DALILI ZA KIAMA

 
Mitume

Tumezungumzia kanuni zisizobadilika ambazo zimewekwa na Allah tokea kuumbwa kwa ulimwengu.kanuni ya Allah nikuwa yeye hatoiadhibu jamii ambayo hajaipelekea mjumbe.ahadi hii imetolewa katika aya zifuatazo: Na Mola wako haangamizi miji mpaka ampeleke mtume katika mji wao mkuu,awasomee Aya zetu [wakatae ndio wangamizwe]walahatuiangamizi miji mpaka watu wake wamekuwa madhalimu. (28:59) Na sisi si wenye kuwadhibisha[viumbe]mpaka tuwapelekee mtume.(17;15). Wala hatukuangamiza mji wowote ilaulikuwa na waonyajikuakumbusha wala hatukuwa madhalimu.(26;208-209).

Aya hizi zinabainisha kuwa Mwenyezi Mungu kuwatuma Mitume kwenye miji mikuu kuwaonya watu. Mitume hawa huyahubiri maamrisho ya Mwenyzi Mungu lakini makafiri katika kila zama wamewadhihaki Mitume hawa nakuwaita waongo,wandawazimu na kuwasingizia kila jambo. Kwa sababu hiyo Mwenyezi Mungu huziangamiza jamii zinazoendelea kuishi katika maovu. Huwapelekea mangamizi katika wakati wasiotarajia kabisa. Kuangamia kwa watu wa Nuhu , Lutwi, Aadi, Thamuud na wengine waliotajwa katika Qur'an ni mifano ya aina ya maangamizi haya.

Katika Qur'an , Mwenyezi Mungu anabainisha sababu ya kutuma mitume;nayo ni kutoa habari njema katika jamii, kuwapa watu fursa muhimu ya kuachana na imani zao potofu na kuishi kwa kufuata dini ya Allah na kuwaonya watu ili wasipate kisingizio siku ya mwisho. Aya hii ya Qur'an inasema:
Hao ni mitume waliotoa habari nzuri kwa watu , wakawaonya ili wasiwe na hoja juu ya Mwenyezi Mungu baada ya kuletwa mitume. NaMwenyezi Mungu ni mwenye nguvu na mwenye Hekima.(4:165) Kama inavyosema aya ya 40 ya suratil Ahzab , Mtume Muhammad ni mtume wa mwisho, 'Muhammad ni mtume wa Mungu na mwisho wa mitume.'

Kwa maneno mengine, baada ya Mtume Muhammad, Wahy kutoka kwa Allah umekamilika. Hata hivyo jukumu la kuwafikishia watu ujumbe na kuwakumbusha watu limebakia kwa kila Muislamu hadi siku ya mwisho. Miongoni mwa maudhui ya Qur'an ni yale yanayohusu watu ambao Mwenyezi Mungu amewangamiza kwasababu ya uovu na uasi wao. Na mafundisho yanayopatikana kutokana na maangamizi yaliyowafika watu hao. Kuna mlingano mkubwa kati ya jamii hizo zilizopita na jamii yetu ya leo.

Hivi leo kuna watu ambao tabia na mwenendo wao wa maisha ni mbaya zaidi kuliko hata ule mwenendo mchafu wa watu wa Lut, au ule wa dhulma wa watu wa Madian au ule wa kibri na dharau wa watu wa Nuhu au ule wa uasi na uovu wa watu wa Thamud au ule wa kukosa shukrani wa watu wa Iram pamoja na jamii nyingine zilizoangamizwa. Sababu ya wazi ya upotevu wa kimaadili wa watu hao ni kuwa walimsahau Mwenyezi Mungu na lengo la kuumbwa kwao.

