MISINGI YA DINI NA MENGINEYO
 
IMAM WA TISA: IMAM JAWAAD (A.S)
Yeye ni Imam Mohammad bin Ali Al-jawaad (a.s) na mama yake ni Sayyidah Sabiika, alizaliwa (a.s) siku ya Ijumaa tarehe (10) katika mwezi mtukufu wa Rajab, mwaka (195) hijiria, katika mji wa Madinatul munawwarah na kufa shahidi kwa sumu katika mji wa Baghdaad, mwishoni mwa mwezi wa Dhul-qaadah (mfungo pili) mwaka (220) hijiria, na mwanae Imam Al-hadiy (a.s) kusimamia maandalizi ya mazishi yake na kumzika kwenye maburi ya Makuraishi pembezoni mwa kaburi la babu yake Muusa bin Jaafar (a.s) katika mji wa Kaadhimiyyah mahala lilipo kaburi lake kwa hivi sasa.

Na Imam (a.s) alikuwa ni mjuzi zaidi kati ya watu wa zama zake na mbora zaidi kuliko watu wote, mkarimu, pia mwingi wa kutoa na mwenye vikao vizuri, na alikuwa ni mwenye tabia njema, mfasaha na kila alipo kuwa akipanda mnyama wake hubeba Dhahabu na Fedha na hakuna aliekuwa akimuomba isipokuwa humpatia, na alie kuwa akimuomba pamoja na wingi wao alikuwa hampatiii chini ya Dinari Khamsini (50) na alie kuwa akimuomba kati ya shangazi zake alikuwa hampi chini ya Dinari ishirini na tano (25).


Na miongoni mwa elimu yake kubwa ambayo ilidhihiri kwa watu: Ni kuwa wanazuoni thamanini kati ya wanazuoni wa miji mbalimbali walikusanyika kwake baada ya kurudi kwao kutoka kwenye ibada ya hijja na kumuuliza kuhusiana na mas'ala mbali mbali na yeye (a.s) kuwajibu, namiongoni mwa mambo ya ajabu yaliyo simuliwa kutoka kwake (a.s) ni kuwa watu wengi walikusanyika kwake na kumuuliza mas'ala thelethini elfu-katika kikao kimoja nacho ni kikao kiitwacho kwa siku hizi kwa jina la kongamamno, kongamano ambalo hufanyika na kuendelea kwa muda wa siku kadhaa na Imam kuwajibu mas'ala hayo bila kusita kufanya hivyo wala kukosea na wakati huo akiwa na umri wa miaka tisa (9), lakini jambo kama hili si jambo la ajabu na la kushangaza kutokea kwa Ahlul bayti-watu wa nyumba ya Wahyi na mahala alipokuwa Jibril (a.s) akitelemka akiwa na Qur'ani na hasa baada ya Qur'ani kuzungumzia kuhusiana na kupewa kwa Issa bin Maryam kitabu na Utume hali ya kuwa bado yuko kwenye kitanda chake akiwa mtoto mchanga. Kisha ni kuwa khalifa Alimuoza binti yake na hilo lilifanyika baada ya kumtahini kwa maswali (mas'ala) muhimu na kuyajibu yote-katika kisa mashuhuri.


IMAMA WA KUMI: IMAM AL-HADIY (A.S)
Yeye ni Imam Ali bin Mohammad Al-hadiy (a.s) mama yake ni Sayyidah Samanah. Alizaliwa (a.s) katika mji wa Madinatul-munawwarah siku ya Ijumaa tarehe (2) mwezi mtukufu wa Rajab, mwaka (212) hijiria na kufa shahidi kwa sumu kwenye mji wa Samarraa siku ya juma tatu tarehe (3) mwezi wa Rajab, mwaka (254) hijiria, na mwanae Imam Askariy (a.s) kusimamia maandalizi ya mazishi yake, na kumzika ndani ya nyumba yake kwenye mji wa Samarraa mahala lilipo kaburi lake kwa hivi sasa na mahala kilipo lazwa kiwili wili chake kitukufu. Na Imam (a.s) alikuwa ni mtu bora kati ya watu wa zama zake na alikuwa ni mwenye elimu zaidi na alie kusanya fadhila zote na mkarimu sana na mwingi wa kutoa na alikuwa ni mwenye maneno laini na aliekuwa akimuabudu sana Mwenyezi Mungu na mwenye sera nzuri nasafi na mwenye tabia njema.


