DALILI ZA KIAMA

 
Kukua kwa Sayansi na Teknolojia

Mtume Muhammad(saw), kama sote tujuavyo aliishi karne kumi na nane zilizopita. Kumbukumbu za Historia zinaonesha kuwa wakati Qur'an ilipofunuliwa jamii ya Waarabu haikuwa na teknolojia ya kuwawezesha kufanya tafiti za dunia au ulimwengu.

Kwa sababu hiyo kuna tofauti kubwa kati ya kiwango cha sayansi na Teknolojia cha wakati wa alioishi Mtume(s.a.w) na wakati huu wetu. Tofauti hii ilianza kuwa kubwa hasa zaidi mwanzoni mwa karne ya ishirini. Kielezeo cha wazi cha hilo ni mageuzi makubwa ya kiteknolojia yanayoonekana katika wakati wetu huu ambayo, hayakupata kuonekana sio tu wakati wa Mtume bali hata katika miongo michache iliyopita. Licha ya tofauti hiyo, bado katika karne ya saba Mtume(s.a.w) alizungumzia mambo mengi ya hakika juu ya maisha. Hapa tutaziangalia Hadithi zinazoelezea kiwango cha maarifa ya sayansi na Teknolojia katika zama za mwisho. Tutaona kuwa yale aliyoyabainisha Mtume(s.a.w) karne kumi na nne zilizopita yanadhihirika leo.

Elimu
Tofauti kubwa inayobainika kati ya krne za 20 na 21 na zama zilizopita ni kuongezeka kwa mwamko wa elimu. Huko nyuma uwezo wa kusoma na kuandika ulihodhiwa na watu wachache. Lakini kuanzia mwishoni mwa karne ya ishirini UNESCO na taasisi za serikali pamoja na mashirika binafsi yamefanya kazi kubwa ya kusambaza elimu.

Kwa mujibu wa ripoti ya UNESCO, kiwango cha elimu ya kujua kusoma na kuandika kilifikia asilimia 77.4 mwaka 1997. Kiwango hiki ni kikubwa mno. Mtume(s.a.w) aliielezea hali hii kama ni dalili mojawapo ya zama za mwisho; "Mwamko wa elimu(literacy) utaongezeka pale hukumu inapokaribia"(Ahmad Diyaal-Din-Alkhamush Khanawi, Ramuz-al-Ahadith). i

Teknolojia ya ujenzi
Dalili nyingine ambayo Mtume(s.a.w) ameitaja kuhusiana na zama za mwisho ni ujenzi wa maghorofa marefu:
"Hakutakuwa na hukumu hadi pale maghorofa marefu sana yatakayojengwa"(imesimuliwa na Abu Huraira) "Kiama hakitasimama mpaka watu washindane kujenga maghorofa marefu.(Bukhari)

Tukiingalia historia ya usanifu majengo na uhandisi, tunaona kuwa maghorofa mengi marefu yalianza kujengwa na mwishoni mwa karne ya kumi na tisa. Maendeleo ya Teknolojia kuongezeka kwa matumizi ya chuma cha pua na matumizi ya Kambarau(lifti za kupandia maghorofani) kumeongezeka kasi ya ujenzi wa maghorofa. Maghorofa marefu yameshamiri kweli kweli hivi leo. Alichokisema Mtume(s.a.w) katika Hadithi kinadhihirika wazi wazi. Watu na mataifa yanashindana kuongeza maroshani ya ghorofa.

Teknolojia ya usafiri
Katika historia yote, kumekuwa na uhusiano kati ya maendeleo na mawasiliano. Jamii ambazo zimeweza kujiwekea miundo mbinu bora ikiwa ni pamoja na mifumo bora ya usafiri zimejipatia maendeleo. Akizungumzia dalili za zama za mwisho, Mtume(s.a.w) kayataja maendeleo ya usafiri. "Kiama hakitasimama… hadi muda utakapopita upesi upesi(Bukhari) Masafa ya mbali mno yatafikiwa kwa muda mfupi.(Ahmad Musnad)

Ujumbe unaobebwa na Hadithi hiyo unadhihirika wazi wazi hivi leo. Katika zama hizi masafa ya mbali yanafikiwa kwa muda mfupi tu. Madege, magari na Treni ni vyombo vinavyoweza kusafiri masafa ya mbali kwa muda mfupi. Huko nyuma safari za masafa marefu zilichukua miezi. Qur'an pia inavielezea vyombo hivi:
"Na amewaumbia Farasi na nyumbu na punda ili muwapande na (wawe) mapambo. Na ataumba vipano) msivyovijua (6:8). Hebu tuutafakari huu usemi wa muda utapita upesi upesi katika ile hadithi ya kwanza. Kwa kuzingatia yale tuliyoyaeleza, ni wazi kama Mtume(s.a.w) alivyonena kuwa katika zama za mwisho, kazi zitafanywa kwa muda mfupi kuliko zilivyokuwa zikifanywa huko nyuma.

Kwa kweli maendeleo ya sayansi yamewezesha mambo mengi kutimizwa kwa muda mfupi zaidi. Hadithi hiyo hiyo inathibitisha jambo hili: Kiama hakitakuja kabla muda kupungua. Mwaka uwe kama mwezi, mwezi uwe kama wiki na wiki iwe kama siku…(Tirmidh).

Mathalani zama zilizopita, mawasiliano ya kimataifa yalichukua majuma mengi lakini sasa yanafanyika kwa sekunde tu kwa tovuti na teknolojia nyinginezo za mawasiliano. Kurahisishwa kwa mawasiliano kumewezesha chombo cha anga cha Marekani kutumwa katika sayari Mars zaidi ya maili milioni 106 ambacho hivi kinaendelea kuleta taarifa mbali mbali za kiuchunguzi duniani pamoja na picha kwa muda mfupi sana.

Katika zama za nyuma bidhaa zilifika kule zilikopelekwa baada ya safari ndefu za miezi, hivi leo zinafika mapema kabisa. Hivi sasa mamilioni ya vitabu yanaweza kuchapwa kwa muda uliotumika kuchapwa kitabu kimoja karne chache zilizopita. Katika masuala ya afya na njia za utayarishaji wa vyakula hapahitajiki tena muda mrefu wa kushughulikia kutokana na Teknolojia ya sasa.

Unaweza kutoa mifano mingi mno. Hata hivyo tumalizie hapa kwa kusema kuwa dalili zote alizozieleza Mtume(s.a.w) katika karne ya saba zinaonekana wazi wazi hivi sasa. Dalili nyingine aliyoitaja Mtume(s.a.w) ni kuongezeka kwa biashara, kama iliyoripotiwa na Ibn Mas'uud(r.a). Biashara inakwenda pamoja na maendeleo ya Teknolojia na usafirishaji wa kisasa umeiwezesha kila nchi duniani kujenga uhusiano na ushirikiano wa karibu wa kibishara na nchi nyingine.