MISINGI YA DINI NA MENGINEYO
 
DHAMANA YA KIJAMII KATIKA UISLAAM [10]
SWALI:
Je katika Uislaam kuna dhamana ya kijamii?
JAWABU:
Ndio na ni bora kabisa kati ya aina ya dhamana za kijamii na za kiwango cha juu kabisa.
SWALI:
Je mnaweza kutubainishia na kutufafanulia sehemu fulani ya dhamana hiyo ya kijamii katika Uislaam?
JAWABU:
Dhamana ya kijamii katika Uislaam inatokana na shauku na mapenzi ya kibinadamu na kiutu tena ya kiwango cha juu kabisa kwa maana hiyo hakika Uislaam una anzia kwenye nukta ya utu au ubinadamu, na huitoa dhamana hii ikiafikiana na hali ya kibinadamu na kiutu na ikilenga kwenye upeo wake na katika nyanja zake za ubora na kwa kusisitiza hilo historia haikuwahi kushuhudia kabla ya Uislaam na historia haikunukuu utamaduni wa aina yoyote baada ya Uislaam hadi hivi leo dhamana ya kijamii yenye kina kilicho sawa na kina cha dhamana ya kijamii katika Uislaam.


MIFANO YA DHAMANA YA KIJAMII YA KIISLAAM
Hakika dhamana ya kijamii katika Uislaam inasema yafuatayo:
1- Hakika kila mtu anae kufa hali ya kuwa na madeni, au ameacha familia bila msimamizi na mtu wa kuitunza familia yake, ni juu ya Imam wa Waislaam kulipa madeni yake, kama ambavyo ni juu yake kuitunza na kuilea familia yake.
2-Kila anae fariki hali ya kuwa ana mali, mali yote ni ya warithi wake.
3- Pamoja na hayo, huduma za kimali ambazo hutolewa na Baitul mali ya Waislaam kwa kila mtu katika umma wa kiislaam, ni kwa ajili ya kukidhi mahitaji yao ya mwanzo na kwa ajili ya kujipatia maisha mema.


Je unadhani-pamoja na yote hayo- unadhani kunadhamana kama hii ambayo imo ndani ya Uislaam, hata kama ni katika utamaduni ulio endelea na wenye kina kikubwa zaidi? Kwa hakika na bila shaka yoyote hakuna kitu kama hicho, bali ukweli ni kuwa mifumo mingine ya utawala ya kiulimwengu na ya kijahili iliyo kuwepo kabala ya Uislaam vilevile mifumo ya ulimwengu inayo dai kuwa imeendelea na iliyo kuwa na maendeleo ya kielimu na iliyo staarabika katika zama zetu hizi huwajibisha kutoa mapato makubwa kwenye urithi, kama ambavyo wao hawalipi deni la yeyote na wala hawabebi jukumu la kuitunza familia ya marehemu na hakuna shaka hapa kutaja baadhi ya mifano ya kiislaam juu ya jambo hili.


MFANO WA KWANZA
Katika Nusuus (dalili) za kisheria za kiislaam, kuna dalili nyingi zinazo tilia mkazo juu ya haya tuliyo yataja ya dhamana ya kijamii ya kiislaam na dalili hizo bila shaka zinatujulisha juu ya namna Uislaam unavyotilia mkazo na hima juu ya jamabo hili na katika upande huu wa kibinadamu na kijamii ulio mkubwa, kiasi kwamba imekaririwa kwa mara kadha zikinukuliwa dalili juu ya suala hilo kutoka kwa Mtume wa Uislaam (s.a.w) na maimam wa kizazi kitwaharifu cha Mtume (s.a.w). Kwa mfano imepokelewa kutoka kwa Abi Abdillah Jaafar bin Mohammad As-swaadiq (a.s) Imam wa sita wa Ahlul bayti (a.s), ya kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) amesema:
(انا اولي بكل مؤمن من نفسه و علي (ع) اولي به من بعدي)
(Mimi ni bora kabisa au mwenye haki zaidi kwa kila muumini kuliko nafsi yake na Ali (a.s) ni bora zidi na mwenye haki zaidi kwa kila muumini kuliko nafsi yake baada yangu). Akaulizwa:Nini maana ya maneno hayo? Akasema: Kauli ya Mtume (s.a.w): (Mwenye kuacha deni, au familia basi ni juu yangu mambo hayo na mwenye kuacha mali basi ni ya warithi wake).[11]


