HADITHI YA MUFAZZAL

 
N A B I I D A U D I
Je, Mtume huzini? Hawezi. Je, Mtume humnywesha mtu mvinyo? Hawezi. Ati Mtume humdanganya mtu ili amwue? Hawezi. Lakinu katika Biblia Mtume Daudi (a.s) amesingiziwa yote haya juu. Tazama kitabu cha pili cha Samweli, sura 11, aya 2-27, yasema hivi:"Ikawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, akatembea juu ya dari ya jumba la Mfalme: na alipokuwa juu ya dari aliona Mwanamke anaoga: naye huyo Mwanamke alikuwa mzuri sana, wa kupendeza macho. Naye Daudi akapeleka, akauliza habari za yule Mwanamke. Mtu mmoja akasema, Je: huyu siye bath-sheeba, binti Eliamu, mkewe Uria, Mhiti? Basi Daudi akapeleka wajumbe , akamtwa: naye akaingia kwake, naye akalala naye (maana yule mwanamke amekwisha kutakasika unajisi wake): kasha akarudi nyumbani kwake. Yule mwanamke akachukua mimba: basi akapeleka na kumwambia Daudi, akasema, Ni Daudi akapeleka kwa Yoabu, akisema, Unipelekae Uria kwa Daudi.. Daudi akamwambia Uria, Haya, Shuka nyumbani kwako, ukanawe miguu yako…wala hakushuka nyumbani kwako.Daudi akamwambia Uria, Je' hukutoka safarini? Mbona hukushuka nyumbani kwako? Naye Uria akamwambia Daaudi, Sanduku, la Israeili na Yuda wanakaa vibandani nami niende nyumbani kwangu kula na kunywa, na kulala na Mke wangu?… Naye Daudi akamwalika, akalala, akanywa mbele yake; naye akamlevya hata wakati wa jioni akatoka kwenda kulala kitandani mwake… lakini hakushuka nyumbani kwake. Hata ikawa asubuhi Yoabu Waraka, kusema, Mwekeni Uria mbele ya watu penye vita vikali, kisha ondokeni, mwache, ili apigwe akafe. Akamweka Uria mahali alipojua ya kuwa pana mashujaa… wakapigana na Yoabu,… Na yule mke wa Daudi, wakaanguka; Uria Mhiti naye akafa… Na yule mke wa Uria alipopata habari kuwa Uria mumewe amekufa, akamwomboleza mumewe. Hata maombolezo hayo yalipokwisha, Daudi akatuma mtu, akamtwaa akamtia nyumbani mwake; naye akawa mkewe… Lakini jambo lile alilolitenda Daudi, likamchukiza Bwana."


Je, umesikia kisa namna alivyofanya hila ya kumwua Uria; Na kwamba Daudi alizini na mke wa Uria baadaye akamlewesha ili apate kulala na mkewe, jambo lisiloridhisha, na kumpeleka Uria vitani kwa hadaa ili auawe, na wakatenda hata akauwawa? Basi sasa sikia tokeo la hayo kwa yule mwanamke mwenye mume aliyezini naye Daudi! Tazama Injili ya Mateyo, sura 1, aya ya 6-9, inasema hivi: " Yese akamzaa Mfalme Daudi. Daudi akamzaaa Sulemani kwa yule mke wa Uria." Vile vile tazama kitabu cha pili cha Samweli, sura 12, aya ya 9, inasema hivi:- Bwana, Mungu wa Israeli asema hivi: "Umempiga Uria, Mhiti, kwa upanga, nawe umemtwaa mkewe awe mke wako?" Basi sasa sikia iliokuwa ajabu zaidi!Agano zote mbili za sema kwamba Mwenyezi Mungu amemjaazi Mtume Daudi kwa kuwasalitisha wanawe juu ya wake zake hata wakazini nao! Tazama kitabu cha pili cha Samweli, sura 12, aya 11 na 12, inasema hivi:- Bwana asema hivi, Angalia, nitakuondokesha uovu katika nyumba yako, nami nitawatwaa wake zako mbele ya macho yako, na kumpa jirani yako, naye atalala na wake zako mbele ya jua hili. Maana wewe ulifanya jambo hili kwa siri; bali mimi nitalifanya jambo hili mbele ya Israili wote na mbele ya jua. Tena tazama sura16, aya 22, inasema hivi"- Basi wakamtandikia Absalomu hema juu ya nyumba darini; naye Absalomu akaingia kwa masuria ya babaye machoni pa Israeli wote.
NABII LUTU
Biblia haitoshelezi kusingizia kuwa licha ya kutenda uzinzi wa kawaida, Mtume alizini pia na binti zake.
Swali: Je, Mtume anaweza kuzini na binti zake au kulewa divai?
Jibu: Haiwezekani kamwe mambo hayo, yote ni masingizio tu. Kwani mwenye akili yeyote hawezi kufanya mambo kama haya: Sembuse Mtume? Basi tazama Biblia kitabu cha kwanza, sura ya 19, aya ya 30-38, inasema hivi: lutu akapanda kutoka Soari akakaa mlimani na binti zake wawili. Yule mkubwa akamwambia mdogo, Baba yetu ni mzee, wala hakuna mtu mume katika nchi atuingilie kama ilivyo desturi ya dunia yote. Haya, na tumnweshe baba yetu mvinyo, tukalale naye, ili tumhifadhie


Baba yetu uzao. Wakamnywesha baba yao mvinyo usiku ule, akaondoka huyo mkubwa akalala naye. Wala yeye hana habari alipolala wala alipoondoka. Ikawa siku ya pili , mkubwa akamwambia mdogo, tazama, nimelala jana na baba yangu, tumnyweshe tena baba yao mvinyo usiku ule akaondoka mdogo akalala naye wala yeye hana habari alipolala wala alipoondoka, Basi hao binti wote wawili wa wa Lutu wakapata mimba kwa baba yao. Yule mkubwa akazaa mwana, akamwita jina lake Moabu: huyo ndiye baba wa Wamoabi, hata leo . Na yule mdogonaye akazaa mwana akamwita jina lake Benabi: huyo ndiye baba wa Waamoni hata leo.


