburini." Bihar al-Anwar, J.6, uk. 220
4. Kuteketeza na kufuja Neema za Allah swt
Yaani kutokutumia yema na ipasavyo neema za Allah swt alizomjaalia mwanadamu ziwe katika hali ya siha yake, watoto au mali. Ama mali ni kule kutumia kupita kiasi kinachohitajika au kutumia visivyo muhimu.
5. Kunkatalia mume kujamiiiana
Kunawahi kutokea mara nyingi miongoni mwa watu kuwa mume anapohitaji kujamiiana na mke wake, mke humyima mume wake tendo hilo la kutimiza haja yake. Kwa hapa mwanamke kama huyu ndiye anatishio kubwa la adhabu kali za kaburini.
6. Kupuuzia na kudharau Sala
Sisi tunatabia ya kupuuzia na kuidharau Sala tano za siku na zinginenezo zilizofaradhishwa. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. , "Yeyote yule anayeipuuzia Sala, si miongoni mwetu." Na vile vile amesema, "Mtu kama huyo hatapata nusura yetu Siku ya Qiyama."
Vile vile Al-Imam Musa al-Kadhim a.s. amesema kuwa baba yake mzazi Al-Imam Ja'afar as-Sadiq a.s. amesema, "Wakati wake wa mwisho, alimwambia kuwa 'mtu yeyote anayeipuuzia Sala basi hatapata nusura zetu Siku ya Qiyama.'"
7. Kuwatetea wadhulumiwa
Mara nyingi tunaona kuwa wadhalimu wanawadhulumu watu wengine na sisi katika hali kama hiyo tukibakia kimya bila ya kujaribu kuwatetea hao wanaodhulumiwa, basi hivyo ndivyo itakuwa ndivyo sababu yetu ya kuadhibiwa kaburini.
8. Kuwasengenya watu wengine
Siku hizi tumekuwa na tabia moja ya kujiburudisha na yo ni kuandaa mabaraza ya kukaa na kuwakejeli na kuwasengenya watu, kuchimbua aibu zao na kuongezea chumvi na pilipili katika maneno yetu ili kunogesha hadithi zetu. Tunasahau kuwa kufanya hivi sisi tunamharibia jina na sifa za mtu ambaye labda hakuyafanya hayo.