MFANO WA PILI
Ali bin Ibrahiim katika tafsiri yake ametoa hadithi, kwa sanadi yake iliyo tajwa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) ya kuwa yeye alikuwa akisema: (Hakuna mdai yeyote alie kwenda na mdaiwa wake kwa mtawala kati ya watawala wa kiislaam na ikabainika kwa yule walii ya kuwa ni tajiri na mwenye uwezo, isipokuwa humuokoa yule fakiri kutokana na deni lake, na deni hilo kuhamia kwenye dhima ya mtawala yule wa Waislaam kutokana na mali iliyoko mikononi mwake kati ya mali za Waislaam).[12] Amesema Imam Swadiq (a.s) baada ya kunukuu hadithi hii kutoka kwa Mutme (s.a.w): (Na hakukuwa na sababu ya kusilimu Mayahudi wote isipokuwa baada ya kusikia kauli hii kutoka kwa Mtume (s.a.w) na kwamba wao walipata tumaini juu ya nafsi zao na juu ya familia zao.[13]


MFANO WA TATU
Shekh Mufiid (Quddisa sirruhu) ametoa hadithi katika kitabu chake Al-majaalis, kwa sanadi yake kutoka kwa Imam Abi Abdillah As-swadiq (a.s) ya kuwa alikuwa akisema: (Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) alipanda kwenye Mimbari, vitukuta vyake vikabadilika na rangi yake kumeremeta, kisha akageuza uso wake na kusema: Enye waislaam! Hakika si jambo jingine mimi nimetumwa na kiama, kama vitu viwili hivi- hadi akasema- enyi watu! Mwenye kufariki na kuacha mali basi mali hiyo ni ya warithi wake na mwenye kuacha deni au familia bila muangalizi, ni juu yangu na hurejeshwa kwangu)[14] Pia ametoa hadithi kutoka kwa Abi Abdillah As-swadiq (a.s) ya kuwa amesema: (Yeyote atakae kuwa na mali (yaani atakae chukua deni) kwa mtu fulani na hakuitumia mali hiyo vibaya (kwa israfu), au katika maasi, na ikamuwia vigumu kulipa deni hilo, ni juu ya mwenye mali kumpa muhula (muda) mpaka Mwenyezi Mungu amruzuku na aweze kulipa deni hilo na ikiwa Imam muadilifu yupo, ni juu yake kumlipia deni hilo, kutokana na kauli ya Mtume (s.a.w): Yeyote atakae acha mali basi mali hiyo ni ya warithi wake na mwenye kuacha deni au familia, ni langu na ni juu yangu na ni juu ya Imam kuchukua dhamana aliyo ichukua Mtume (s.a.w)).[15]


MFANO WA NNE
Hakika Uislaam- kwa ubora wa mfumo na nidhamu yake uliyo nayo ya Baytil mali ya Waislaam na dhamana ya kijamii ya kiislaam- imeufanya umma wa kiislaam kuwa tajiri na ufakiri katika dola hilo umekaribia kuwa sawa na khabari ya kana (khabari iliyo kuwa) kutokana na dola la kiislaam, ambalo lemeenea kila mahala, na lenye ardhi kubwa na pana na zilizo mbali, ardhi ambayo takariban zaidi ya tatu ya nne ya ardhi hiyo ni yenye kukaliwa na watu, na yenye wakazi wengi. Ndio, hakika Shekh Hurrul Amiliy ametaja katika kitabu chake maarufu: (Wasaailu-shia) kisa kifuatacho akisema: Hakika Imam Amirul muuminiin Ali bin Abi Twalib (a.s) alikuwa akitembea katika mitaa na vichochoro vya mji wa Al-kufa, ghafla akamuona mtu mmoja akiomba watu misaada: akastaajabu sana kutokana na mtu huyo na akawageukia walio kuwa pembezoni mwake akijiuliza: Ni kitu gani hiki?