N A B I I Y A K O B O
Je, wadhani kuwa Mtume aweza kudanganya? Au kumbusu mwanamke mgeni? Au wadhani Mwenyezi Mungu huweza kupigana mieleka na Mtume Wake, na wala Asiwe Kumshinda?
Swali: Ati inawezekana Mtume ambusu mwanamke asiyemhusu?
Jibu: Mambo haya hafanyi mwenye akili yeyote sembuse Mtume wa Mungu.
Swali: Ati Mtume hushindana mweleka na Mungu?
Jibu: Sivyo kabisa, kwani Mwenyezi Mungu hana kiwiliwili hata mtu ashindana mweleka naye.
Swali: Ati Mtume hudanganya?
Jibu: Kudanganya ni aibu na Mtume amekamilishwa na Mwenyezi Mungu. Lakini katika Biblia yote hayo wamesingiziwa. Tazama kitabu cha Mwanzo, sura 29, aya 11, inasema hivi: Yakobu akambusu Raheli, akainua sauti yake akalia. Huyu Raheli akaolewa na huyu Yakobu baada ya miaka saba.Vile vile tazama sura ya 32, aya ya 24-30 inasema hivi: Yakobu akakaa peke yake; na mtu mmoja akashindana naye mweleka hata alfajiri…akamwambia, jina lake hutaitwa tena Yakobu, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu. Akambariki huko. Yakobu akapata mahali pale, penueli, maana alisema, Nimeonana na Mungu uso ka uso na nafsi yangu imeokoka. Vilevile tazama sura27, aya1-35 inaseama hivi: Ikawa Iseka alipokewa mzoe, na macho yake yamepofuka asione, akamwita Esau mwanawe mkubwa, akamwambia, Mwanangu…. Basi, nakuomba chukua mata yako, podo lako


Na upinde wako, ukaende nyikani uniwindie mawindo; ukanifanyie chakula kitamu namna ile niipendayo, ukiniletea, ili nile; na roho yangu ikubariki, kabla sijafa. Na Rabeka akasikia, Isaka aliposema na Esau mwanawe… Kisha Rebeka akatwaa mavazi mazuri ya Esau mwana mkubwa, aliyokuwa nayo nyumbani, akamvika Yakobu mwanawe mdogo… Akaja kwa baba yake, akasema, Babangu. Akasema, mimi hapa, Unani wewe mwanangu Yakobu akamwambia babaye, Mimi ni Esau, mzaliwa wako wa kwanza nimefanya kama ulivyoniambia.. Akasema, Niletee karibu nami nipate kula mawindo ya mwanangu, ili roho yangu ikubariki. Akamsogezea karibu,naye akala: kisha akamletea mvinyo, akanywa. Isaka, baba yake, akamwambia, Njoo karibu sasa, ukanibusu, mwanangu.


Akakaribia akambusu. Naye akasikia harufu ya mavazi yake, akambariki akasema… Ikawa Isaka alipokwisha kumbariki Yakobo ndiyo kwanza ametoka mbele ya Isaka baba yake, mara Esau ndugu yake akaja kutika katika kuwinda kwake … Isaka, baba yake, akamwuliza, U nani wewe? Akasema, Mmi ni mwanao, Esau, mzaliwa wako wa kwanza.Isaka akatetemeka tetemeko kuu sana, akasema… Nduguyo amekuja kwa hila , akachukua mbaraka wako." Ni ajabu mno na masingizio kwa Mtume kumbusu mwanamke, na kuhadaa , au kushindana mweleka na Mingu na kuchukua utume kwa nguvu na hadaa! Yaweza kuwa hayo ni kweli?


N A B I I S U L E M A N I
Kiongozi wa dini wa Biblia anashugulika kufanya mambo yaliyokatazwa na Mungu: moyo wake umeelekea kwenye masanamu: ana ufupi, moyo wake unapotoka na Mwenyezi Mungu. Je, uongozi gani huu ?
Swali: je , anaweza Mtume kutenda mamabo aliyoyakataza Mwenyezi Mungu?
Jibu: Haiwezekani kamwe.
Swali: Je , inamkinika moyo wa Mtume uelekeye kwenye masanamu?
Jibu: Haimkiniki kamwe hivyo.
Swali: Je, inawezekana Mtu ajenge nyumba ya kuabudia masanamu?
Jibu: Kabisa haiwezekani Mtume yeyote kufanya hivyo.
Swali: Ati inamkinika moyo wa Mtume upotoke na Mwenyezi Mungu?
Jibu: Haiwezekani Kamwe!LAKINI: Biblia katika kitabu cha Wafalme,Sura 11 , aya za kwanza inasema hivi: Mfalme Suleman akawapenda wanawake wengi wageni, pamoja na binti yake Farao… Na wa mataifa Bwana aliyowaambia wana wa Israeli, Msiingie kwenu: kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu yao. Suleimani akaambatana nao kwa kuwa penda. Akawa na wanawake saba binti za kifalme, na masuria mia tatu: nao wakeze wakamgeuza moyo Maana Ikawa, Suleimani alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake , afuate miungu mingine wala moyo wake haukuwa mkamilifu kwa Bwanba, Mungu wake , kama moyo wa Daudi baba yake.