Na miongoni mwa ukarimu wake ni kisa kilicho pokelewa na (Ardabiliy) katika kisa chake ya kuwa: Khalifa alimtumia Dirham elfu thalathini, Imam akampatia bedui mmoja wa Al-kufa kama zawadi na akamwambia: Toa kiasi ulipe madeni yako na kiasi kitakacho bakia kitumie kwa ajili ya matumizi na mahitaji ya familia yako na ahali zako na utusamehe. Yule bedui akamwambia Imam: Ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu hakika deni nililo kuwa nalo halifikii theluthi ya pesa hii. (Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kufahamu vema mahala pakuuweka ujumbe wake), na akachukua pesa zile na kwenda zake.[28]


IMAM WA KUMI NA MOJA: IMAM ASKARIY (A.S)
Yeye ni Imam Hassan bin Ali Al-askariy (a.s) na mama yake ni Sayyidah Hadiitha. Alizaliwa katika mji wa Madinatul-munawwarah siku ya Ijumaa tarhe nane (8) mwezi wa Rabiul-aakhir, na inasemekana kuwa amezaliwa tarehe kumi na mbili (12) Rabiul-aakhir [29] mwaka (232) hijiria na kufa shahidi kwa Sumu siku ya Ijumaa tarehe nane (8) mwezi wa Rabiul-awwal mwaka (206) hijiria, na mwanae Imam Hujjatul-muntadhar (mwenye kungojewa) ndie alie simamia maandalizi ya mazishi yake na kumzika karibu na kaburi la baba yake Imam Al-hadiy (a.s) katika mji wa Samarra, mahala ambapo ndipo lilipo kaburi lake kwa hivi sasa.


Na Imam (a.s) alikuwa ni mfano wa juu kabisa katika ubora, elimu, utoaji, sharafu, furaha na ukarimu, ibada, unyenyekevu na tabia zingine nyingi njema, na alikuwa ni mfano wa kuigwa na kigezo chema kwa wengine, na alikuwa ni mwenye urefu wa wastani na mzuri wa umbile, mwenye uso mzuri na kiwiliwili cha wastani, mwenye heshima na hadhi kubwa kwenye nyoyo na mwenye nafasi ya juu na tukufu katika nafsi za watu, na Imam (a.s) alikuwa akimfanana sana babu yake Mtume (s.a.w) katika tabia zake na mwendo wake mwema na uzuri wa kuishi vema na watu.


Na miongoni mwa visa vya ukarimu wake ni kisa kilicho pokelewa na Ismail kisemacho: Nilimkalia na kumsubiri Imam (a.s) katikati ya njia, alipo fika na kupita mahala nilipo kuwa nikamueleza ufukara wangu. Imam akasema (a.s): Unaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwa uongo kwani umefukia Dinari miambili chini ya Ardhi na kusema kwangu maneno haya si kwa sababu ya kuto taka kukupa, ewe ghulam (Mhudumu) mpatie ulicho nacho, akasema: Yule mhudumu akanipatia Dinari mia moja.[30] Na kuna mtu mwingine alimwendea Imam-alipo sikia ukunjufu wake na ukarimu wake-na alikuwa akihitaji Dirhamu mia tano, Imam (a.s) akampatia Dirham mia tano na kumuongezea Dirhamu zingine mia tatu.[31]

Na kwa hakika watu wote walitoa ushahidi na kuthibitisha ubora wake na ukarimu wake, hata wakiristo walimshuhudia (a.s) ya kuwa yeye anafanana na masihi (Yesu) katika ubora, elimu, ukarimu na miujiza yake, na Imam (a.s) alikuwa ni mwenye kufanya sana ibada, akisali sala za usiku (tahajjud) daiama na alikuwa ni mwenye mandhari ya wema, na mwenye heba kubwa.


