DALILI ZA KIAMA

 
Teknolojia ya mawasiliano

Baadhi ya Hadithi za Mtume(s.a.w) zimeelezea Teknolojia ya leo ya mawasiliano;
"Saa ya mwisho haitafika kabla jumbe hajasemeshwa na fimbo yake.(Tirmidh) Tukiiangalia hadithi kwa makini, twaweza kuona ukweli uliomo ndani yake. Katika zama zilizopita fimbo ilitumika kuendeshea wanyama wa kupanda hasa hasa ngamia na farasi. Hapa tunaona Mtume(s.a.w). Hapa tunaona Mtume(s.a.w) ametumia tamathali.

Hebu tujiulize ni kitu gani kinachosema ambacho twaweza kukilinganisha na fimbo kwa sifa za maumbile? Jibu la kwamza laweza kuwa simu. Au vyombo vingine vya mawasiliano. Vyombo vya mawasiliano visivyotumia waya kama vile simu za mkononi na simu za upepo kama sattilaiti ni vyombo vya hivi karibuni kabisa. Kwa kuvitazama vyombo tutaona wazi wazi kule kutimia kwa bishara ya Mtume(s.a.w) iliyotolewa miaka 1400 iliyopita. Kwa hivyo huu ni ushahidi kuwa zama zetu ziko jirani na siku ya hukumu. Katika Hadithi nyingine Mtume(s.a.w) anaelezea maendeleo ya Teknolojia ya mawasiliano:

"Hakutakuwa na hukumu mpaka sauti ya mtu imsemeshe yeye mwenyewe(Hadi mtu asemeshwe na sauti yake.(Mukhtasar Tazkira; Allama Qurtubi). Ujumbe wa Hadithi hii unathibitika hivi leo.Ili mtu aisikiye sauti yake kwanza hurekodiwa na kisha kusikilizishwa. Teknolojia ya kunasa na kutoa sauti ni ya karne ya ishirini. Huu ndio ulikuwa mwanzo wa maendeleo ya sayansi ambayo ndio imezaa vyombo vya mawasiliano na habari. Unasaji wa sauti sasa umefikia kiwango cha juu kutokana na matumizi ya kompyuta.

Kwa kifupi vyombo vya elektroniki vya hivi leo kuna vipaza sauti ambavyo vimewezesha mtu kujinasa na kujisikia sauti yake mbali ya kanda za rekodi na vionesho vya picha(video). Hii inadhihirisha kuwa Hadithi ya Mtume iliyonukuliwa hapo imetimia. Kwa hiyo hii ni dalili nyingine ya kiama. Si hadithi hizo tu bali kuna ishara nyingine zilizotajwa na Hadithi zifuatazo:

Mkono utanyooshwa kutoka angani na watu watautazama na kuuona.(Ibn Hajar Haythami, AlQawl al Mukhtasar fil alamat al Mahdi al Muntanzir. Dalili ya siku hiyo mkono kunyooshwa angani na watu kuacha kuangalia.(Al-Muttaqil al Hindi, AlBurhan fi Ahmad al-Mahdi Akhir al-Zaman)

Ni dhahiri kuwa neno "mkono" katika hadithi hiyo limetumika kwa tamathali. Katika zama zilizopita neno hili huenda halikueleweka zaidi. Lakini ikitazamwa teknolojia ya leo, kauli yaweza kutafsiriwa kwa namna nyingi. Kwa mfano Televisheni ambayo imekuwa sehemu muhimu ya maisha ya leo pamoja na kamera na Kompyuta zaweza kubeba tafsiri ya kauli hiyo.

Neno "mkono" yawezekana limetumika likiwa na maana ya uwezo. Yaweza kuwa na maana pia taswira zinazotoka angani kwa sura ya mawimbi ambayo ni televisheni:

"Sauti itamwita mtu kwa jina lake na hata watu wa magharibi na mashariki watasikia.(Ibn Hajar Haythami, Al Qawl al Mukhtasar fi alamat ala Mahdi al Muntazar). Sauti hii itavuma itaenea duniani kote na kila kabila litaisikia kwa lugha yao wenyewe(Al-Muttaq al Hindi, al Burhani fi alamat al Mahd Akhir al Zaman).

Sauti kutoka mbinguni ambayo kila mtu ataisikia kwa lugha yake. (Al-Muttaq al Hindi, al Burhani fi alamat al Mahd Akhir al Zaman). Hadithi hapa zinataja sauti ambayo itasikika dunia nzima na kwa lugha ya kila mtu. Ni dhahiri hii ina maana ya Radio, Televisheni, simu za mikononi na nyenzo nyingine za mawasiliano. Huu ni muujiza kwamba Mtume(s.a.w) alitaja maendeleo ambayo hayakufikirika katika kipindi cha miaka mia moja tu iliyopita. Mfasiri maarufu Badiuzzaman wakati akifasiri hadithi hizi alieleza kuwa, zimebashiri kimiujiza kuja kwa radio, televisheni na vyombo vingine vya aina hiyo.