Kwa kuwa Sulemani akamfuata Ashtorethi, Mungu wa Wasidoni, na Milkomu, chukizo la waamoni. Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, wala hakumfumfuata Bwana kwa utimilifu, kama Daudi baba yake. Suleimani akamjengea kemoshi, chukizo la wamoabi, mahala pa juu, katika mlima uliokabili Yerusalenu, na Moleki, chukizo la wana wa Amoni. Na kadhalika ndivyo alivyo wafanyia wake zake wa nchi za kigeni, waliofukiza uvumba, wakawatolea miungu yao dhabibu. Basi Bwana akamghadhibikia Sulemani kwa sababu moyo wake umegeuka, naye amemwacha Bwana, Mungu wa Israeli, aliyemtokea mara mbili, akamwamuru katika habari ya jambo lilo hilo asifuate miungu mingine: lakini yeye hakuyashika aliyoyaamuru Bwana.N A B I I M U S A
Je , umepata kusikia chuki baina ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake? Je, umepata kusikia kuwa Mtume ni dhalimu? La sivyo , basi soma haya:
Swali: Ati inamkinika iwe chuki na uaduwi kati ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake hadi atake kumuua
Jibu: Haimkiniki kamwe;
LAKINI: Biblia katika Agano jipya na Agano la kale inasema kama Mwenyezi Mungu alitaka kumuua Musa lakini mke wake Sipora ndio aliomwokoa!!! Tazama kitabu cha pili cha Musa , kiitwaacho KUTOKA, sura ya 4, aya mbali mbali: Bwana akamwamia Musa, hapo utakaporudi Misri, angalia ukazifanye mbele ya Farao zile ajabu zote nilizo-zitia mkononi mwako. Ili kuwa walipokuwa njiani mahala, pa kulala , Bwana akakutana naye akataka naye akataka kumwua. Ndipo Sipora akashika jiwe gumu na kuikata govi ya zungu la mwanawe, na kuibwaga miguuni pake akasema , Hakika wewe u bwana arusi wa damu kwangu mimi. Basi akamwacha. Ndivyo huyo mkewe akanena, u bwana arusi wa damu wewe kwa ajili ya kutahiri.Swali: Je , inawezekana Mtume awe dhalimu na kuamrisha wauawe watoto na mengineyo kama hayo, na kuteketeza majumba kwa moto?
Jibu: Mtume hawezi kuwa hivyo wala hawezi kamwe kutenda dhuluma. Lakini Biblia katika Agono jipya na Agono la kale husema kama Musa (a.s) alifanya hivyo" Tazama kitabu cha nne cha Musa, kiitwacho HESABU sura ya 31 aya mbalimbali:

Wana wa Israeli wakawachukua mateka wanawake wa Midiani na watoto wao: na ngonbe zao wote na mali zao zote, wakachukua nyara . Na miji yao yote, kila mahali walipokuwa wakikaa, na marago yao yote wakayateketeza nyara zote, na mateka yote , ya wanadamu na ya wanyama, . . . Basi Musa, na Eleazari kuhani, na wakuu wote wa huo mkutano, wakatoka nje kwenda kuwalaki nje ya marago. Musa akawakasirikia majemadari wa jeshi . .…Musa akawauliza, je mmewaponya wanawake wote hai? . . Basi kwa ajili hiyo mwueni kila mume katika hao watoto, na kila mwanamke aliyemjua mume kwa kulala pamoja naye . lakini hao watoto wote wa kike ambao hawakumjua mume kwa kulala pamoja naye, mtawaweka hai kwa hajili yenu.