IMAM WA KUMI NA MBILI: IMAM AL-MUNTADHAR (A.S)
(Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake) Yeye ndie Imam na Al-hujjatul-mahdiy (a.s), Mohammad bin Hassan (a.s) na mama yake ni Sayyidah Narjis. Alizaliwa (a.s) katika mji wa Samarraa usiku wa nusu ya mwezi wa Shaaban, mwaka (255) hijiria. Na yeye (a.s) ndio hoja wa mwisho wa Mwenyezi Mungu juu ya ardhi na Khalifa wa mwisho wa Mtume (s.a.w) na Imam wa mwisho wa Waislaam, maimam ambao ni kumi na mbili na Mwenyezi Mungu-kwa utashi wake-ameurefusha umri wake mtukufu katika Dunia hii ili ardhi isibakie bila hujja wa Mwenyezi Mungu, kwani kama kusinge kuwa na hujja basi ardhi inge didimia pamoja na watu wake na yeye Imam haonekani kwa watu na Mwenyezi Mungu atamdhihirisha katika Aakhiriz-zamani (Zama za mwisho) baada ya Dunia kujawa na dhuluma na ujeuri (uovu), ili aijaze dunia hiyo kwa uadilifu na usawa.


Hakika Mtume (s.a.w) na maimam watwaharifu walitoa habari ya kuwa yeye atakuwa na ghaibah (Atatoweka na kuto onekana) kwa muda mrefu, na hatakuwa thabiti kwenye juu ya Uimam na wilaya yake na kumuamini isipokuwa yule ambae Mwenyezi Mungu ameujaribu moyo wake kwa Imani, na katika siku za ghaiba yake atakuwa katika hali ya kuwafikishia manufaa watu wa Ardhini kama jua lifikishavyo manufaa na faida zake kwa watu hao hata kama litakuwa limefunikwa na mawingu, na Mwenyezi Mungu atambakiza hai mpaka utakapo fika wakati wa kudhihiri kwake, na hapo kudhihiri kwa idhini yake Mwenyezi Mungu mtukufu na kuimiliki (kuitawala) Dunia yote na kueneza uadilifu na usawa Duniani na kueneza Uislaam na misingi yake yote na kuitekeleza Qur'ani na amri zake kwa watu wote na katika nyanja zake zote za maisha, na hapo Kheri kuenea na saada kutangaa kwenye miji yote na kuwaenea waja wote na kuthibitika kauli yake Mwenyezi Mungu isemayo:
[32]
ليظهره علي الدين كله ولو كره المشركون)

Ili auidhihirishe Uislaam juu ya dini zote hata kuma washirikina watachukia. Ewe Mwenyezi Mungu harakisha faraja yake na kufanye kwepesi kudhihiri kwake na utujaalie tuwe miongoni mwa wasaidizi na answari wake. Baada ya hayo ni jambo lililo wazi ya kuwa Imam Al-mahdiy (a.s) alipokuja kuandaa mazishi ya baba yake Imam As-kariy (a.s) na kumsalia watawala waovu walifahamu kuwepo kwa mrithi na mshika nafasi baada ya Imam Askariy (a.s) na hili lili waogopesha sana juu ya utawala wao na wakafikiria njia ya kumkamata na kumuua kama walivyo waua baba zake (a.s) ili kwa kufanya hivyo waokoke na kujinusuru na habari zilizo wafikia kutoka kwa Mtume (s.a.w) kuhusiana na habari za Imam wa kumi na mbili na kwamba yeye ndie ambae atakae maliza na kuangamiza utawala wa waovu na kuchukua utawala huo, na Imam Mahdiy (a.s) alikuwa ameamuriwa na Mwenyezi Mungu mtukufu kuwa kwenye ghaiba na kuto onekana kwa watu.