Akajibiwa: kuwa ni Mkiristo amezeeka na kuwa na umri mkubwa na hana tena uwezo wa kufanya kazi na hana mali ya kumuwezesha kuishi, kwa hivyo ndio maana anawanyooshea watu mkono kwa kuomba. Imam (a.s) akasema hali ya kuwa ni mwenye ghadhabu: Mmemfanyisha kazi wakati akiwa kijana mpaka alipo fikia utu uzima na uzee mkamtelekeza na kumuacha? Kisha Imam (a.s) akaamuru atengewe fungu yule Mkiristo katika baytul mali ya Waislaam litakalo mfanya aishi maadamu bado yuko hai.[16] Hakika kisa hiki kinatufahamisha ya kuwa ufukara ulikaribia kutokuwa na nafasi katika dola la kiislaam, hadi ilifikia Imam Amirul muuminiin (a.s) akimuona fakiri mmoja hushangaa na kustaajabu na kuliona tukio hilo kuwa ni tukio lisilo la kawaida na hali isiyo ya kawaida na halinasibiani na jamii ya kiislaam na dola au nidhamu ya kiislaam, kisha wakati huo akamuwekea fungu litakalo mfanya aishi maisha mazuri na yenye furaha pamoja na kuwa ni Mkiristo na hafuati dini ya kiislaam, na alifanya hivyo ili kusiwe katika nchi ya kiisalaam mfano au tukio moja linalo onyesha hali ya ufukara na kutokuwa na kitu na ili ulimwengu ufahamu hali waliyo nayo Waislaam: Ya kuwa serikali ya kiislaam inampango wa kuangamiza janga la ufukara na kuinua hali ya maisha ya mafakiri na masikini na si kwa mustawa wa Waislaam pekee yao, bali inaupiga vita ufukara hata kwa Makafiri maadamu wako chini ya uangalizi wa dola la kiislaam.MFANO WA TANO
Shekh Kulayni ametoa hadithi kwa sanadi yake iliyo tajwa kutoka kwa Hassan amesema: (Hakika Ali alipo washinda Twalha na Zubayri) katika vita vya Jamal na katika vita vyake alivyo pigana pamoja na wapingaji (Naakithiin) watu walirejea wakiwa wameshindwa, na wakampitia mwanamke mmoja alie kuwa mja mzito njiani, na alipo waona akashikwa na fazaa na mshutuko mkubwa na ikawa ni sababu ya kutoka kwa kilicho kuwa tumboni mwake kikiwa hai na kutatizika hadi akafariki, kisha mama wa mtoto huyo nae kafariki baadae, Imam Ali (a.s) akampitia mama huyo yeye na maswahaba zake hali ya kuwa mama yule akiwa amelala chini na mwanae akiwa njiani, akawauliza kuhusiana na kilicho msibu mama huyo? Wakasema: Hakika alikuwa ni mja mzito na akashikwa na fazaa na mshutuko wakati alipo ona mapigano na namna walivyo shindwa.


Akasema: Akawauliza: Ni yupi alifariki kabla ya mwengine? Akajibiwa: Hakika mwanae ndie alie fariki kabla ya mama. Akasema: Imam (a.s) akamuita mumewe baba wa mtoto alie fariki akampa theluthi ya fidia kama urithi wa mwane, kisha akamrithisha mama yake theluthi nyingine ya fidia, kisha akamrithisha mume vilevile kutoka kwa mkewe nusu ya fidia ambayo aliirithi kutoka kwa mwanae na kuwarithisha jamaa au ndugu wa mke alie fariki fidia iliyo bakia, kisha akamrithisha mume pia katika fidia ya mkewe alie fariki nusu ya fidia nayo ni: Dirhamu elfu mbili na miatano na jamaa za mwanamke alie fariki akawarithisha nusu ya fidia nayo ni:Dirhamu elfu mbili na mia tano na alimpa kiasi hicho kutokana na kutokuwa na motto mwingine tofauti na yule alie toka kutokana na fazaa iliyo mshika.


Akasema: Na Imam (a.s) alitoa mali yote hiyo kwenye Baytul mali ya Basrah.[17] Ndio, hivi ndivyo Uislaam ulivyo weka Baytul mali ya Waislaam kwa ajili ya manufaa ya Umma na kutatua matatizo yao na kuwapa haki zao, kwani-kama ilivyo pokelewa katika hadithi tukufu- (Haki ya muislaam haipotei)na katika hadithi nyingine imepokewa ikisema (Damu ya Muislaam haimwagiki bure)[18] na kwa dalili hizo Uislaam ukauwekea Umma wa kiisalaam mahitaji yenye kumtosheleza kupitia mpango wake wa dhamana yake ya kijamii yenye uadilifu.