Ukagawanye nyara mafungu mawili: Kati ya watu waliozoea vita, waliotoka nje waende vitandani . . . wanadamu jumla yao ilikuwa thelathini na mbili elfu, katika hao wa nawake ambao hawakumjua mume kwa kulala pamoja naye. Basi sasa na tuulize idadi gani waliangamizwa kwa kuona haram na uchungu? Bila ya shaka ni zaidi kuliko waliowachwa hai !! Kwa hivyo inatubidi tushukuru hiyo huruma na msamaha kwa kuwekwa hai watoto wa kike ambao hawakumjua mume kwa kulala pamoja naye: ijapokuwa tumeshajua kwamba (agano zote mbili) imesema katika kisa kingine ameuuwaua watu wote hata hawo watoto wa kike bikira?(Tazama kumbukumbu la Torati , sura 2 , kuanzia aya 31). Kisha Bwana akaniambia Tazama nimeanza kumtoa sihoni na nchi yake mbele yako: anza kuimiliki, upate kuirithi nchi yake. Ndipo Sihoni alipotutokea juu yetu, yeye na watu wake wote, kupigana huko Yahasa. Bwana, Mungu wetu, akamtoa mbele yetu, tukampiga yeye na wanawe, na watu wake wote. Tukatwaa miji yake yote wakati hou, tukaharibu kabisa kila mji uliokuwa na watu, pamoja na wanawake na wadogo :tusimsaze hata mmoja :ila ngombe zao tuliwatazama kuwa mawindo yetu, pamoja na nyara za miji tuliyoitwaa.Agano zote mbili ina haki ya kusema, kwa nini mnanilipizia kisasi? Kwa nini mimi ndio naliomsingizia Mtume Musa kuwauwa watu waume, wake na watoto? Kwani hamwangalii vipi amesingiziwa Mwenyezi Mungu, kwa kuwaamrisha wauwawe kila chenye roho hata wanyama? (tazama kumbukumbu la Torati, sura 20, kuanzia aya 13) Na Bwana, Mungu wako, autiapo mkononi mwako, mpige kila mume aliyemo kwa makali ya upanga: Lakini wanawake na watoto, na vilivyo mjini vyote, navyo ni nyara zake zote , uvitwae viwe mateka kwako: Nawe utakula nyara za adui zako alizokupa Bwana Mungu wako. Utaifanyia vivyo miji yote iliyo mbali sana nawe, isiyokuwa miji ya mataifa haya. Lakini katika miji ya mataifa haya akupayo Bwana Mungu wako, kuwa urithi, usihifadhi kuwa hai kitu chochote kipumzikacho: lakini uwaangamize kabisa, Mhiti, na Mwamori, na Mhivina Myebusi, kama alivyokuamuru Bwana, Mungu wako.Swali: je, inawezekana Mtume awe mkali anapozungumza na Mwenyezi Mungu na kumtaka amfutiliye mbali katika Utume?
Jibu: Haiwezekani kamwe: Lakini Biblia katika kitabu cha pili cha Musa kiitwacho KUTOKA sura 32, kuanzia aya 31 linasema hivi: Musa akarejea kwa Bwana, akasema Aa ' watu hawa wametenda dhambi kuu , wamejifanyia miungu ya dhahabu. Walakini sasa, ikiwa utawasamehe dhambi yao _ na kama sivyo, unifute, nakusihi , katika kitabu chako ulichokiandika.N A B I I I S A Y A
Swali: Je, inawezekana Mwenyezi Mungu amuamrishe Mtume wake atembee uchi kati ya watu kwa miaka na kwa nini? Kwa ajili ya ubarudhuli kwa ilhani yeye ni wa kupigwa mifano? Jibu: Haiwezekani kamwe kwa Mwenyezi Mungu kuamrisha hivyo, kwa sababu Mwenyezi Mungu Anakataza kukaa uchi mbele ya watu! Hii ni mambo ya kiwendawazimu lakini Biblia katika kitabu cha Nabii Isaya, sura ya 20 aya ya pili hadi mwisho wa aya ya nne inasema hivi:

Wakati huo Bwana alinena kwa kinywa cha Isaya, mwana wa amozi, akisema, Haya, uvue nguu ya magunia viunoni mwako, na viatu vyako migu Uni mwako. Naye akafanya hivyo akaenda uchi, miguu yake haina viatu. Bwana akasema, kama vile mtumishi wangu Isaya anavyokwenda uchi, hana viatu, awe ishara na ajabu kwa muda wa miaka mitatu juu ya Misri na juu ya kushi:vivyo hivyo Mfalme wa Ashuru atawachukua uchi, wafungwa wa Misri, na watu wa kushi waliohamishwa, watoto kwa wazee, hawana viatu, matako yao wazi Misri iaibishwe.N A B I I I B R A H I M U
Swali: Ati inawezekana Mtume asisadiki Maneno ya Mwenyezi Mungu hadi akamtaka thibitisho la ukweli wa maneno yake?
Jibu: Hasha Mtume kuwa na shaka juu ya maneno ya Mwenyezi Mungu hata atake ushahidi! Lakini agano mbili zamsingizia Mtume Ibrahim kwa hayo! Tazama kitabu cha kwa kwanza cha Musa, kiitwacho, Mwanza, sura ya 15 aya ya kwanza na ya saba, inasema hivi: Baada ya mambo likamjia Abramu katika njozi, likinena . . . . . .Mimi ni Bwana, niliyekuleta kutoka Uru wa Wakaldayo nikupe nchi hii ili urithi. Akasema, Ee bwana Mungu, ni pateje kujua ya kwamba nita Rithi? Akamwambia, Unipatie ndama wa miaka mitatu: na mbuzi mke wa miaka mitatu, na hua na mwana njiwa Akampatia hao wote, akaweka kila kipande kuelekea mwenzake, ila ndege hakuwapasua Hata tai walipotua juu ya mizoga Abramu akawafukuza. Basi tazama vipi hivi? Kuna uhusiano gani kati ya maneno ya mbele na baadaye. Naam (Agano) husimulia kisa namna hivyo ya kurukaruka na kutinga haina uhusiano na mwenziwe.N A B I I E Z E K I E L I
Sasa, Mungu wa Biblia anamwamuru Mtume mmoja kula mkate uliochanganywa na mavi ya mtu. Ubora wa mafundisho haya ni upi?
Swali: Ati Mwenyezi Mungu humuamrisha Mtume wake ale mkate uliokandwa na mavi ya binadamu? Kwa nini hivyo kuamrishwa?
Jibu: Haiwezekani kamwe Mola kamuamrisha Mtume wake hivyo! Lakini Biblia inasema hivyo! Tazama kitabu cha Nabii Ezekieli, sura ya 4, aya ya 12 inasema hivi: Nawe (Ezekieli) utakila kama mkate wa shayiri, nawe utakioka mbele ya macho yao juu ya mashonde yatokayo katika mwanadamu. Bwana akasema, Hivyo ndivyo wana wa Israeli watakavyo kula chakula chao, hali kimetiwa Unajisi, kati ya mataifa nitakakowafukuza.


Lakini Nabii Ezekieli alikuwa mwenye akili . . . atakula vipi mkate uliokandwa na mavi ya binadamu? Akataka msamaha kwa jambo hili la kuchekesha na Mwenyezi Mungu alimkubalia na akatukuka na akabadilishiwa mavi ya binadamu kwa mavi ya ngombe. Na katika sura hiyo hiyo, aya ya 14 na 15 , inasema hivi: Ndipo nikasema, Ee Bwana Mungu, tazama roho yangu haikutiwa unajisi: maana tangu ujana waangu hata sasa sijala nyamafu, wala nyama ichukizayo haikuingia kinywani mwangu. Ndipo akaniambia, Tazama, nimekupa mashonde ya ngombe badala ya mashonde ya mwanadamu, nawe utakipika chakula chako juu ya hayo.