2. Sababu za kupunguzwa kwa adhabu za Kaburini
Kama vile tulivyokwisha kuona kuwa zipo sababu zinazosababisha adhabu za kaburini basi tusife moyo kuwa hakuna njia ya kupunguzwa au kuwa hafifu. La, si hivyo, daima zipo sababu za kupunguziwa adhabu hizo za kaburini na vile vile hali yetu ikawa njema zaidi humo kaburini.
1. Sala za Tahajjudi au Salatil Layl
Inambidi mtu asali sala raka'a nane za salatil Layl na raka'a mbili za shufa'a na raka'a moja ya witri ambamo katika qunuti yake kunasomwa Astagh firullah wa atubu Ilaihi mara sabini. Basi zipo Ahadith zinazosadikiwa hususan kutokea kwa Al-Imam 'Ali ar-Ridha a.s. katika Safinatul Bihar,J.2, Uk.397 maudhui Kuhusu Kaburi kwamba : "Iwapo mja anasali raka'a nane za salatil Layl na raka'a mbili za shufa'a na raka'a moja ya witri ambamo katika qunuti yake kunasomwa Astagh firullah wa atubu Ilaihi mara sabini, basi hatakosa faida zake kama zifuatazo, atakuwa amepona fishar-i-kabr na ataepukana na Moto wa Jahannam , umri wake utakuwa mrefu, Allah swt ataongezea baraka katika riziqi yake."
2. Kutekeleza Rukuu na Sujuda kwa usahihi katika Sala
Kwa mtu ambaye anasali sala zake vile ipasavyo, basi hatakuwa na sababu ya kujibiringita kama kwamba anafanya mazoezi ya mwili, kumbe masikini anasali. Tunawaona wengi sana wakisali lakini kwa mbio kama kwamba wanashindana na katika hali kama hii hata usomaji na matamshi pia hayawezi kamwe kuwa sahihi. Tunasali ilimradi tu tumesali, sasa sala hiyo inamaana yoyote mbele ya Allah swt ?
3. Kusali Sala zilizo Sunnah na kutoa Sadaqah
Tunasisitizwa mno kutimiza Sala zilizofaradhishwa na vile vile tupate muda wa kusali zilizo Sunnah na vile vile kusoma Dua kidogo na vyote hivyo kwa unyenyekevu na kwa moyo uliotulia. Sambamba na hayo tutoe sadaqah kuwasaidi masikini ambavyo kuna faida kwa pande zote mbili.
4. Kusali Sala ya Wahshat
Anapokufa Mumiin basi inatubidi kusali sala hiyo usiku wa kwanza kuzikwa kwake kwani inamsaidia maiti huyo na vile vile iwapo tutawasalia wengine basi Allah swt atatujaalia watu wa kutusalia pale tutakapokufa ili nasi tufaidike na thawabu hizo ambazo zitatupunguzia adahabu zetu,
5. Kwenda Makkah kwa ajili ya Kuhiji
Inatubidi sisi katika maisha yetu kwa mara moja kwenda Kuhiji, lakini kwa kutimiza masharti ya amri hiyo. Na tuwe na moyo kwa ajili ya hivyo. Wapo watu wengi ambao wanapuuzia swala hili ambalo ni faradhi kwao.
6. Kifo katika usiku wa kuamkia Ijumaa au siku ya Ijumaa
Iwapo mtu atabahatika kufa katika usiku wa kuamkia Ijumaa au siku yenyewe ya Ijumaa, basi adhabu za kaburini zitapungua. Sisi hatutambui fadhila na Baraka za usiku huu na siku ya Ijumaa katika maisha yetu. Lau mtu atafanya utafiti kujua zaidi basi atashangaa kusikia au kusoma fadhila na baraka zake.
7. Jariratain
Wakati wa kumzika maiti huwekewa matawi mawili yalio mabichi. Inasemekana kuwa mtu huyo hatakuwa na adhabu za kaburi kwa kipidi cha kubakia ubichi ka matawi hayo.
8. Kumwagia maji juu ya kaburi
Ipo riwaya kuwa kwa kumwagia maji juu ya kaburi kutamfanya mtu huyo aliyezikwa humo asipate adhabu za kaburini hadi hapo kutapokauka maji juu ya kaburi hilo.
9. Kusomwa kwa Surah maalum za Qur'an Tukufu
Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema kuwa , "Mtu yeyote atakayesoma Surah Al-Hakumu Takathurů atapona adhabu za kaburi." Na vile vile Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema kuwa "Yeyote atakayeisoma Surah al-Nisaa kila siku ya Ijumaa basi huyo atapona adhabu za kaburi ." Safinat al-Bihar, J.2, Uk. 397
Na Al-Imam Ja'afar as-Sadiq a.s. amesema kuwa ,"Mtu yeyote atakayesoma Surah al- Qalam, hatapata adhabu za kaburini." Na vile vile iwapo atasma Sura Zukhruf au kusomwa kwa Sura al-Ya-Sin (ambayo inajulikana kama ndiyo moyo wa Qur'an Tukufu ) ama wakati wa magharibi au usiku kabla ya kulala, hatapata adhabu za kaburi."
Vile vile kusomwa kwa Ayah za mwisho katika Surah al-Baqarah, kutamwepusha na adhabu za kaburi, Ayah zenyewe ni :
