MISINGI YA DINI NA MENGINEYO
 
MAREJEO YA KIAMA
Maana yake ni kuwa: Mwenyezi Mungu mtukufu anamuhuisha na kumfanya mwanadamu awe hai katika Akhera baada ya kumfisha duniani, ili amlipe thawabu mtu mwema juu ya wema wake na kumlipa muovu kwa uovu alio ufanya. Kwa hivyo basi mwenye kuamini na kutenda matendo mema na kusali, kufunga, katoa sadaka (zaka) na kumtakasia nia Mwenyezi Mungu (kuwa na ikhals) na kuwahifadhi Mayatima na kuwalisha Masikini na mengineyo mengi, hakika yeye Mwenyezi Mungu humpa thawabu mtu huyo kwa kumuingiza kwenye pepo yenye neema ambayo hutiririka chinio yake mito, na yenye vivuli vyenye kumfunika na yenye rehma nyingi sana na majumba ya kifalme na kifakhari na mahurulaini walio fungiwa kwenye majumba yao na kupata maridhio ya Mwenyezi Mungu ni kukubwa zaidi.


Na mwenye kukufuru na kufanya matendo mabaya na kusema uongo, kufanya khiyana, kuua, kuiba, kuzini, kunywa pombe, na mfano wa hayo, hakika Mwenyezi Mungu humlipa kwa kumuingiza katika jahannama iliyo jawa na moto na adhabu, na chakula chake ni cha miti ya miba na kinywaji chake ni maji ya moto na wakati yuko kwenye matatizo na adhabu yenye kudhalilisha na ya milele isio katika wala kukoma.

Na kuna visimamo vingine viwili kabla ya moto na pepo: 1-Kaburi: Nayo ni sehemu au hatua ya kwanza kati ya hatua za ulimwengu wa barzakh baada ya kuwa mauti ni mlango wa kuingia kwenye ulimwengu huo, kwa hivyo kila mmoja huulizwa aliyo yafanya akiwa kaburini mwake, na kupewa thawabu kwa matendo mema aliyo yatenda na kuadhibiwa juu ya matendo mabaya na kutokana na hayo Mtume (s.a.w) akasema: (Kaburi ima ni shimo kati ya mashimo ya moto, au ni bustani kati ya mabustani ya peponi) [1] na hali ya mwanadamu akiwa kaburini kwa mfano na kwa kutaka kukuletea karibu maana na hali yake ni kuwa: ni kama hali ya mtu alie lala ambae anaota ndoto nzuri na kufurahi kwa ndoto hiyo, au kuota ndoto mbaya na kuteseka na kuadhibika kwa ndoto hiyo, wakati ambapo yule ambae humkaribia yule mtu alie lala na kumuona, hafahamu ya kuwa yuko kwenye raha au kwenye adhabu, vilevile walio hai huwaoni watu walio kufa katika hali ya kuwa ni vilivyo haribika, ama kujua ya kuwa wana adhibiwa au wako kwenye neema, hawalihisi hilo na hilo linatokana na ukweli kuwa vipimo katika ulimwengu wa barzakh ni vipimo vipya tofauti na vipimo vya duniani, na havifanani na vipimo vya maisha ya kidunia ambavyo tunavifahamu na tumevizowea.


2-Kiama: Nayo ni kuwa baada ya kuvifufua viwiwili hivi na kuvitoa kwenye makaburi, kiasi kwamba Mwenyezi Mungu mtukufu atavifufua katika siku hiyo vyote katika jangwa kubwa na pana kwa ajili ya hesabu na malipo na huko kuwekwa mahakama kubwa na kuwekwa vipimo na mahakimu kuhudhuria-nao ni mitume wa Mwenyezi Mungu na mawasii wao-na kugawiwa madaftari ya matendo: Nyaraka za matendo ya waja na mashahidi kwa ajili ya kutoa ushahidi, na viungo vya mwanadamu kukiri juu ya matendo yaliyo tendwa na mwanadamu na kuyafanya, na waumini wale ambao walifanya matendo mema duniani kuneemeka kwa kuingia peponi na waovu wale ambao walikuwa wakitenda maovu duniani kuwa katika hali mbaya ya uovu na kuingia motoni. Kwa hivyo ni juu ya mwanadamu kujitahidi kwa kadri ya uwezo wake katika kutekeleza matendo mema na kujiepusha na matendo maovu, ili asije kuwa muovu huko katika Akhera uovu wa milele na milele, uovu usio kuwa na makimbilio wala muokozi, kiasi kwamba waovu watabakia jela wakati wote na wakiwa kwenye adhabu ya milelel.