Swali: Ati Mwenyezi Mungu humuamrisha Mtume wake kunyoa kichwa chake na ndevu zake? Kwa nini hivyo? Kwa jambo la upuzi tu! Lakini masikini Nabii Ezekieli alifikiwa na mambo ya kuchekesha. Akawa anakula mavi ya ngombe baada ya kuhurumiwa na kama si hivyo aliamrishwa ale mavi ya binadamu. Na mara akajigeuza kwa kujinyoa kichwa na ndevu zake. Kitabu cha Nabii Elekieli, katika sura ya 5, aya ya 1, inasema hivi:


Nawe, mwanadamu ujipatie upanga mkali, kama wembe wa kinyozi ujipatie, ukaupitishe juu ya kichwa chako na ndevu zako:kisha ujipatie mizani ya kupimia, ukazigawanye nywele hizo. Theluthi ya hizo zinakapotimia: nawe utatwaa thelusi, na kuipiga kwa upanga pande zote; nawe utatawanya theluthi ichukuliwe na upepo. Baadaye inaonyesha makusudi ya kutoa mfano huo ni kuwajulisha kwamba, theluthi ya watu wa Orshibna watakufa kwa tauni, na kwa njaa watakomeshwa, na theluthi watakomeshwa, kwa upanga, na theluthi atawatawanya kwa upepo. Tazama mifano na wakatolewa mifino! Angalia mfano huu na mwenye kufanyika kwake mfano huo.Swali: Ati inapendeza kwa Mwenyezi Mungu amkufishe mke wa Mtume kwa ajili ya kuonyesha mfano ya kijinga kwa ilhali ingewezekana kueleza kwa maneno tu?
Jibu: Ndio… Mtume Ezekieli alipatwa na masaibu mawili (katika agano zote mbili) na akawa mifano ya kiupuzi, bila shaka si halali kwa Mwenyezi Mungu na Mitume wake na mambo kama hayo. Lakini Biblia katika kitabu cha Nabii Ezekieli Sura ya 24 kuanzia aya ya 15 hadi mwisho wa aya 24 inasema hivi: Neno la Bwana likanijia tena, kusema, Mwanadamu, tazama, ninakuondolea kwa pigo moja tunu, mteule wa macho yako mke wako) wa lakini hutaomboleza wala yasiohuruzike machozi yako. Ugua, lakini si kwa sauti ya kusikiwa:usifanye matanga kwa ajili yake Yeye aliyekufa: jipige kilemba chako, ukavae viatu vyako, wala usile chakula cha watu. Basi nalisema na watu asubuhi: Na jioni mke wangu akafa: nami nalifanya asubuhi kama nilivyoagizwa. Watu hao wakaniambia, je! hutaki kutuambia maana ya mambo haya kwetu, hata umefanya kama vile ufanyavyo. Neno la Bwana lilinijia, kusema, uwaambie nyumba ya Israeli, Bwana Mungu asema hivi: Angalieni, nitapatia unajisi patakatifu pangu, fahari ya uwezo wenu, mahala pa kutamaniwa na machoN A B I I H O S E A
Iwapo hayo hayatoshi, angalia jinsi Mwenyezi Mungu anavyomwamuru Mtuma mmoja kutwaa mwanamke na kuzini naye. Na baada Mtume Ezekieli agano zote mbili inamlenga mishale za mifano za upuzi kumkusudia Mtume Hosea. Basi natuulize.
Swali: Ati inaelekea kwamba amuamrishe Mtume wake akatwae na kumwoa mke wa uzinzi, na watoto wa uzinzi? Na kwa nini? Kwa sababu nchi ilifanya uzinzi, kwa kumwacha Bwana. Au ilikuwa onyo na mawaidha kwa nyumba ya Israeli kwa kuwataja majina ya watoto aliwazaa yule mwanamke, na kutaja vipi alizini?
Jibu: Hasha! Mwenyezi Mungu kamwe hakumuamrisha Mtume wake yeyote kufanya hivyo. Lakini Biblia katika kitabu cha Mtume Hosea sura ya kwanza, toka aya ya pili hadi mwisho wa aya ya nne, inasema: Hapo kwanza Bwana aliponena kwa kinywa cha Hosea, E nenda ukatwae mke wa uzinzi: kwa maana nchi hii inafanya uzinzi, na watoto wa uzinzi: Kwa maana nchi hii inafanya uzinzi mwingi, kwa kumwacha Bwana. Basi akaenda akamwoa Gomeri, binti Didlaimu:naye akachukua mimba, akamzalia mtoto mwanamume. Bwana akamwambia, Mwite jina lake Yezreeli: Kwa maana bado kitambo kidogo, nitaipatiliza nyuba ya YehuDamu ya Yezreeli, na kuukomesha ufalme wa nyumba ya Israeli. Msihini mama yenu, msihini; kwa maana yeye si mke wangu, wala mimi si mume wake; na ayawekee mbali mambo ya uasherati wake yasiwe mbele ya uso wake, na mambo ya uzinzi wake yasiwe kati ya maziwa yake; nisije nikamvua nguo zake akawa uchi, nikamweka katika hali aliyokuwa nayo siku ya kuzaliwa kwake, na kumfanya kama jangwa, na kumweka kama nchi kame. Na kumfisha kwa kiu; naam , sitawaonea rehema watoto wake: kwa maana ni watoto wa uzinzi. Maana mama yao amezini; yeye aliyewachukua mimba ametenda mamabo ya aibu.