Kuzuka kwa manabii wa uongo
Inafahamika kuwa katika kipindi chote cha historia, kumekuwa na manabii wengi wa uongo. Katika hadithi inabainishwa kuwa Manabii wa uongo watazuka kabla ya siku ya hukumu. Saa ya mwisho haitafika kabla ya kuja kwa Madajali(Wadanganyifu) thelathini kila mmoja akijitambulisha kama nabii wa Allah.(Abu Dawood) Kwa kutumia fursa ya matazamio ya Waislamu na itikadi ya dini ya kikristo kuwa Nabii Isa au Yesu atarejea, idadi kubwa ya watu wadanganyifu wamejitokeza kudai unabii.

Kumbukumbu zinaonesha kuwa , Manabii wa uongo walianza kujitokeza katika miaka ya 70. Ifuatayo ni baadhi ya mikasa iliyotokana na madai ya unabii yaliyojitolewa na watu mbali mblia katika nchi mbali mbali. Maafa ya moto; David Koresh na wafuasi wake wapatao 74 katika eneo la Waco, Texas walikufa kwa kujiwasha moto.

Wiki moja kabla ya hapo maeneo mawili ya Uswisi na moja nchni Canada, walikufa jumla ya Wafuasi 53 wa Jouret, wakiwemo na watoto wao. Polisi katika nchi hizo mbili wanafanya uchunguzi kujua kama vifo hivyo ni vya kujiua, kuuawa au yote mawili kutokana na imani za ajabu.

Sun Myung Moon, mwasisi wa Kanisa la Unification anadai yeye ni Masihi aliyekuja kwa mara ya pili. Kanisa la Unification lilianzishwa rasmi na Moon mnamo mwaka 1954. Moon anadai kuwa mwaka 1936 yeye alipokuwa na umri wa miaka 16, Yesu alimtokea upande wa mlimani kaskazini magharibi mwa Korea na kumwambia kuwa Mungu amemchagua kwa kazi ya utume wa kusimamisha Ufalme wa mbinguni na ardhini.

Zaidi ya watu 1000 wahofiwa kufa baada ya kugundulika kwa makaburi mengi zaidi nchini Uganda. Hao walikuwa wafuasi wa mtu aliyedai kuwa nabii Kibwetere. Zaidi ya watu 900, wafuasi wa dhehebu moja, walikutwa wamekufa pamoja katika msitu wa Amerika kusini. Watu wote waliokufa walikuwa wafuasi wa Mchungaji Jim Jones, kiongozi wa hekalu mjini San Francisco.

Qur'an pia inaeleza kuja kwa mnabii wa uongo; Na ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule amtungiyae uongo Mwenyezi Mungu au mwenye kusema: Nimeletewa Wahyi", na hali hakufunuliwa chochote; na yule asemaye: Nimeteremsha(ufunuo) kama ule aliouteremsha Mwenyezi Mungu. Na kama ungewaona madhalimu watakapokuwa katika mahangaiko ya mauti na malaika wamewanyooshea mikono(kuwaambia) zitoeni roho zenu! Leo mtalipwa adhabu ifedheheshayo kwa sababu ya yale mliyokuwa mkizifanyia kiburi Aya zake(ungeona namna gain wanavyopapatika) (6:93).

Kama inavyoelezwa katika aya hiyo watu hawa wazushi kwa hakika watapata malipo yao kwa uongo waliozusha. Hapana shaka kuwa utafika wakati ambapo uongo wote wa manabii wa uongo utafutiliwa mbali. Mtume(s.a.w) akasema kuwa baada ya warongo hawa kuondoka ndipo Isa(s.a) atakapokuja tena.

Kama tulivyoeleza kurasa za nyuma kuwa Qur'an inatufahamisha kurejea kwake duniani, na kwamba Waislamu na Wakristo, kwa hamu, wanasubiri ujio wake, kuna Hadithi chache za Mtume(s.a.w). Mwanazuoni wa kiislamu Shawkani kasema kuwa kuna Hadithi 29 zinazoelezea kurejea kwa Issa na kwamba maelezo yaliyomo katika hadithi hizi hayawezi kupotoshwa.(Ibn Majah)

Kuna jambo moja muhimu linalotujia kutokana na Haithi hizi. Kurejea kwa Isa kutatokea awamu ya pili ya zama za mwisho na ndio itakuwa ishara muhimu(dalili kuu) ya siku ya hukumu. Hadithi zinazohusiana na jambo hili ni hizi;

Saa ya mwisho haitafika mpaka muone mshuko wa Issa(a.s) mwana wa Mariamu(Muslim). Naapa kwa yule ambaye roho yangu iko mikononi mwake. Mwana wa Maryamu, muda si mrefu atashuka miongoni mwenu(Waislamu) kama mtawala mwadilifu wa haki(Bukheri).

Saa haitasimama hadi pale atakaposhuka mwana wa Maryamu miongoni mwenu kama mtawala mwadilifu(Bukhari) Mtume(s.a.w) anatueleza kile atakachofanya Isa pale atakaporejea; unapowadia wakati wa kifo chake Isa atakuwa ameonekana tena duniani kwa kipindi cha miaka 40.(Abu Dawuud).

Isa(a.s) mwana wa Maryamu atashuka kutawala kwa miaka arobaini kwa kitabu cha Allah na kwa Sunna yangu hadi anapokufa. (Al-Muttaqi al Hindi, Al Burhani fi Alamat al Mahdi Akhir al zaman)