Na pindi majasusi wa Khalifa walipo muona na kuivamia nyumba yake akaghibu na kutoweka na kuto onekana kwa watu na kufichika kunako macho yao, na hilo lilifanyika kwa Imam kutokea kwenye mlango mwingine ulio kuwa wazi wenye kutokea kwenye Sirdab (nyumba ya chini) iliyo kuwa na mlango wa kutokea nje bila yeyote kati yao kumuona, na kutokana na ukweli kwamba sehemu ambayo ilikuwa ndio mahala pa kughibu kwake ni nyumba yake (a.s) Waislaam wakaifanya ile sehemu inasibishwayo kwake-katika mji wa Samarra-iliyo mashuhuri kuwa ni sirdab ya kughibu kwake, wakaifanya kuwa msikiti na mahala pa kufanyia ziara (kutembelea).

________________________________________
[1] Na inawezekana kuiffafanua kwa kutoa mfano ufuatao: nao ni kwamba chi ya Iraq na Japan baada ya vita vya pili vya dunia, chi hizi mbili zilikuwa katika msitari mmoja wa uharibifu na ubomozi na kurudi nyuma kimaendeleo, na kuto songa mbele kimaendeleo, lakini Japan baada ya muda kadhaa iliweza kuwa sawa bali kuzipita kwa kiwango kikubwa nchi na madola makubwa ya magharibi katika fani mbali mbali na katika viwanda, maendeleo na kushamiri kwake, wakati ambapo Iraq ilibakia ikiwa ni yenye kuharibika na kurudi nyuma kimaendeleo ikiwa masikini mwenye kuhitaji, ikiingiza kila kitu kutoka nje ya nchi hata ngano na nyama na hata nyuzi za kushonea na sindano, na wataalam pia wachambuzi wa mambo walio toa sababu na illa ya tofauti kati ya nchi mbili hizo ya kuwa viongozi wan chi ya Japan walikuwa ni wenye uwezo wa kuongoza na viongozi walio iongoza Iraq hawakuwa na uwezo wa kustahili kuongoza, haya ni katika upande wa kimadda, ama kwa upande wa kimaanawia pia ni jambo lililo wazi, kwa hivyo katika hadithi tukufu isemayo:
(من لا معاش له لا معاد له)
(asie kuwa na maisha hana marejeo) inamaanisha kuwa: Ufukara wa duniani ni hasara katika Akhera, ukionhezea na mengine yaliyo pokelewa kutoka kwa Fatuma Zahraa (a.s) ya kuwa amesema: Lau kama wasinge upora ukhalifa, dunia wa watu ing kuwa njema na yenye neema na Akhera yao pia na kusinge kuwa na tofauti tofauti kati ya watu wawili.


[2] Akiashiria kwenye kauli yake Mtume (s.a.w) isemayo:
الخلفاء من بعدي اثنا عشر
(Makhalifa baada yangu ni kumi na mbili) Na hadithi hii ni (Muttafaqun alyhi) yaani maulamaa wamewafikiana juu ya usahihi wake na ni mashuhuri kati ya waislaam wote Sunnah na Shia. Rejea kwenye kitabu Al-khiswal: ukurasa 478, hadithi ya 43, Makhalifa na maimamu naada ya Mtume (s.a.w), pia kitabu Al-irshaad: Mujallad wa 2/ 345 mlango Majaalis fin nassi….., Kashful ghummah: Mujallad wa 2/ 447, mlango wa Maa jaa'a minan-nassi………, Aalaamul waraa: Ukurasa 396 sehemu ya pili, Kitabu saliim bin Qaysi: Ukurasa 141 na rejea Sihahus- sittaza Ahli sunna.

