MISINGI YA DINI NA MENGINEYO
 
UISLAAM NA JESHI
SWALI:
Je katika Uislaam kuna jeshi maalum lililo pangwa na lenye nidham maalum?
JAWABU:
Ndio na lenye nidhamu iliyo bora kabisa na lililo pangwa katika sura iliyo bora kabisa.
SWALI:
Je katika Uislaam kuna sheria ya kujiunga na jeshi kwa lazima bila ya hiari?
JAWABU:
Hapana, kujiunga na jeshi katika Uislaam ni suala la hiari.[19]
SWALI:
Basi inakuwa vipi kujiunga kwake na uandaaji wa jeshi?
JAWABU:
Hakika dola au serikali ya kiislaam huandaa sehemu kubwa na mahala maalum nje ya miji, iliyo andaliwa kwa aina tofauti za silaha na kuwahiarisha watu kwenda kushiriki katika mazoezi ya kijeshi katika sehemu hizo katika nyakati zao za faragha kama siku ya Ijumaa na ziku zinginezo ambazo hawako kazini, bila ya kutofautisha kati ya yeyote atakae kushiriki, wakubwa kwa wadogo.[20] Na kwa njia hii takriban watu wote hushiriki katika hufanya mazoezi na kuiondolea serikali matumizi ambayo inge yatoa kwa ajili ya jeshi, kama ambavyo wafanya kazi hubakia makazini na kwenye familia zao, kwa hivyo kila mtu hufanya mazoezi kila siku-kwa muda wa saa moja au masaa mawili, kwa mfano-kisha kurudi kwenye kazi yake na kubakia na familia yake. Na pindi adui anapo ivamia nchi au dola inakuwa ni wajibu kwa wote kupigana kwa kuutetea Uislaam na mwenye kupendezewa kulitumikia dola na serikali kwa hiari yake, hupangiwa mshahara maalum, ili abakie wakati wote na bila kusimama akiwa ni mhudumu wa dola la kiislaam.


VIFAA VYA KIVITA
SWALI: Ni upi mtizamo wa kiislaam kuhusiana na vifaa vya kisasa vya kivita? JAWABU:Mtazamo wa kiislaam ni kuwa niwajibu kutengeneza na kuwa na vifaa vitakavyo liwezesha dola au serikali ya kiislaam kujibu mashambulizi na kujilinda na kulinda heshima ya Uislaam na amani ya waislaam[21] na hilo linatokana na kauli yake Mwenyezi Mungu:
(وأعد وا لهم ما استطعتم من قوة)[22]
(Na waandalieni nguvu kwa kadri ya uwezo wenu)
SWALI:
Dola au serikali huwa na mipango gani kuhusiana na familia za wanajeshi wanao kufa vitani?
JAWABU:
Ikiwa familia hiyo ni mafukara na wasio jiweza, hupewa kiwango cha kutosheleza mahitaji yao kulingana na hadhi yake na kama familia hiyo haikuwa hivyo, haipewi kitu isipokuwa ikiwa katika kuwapa chochote kuna maslaha na mfano wa hayo.
SWALI:
Ni upi msimamo wa Uislaam kuhusiana na amani na vita?
JAWABU:
Uislaam ni dini ya amani na utulivu kama alivyo sema Mwenyezi Mungu alie tukaka:
يا أيها الذ ين آمنوا أد خلوا في السلم كافة [23]
(Enyi mlio amini ingieni kwenye Uislaam wote) na Uislaam hufanya kazi ya kueneza amani na usalama ulimwenguni na huenda mbio kuzima chochoko ya vita na kuzima moto wake wenye kulindima na kung'oa mizizi ya chanzo chake kati ya watu, kwa kung'oa vyanzo na sababu zipelekeazo kutokea kwa vita na badala yake kuweka vyanzo vinavyo chochea mapenzi na kuelewana na vinavyo chochea kuwepo sulhu na utulivu na kuacha kabisa suala la vita na kuwa na utulivu hata kama adui atakuwa anafanya hadaa na kutoa wito wa kutaka kuwepo amani, amesema Mwenyezi Mungu alie takasika: [24]
وإن جنحوا للسلم فاجنح لها
(Na ikiwa wataelekea na kumili kwenye amani basi nanyi elekeeni kwenye amani). Na wakati huo huo Uislaam unaharamisha mambo ya kutumia nguvu na vitisho na mauaji ya kuvizia au mauji ya kawaida na inapiga vita kila jambo lipelekealo kuwa na khofu na kuogopa na wasiwasi na kutokuwa na utulivu kati ya watu.