Na katika sura ya pili, aya ya pili inaeleza hivi: Bwana akanwambia, E nenda tena, mpande mwamanke apendavye na rafiki yake, naye ni mzini; kama vile Bwana awapandavyo wana wa Israeli, Ingawa wanaigeukia miungu mingine, na kupenda mikte ya zabibu kavu. Basi nikajinunulia mwanamke huyo kwa vipande kumi na vitano vya fedha, na homeri moja ya shayiri, na nusu ya homeri ya shayiri; nami nikamwambia, utatawa kwa ajili yangu siku nyingi; hutafanya mambo ya ukahaba, wala ingawa wanaigeukia miungu mingine, na kupenda mikte ya zabibu kavu. Basi nikajinunulia mwanamke huyo kwa vipande kumi na vitano vya fedha, na homeri moja ya shayiri, na nusu ya homeri ya shayiri; nami nikamwambia, utatawa kwa ajili yangu siku nyingi; hutafanya mambo ya ukahaba, wala hutakuwa mke wa mtu awaye yote; nami nitakuwa hali iyo hiyo kwa ajili yako. Kwa maana wana wa Israeli watakaa siku nyingi bila mfalme , wala mtu mkuu.


Kisa kama hii ambao ni hasara kuandikwa vitabuni licha kuandikwa katika kitabu (tukufu). Na ikiwa Mtume hafanyi hivyo basi nini itakuwa kwa watu wengine? Namikiwa mkubwa wa nyumba anapenda jambo Fulani baya, basi hakuna shaka watu wa nyumbani wote wataingia katika maovu yote Isitoshe hayo ampende mwanamke apaendwaye na rafiki naye ni mzini kama vile Bwana awapendavyo wana wa Israeli. Maneno kama hayo Kufananisha na Mwenyezi Mungu yafaa?


NABII HARUNI
Biblia Yapaswa ufundisha upweke wake Mwenyezi Mungu. Lakini Mtume wake huabudu miungu! Je, hiki si kinyume?
Swali: Je inamkinika Mtume kutengenza masanamu nakuwapoteza watu kwa kuabudu masanamu?
Jibu: Haiwezekani kamwe kwani kuabudu masanamu ni kazi ya makafiri na mushriki na Mwenyezi Mungu hapendezwi na hayo kabisa. Lakini Biblia katika kitabu cha pili cha Musa, kiitwacho kutoka, sura ya 2 kuanzia aya ya kwanza hadi mwisho wa aya ya sita, inasema:


Hata watu walipoona ya kuwa Musa amekawia kushuka katika mlima, wakakusanyana wakamwendea Haruni, wakamwambia, Haya! Katufanyizie miungu itakayokwenda mbele yetu, kwa maana Musa huyo aliyetutoa katika nchi ya Misri hatujui yaliyompata. Haruni akawaambia, Zivunjeni pete za dhahabu zilizo katika masikio ya wake zenu, mkaniletee. Watu wote wakazivunja pete za dhahabu zilizo katika masikio yao, wakamletea Haruni. Akaipokea mikononi mwao akaitengeneza kwa patasi, akaifanya iwe sanamu ya ndama kwa kuiyeyusha: Na wakasema, Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri. Naye Haruni alipoona jambo hili, akajenga madhabahu mbele yake; Haruni akatangaza akasema, Kesho itakuwa siku kuu kwa Bwana. Wakaondoka asubuhi na mapema, wakatoa dhahabu, wakaleta sadaka za amani, watu wakaketi kula na kunywa, wakaondoka wakacheza.


Swali: Ati Mwenyezi Mungu hufanya hasira? Au Mungu kubishana na Mtume wake na baadaye akajuta?
Jibu: Hasira na kutetana si jambo zuri kabisa kwa hivyo haiwezekani kamwe Mwenyezi Mungu atende tena na Mtume wake Mtukufu! Lakini Biblie inaedelea kusema,kutoka aya ya 10,hadi mwisho wa aya ya 14: Basi sasa niache ili harisa zangu ziwake juu yao, niwa angamize: Nami nitakufanya wewe uwe taifa kuu. Musa akamsihi sana Bwana, Mungu wake, na kusema, Bwana, kwa nini hasira zako kuwakaa juu ya watu wako uliowaleta kutoka nchi ya Misri kwa uweza mkuu, na kwa mkono wenye nguvu?. . Geuka katika hasira yako kali, ughairi uovu huu ulio nao juu ya watu wako . . . .Na Bwana akaughairi ule uovu alisema ya kwamba atawatenda watu wake.


