DALILI ZA KIAMA

 
Zama bora

Sifa za zama bora zilizoelezewa kwa kina na Mtume(s.a.w) ni dalili muhimu ya siku ya hukumu. Kipindi hicho kinachoitwa "Golden age" kitakuwa bora kwa sababu ya kule kulinganishwa kwake na pepo kwa maelezo ya Mwanachuoni wa kiislamu.

Imeelezwa katika Hadithi kuwa zama hizo bora zitakuwa katika awamu ya pili ya zama za mwisho. Sifa moja kuu ya kipindi hiki cha furaha itakuwa ni ule utajiri wake mkubwa wa mali. Hadithi zinasema kuwa utajiri huo hautakuwa na mfanowe katika historia:
Umma wangu utapata hali bora katika zama hiyo ambayo mfano wake haujapata kuonekana hapo kabla(ibn Majah). Umma wangu wa wema na wabaya utaneemeshwa neema ambazo haukupata kuziona kabla(Al-Muttaq al Hind Al Burhan fi Alamat al Mahd Akhira Zaman).

Hadithi nyingine inaelezea utajiri wa zama hizo. Katika kipindi hicho, ardhi itatupa nje hazina yake.(Ibn Hajar Haythami, AlQawli al Mukhtasar fii alamat al Mahdi al Muntazar) Hadithi nyingine zinaelezea kuwa miaka ya mashaka na huzuni itakwisha. Hakuna mtu atakayekuwa katika shida. Hakuna mtu atakayetakiwa kutoa zaka.

"Toeni zaka kwani utakuja wakati ambapo mtu atakwenda na zaka yake huku na kule asipate mtu wa kuipokea(Bukhari). Kwa hakika bidhaa zitakuwa nyingi na zitamwagika kama maji lakini hakuna atakayeziokota(Al Halimi). Sifa nyingine ya zama bora itakuwa ni kushitadi kwa haki na ukweli. Utakuwa wakati ambapo sheria na haki zitachukua nafasi ya hofu, mfarakano na dhuluma.

Kama tunavyosema katika Hadithi, dunia itajaa haki badala ya ukandamizaji na mateso(Ahmad Diya'al Din al Kamushkanawi, Ramuz al Ahadithi) Miongoni mwa sifa bora za kipindi hicho ni kunyamaa kwa silaha(kutulia kwa milio ya silaha), kutoweka kwa uadui, migogoro na kukoma kwa misambaratiko ya kijamii. Badala yake kutashamiri urafiki na mapenzi miongoni mwa watu. Kiasi kikubwa cha pesa kilichotumika kugharimia vita na viwanda vya silaha sasa kitawekezwa kwenye chakula, afya, maendeleo, utamaduni na mambo yatakayoleta furaha kwa watu wote.

Sifa nyingine ya kipindi hiki cha neema itakuwa ni kurejea katika misingi ya dini ya Mwenyezi Mungu kama ilivyofundishwa na Mtume(s.a.w). Zile sheria na mila zilizobuniwa baada ya Uislamu zitaondoshwa. Tafauti za Waislamu katika kuitekeleza dini yao zitakoma.

Kwa kifupi, zama bora ni kipindi cha neema nyingi, maisha bora, amani furaha, utajiri na faraja. Utakuwa ni wakati ambao maendeleo katika sanaa, tiba, mawasiliano, uzalishaji, usafirishaji na katika maeneo mengine ya maisha yatakuwa katika sura ambayo haikuwahi kuonekana katika historia ya dunia. Na watu wataishi kwa kuzingatia mafundisho ya Qur'an.

Baada ya zama bora
Tunaposoma habari za Mitume katika Qur'an tunaona kuwa kanuni ya Mwenyezi Mungu imefanyakazi katika zama zote. Jamii zinazomkadhibisha Mtume wa Mwenyezi Mungu na kumpiga vita basi huishia kuangamizwa. Lakini wale wanaomtii Mtume hupata neema nyingi za kidunia na Ustawi wa Kiroho ambao dini sahihi huwaletea. Lakini baada ya kupita mitume hawa, baadhi ya Watu huanza kukengeuka na kuikanusha dini sahihi kuanza kuishirikisha na Mwenyezi Mungu.

Mifarakano na migongano hutokea. Kwa kweli watu wa jamii hizi wamejikuta wakiangamia kwa mikono yao wenyewe. Kanuni, hapana shaka, itafanya kazi katika zama za mwisho. Mtume(s.a.w) amebainisha kuwa kiama kitakuja baada ya kifo cha Isa(a.s) na mwishoni mwa zama bora kama tulivyosoma.

"Baada ya yake(Nabii Isa) siku ya hukumu itakuwa jambo la muda mfupi mbele(Ahmad Diy'aal Din al Kamushkanawi, Ramuz Al Ahadith). Siku ya hukumu itakuja baada yake(Nabii Isa)( Ahmad Diy'aal Din al Kamushkanawi, Ramuz Al Ahadith.

Hapana shaka zama mwisho na zama bora vitakuwa vipindi ambapo onyo la mwisho litatolewa kwa Wanaadamu. Hadithi nyingi zinaelezea kuwa hapatakuwa na mema baada ya kipindi hiki.

Hivyo tunaona kuwa muda mfupi baada ya kifo cha Isa(a.s) watu duniani watakuwa waovu na wataitupa dini sahihi. Ule wingi wa mali katika zama bora utawazuzua na hivyo kuharibikiwa. Hapa twaweza kusema kuwa katika mazingira haya ndipo kiama kitakapotokea lakini Allah ndiye ajuaye.

Kwa jinsi tulivyoziona dalili za kiama, yaweza kusemwa kuwa Karne hii ya ishirini na moja inaashiria mwanzo wa enzi mpya kabisa za historia ya dunia. Tunamuomba Allah atufishe na kutufufua hali ya kuwa ni Waislamu.