UHURU KATIKA UISLAAM
SWALI:
Je kuna uhuru katika Uislaam?
JAWABU:
Ndio, tena uhuru ulio bora kabisa kati ya migawanyo ya uhuru, na ambao ulimwengu hauja wahi kuufikiria wala kuuotea katika utamaduni wa juu kabisa kati ya tamaduni za hapa ardhini.
SWALI:
Ni upi uhuru wa kiislaam?
JAWABU:
Uhuru wa kiislaam ni wa aina nyingi, na hapa tutataja baadhi tu kati ya aina hizo za uhuru huo kama ifuatavyo:


UHURU WA BIASHARA NA UCHUUZI
1-Uhuru wa kufanya kazi na kufanya Biashara, kila mtu kati ya watu wa Umma wa kiislaam anayo haki ya kujichagulia kazi au shughuli aitakayo kuifanya kwa ajili ya uchuuzi au kuwa ndio chanzo cha mapato yake, kwa hivyo akichagua uwindaji ni juu yake, au kuchimba madini na ngawira zilizoko ardhini, au kukusanya mambo ya mubaha na kuyamiliki na mengineyo kati ya vyanzo halali vya uchuuzi, kama ambavyo ni ni haki ya mfanya biashara kuingiza nchini bidhaa azitakazo au kusafirisha nje ya nchi bidhaa azitakazo, au kununua na kuuza bidhaa azitakazo, katika upande huo kahakuna kizuizi kamwe, katika Uislaam hakuna ushuru (Tax) wala hakuna Leseni ya biashara wala sharti, ndio hushurutishwa bidhaa zisiwe za haramu-kama mvinyo-(vileo) na kusiwe na riba katika biashara hiyo au isiwe ni biashara ya haramu na mfanya biasha asifiche bidhaa wakati wa mahitaji kwa ajili ya kusubiri msimu ambao kutakuwa na uhaba wa bidhaa hizo na katika biasha hiyo kusiwe na madhara kwa watu na katika uchumi wao.


UHURU WA VIWANDA NA UKULIMA
2-Uhuru katika kilimo na viwanda, kwa maana mwenye kutaka kujishughulisha na kilimo kiasi chochote cha ardhi akitakacho na kwa aina yoyote ile aitakayo, anayo haki ya kufanya hivyo na wala hakuna katika Uislaam kitu kiitwacho ( kilimo cha kisasa) mpango ulio ingizwa kutoka katika nchi zisizo za kiislaam, ndio ardhi hiyo ikiwa ni ardhi iliyo (kombolewa kwa nguvu) ni wajibu kwa mkulima kutoa malipo ya ukodishaji wa ardhi hiyo-kwa kiasi kidogo sana-na kuilipa serikali au dola na hiyo ndio iitwayo kwajina la (kodi) ya ardhi, na mkulima ikiwa ni fakiri ni wajibu kwa serikali kumkidhia haja yake kulingana na hadhi au hali yake na hakuna kizuizi cha mtu kulima kiasi chochote cha ardhi akitakacho kwa sharti kwamba asiwanyime wengine nafasi na fursa ya kulima na alime mazao yoyote ayatakayo isipokuwa yatakayo kuwa na madhara kama na serikali haina haki kuchukua mapato isipokuwa (Khumsi) na (Zaka) pamoja na kuchunga masharti yake kama tulivyo eleza hapo kabla, na vilevile viwanda vyote, viko huru- kwa maana kamili ya uhuru-isipokuwa katika vitu vilivyo haramu katika Uislaam kama viwanda vya pombe (Vileo) na madawa ya kulevya.