W A N A WA U Z I N Z I
Je, aweza Mtume kuwa mwana wa haramu? Biblia inasema Sivyo Biblia inasema "Ndivyo!
Swali; Je, aweza Mtume kuwa mwana wa haramu au mwana wa mwanamke kahaba?
Jibu: Hawezi kuwa kamwe. Kwa sababu kuzaliwa haramu ni 'aibu' kwa mwana: Kunamwadhili mwana wa haramu machoni na myoyonimwa watu. Hivyo watu hawawezi kumsikiliza wala kupokea maneno yake. Kwa vile jambo hili halilingani na kusudio la utume, Mwenyezi Mungu hakutuma mtu yeyote wa aina hiyo akawa Mtume.
BIBLIA: Vile vile inasema wazi wazi katika kumbukumbubu la Torati, 23:2, 'Mwana wa haramu asiingie katika mkutano wa Bwana: Hata kizazi cha kumi asiingie aliye wake katika mkutano wa Bwana." Kwa hiyo, Mtume hawezi kuwa 'mwana wa haramu.'
LAKINI: Biblia yenyewe hiyo inasema kwamba baadhi ya Mitume walikuwa wana wa haramu!
(1) Waamuzi, sura ya 11:1, inasema: Basi huyo Yeftha, Mgileadi, alikuwa mtu shujaa sana, naye alikuwa ni mwana wa mwanamke kahaba:' Na halafu inasema katika sura hiyo hiyo , aya ya 29, 'Ndipo roho wa Bwana akamjilia juu yake Yeftha.'Hii ina maana kwamba alikuwa Mtume!
(2) Mwanzo, 38:6-30, Yuda akamwoza mke ni Tamari. Naye Eri, mzaliwa wa kwanzawa Yuda, alikuwa mbaya machoni pa Bwana: Na Bwana akamvua. Yuda akamwambia O nani, Uingie kwa mke wa nani, Uingie kwa mke wa nduguyo, ukamwoe, ukamwinulie nduguyo uzao. OnaniAlijua ya kwamba huo uzao hautakuwa wake, ikawa, alipoingia kwa mke wa nduguye, akamwangalia chini asipe nduguye uzao. Neno hili alilolifanya likawa baya machoni pa Bwana, basi akamwua yeye naye. Yuda akmwambia Tamari mkwewe, Ukae mjane nyumbani mwa baba yako hata shela mwanangu atakapokuwa mtu mzima, maana alisema, asipate kufa yeye kama nduguze. Basi Tamari akaenda, akakaa nyumbani mwa babaye. Siku nyingi zikapita. . . .


Huyo Tamari akapewa habari, kusema, Mkweo anakwenda Timna . . . , akakaa mlangoni pa Enaumu, Karibu na njia ya kuenda Timna. Yuda alipomwona alimdhania kuwa ni kahaba, maana amejifunika uso. Akakaa mlangoni pa Enaumu, karibu na njia ya kuendea Timna. Yuda alipomwona alimdhania kuwa ni kahaba, maana amejifunika uso. Akamgeukia kando ya njia, akisema, Niruhusu niingie kwako. Maana hakujua ya, kuwa ni mkwewe. Akamwuliza, utanipa nini? Ukiingia kwangu? . . . . Basi akampa, akaingiake, naye akapata mimba mitatu Yuda akapewa habari kwamba, Mkweo, Tamari amefanya uzinifu, naye ana mimba ya haramu. Ikawa, wakati wake wa kuzaa walikuwapo mapacha tumboni mwake . . . . kwa jina lake likaitwa Peresi. Akatoka Ndugu yake baadaye, . . naye akaitwa jina lake Zera." Na huyu Peresi ni babu yake Daudi kama ilivyoelezwa wazi katika Biblia, kitabu cha Mambo ya Nyakati cha kwanza, sura ya 2, aya ya 5, imeandikwa nasaba ya Daudi mwana wa Yese mwana wa Obedi mwana wa salmoni mwana wa Nashoni mwana wa Aminadabu mwana wa Ramu mwana wa Hesroni mwana wa Peresi. Kwa hiyo, Daudi alikuwa Nabii na alikuwa katika kizazi cha kumi asiingie aliye wake katika mkutano wa Bwana!!!"


(3) Samue 11; sura 12;24, inasem; Naye Daudi akamfariji Bath-sheba mkewe, akaingia kwake. Akalala naye; naye akazaa mwana, akamwita jina lake Sulemani. Naye Bwana akampenda;" Kwa hivyo, Mtume Sulemani alikuwa mwana wa Beth- sheba. Na katika Samuel 11, Sura 11: 2- 27, yasema hivi: Ikawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, akatembea juu ya dari ya jumba la Mfalme: na alipokuwa juu ya dari aliona mwanamke anaoga: naye huyo mwanamke alikuwa mzuri sana, wa kupendeza macho naye Daudi akapeleka, akauliza habari za yule mwanamke, Mtu mmoja akasema, je! Huyu siye Bath- sheba, binti Eliamu, mkewe Uria, Mhiti? Basi Daudi akapeleka wajumbe, akatwaa: Naye akaingia kwake, naye akalala naye (maana yule mwanamke amekwisha kutakasika unajisi wake); kisha akarudi nyumbani kwake akachukua mimba; basi akapeleka na kumwambia Daudi, akasema, Ni mja-mzito'' katika sura ya 3, uk .16 umeona namna alivyofanya hila ya kumwua Uria! Na kwamba Daudi alizini na Mke wa Uria, baadaye kamlewesha ili apate kulala na mkewe, Jambo lisiloridhisha,Na kumpeleka Uria vitandani kwa hadaa ili auawe, na wakatenda hata akauawa? Tazama, Biblia inaonyesha utakatifu gani wa Daudi na Beth- sheba, wazazi wake Sulemani ("naye Bwana akapenda!!)

(4) Sasa tazameni kwamba Biblia inamsingizia. Yesu pia kutokana na Peresi ambaye ni mwana wa haramu! TAZAMA: Injili ya Mathayo Mtakatifu, sura 1, aya ya 1-16, yasema hivi: Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo. Mwana wa Ibrahimu. Ibrahimu alimzaa Isaka, Isaka akamzaa Yakobo , Yakobo akamzaa Yuda na ndugu zake; Yuda akamzaa Peresi na Zera kwa Tamari: Peresi akamzaa Esromu; . . . . . . Yakobo akamzaa Yusufu mumewe Mariamu aliyemzaa Yesu aitwaye Kristo.