Rabbana la tuakhidhna in nasina au akhta'ana. Rabbana wala tuhamilna 'alayna isran kama hamaltahu 'alal ladhina min qablina Rabbana wala tuhammilna ma la taqatalana bihi wa'afu 'anna waghfirlana warhamna anta Mawlana fansurna 'alal qawmil kafiriin.
10. Kuuawa katika njia ya Allah swt
Iwapo mtu atafariki akiwa katika njia ya Allah swt kama katika vita , basi mtu huyo hana adhabu ya kaburi. Na hivyo ndivyoamesema Allah swt katika Qur'an Tukufu, Surah Ali-Imran , Ayah 169 - 170 yaani ni kwamba wale wanaouawa katika njia ya Allah swt si watu waliokufa bali ni mashahidi na wapo hai.
11. Kumsalia Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na Ahlul Bayt a.s.
Na kwa kumsalia Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. pamoja Ahl ul-Bayti a.s. kwa wingi kutamwepusha mtu na adhabu za kaburini.
Vile vile ipo katika riwaya kuwa mtu yeyote aanzaye dua yake kwa Bismillahir Rahmanir Rahiim na Salawati (Allahumma Salli 'ala Muhammadin wa Ale (ahali) Muhammad ) na kumalizia kwa Salawati, basi kamwe dua yake hiyo haitarudishwa kwani salawati inakubaliwa na Allah swt. Sasa itawezekanaje mwanzo wa dua na mwisho wa dua vikakubaliwa na vya katikati vikatupiliwa mbali ?
12. Mapenzi ya Ahlul Bayt a.s.
Tunaelewa waziwazi vile fadhila za Ahlul Bayt a.s. zilivyo na vile Allah swt pamoja Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. walivyokuwa wakiwasifu hao na kutufaradhishia mapenzi yao juu yetu na hata kama salaikisaliwa bila ya kusomwa kwa salawati ndani yake basi sala hiyo itakuwa batili.
Kuwapenda Ahlul Bayt a.s. ni kuwapenda wafuasi na marafiki zao na kuwachukia na kuwalaani maadui wao. Je itawezekanaje adui wa kiongozi na mpenzi wako akawa rafiki yako ?
13. Mwanamke kufanyia subira umasikini na shida za mume wake
Kwa hakika katika maisha yetu haya ya duniani kuna mambo mengi mno ambayo yanajitokeza katika maisha ya ndoa. Kuna wakati ambapo mume huwa ni masikini, hivyo inambidi mwanamke aumke kufanya subira na kustahimili shida zinazojitokeza na kumpata hima bwana wake ili sivunjike moyo bali aendelee na jitihada zake za kuondokana na umasikini. Vile vile kunawezekana kwa mume kuwa mtu mwovu ambaye hana matendo mema kama mlevi, mgomvi n.k. Katika sura zote hizo na zinginezo, inambidi mwanamke afanye subira na kujaribu kustahimili katika mazingira hayo, na wla si kuamua kumpa talaka mume au kutoroka nyumbani. (Ingawaje talaka ni neema mojawapo ya Allah swt, hivyo isitumie vibaya ).
14. Kusoma Ziyarah ya Imam Hussein a.s.
Imesisitizwa kuzuru kaburi la Imam Hussein a.s. usiku wa kuamkia Ijumaa na kusoma Ziyarah. Kwa hakika sisi tukiwa mbali mno, huwa tunasoma Ziyarah ambavyo kwa hakika kutatuepusha na adhabu za kaburi.
15. Kuzikwa Najaf
Iwapo mtu atazikwa katika maeneo yanayozunguka kaburi la Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. huko Najaf, basi hatakuwa na adhabu za kaburi.
16. Kuwasaidia masikini na wasiojiweza
Kwa kutoa misaada kwa ajili ya kuwasaidia masikini na wasiojiweza na wale wanaohitaji misaada, kwa hakika kutamwepusha mtu na adhabu za kaburi. Inawezekana mtu akatoa hivyo katika uhai wake kwa ajili ya kupata thawabu yeye mwenyewe au akatoa kwa niaba ya wale waliokwisha fariki dunia hii, basi thatwabu hizo zitawafikia hao marehemu.
Siku moja alifariki mtu mmoja katika zama za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ambaye alikuwa tajiri mno. Aliacha wusia kuwa mali zote zilizokuwa zimejaa mabohari yake zigawiwe sadaqah kwa masikini, baada ya kifo chake. Kwa hivyo, kwa mujibu wa wusia wake, baada ya kifo chake, mabohari yalianzwa kugawia vyakula kwa masikini. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alikuwepo hapo na mwishoni wakati wanapitisha ufagio, waliokota kipande cha tende moja, na kwa kuiondoa hiyo, Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alisema, "Lau huyu mtu angalikuwa ametoa angalau hata kama mbegu moja kama hii ya tende katika uhai wake, basi mbegu moja ya tende ungali kuwa na thawabu ya mlima wa Abu Qobays (mlima mkubwa mno)."
Makala mchanganyiko
1. SABABU ZINAZOFANYA NYOYO KUFA