UHURU WA UJENZI NA UENDELEZAJI WA MIJI
3-Uhuru wa ujenzi na uendelezaji wa ujenzi wa nchi na miji, mwenye kutaka kuiendeleza ardhi kwa namna yoyote ile iwayo, anayo haki ya kufanya hivyo, kwa hivyo basi mtu yeyote chini ya kivuli cha serikali ya kiislaam anayo haki ya kujitengea ardhi ya halali na kujenga akitakacho kwenye ardhi hiyo kama nyumba au sehemu ya kibiashara, au kiwanda, msikiti, Husainiyya, Madrasa, Dispensari, Hospitali, au mfano wa havyo kwa uhuru kamili na katika ujenzi na uendelezaji hakuna kabisa kitu kiitwacho Leseni na serikali au dola halina haki kuchukua chochote kwa mtu huyo walau senti moja kwa ajili ya ardhi au kinginecho, hakika Uislaam umeweka kanuni isemayo kuwa (Mwenye kuhuisha ardhi zilizo kufa yaani zilizo telekezwa basi ardhi hiyo ni milki yake)[25] isipokuwa ardhi hiyo ikiwa (imekombolewa kwa nguvu) wakati huo ni juu ya mwenye kuiendeleze ardhi hiyo kutoa malipo ya ukodishaji kwa serikali. Na ikiwa hukumu hii itatekelezwa katika ardhi na uendelezaji wa ardhi basi itakuwa inatosheleza kukidhi haja za watu katika suala la makazi, na kutoweka tatizo la makazi lililo enea katika nchi zote za kiislaam.


UHURU WA MTU KUISHI NA KUSAFIRI MAHALA APATAKAPO
4-Uhuru wa kusafiri na kuishi, yaani mwenye kutaka kuishi mahala fulani, au kusafiri mahali fulani anahiari ya kufanya hivyo bila sharti wala kikwazo, katika Uislaam hakuna mipaka ya mahala, wala vikwazo vya kijinsia wala ubaguzi wa kirangi, lugha na kwa uhuru huu suala la uraia na jinsia na suala la pasport za kusafiria huporomoka na mengine yote yanayo ambatana na hayo, kama ambavyo nchi nyingi za ulaya zilivyo andoa vitu hivyo na kupinga bidaa hii yenye kuwaudhi na kuwakera wananchi wake na nchi zao.


UHURU WA NASHATI ZA KIJAMII NA KISIASA
5-Uhuru wa kutoa huduma za kijamii au kuihudumia jamii na harakati za kisiasa bila kuwa na vikwazo,-isipokuwa harakati zilizo haramishwa na Uislaam nazo ni chache sana, kwa maana hiyo hakuna idara ya upelelezi kamwe, kwani haijuzu kumfanyia yeyote upelelezi au tajassusi, kwa hivyo katika Uislaam hakuna wizara ibebayo jina la Wizara ya upelelezi na mfano wa hayo, isipokuwa wizara ya kukusanya habari (Wizara ya habari) kwa ajili ya maslahi ya Umma na kwa ajili ya kulinda usalama wa nchi na usalama wake, kwa hivyo katika dola la kiisalaam[26] kila mtu yuko huru kuandika na kubainisha ayatakayo na katika maneno yake na auandishi wake wa vitabu na yuko huru kuunda vikundi mbali mbali vya kijamii na jumuia na vikundi vya ushirika na vikundi vya kheri na kukusanya misaada mbali mbali na vitu vya kujitolea na kutoa au kuchapisha majarida mbali mabli na magazeti na kuanzisha redio na televisheni na visivyo kuwa hivyo.


UHURU WA HARAKATI NA NASHATI ZINGINEZO
6- Uhuru wa nashati zingine za mtu mmoja mmoja au za kijamii, kwa mfano: kila mtu mwenye kufahamu udreva, yuko huru kuendesha bila ya haja ya kumpatia leseni au mfano wake, kama ambavyo maiti hahitajii ruhusa ili aandaliwe na kuzikwa, bali ni juu ya jamaa zake kusimamia suala la kumuandaa na kumzika sehemu yoyote waitakayo au sehemu aliyo iusia yeye mwenyewe marehemu, bila ya haja ya kutoa kodi au Risiti au mfano wa hayo na hukumu ni hiyo hiyo katika mambo mengine. SWALI: Kutokana na mliyo yataja itapelekea kufungwa kwa ofisi na idara nyingi? JAWABU: Ndio…na hivyo ndivyo dola la kiislaam lilivyo kuwa, halikuwa na idara isipokuwa chache sana na kwa maana hiyo ndio maana tukasema-hapo kabla-ya kuwa wafanya kazi katika dola au serikali ya kiislaam ni wachache sana, na ni wachache kupita kiasi na kwa sababu ya uchache wa wafanya kazi majukumu ya serikali na mzigo wa serikali na dola la kiislaam utapungua na wala muundo wa serikali au dola hauta beba mzigo wa matumizi mengi ya pesa (yaani dola halita tumia pesa nyingi katika bajeti yake).