Mwenyeziu Mungu anasema:
(فمن يعمل مثقال ذ رة خيرا يره. ومن يعمل مثقال ذ رة شرا يره)
[2] Mwenye kufanya matendo ya kheri hata kama ni kiasi cha tembe moja atayaona. Na mwenye kufanmya matendo ya shari kiasi cha tembe moja atayaona.
________________________________________

[1] - Rejea kwenye kitabu Al-aamaaly cha Shekh Mufiid, ukurasa 265, majlis ya thalathini na moja (31). [2]- Suratuz-zilzaalah aya 7-8.
SEHEMU YA PILI
MATAWI YA DINI
Kabla ya kuanza kubainisha na kufafanua sehemu ya pili katika mafunzo ya juu ya Uislaam, hapana budi kuashiria hapa ya kuwa sehemu ya kwanza ya mafunzo ya kiislaam ya hali ya juu na yaliyo matukufu yaani: Usulud-dini ambazo tumezi zungumzia, ni lazima mwanadamu aziitakidi au awe na itikadi nazo-kwani misingi hiyo ndio inayo husiana na ukafiri na itikadi- kutokana na ijtihadi na kwa kutegemea dalili na wala haitoshi kwenye misingi hiyo kujitegemeza sehemu fulani au kwa mtu fulani na kumfuata mtu huyo.

Wakati ambapo Furuud-dini (matawi ya dini), ambayo hivi sasa tuko mbioni kuyafafanua na kuyazungumzia, hakika matawi hayo yameenea na kuzihusu sehemu na nyanja zote za maisha na yanazihusu harakati zote za mwanadamu na matendo yake yote kabla ya kuzaliwa kwake mpaka baada ya kufariki kwake na maranyingi mwanadam-kwa sababu ni mambo yanayo husiana na matendo kama harakati za mwanadamu na kutulia kwake na utendaji au utekelezaji wa mambo ya aina tofauti na mabadiliko-hawezi kufanya ijtihadi (kujitahihi) katika mambo yote hayo na kufahamu hukumu zake kutokana na dalili zake kwa uchambuzi wake ulio tajwa katika vyanzo vine vya sheria: Qur'ani tukufu, Sunna sharifu- Yaani hadithi za Mtume (s.a.w) na riwaya za Ahlul bayti (a.s)- na Ijmaa (Makubaliano ya wanazuoni) na Akili, kwa hivyo Uislaam ukajuzisha (ukamruhusu) kwa mwanadamu kumfuata mujtahidi alie kusanya masharti ya kufuatwa (kufanyiwa taqliid) kwenye mas'ala hayo na kurejea kwake katika mas'ala hayo kwa ajili ya kumfanyia wepesi na kumrahisishia mambo.


Ndio, hakika matawi ya dini ni mengi sana na sisi tuta ashiria yale yaliyo muhimu sana nayo ni kumu yaliyo maarufu, kisha tutabainisha na kufafanua yale ambayo yanahitaji kufafanuliwa kati ya hayo inshaa allah taala ama matawi hayo kumi yaliyo maarufu ni kama yafuatayo:
1-Sala
2-Saumu (Funga)
3-Khumsi
4-Zaka
5-Hajji
6-Jihadi
7-Kuamrisha mema
8-Kukataza maovu
9-Kuwatawalisha mawalii wa Mwenyezi Mungu
10-kujhitenga na kujiepusha na maadui wa Mwenyezi Mungu
Kwa kuyafahamu hayo ni jambo lililo wazi kuwa matawi haya pamoja na kuongezea matawi mengine kama uuzaji (bayii) na ununuzi na Nikah (Ndoa) na Talaka, Kisasi na Diyaa (fidia), hayo yamefafanuliwa na kufanyiwa bahthi kwa upana zaidi katika kitabu hiki-katika kifungu cha masaail-lakini baadhi yaliyo muhimu kati ya hayo yamebakia na ambayo ni katika mambo yaliyo sambamba na yenye kuwiana na zama hizi tunazo ishi, kama jamii ya wanadamu na nidhamu ya kijamii na kisiasa, Uchumi, Jeshi na nguvu zadola, kama Jeshi la ulinzi na polisi, Mahakama na utoaji hukumu, Utamaduni na Vyombo vya habari, Afya na nyenzo za tiba, Uhuru wa kila mtu mmoja mmoja na uhuru wa jamii na mengineyo, haya ndio ambayo tutayazungumzia katika sehemu hii kwa utashi wake Allah.


JAMII NA DOLA (NIDHAM) LA KIISLAAM
Hakuna shaka ya kuwa Uislaam unayo nidhamu maalum ya utawala na uendeshaji wa mambo ya kijamii, kama ambavyo hakuna shaka ya kuwa nidhamu hii maalum ya kiislaam imekuwa ikitekelezwa katika nchi za kiislaam kwa muda wote wa karne kumi na tatu (13) mpaka lilipo anguka dola la kiislaam kabla ya zaidi ya nusu karne -sawa utekelezaji huo ulikuwa ni utekelezaji kamili wa kanuni zote au ulikuwa ni utekelezaji pungufu- Kisha mtu ana weza kusikia ya kuwa utamaduni wa kiislaam (Al-hadharatul- islaamiyyah) ulikuwa ni utamaduni wa aina yake na bora kwa kiwango kikubwa na ulio pituka tamaduni zingine zote, na anaweza kusikia ya kuwa Uislaam-kutokana na hekima za kanuni zake zitokazo mbinguni na zilizo na uadilifu-umebeba jukumu la kutatua matatizo yote ya ulimwengu na kwamba kanuni hizo lau kama zitatumika na kurudishwa kwenye utawala, dunia itabadilika na kuwa pepo yenye neema na watu kuishi kwenye kivuli na neema zake raha mustarehe, na wangeishi maisha mema na yenye raha tele.