Makala haya yametarjumiwa na kushereheshwa na:
Amiraly M.H.Datoo P.O.Box 838 Bukoba - Tanzania
Hadithi hii ilisomwa na : Sheikh Akmal Hussein Taheri - Bukoba
Al - Imam Ja'afer as-Sadiq a.s amesema kuwa Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema kuwa mambo manne husababisha nyoyo za watu kufa ambazo ni:
1.Kutenda dhambi baada ya nyingine
Mwanadamu anapoanza kutenda madhambi nafsi yake inamzuia na kumtolea lawama ili asitende maovu. Lakini pindi anapoanza kukaribia madhambi, roho yake inaanza kuzoea na ile hali ya kujilaumu inaanza kupungua nguvu na hivyo ndivyo anavyojizoeza na hatimaye anahisi kuwa ni jambo la kawaida wakati wa kutenda dhambi. Kwa hivyo anatenda ovu moja na kuendelea kuyatenda mengine mengi bila ya kuhisi kuwa na dhambi na hata unafika wakati ambapo hajisikii vema hadi hapo anapokuwa ametenda madahmbi. Kwa kutoa mifano, ipo mifano mingi mno mbele yetu zilizo bayana. Mtu mmoja anapokaribia kunywa pombe, atakataa kata kata, lakini utaona akibembelezwa na kushurutishwa na marafiki zake walio waovu wenye kuwa ajaribu kidogo, na akishajaribu kidogo watamlazimisha anywe zaidi na zaidi. Na hali hii itakapoendelea bele hivi hivi, utaona mtu huyo ndiye wa kwanza kuagiza pombe na vile vile atakuwa akijiwekea nyumbani mwake. Heshima zote atakuwa amezipoteza na maovu yote yatakuwa yametundikwa shingomi mwake kwani atapoteza fedha, ataharibu siha yake, atawatukana wazazi, kaka, ndugu, majamaa na hata kuthubutu kuwapiga mke na watoto wake. Kwa kifupi familia nzima itakuwa imetumbukizwa katika janga kubwa. Huyu pamoja na pombe ataongezea dhambi lingine la kuwatafuta malaya na kuvuta bangi na madawa ya kulevya. Haya ndiyo maangamizo makubwa kabisa.
Allah swt amewaamrisha Malaika kuwa: Mtu anaponuia kutenda jambo jema wamwamdikie thawabu. Na anapoanza kutembea katika kulifanya tendo jema basi hapo pia anaongezewa thawabu nyingi na pale anapolianza kutenda tendo jema basi huongezewa zaidi ya hayo na anapomaliza kulitenda tendo jema basi hapo analipwa thawabu nyingi mno zisizo na hisabu.
Lakini mtu anaponuia kutenda dhambi basi hapo haandikiwi adhabu, na anajitoa kwenda kutenda dhambi napo pia haandikiwi kwa sababu inawezekana akarudia njiani na anapolianza tendo ovu pia kuna uwezekano wa kutolikamilisha na kwa masikitiko makubwa, anapolikamilisha basi kwa huruma zake Allah swt, huandikiwa dhambi moja tu.
2. Kuongea zaidi pamoja na wanawake
Islam haitukatazi kuongea na wanawake wasio wake zetu lakini kinachokatazwa ni ile hali ya watu kuongea mambo ambayo yanapita mipaka na huku ndiko kunapoanza kuteketea maadili. Utawasikia watu wakizungumza pamoja na wanawake mambo ambayo hayana heshima na kufanyiana dhihaka na hatimaye wanapozoeana katika tabia hii utakuta wanaanza maneno ya kudalilisha kuwa wanapendana na wanahamu ya kuingiliana, na haya ndiyo yanayo tokea. Bwana Daud alimwusia mwanae kuwa ajiepushe na mazungumzo pamoja na wanawake kwani mwanamme anapokutana na mwanamke, katikati yao huwa yupo Sheitani kwa ajili ya kuleta madhambi.
Uislamu unamtaka mwanamke abakie katika hadhi na heshima aliyopewa na Allah swt. Hivyo mwanamke anapoongea na mwanamme inambidi asitoe sauti nyororo yenye kuvutia bali inambidi atoe sauti ambayo haitamfurahisha mwanamme na hivyo asitamani kuongea tena na mwanamke huyo. Na kwa misingi hii, mwanamme hatakiwi kumtolea salaam mwanamke ili asije akaisikia sauti yake. Lakini dunia hii imebadilika, leo katika maredio na televisheni utawaona wanawake hata wanasoma Qur'an kwa sauti za kuvutia.
Vile vile tusisahau kuwa kuwadokozea macho wanawake pia ni dhambi. Zipo zinaa za macho na midomo.
3. Kuzozana pamoja na mwehu
Yeye atasema na wewe utasema bila ya kufikia maelewano baina yenu. Mutazozana kwa muda mrefu wakati ambapo watu watakaokuwa wakiwaona hawatajua tofauti baina yenu. Mwishoni hamtafikia jambo la kheri.
Hao ni watu ambao hawaongei katika mipaka ya ilimu, dini na adabu.
4. Kukaa pamoja na watu waliokufa
Kwa kukaa na kufanya mazoea ya urafiki pamoja na watu waliopotoka, kutatufanya na sisi pia tupotee na kutumbukia katika ujeuri, majivuno na takaburi mambo ambayo Allah swt hayapendi na anyachukia na kuyaadhibu. Qur'an inatuambia kuwa nyoyo zao zina magonjwa na Allah swt anawaongezea magonjwa baada ya magonjwa kwa kutokana na maovu yao yanavyoongezeka.
Kwa hayo Waislamu walimwulizaa Mtume s.a.w.w. Je ni wakina nani waliokufa? Mtume s.a.w.w. aliwajibu Kwa waliokufa wanamaanishwa wale matajiri wenye takabburi na majivuno. Urafiki pamoja na watu kama hawa utakufanya wewe uwe na tamaa ya dunia na kujipatia mali ufahari na majivuno. Hao wanachokithamini ni kile kinachowaletea faida wao tu. Dharau majivuno ndiyo mavazi yao.
Hapa kuna aina nne ya watu: (1). Wale wanaokula na kuwalisha wengine (2) Wale wanaokula na kuwanyima wengine (3) Wale hawali wenyewe na wala hawawapi wengine wale (4) Wale wanaowanyan'ganya wengine ili wale peke yao.
Nasiha: Inatubidi sisi tujiepushe na mambo yote ambayo Allah swt hapendezewi na tufuate Hadithi na Sunna za Mtume s.a.w.w. pamoja na Maimamu 12 a.s. na vile vile tufanye tawba kwa yale tuliyokwisha ya tenda katika hali ya ujahili wetu na kamwe tusirudie kuyatenda. Allah swt ndiye Mwenye kuyaona, kuyasikia na kuyafamu yote.
25th June 2000
2. MAADILI YA ISLAM