UTOAJI WA HUKUMU NDANI YA UISLAAM
SWALI:
Je katika Uislaam kuna hakimu na utoaji wa hukumu?
JAWABU:
Ndio, katika Uislaam kuna aina nzuri sana ya utoaji hukumu na kuna mahakimu walio waadilifu zaidi.
SWALI:
Hakimu na utoaji wa hukumu huwa vipi katika Uislaam?
JAWABU:
Katika Uislaam Hakim ni wajibu au ni lazima awe ni muumini na muadilifu, mwenye elimu ya utoaji hukumu na awe ni Mujtahidi katika mas'ala ya utoaji hukumu na katika hukumu zake na utoaji hukumu ni wajibu uwe kwa kutegemea dalili na viapo, bila kuwa na vikwazo katika mahakama wala kusiwe na mizunguko na bila ya kuwepo ufunguzi wa mafaili wala stakabadhi wala ulipaji wa malipo kamwe na hakuna haja ya kutanguliza ufunguaji wa faili la mashtaka na mfano wa hayo kama mafaili ya mashtaka yatumikayo katika zama hizi kwenye mahakama mbalimbali na katika utoaji wa hukumu. Na kwa ajili ya urahisishaji, uadilifu huu uliopo kwenye mahakama za kiislaam na kutoa egemea au kumili sehemu fulani kuliko shurutishwa kwa Hakimu katika Uislaam, Hakimu au Kaadhi mmoja anaweza kusikiliza madai ya pande zote mbili mshitaki na mshitakiwa na kutoa hukumu kwa haraka sana iwezekanavyo na hilo hufanyika juu ya vipimo na misingi ya Uislaam na ushahidi wa mashahidi walio waadilifu na kutokana na hali hiyo ndio maana Kaadhi mmoja alikuwa akihukumu mji mmoja wenye (Mamilioni) ya watu kiasi kwamba hakuna tatizo lolote libakialo linalo husiana na mambo ya mahakama au utoaji hukumu kamwe.
SWALI:
Hakimu hupata wapi riziki yake kwa kazi aifanyayo?
JAWBU:
Hupata riziki yake kutoka kwenye Baytul mali.
SWALI:
Ni ipi kazi ya Kaadhi (Hakimu)?
JAWABU:
Kadhi kwa kusaidiwa na wasaidizi wake hufanya kazi zifanywazo na ofisi au idara nyingi katika serikali tawala, katika zama hizi, hakika yeye husimamia mambo ya waqfu na kuwasimamia watumishi wa waqfu hizo na hukusanya mali ya watoto wadogo na kuiihifadhi ili baadae awape wenyewe pindi masharti yanapo kamilika na huizuia mali ya punguwani na kufungisha ndoa na kutoa au kusimamia suala la talaka na huuza na kununua na kuwekesha reheni na kukodisha na kutatua mizozo kati ya watu na kutekeleza hududi za kisheria kati yao na mengineyo.[27]


