DALILI ZA KIAMA

 
Saa inakaribia

Watu wengi angalau hujuwa jambo fulani kuhusu siku ya mwisho na karibu kila mmoja amesikia jambo hili au lile kuhusu kishindo cha saa hiyo. Hata hivyo wengi wanaonekana kuwa na mwenendo ule ule juu ya suaala hili kama walivyo katika masuala mengine yenye uzito mkubwa. Kwamba hawataki kulizungumzia au hata kulifikira jambo hili.

Wanajitahidi kwa kila hali kujighafilisha na khofu watakayo ipata siku ya mwisho. Hawajali ukumbusho wa siku ya mwisho uliomo katika kitabu juu ya msiba wa kuhuzunisha. Wanaepuka kuutafakari ukweli kuwa siku hiyo hapana shaka itafika. Hawataki kuwasikiliza watu wanaoizungumzia siku hii nzito au kusoma maandiko juu siku hiyo.


Hizi ni baadhi ya hila ambazo watu wamezidumisha ili kuepuka kuifikiria hatari ya siku ya mwisho. Wengi hawaamini kwa dhati kuwa saa hiyo inakuja. Tumepewa mfano wa watu hawa katika aya moja ya suratil-al-Kahf inayomzungumzia tajiri aliyemiliki bustani; ambaye alikitilia shaka Kiama; Wala sidhani kuwa Kiama kitatokea. Na kama (kitatokea hicho Kiama) nikarudishwa kwa Mola wangu, bila shaka nitakuta kikao chema kuliko hiki (alichonipa Ulimwenguni) (18:36)

Aya hiyo inabainisha taasubi ya mtu anayemuamini Allah lakini anayekwepa kufikiria hakika ya siku ya mwisho na anatoa madai yanayopingana na aya za Qur'an. Aya nyingine inaelezea wasi wasi na mashaka yaliyowajaa makafiri kuhusiana na siku ya mwisho;

Na wale waliokufuru wataambiwa je! Hazikuwa aya zangu zikisomwa kwenu, nanyi mkajivuna na mkawa watu waovu? Na inaposemwa hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli na Kiama hakina shaka mlikuwa mkisema; hatujuwi Kiama ndio nini; hatudhani ila dhana tu wala hatuna yakini. (45:31-32).


Watu wengine ndio kabisa wanakana kuwa Kiama kipo. Wale wenye dhana hii wanatajwa hivi katika Qur'an: Bali wanakadhibisha Kiama na tumewaandalia wanaokadhibisha Kiama Moto mkali kabisa. (Moto huo utakapowaona tokea mbali kabisa watasikia hasira yake na ngurumo yake). (25:11). Chanzo kinachoweza kutuongoza katika njia sahihi na kutubainishia ukweli ni Qur'an. Tunapoangalia yale inayoyaelezea, tunabaini ukweli ulio dhahiri. Wale wanaojidanya kuhusu siku ya mwisho wanafanya dhambi kubwa sana, kwani Allah anabainisha katika Qur'an kuwa hakuna shaka yoyote siku ya mwisho ikaribu:

Na kwamba Kiama kitakuja, hapana shaka ndani yake; na kwa hakika Mwenyezi Mungu atawafufua walio makaburini (22:7) Na hatukuziumba Mbingu na Ardhi na vilivyomo ndani yake ispokuwa kwa haki. Na bila shaka Kiama kitafika (15:85) Kwa yakini Kiama kitakuja, nacho hakina shaka lakini watu wengi hawaamini (40:59). Yawezekana kuna watu wanaodhani ujumbe wa Quraan kuhusiana na siku ya mwisho ulifunuliwa zaidi ya miaka 1400 iliyopita na kwamba hiki ni kipindi kirefu kulinganisha na muda wa maisha ya binadamu. Lakini hapa ni suala la mwisho wa dunia, jua, nyota na kwa kifupi ulimwengu mzima. Tunapo chukulia kuwa ulimwengu una umri wa mabilioni ya miaka, karne kumi na nne ni kipindi kifupi sana cha wakati. Mwanazuoni mkubwa wa kiislamu wa zama hizi, Bediuzzaman Said Nursi alilijibu swali hilo namna hii :