Makala haya yamekusanywa na kutarjumiwa na
Amiraly M.H.Datoo - Bukoba Tanzania
Masomo ya akhlaq- maadili katika Islam ni mojawapo ya bora ya sayansi na inamwelekeza asomaye hadi katika elimu ya kujielewa nafsi yake mwenyewe ambayo Islam inaamini kuwa ni fardhi. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: "Yeyote yule aliyeitambua nafsi yake (mwenyewe) basi hakika ametambua Allah."
Hivyo hivyo kuna mapokezi mengi ya habari kuhusu umuhimu wa somo hili hata Mtume Mtukufu (s.a.w.w) amebainisha kuwa: "Mimi nimetumwa kuja kukamilisha maadili.
Tuanze kuzichambua aina za nafsi alizonazo mwanadamu vile alivyo:
Hapana shaka kuwa mwanadamu hana zaidi ya moja, lakini hii nafsi au roho inayo masharti fulani fulani. Kwa hiyo, hali ya kuonyesha kama 'nafsi ya kujilaumu' 'au nafsi ya kuamrisha' 'nafsi inayotosheka' (kama vile vielezwavyo katika Qu'rani), na hivyo haidhihirishi idadi ya nafsi. Upande mwingine, yote haya ni miongoni mwa ngazi za sifa ambazo zinaleta kwa ukamilifu na ustawi wa hali ya nafsi, pamoja na yale yanayoozesha nafsi na kuleta maovu.