UWAKILI KATIKA UISLAAM
SWALI:
Je katika Uislaam kuna mfumo wa mawakili, kwa namna hii ijulikanayo katika mahakama za kisasa?
JAWABU:
Katika Uislaam hakuna mfumo wa uwakili kwa namna hii iliyopo hivi sasa na wala Uislaam hauhitaji idadi hii kubwa ya mawakili, kwani mambo yote na hasa mambo ya mahakama na utoaji hukumu katika dola la kiislaam huendeshwa kwa njia nyepesi na kwa urahisi sana tena kwa amani na uaminifu.
SWALI:
Uislaam huwafanyisha nini au huwatumikisha vipi mawakili na wafanyakazi ambao dola la kiislaam haliwatambui kutokana na kazi zao, ikiwa utashika hatamu ya uongozi na kuendesha serikali?
JAWABU:
Hakika Uislaam hauushutukizi umma au watu kwa mabadiliko au marekebisho ya ghafla bali katika kufanya mabadiliko na marekebisho huwa nao sambamba na kwa njia ya taratibu, kwanza kabisa wale ambao haizitambui kazi zao huwaandalia kazi zinazo wiana na hadhi au utaalamu wao au zinazo nasibiana nao, kisha kuwalipa kutoka kwenye hazina ya dola au serikali kiwango kitakacho weza kuwasaidia katika mambo yao ya kimaisha, mpaka ifikie kupata kazi ambazo wao wenyewe wanataka kuzifanya, je baada ya hatua hizi kuna yeyote kati ya wale ambao serikali haizitambui na kuzikiri kazi zao atakae chukua hatua yeye mwenyewe na kuitilia mgomo serikali ya kiislaam baada ya kuwa serikali ya kiislaa imemuandalia kazi inayo nasibiana na utaalamu wake au nafasi yake kati ya kazi zilizo huru na zenye manufaa na kumsaidia mpaka akawa na uwezo wa kufanya kazi hiyo kwa fakhari na kwa raha mustarehe bila ya kukereka? Na vilevile Uislaam hufunga kabisa sehemu ziuzazo pombe kama Mabaa na majumba ya ufuska na mfano wa hayo pamoja na kutilia mkazo kwa kiwango kikubwa mambo ya maisha yao na kuanzisha vituo au kazi zinazo wiana na sehemu na hadhi zao kama kazi ambazo zitawafanya wapate riziki zao za halali na kuwazuwia kazi hizo kufanya matendo ya haramu.


SWIHHA NA AFYA KATIKA UISLAAM
SWALI:
Je katika Uislaam kuna nidham na mfumo wa mambo ya kiafya?
JAWABU:
Ndio na mfumo ulio bora kabisa kuliko mifumo na nidhamu iliyopo ya kinga na utibabu, na inamifumo iliyo makini zaidi na mipana na yenye kuhusika na nyanja zote, kwa mfano inayo mifumo inayo husu afya ya mwili, roho na afya ya mtu mmoja mmoja na jamii na mifumo ya usalama wa hali ya hewa anga na mazingira.
SWALI:
Mfumo wa kiislaa wa kiafya uko vipi?
JAWABU:
Uislaam huweka jedwari kwa sura ya ujumla linalo husiana na afya ya ujumla kwa kuweka kanuni ya mambo matatu: 1-Kanuni ya kinga: Hakika kanuni hii hulinda na kumhifadhi mtu mmoja mmoja, Jamii na Mazingira ili yasienewe na maradhi ya kuambukiza au kuhamia kwa watu wengine na kinga hiyo hutimia kwa mambo yafuatayo: (a): Kuharamisha vitu ambavyo ni sababu ya kuzuka kwa maradhi na uambukizaji., kwa mfano: Pombe, madawa ya kulevya, uzinifu, kulawitiana, kusagana kati ya wanawake, mambo yenye madhara, miziki na mambo yasababishayo kero na Mabaa (sehemu za kuuza vileo) na madanguro (majumba ya ufuska) na vikao ambavyo watu hukaa uchi (yaani sehemu za shoo ambapo wanawake hukaa uchi) na mfano wa hayo.


(b) Kwa kuweka kanuni ya mambo na adabu kumi za sunna zenye kumuelekea mtu mmoja mmoja na jamii, kama kanuni ya Usafi, Kuoga, Kutoa damu kwa ajili ya kusafisha mwili (Hijaama) na kutoa damu katika baadhi ya mishipa kwa kuchanja (Al-fasdi), kufunga, Kujipaka mafuta, Kuoa, kutumia tiba ya kunusa dawa, kutumia wanja, na kutumia (Nura) dawa ya asili kwa kujisafishia, namna ya kula na kunywa na namna ya kuvaa, sehemu ya kuishi, kulala, kuamka, na mengiyo. 2-Tiba: Na hutimu hilo kwa kuelekeza baadhi ya madawa ya miti shamba na vyakula vyenye manufaa na vinavyo saidia katika kutibu magonjwa na yote hayo hufanyika kwa njia ya kawaida na nyepesi na njia hii japokuwa haienei na kuyahusu magonjwa yote, isipokuwa ukweli ni kuwa hufukuza marahi na hasa yanapo kuwa yana anza, kama ilivyo elezwa katika kitabu (Twibbun-nabiiy) (s.a.w) na katika kitabu (Twibbul-aimmah) (a.s) na mfano wa hayo.