Saa (ya kufika kiyama) imekaribia (54 :1) kwamba siku ya mwisho iko karibu. Hata kama ni baada ya miaka elfu moja au miaka mingi zaidi ya hii bado hili halivurugi ukaribu wake. Kwa sababu siku ya mwisho ni saa iliyopangwa kwa ajili ya ulimwengu, na katika uwiano wa maisha ya ulimwengu, miaka elfu moja au elfu mbili ni sawa na dakika moja au mbili katika mwaka. Kwa hiyo siku ya mwisho sio tu ni saa iliyopanga kwa ajili ya binadamu kwamba ionekane iko mbali sana.


Kuhubiriwa kwa mafundisho ya Qur'an ulimwenguni
Katika Quran, tunakuta maneno yanayorudiwarudiwa; suna ya Allah yaani kawaida au dasturi [Sunnat Lllahi]: huu ni msemo wenye maana ya njia au sheria ya MwenyeziMungu. Kwa mujibu wa Quraan,sheria hizi hazibadiliki daima. Aya inasema: Hii ni kawaida ya mwenyezimungu iliyokuwa kwa wale waliopita zamani; walahutapata mabadiliko katika kawaida ya mwenyezimungu. (33:62)

Kanuni mojawapo ya mwenyezimungu isio badilika nikuwa, kabla ya mangamizi,kwanza jamii hupelekewa muonyaji[mjumbe].ukweli huu unabainishwa kwa maneno haya: Walahatukuangamiza mji wowote ila ulikuwa na waonyaji wa kuwakumbusha wala hatukuwa madhalim,tukawawngamiza pasina kuwapelekea waonyaji] (26:208-209). Katika historia yote, Mwenyezi Mungu ametuma muonyaji au mkumbushaji kakika kila jamii iliyokengeuka, akiwalingania kufuata njia sahihi. Sasa wale walio endelea nauovu wao ndio walio angamizwa baada ya kutimiza ule muda waliopangiwa na wakawa fundisho kwa vizazi vilivyo fuata. Tunapo iangalia kanuni hii ya mwenyezi Mungu siri nyingi muhimu zina bainika kwetu . Siku ya mwisho ni msiba wa mwisho utakao ukumba ulimwengu. Quraan ni kitabu cha mwisho cha mwenyezi Mungu kilichoshushwa kuwanasihi walimwengu. Muongozo wa Qur'an utabakia hadi mwisho wa dunia. Moja ya aya zake inasema-


Hayakuwa haya ila nimawaidha kwa watu wote (6:90). Wale wanaodhani kuwa Qur'an inazungumzia wakati au mahali fulani wanakosea sana kwasababu Qur'an ni wito wa jumla kwa walimwengu wote. Tokea wakati wa Mtume(saw) ujumbe wa Qur'an ulikwishaenea duniani kote. Kutokana na maendeleo ya makubwa ya Teknolojia ya zama zetu,Qur'an yaweza kusambazwa kwa wanadamu wote. Hivi leo, sayansi, elimu, mawasiliano na usafilishaji vinafikia hatua ya mwisho ya maendeleo yao hasa hasa tekinolojia ya kompiuta na mtandao wa Internent, watu katika sehemu mbalimbali wanaweza kubadilishana taarifa papo kwa hapo.


Mapinduzi ya sayansi na tekinolojia yameunganisha mataifa yote ya dunia nzima maneno kama utandawazi (Globolization) yameongezwa katika msamiati. Kwa kifupi vikwazo vyote vinavyo kwaza umoja wa walimwengu vinaondoshwa kirahisi tu. Kwakuzingatia ukweli huu ni rahisi kusema kuwa katika zama zetu hizi za mawasiliano ya papo kwa hapo, Mwenyezi Mungu ameweka aina zote za maendeleo ya tekinolojia kwa manufaa yetu ni jukumu la Waislamu kutumia vema tekinolojia hizi kwa ajili ya dawa katika maisha yote ili watu wayapate mafundisho ya Qur'an.