NAFSI SAFI AU THABITI (nafsi au thabiti.)

Katika Qur'rani Tukufu, aina mbili hizo za masharti za nafsi zinaelezwa:-"Isipokuwa mwenye kuja kwa Mwenyezi Mungu na moyo safi" (26:89)
Uhalisi huu ni aina ya moyo, na moyo halisi (safi) ni ule ambao haufungamani na upande wa kuhangaika wala upande ule wa wapotofu.
Imenakiliwa kutoka kwa Imamu Sadique (a.s) kuwa: "Moyo ulio msafi- halisi ni ule ambamo hakuna chochote kile ila Allhah (s.w.t) tu"
Katika hali hii, Nafsi imetunukiwa hatua mojawapo ya umuhimu kuwa kamilifu. Hivyo inamaanisha kuwa hakutakuwa na mapenzi mbali na ile ya Allhah tu.
Kuna habari nyigine iliyonakiliwa kutoka kwa Mtume Mtumfu (s.a.w.w.) ambamo twaambiwa: "Imani ya mtu haitokamilika hadi hapo mimi niwe mpenzi wake kuliko hata baba yake, mama yake, watoto wake mali yake na hata kuliko maisha yake."
Ndivyo hivyo, nafsi safi ni nafsi ambamo hakuna mapendo mengine yoyote yale isipokuwa Allah (s.w.t.) na wale wapendwao kwa ajili ya Allah (Mtume na Ahali yake)

NAFSI YENYE KUTUBU (al-Nafs al- Muniib).

Sharti lingine la moyo au Nafsi ni 'kutubu' na hivyo huitwa moyo wenye kutubu au nafsi yenye kutubu. Hivyo huwa daima inarudi kwa Mwenyezi Mungu.
"................ Na anayemuogopa ( Mwenyezi Mungu Mwingi wa kurehemu, na hali ya kuwa humuoni na akaja kwa m oyo ulioelekea ( kwa Mwenyezi Mungu)." (50:33)
Kuwa na khofu ya Mwenyezi Mungu pale mtu awapo peke yake ni mojawapo ya masharti bora ya nafsi, na hii ina maanisha kuwa nafsi imemtambua Allah (s.w.t) kiasi kile kuwa hakutakuwa na tofauti yoyote itakapokuwa pekee yake au katika kundi la watu. Hata kama hakutakuwa na mtu yeyote karibu nayo, basi ile khofu ya Allah (s.w.t.) imo ndani yake thabiti. Hii haipo katika kundi la zile nafsi zilizo ghafilika katika maasi na matendo maovu wakiwa katika kundi la watu au wakati wengine watakapokuja julishwa, na hawatajizuia nayo na hata kama iwapo watakapopewa habari zilizo bainika. Hii ni ile aina ya nafsi ambayo haielewi kuwa Mwenyezi Mungu yupo anaangalia yote na Aliye dhahiri popote pale na kwa hakika aina hii ya nafsi haipo pamoja na Allah na wala haitorudi kamwe kwa Allah.

NAFSI MWONGOZI (al- Nafs al- Muhtadi).

Sharti lingine la nafsi ni ile iongozwayo. Qur'rani inatuambia: (64:11).
"................Anayemuamini Mwenyezi Mungu huuongoza moyo wake"
Mtu ambaye moyo wake ukiwa umeongozwa na kujitosa katika habari ya imani na sheria Tukufu za Allah (subahana wa Tala), yeye anaielewa njia yake vyema kabisa. Zile imani atakazokubalia na matendo yake yale yampasa kuyatenda huwa ni dhahiri kwake kuelewa vyote hivyo kwa uadilifu.

NAFSI ILIYO RIDHIKA (al-Nafs al- Mutmaina)