3-Kuchukua tahadhari: Hakika Uislaam huchukua tahadhari na kulinda suala la usafi wa mazingira na hufuatilia suala la usafi wa mazingira kutokana na kuchafuliwa na hufuatilia kwa makini afya ya kila mtu na kumlinda asipatwe na magonjwa ya kuambukiza, kama ambavyo huwachunga matabibu na madaktari kwa makini kabisa na kuwajaza ndani ya nyoyo zao hali ya kiutu na dhamira safi na khofu ya Mwenyezi Mungu na kuwaadhibu pindi wanapo kiuka maadili, kwani utakuwa imefikia kuweka kanuni isemayo (Tabibu au Daktari ni mwenye dhamana hata kama ni hodari na mwenye uhakika na kazi yake) kitu ambacho humfunga na kumtia dhamana Daktari asiweze kupuuzia katika kumuangalia mgonjwa au kupuuzia katika kutoa matibabu, au kuto sema ukweli, bali kanuni hiyo inamfanya awe na hali ya umakini na umadhubuti wa hali ya juu kabisa na tahadhari kubwa na mwenye kujichunga sana katika kumuandikia mgonjwa dawa na katika kuyafanyia uchunguzi maradhi na kuyatibu kwake maradhi hayo.


UISLAAM NA TIBA YA KISASA
SWALI:
Je si kweli kwamba tiba ya kisasa imepata maendeleo makubwa na yenye kushuhudiwa ulimwenguni?
JAWABU:
Hakuna shaka yoyote juu ya maendeleo yaliyo patikana katika tiba ya kisasa lakini ile misingi ambayo tumeitaja na ambayo ndio nguzo na vizingiti vya msingi na sababu za kiafya na swiha, misingi hiyo imevunjwa na kubomolewa, kwa maana hiyo ndio maana tunakuta kwamba maradhi yamekuwa yakiwashambulia wanadamu kwa njia za ajabu sana na kwa sura ya kushangaza, hata imefikia wingi wote huu wa madaktari na maduka ya madawa na mahospitali na mfano wa hivyo, havitoshelezi kurejesha hali nzuri ya kiafya duniani kwa sura ya ujumla. Na kwa msingi huo bado tuna wakumbuka mababu zetu na mababa zetu ambao-kwa kuchunga na kulinda kwao nidhamu ya kiislaam katika mambo ya kiafya-wakiishi raha mustarehe na wakiwa na afya kamili na swiha nzuri na wakiwa na nguvu zao timamu mpaka wanapo fikia hatua ya kufariki, wakati ambapo tunaona katika zama zetu hizi ya kuwa kila nyumba haikosi kuwa na mgonjwa au maradhi na watu wengi utakuta kuwa wamekumbwa na ugonjwa au magonjwa ya aina tofauti.


SWALI:
Sasa ni ipi njia ya kurekebisha na kutibu hali hii?
JAWABU:
Njia ya kurekebisha na kutibu hali hii ni kufanya kila njia na kwenda mbio kurudisha ile mipango na ratiba na kanuni za ujumla za kiafya zilizomo katika Uislaam na kuzifanyisha kazi au kuzitekeleza katika jamii zetu na kuchukua tiba ya kisasa yenye manufaa na mambo mapya yaliyo gunduliwa katika tiba ya kisasa na kutoa mambo ya haramu na mambo yenye madhara katika tiba hiyo na kufungua njia na milango ya kufaidika na tiba ya miti shamba au tiba ya kizamani (kama waiitavyo wataalamu wa kisasa) na ambayo ni mujarrabu, ili zichanganyike tiba hizo mbili tiba ya zamani (yaani ya miti shamba) na tiba ya kisasa na kwa kufanya hivyo wanadamu na viumbe waweze kuokoka na kuepukana na maraadhi au magonjwa pia mabalaa na majanga ya kibina damu chini ya kigezo cha maradhi ya kushutukiza na kuua kwa ghafla.