NABII YEREMIA
Swali: Je, inamkinika Mweneyezi Mungu amuamrishe Mtume wake atengeze utepe au nira na ajivike shingoni kwa nini? Kwa jambo la upuzi kwa ilhali yeye ni mfano mzuuri.
Jibu: Haiwezekani kamwe Mwenyezi Mungu kuamrisha hivyo. Lakini Biblia katika kitabu cha Nabii Yeremia, sura ya 27, aya 1 hadi mwisho wa aya ya nane inasema hivi:-


NABII NUHU
Swali: Ati Mtume hunywa mvinyo na kulewa hadi akawa hoikuvua nguo na kuwa uchi? Jibu: Haiwezekani kamwe kufanya mambo yaliyokatazwa na Mwenyezi Mungu, wala mwenye akili yeyote hawezi kufanya mambo kama haya! Sembuse Mtume? Lakini (agano zote mbili) BiIlia inamsingizia Mtume Nuhu hayo, basi tazama kitabu cha kwanza cha Musa, kiitwacho "Mwanzo" sura ya tisa, aya ya 20 inasema hivi:-


Neno hili likamjia Yeremia, kutoka kwa Bwana, kusema, Bwana ameniambia hivi, Jifanyizie vifungo na nira, ukajivike shingoni; ….. Naitakuwa, taifa lile na mfalme yule asiyetaka Nebukadneze, huyo mfalme wa Babelia, na kutia shingo zao katika nira ya mfalme wa Babeli, mimi nitaliadhibu taifa lile kwa upanga, na kwa njaa na kwa tauni. Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu, akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake. Hamu, baba wa kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje.


N A B I I M Z E E
Swali: Ati Mtume husema uwongo? Akamwambia, karibu kwangu nyumbani, ule chakula. Naye akamwambia, siwezi kurudi pamoja nawe, wala kuingia pamoja nawe; wala sili chakula wala simywi maji pamoja nawe; kwani nimeambiwa kwa neno la Bwana, usile chakula wala usinywe maji huko, wala usirudi kwa njia ile ulioijia. Akamwambia, Mimi nami ni Nabii kama wewe na malaika akaniambia kwa neno la Bwana, husema, mrudishe pamoja nawe nyumbani kwako, ale chakula, akanywe maji. Lakini alisema uongo.
Jibu: Hasha! Mtume hasemi uwongo kamwe kwani Mtume akiwa mwongo atamsadiki nani na kufuata dini yake? Lakini kwa bahati mbaya Bilia inamsingizia hivyo Mtume mmoja. Tazama kitabu cha kwanza cha Wafalme, sura ya kumi na tatu, kutoka aya 11 hadi mwisho wa aya 19, inasema hivi:- Basi Nabii mmoja mzee alikuwa akikaa katika Betheli; akamfuata Mtume wa Mungu, akamkuta ameketi chini ya mwaloni, akamwambia, Je! Wewe ndiwe yule Mtume wa Mungu aliyetoka katika yuda? Akamwambia, Mimi ndiye.N A B I I E L I S H A
Swali: Ati inamkinika Mtume atoe habari kwa ilhali yeye anafahamu kwamba ni uwongo tu? Jibu: Haiwezekani kamwe Mtume kueleza jambo ambayo yeye anajua kwamba ni uongo mtupu. Lakini Biblia linamsingizia hivyo, tazama kitabu cha pili cha Wafalme, sura ya 8, kutoka aya 7 hadi mwisho wa aya 15, inasema hivi;

Kisha, Elisha akaenda dameski; na Ben-hadadi, mfalme wa Shamu, alikuwa hawezi; akamambiwa ya kwamba, yule Mtu wa Mungu ame fika. hapo. Mfalme akamwambia Hazeli, chukua zawadi mkononi mwako, ukaende ili kumlaki yule mtu wa Mungu, ukamulize bwana kwa kimwachake, kusema, je! Nitapona ugonjwa huu? Basi Hazaeli akaenda kumlaki, akachukua zawadi mkononi mwake, zakila kitu chema kilichopatikana Dameski, kiasi cha mzigo ya ngamia arobaini, akaenda akasimsimama mbele yake, akasema, Mwana wako Ben-hadadi, mfalme wa sham, amenituma kwako, kusema, je! Nitapona ugonjwa huu? Elisha akamwambia, E nenda ukamwambie, bila shaka utapona; lakini Bwana umenionyesha ya kwamba Bila shaka atakufa …… akarudi kwa bwana wake; naye akamwambia, Elisha alikwambiaje? Akajibu, aliniambia kuwa bila shaka utapona ikawa siku ya pili yake akatwaa tandiko la kitanda, akali chovya katika maji, akali tangaza juu ya uso wake, hata akafa. Na Hazaeli akatawala badala yake.KATIKA KITABU HIKI
1. Kuhusu Mwenyezi Mungu Jinsi Biblia inavyozungumzia kuhusu Mwenyezi Mungu. Kiasi gani Biblia imetopewa kwa maovu na uwongo kuhusu Mwenyezi Mungu aliyeumba Ulimwengu? Biblia anasema yasiyofaa juu ya Utukufu wa Mwenyezi Mungu.
2. Kuhusu Mitume Mambo gani ambayo Agano jipya na Agano la kale yameongopwa kuhusu Mitume wa Mwenyezi Mungu ? Mambo ambayo hayafai hata kwa duni lichaa ya Mitume wa Mwenyezi Mungu, waliokuwa watukufu zaidi kuliko binadamu wote. Mitume hao hawakutumwa ila kuongoza, kutakasa na kutenda mema. Lakini angalia jinsi Mitume hao walivyosimuliwa katika Biblia.