[3] Inasemekana ya kuwa kufariki kwake ilikuwa ni baada ya siku 75 tanfu kufariki kwa Mtume (s.a.w) na inasemekana ilikuwa ni baada ya siku 95 tangu kufariki kwa Mtume (s.a.w).
[4] Rejea kwenye kitabu: ( Fatwimatuz-zahraa fil qur'ani) cha Ayatullahil udhmaa Sayyid Swaadiq Shiraziy (Mwnyezi Mungu amhifadhi
[5] Rejea kitabu Ihtijaaj ukurasa 354, mahojiano ya Abi Abdillahi (a.s) na katika majadiliano hayo kuna maneno yafuatayo: ya kuwa Mtume (s.a.w) alimwambia Fatuma: (Ewe Fatuma hakika mwenyezi Mungu anachukia kwa kuchukia kwako na anaridhia kwa kuridhia kwako).
[6] Kwa sababu Hajjaj- kama ilivyo nukuliwa kwenye historia ua kuwa alifukua makaburi laki moja akitafuta kaburi lake (a.s).
[7] Kasful ghumma: Mujaalad wa 1/ 263, na Al-ihtijaaj: Ukurasa 391.
[8]Al-aamaaly cha Shekh Swaadiq: Ukurasa 345, majlis ya Khamsini na tano (55).
[9] Al-jamal: ukurasa 81 na Al-fusuulul mukhtaar: Ukurasa 97.


[10] Al-manaaqib: Mujallad wa 3/ 257 katika sehemu izungumziayo: Fii musawaatihi ma'a Daud wa Twaluut wa Sulaiman (Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake).
[11] Suratu Al-imaraan aya 61.
[12] Na inasemekana kuwa ni Safar 28.
[13] Suratun-nisaa aya 86.
[14] Al-manaaqib: Mujallad wa 4/ 19 sehemu ya Makaarimul-Akhlaaq.
[15] Al-irshaad: Mujallad wa 2/ 127, mlango wa Twarafun min fadhaailil-hussein (a.s).
[16] Al-manaaqib: Mujallad wa 4/ 76, sehemu ya Fii ma'aali Umurihi. Na kuna riwaya kutoka kwa Ibnu Omar isemayo: Nilimsikia (s.a.w) akisema:
الحسن والحسين ريحانتاي في الد نيا.[17] Al-aamaliy cha Shekh Swaduuq: Ukurasa 57, hadithi ya 10.
[18] Ilalush-sharaai'I: Ukurasa 211, hadithi ya 2, mlango wa Al-illatullatiy min ajliha swaalahal hassan bin Ali (a.s).
[19] Na inasemekana ya kuwa: Mwaka w tano mwezi wa Shaaban.
[20] Na inasemekana ya kuwa ni tarehe 12 au 18 ya mwezi wa Muharram.
[21] Suratu Al- Imraan aya 134.
[22] Aalamul-waraa: Ukurasa 216, sehemu ya nne: Fii dhikri baadhi mu'ujizaatihi wa manaaqibihi wa Fadhaailihi.
[23] Na inasemekana kuwa ni: Tarehe mosi Mwezi wa Rajab.
[24] Uddatud-daiy: Ukurasa 248, mlango wa tano: Fiima Ulhiqa bidduaa wahuwa Adhikri.
[25] Na inasemekana ni Elfu ishirini.
[26] Attawhiid: Ukurasa 27, mlango wa Arrad alaa lladhiina qaalu Inna llah thaalithu.
[27] Rejea Nahjul balagha: Sharhu ya Ibnu Abil hadiid: Mujallad wa 1/ 188 kisa cha shuraa.
[28] Kashful- ghumma: Mujallad wa 2/374, Dhikru Imamul Aashir Abil Hassan Ali (a.s).
[29] Na inasemekana ni wa: nane.
[30] Al-irshaad: Mujallad wa 2/332, mlango wa Dhikru Twarafun min Akhbaar Abi Mohammad
[31] - Al-irshaad: Mujallad wa 2/326, mlango wa Dhikru Twarafun min Akhbaar Abi Mohammad.
[32]-Suratu-tawbah aya 33