Kwa msingi huo: Basi nidhamu hiyo ni ipi? Na je kuna uwezekano wa Nidhamu na Utawala wa kiisalam kurudi tena kwenye uhai katika zama hizi za upanukaji wa dunia na maendeleo ya kianga na maendelo ya atomi na katika zama za maendeleo ya Internet na kupanuka kwa habari na vyanzo vyake? Na ikiwa Uislaam utachukua Utawala vipi utaweza kutatua matatizo yaliyopo ya kiulimwengu? Hakika haya ni maswali yanayo paswa kupatiwa majibu……


Na Pengine-majibu ya maswali tutakayo yataja hapa -yaka amsha hali ya mshangao na kustaajabu na msomaji kupigwa na butwaa na kudhania ya kuwa sisi tunazungumzia kuhusu mji ulio bora kabisa, pamoja na kuwa sisi tuna maandalizi kamili na tuko tayari kuondoa mshangao huo na kustaajabu huko kwa kutoa dalili na ushahidi wa kiisalaam juu ya majibu hayo,[1] na kutoa mifano hai na ya wazi kabisa kutoka kwenye historia ya utawala wa kiislaam ulio safi na halisi, jambo linalo thibitisha uwezo wa Utawala na Nidhamu ya kiislaam kurudi tena na kwa mara nyingine kwenye uhai na kushika hatamu ya uongozi na kuendesha mambo kwa ujasiri kamili na kwa umadhubuti bila kuteteleka, kwani Nidhamu ya kiisallam ndio Nidhamu pekee kati ya Nidhamu zote za ulimwengu- kuanzia hizo za zamani na za hivi sasa na zitakazo jitokeza kwa siku za baadae-kutokana na hekima za kanuni na sheria zake zitokazo mbinguni- yenye uwezo wa kuuendesha ulimwengu wenye maendeleo na ulio funguka au ulio wazi, uendeshaji uwezao kuufikisha kwenye matarajio yake na kuyathibitisha matumaini yake na kuutatulia matatizo yake na kuuondolea matatizo unayo kabiliana nayo na kuuondolea mambo yanayo usibu kama Uovu Madhara Ujinga Maradhi na kuufikisha ulimwengu huo kwenye ukingo wa Amani na Matumaini na kuufikisha kwenye ufukwe wa sa'aada na Amani, na Nidham hii imekusanya sababu na nyenzo zote za kuuletea maendeleo na kuufisha kileleni na kuyathibitisha yote ayatakayo mwanadamu katika nyanja hizi: kama Siasa Uchumi Uhuru na mengineyo ambayo tutayaelezea kwa muhtasari:[2]


UISLAAM NA SIASA
SWALI:
Je katika Dini ya kiislaam kuna siasa?
JAWABU:
Ndio, ndani ya Uislaam kuna sehemu au fungu bora kabisa kati ya mafungu ya siasa na kuna aina nzuri kabisa kati ya aina za idara na uendeshaji wa nchi na wananchi (waja wa Mwenyezi Mungu).
SWALI:
Je utawala katika Uislaam ni utawala wa kijamhuri au ni utawala wa kifalme?
JAWABU:
Utawala katika Uislaam si utawala wa kijamhuri wala wa kifalme-kwa maana ya kiistilahi ya maneno hayo yalivyo elezwa kwenye kamusi za ulimwengu wa kimagharibi (yaani kama yanavyo elezwa kwenye makamusi ya nchi za magharibi katika zama hizi-bali ni utawala wa mashauriano ya watu na inasihi kuuita kuwa ni utawala wa kijamhuri, kutokana na kuwa ni utawala unao tegemea mashauriano ya wananchi, kwani katika Uislaam hakuna utawala wa kifalme wa kurithishana.
SWALI:
Ni zipi sifa za mtawala (kiongozi) wa kiislaam?


JAWABU:
Kiongozi wa kiislaam ni mtu muumini, mwenye elimu ya sheria ya dini ya kiislaam kikamilifu na mwenye kufahamu mambo ya kidunia na mwenye kusifika na sifa ya uadilifu kikamilifu, kwa hivyo basi mtu yeyote atakae kamilisha masharti haya na watu wengi kumridhia, basi anakuwa mtawala na akipungukiwa na moja wapo kati ya masharti haya atauzuliwa na kutolewa kwenye cheo chake kwa haraka sana lakini ikiwa umma (watu) hawakuridhia abakie kwenye cheo chake hicho na kuwa raisi, na wanayo haki ya kumbadilisha na kumuweka mwingine alie kusanya masharti hayo.
SWALI:
Ni nani anae mteua mtawala wa kiislaam?
JAWABU:
Sehemu kubwa ya umma (watu walio wengi) na hii inahusika tu ikiwa mtawala huyo au kiongozi huyo si maasuum alie teuliwa na Mwenyezi Mungu alie takasika na mtukufu kama Mtume na maimamu watwaharifu (a.s)…..