Sharti lingine lijulikanalo vyema la moyo au nafsi ni "kuridhika. Qur'an:
" Sikiliza: Kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu nyoyo hutulia. "(13:28)
Na vile vile mwishoni mwa sura al-Fajr twaabiwa (89:28)
"Ewe nafsi yenye kutua"!
"Rudi kwa Mola wako, hali ya utaridhika.........."
Nafsi iliyo ridhika ni ile iliyokwisha ridhika, ina maanisha kuwa mtu yupo anapigana vita vikali na matakwa yake na kwa kuyatimiza yale yaliyo fardhi kwake katika dini na kujiepusha na yale yaliyoharamishwa, na anajipa umuhimu kwa kuelimisha na kuikamilisha nafsi yake hadi hapo yeye hapindukii kutii chochote kile isipokuwa Allah (swt) tu. Ni marufuku kwake kuelekea pale penye madhambi na huwa ni mwenye kupenda amani na utulivu na huwa ni mwenye kujiridhikia mwenyewe hadi hapo yeye huwa thabiti kama jabali madhubuti. Hakuna madhambi, matakwa ya ubinafsi, tamaa, mvutano wa dunia, mapenzi ya mali au cheo yatakayoweza kuja kumpotosha yeye na kumwelekeze pengine na vile vile hakuna sheitani atakayeweza mghalimu na kumpotosha yeye.
Hali ya juu kabisa ya sharti hili kama ilivyokuwa katika Mtume mtukufu (s.a.w.w.) na ma - Imamu (a.s.), waliokuwa halisi kuwa hata mawazo ya kutaka kutenda madhambi hayakutokea kamwe.

AL-NAFS AL-MUTTAQI (nafsi ya tahadhari ya uadilifu):

Sifa nyigine ya nafsi inajulikana kama uangalifu wa uadilifu wa nafsi, (The virtuosly cautious self) nafsi ambayo imejaa kwa khofu na tahadhari. Hali hiyo inatokana na nyakati fulani kwa kupotoshwa na (kwa akili na roho) huzungukwa na uchafu na ubovu ili nafsi iingie sharti sawa sawa na itahadharishwe na madhambi. Nafsi ikiwa katika hali hiyo huitwa nafsi ya tahadhari ya uadilifu:-
"..............Anayezihishimu alama za (dini ya ) Mwenyezi Mungu, basi hili
ni jambo la katika utawala wa nyoyo. "(22:32)
Kwa mtu yule ambaye imani yake inafikia kiwango hiki cha "Taqwa" kiwango cha tahadhari ya uadilifu, huheshimu na kumthamini Allhah (s.w.t.) na yele yote yaliyotolewa ishara nae kama Dini, Msikiti, sheriah, waumini wake Makka Ka'aba Tukufu n.k. kwa ufupi. Chochote kile kinachohusika na Mungu huwa kina kuwa na umuhimu na ta 'adhima kubwa kwa mtu kama huyu wa namna hii. Na hii ndiyo kwa hakika matokeo ya 'taqwa'

NAFSI NYENYEKEVU (al- Nafs al- Mukhbit)

Hali nyingineyo ya Nafsi ni unyenyekevu (uvumilivu), yaani humaanisha kuwa mtu mwenye nafsi hali hii huwa mnyenyekevu mbele ya maamrisho ya Allah (swt)
Kwa mara nyingine tena twaambiwa katika Surah al Halj: (22:54)
"................waiamini, na ili zinyenyekee kwake nyoyo zao"
Kwa sababu nyoyo hizi hujiimamisha chini mbele ya Mungu na maamrisho yake, na wale wenye kuwa na nyoyo hizo hujiwakilisha kwa Allhah s.w.t hawavunji kamwe maamrisho ya Mwenyezi Mungu na wala hazisaliti au kuzipinga.

NAFSI HALISI (al-Nafs al-Zakiyyah):

Aina nyigine ya nafsi ni ile nafsi au roho iliyo mtakatifu (the pure self). Katika Qur'ani Tukufu, Mwenyezi Mungu anakula kiapo cha jua, mwezi mbingu, ardhi na vitu vingine na baadaye akisemea nafsi, anatuambia:
"Bila shaka amefaulu aliyeyeitakasa (nafsi yake) na bila shaka amejihasiri aliyeiviza (nafsi yake)" (91:9 & 10)
Ni dhahiri kuwa inambidi mtu afanye jitihada ili kufikia hatua hii. Kabla ya yote yale mengineyo, nafsi lazima iwe huru kutoka sifa zote zile zilizo ovu na hapo ndipo uwanja utakuwa tayari kwakuzitambulisha sifa zilizo nzuri na bora kabisa na kwa uanzishaji na uendelezaji. Mtu ambaye nafsi yake itatakasika, basi amehakikishiwa msamaha (ukovu) na kufikia kipeo cha furaha ya milele. (The person whose self become purified is assured of salvation and bliss!)