Mauaji, dhulma katika jamii, ufisadi, udanganyifu na mmomonyoko wa maadili katika zama hizi vimewafikisha watu mahala pa kukata tamaa. Lakini, isisahaulike kuwa Qur'an inatutaka tusikate tamaa na rehma za Mwenyezi Mungu. Kukata tamaa na kupoteza matumaini ni mambo yasiokubalika kwa waumini. Mwenyezi Mungu ameahidi kuwa wale wanaomuabudia kwa ikhlasi bila kumshirikisha na viumbe vyake kama miungu badala yake na wanaofanya vitendo vizuri, watapata rehma yake na kunyanyuliwa katika nafasi ya juu:

Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walioamini miongoni mwenu na kufanya vitendo vizuri kuwa atawafanya Makhalifa katika ardhi kama alivyowafanya Makhalifa wale waliokuwepo kabla yao na kwa yakini atawasimamishia dini yao aliyowapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu, hawanishirikishi na chochote. Na watakaokufuru baada ya hayo; basi hao ndio wavunjao amri zetu (24:55).

Katika aya nyingi, Qur'an inasema kuwa ni kanuni ya Mwenyezi Mungu kwamba wale waja walioamini na kushikamana na dini sahihi katika nyoyo zao watafanywa warithi wa dunia hii: Na hakika tumeandika katika Zaburi baada ya (kuandika katika) Allawhul Mahfudh ya kwamba ardhi (hii) watairidhi waja wangu walio wema (21:105). Na tutakukalisheni (nyinyi) katika nchi baada yao. Watapata haya wale waliogopa kusimamishwa mbele yangu na wakaogopa maonyo yangu. (14:14).

Na kwa yakini tumekwishaziangamiza umma nyingi kabla yenu, zilipofanya mabaya: Na waliwajia Mitume wao kwa hoja wazi wazi; lakini hawakuwa wenye kuamini. Namna hii tunawalipa watu wanaofanya uovu. Kisha tukakufanyeni nyinyi ndio wenye kushika mahala pao baada ya (kuangamizwa) hao katika ardhi ili tuone jinsi mtakavyotenda. (10:13-14). Musa akawaambia kaumu yake:

Ombeni msaada kwa Mwenyezi Mungu na subirini. Ardhi ni ya Mwenyezi Mungu, atamrithisha amtakaye katika waja wake; na mwisho mwema ni wawamchao. Wakasema: Tumeudhiwa kabla hujatufikia na (pia sasa) baada ya wewe kutujia. (Musa) akasema: Asaa Mola wenu atamwangamiza adui yenu na kukufanyeni watala katika nchi ili aone jinsi mtakavyofanya (7:128-129).

Sanjari na habari njema zilizotolewa katika aya hizo, Mwenyezi Mungu pia ametoa ahadi muhimu sana kwa waumini. Amebainisha katika Qur'an kuwa dini ya Uislamu imeshushwa kwa wanadamu ili izipiku dini zote (iwe juu ya dini zote): Wanataka kuizima Nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, lakini Mwenyezi Mungu amekataa hivyo ataitimiza tu Nuru yake, ijapokuwa Makafiri wanachukia. Yeye ndiye aliyemleta Mtume wake kwa uwongofu na dini ya haki ili aijaalie kushinda dini zotep; ijapokuwa watachukia hao Makafiri (9:32-33).


Wanataka kuzima Nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao na Mwenyezi Mungu atakamilisha Nuru yake ijapokuwa makafiri watachukia. Yeye ndiye aliyemtuma Mtume wake kwa uwongofu na kwa dini ya haki ili kuifanya ishinde dini zote, ijapokuwa makafiri watachukia(61:8-9).

Hapana shaka kuwa Mwenyezi Mungu atatimiza ahadi zake. Muongozo ambao utazishinda Falsafa zote potofu, itikadi potofu na mafundisho ya dini potofu ni muongozo wa Uislamu. Aya zilizonukuliwa hapo juu zinasisitiza kuwa makafiri hawawezi kuzuia jambo hili lisitimie. Wakati ambao muongozo wa Uislamu utakaposimama utakuwa wakati wa upendo, ukarimu, heshima, haki, Amani na ustawi wa kila mtu. Kipindi hiki kimeitwa kipindi kitukufu kwasababu ya kushabihiana kwake na mazingira ya pepo lakini hadi sasa zama hizo bado hazijawa. Zama hizo za kheri zitakuja kabla ya siku ya mwisho; hivi sasa zinasubiri wakati wake ambao Mwenyezi Mungu ameshapanga kuwa utafika tu.