HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W)PAMOJA NA MAIMAMU (A.S)

 
MADHAMBI.
. Kuishi kwako hapa (mbali na utukufu) na dhambi lisiloweza kusamehewa. . Usiogopeshwe na chochote kile isipokuwa madhambi yako mwenyewe. . Madhambi yanaharibu ibada ya Allah swt. . Uharibifu ni matunda ya madhambi. . Madhambi yanampotezea mtu utukufu wake. . Kujiepusha na madhambi ni afadhali kuliko kutenda mema . . Kutenda madhambi ni ugonjwa na dawa yake ni kujiepusha nayo na kufanya tawaba

MAFUNZO YA TAHADHARI.
. Kila mtazamo wako wa fahamu ni fundisho kwako . Walio kufa wamewachia mafunzo kwa ajili ya walio hai. . Nijia walizozipitia wale waliokufa na waliotutangulia ni zenye kutufunza na kututahadharisha sisi tuzifuatazo. . Uhakika wa mambo ni mkufunzi wa kutosha kabisa. . Umri mkubwa ni mkufunzi aliye bora kabisa .

SHAURI
. Kutoa onyo la upole katika umati wa watu ni jambo lililo bure. . Mtoa mashauri asiye na uwema ni sawa na vile upinde unavyokuwa bila uzi. . Mshauri aliye bora kuliko wengine ni yule akuelezeaye makosa na dosari zako.

UAMINIFU,UADILIFU
. Ulimi mtukufu ni ule ulio adilifu. . Kwa kutimiza ahadi ni mfano ulio bora kabisa wa uaminifu na uadilfu. . Ukweli ina maana ya kwamba ulinganifu wa matamko kwa mujibu ya maamrisho ya Allah swt atakavyo.


UDANGANYIFU NA KHIANA
. Urafiki haupo kamwe katika uongo. . Kwa kubadilisha maana halisi ya jambo kuna haribu asili yake. . Kusema uongo kunaharibu habari. . Kusema uongo panapostahili,kutamlindia heshima za mtu. . Kusema uongo na unafiki kunadhalilisha nidhamu na heshima ya mtu.

UKIASI NA UFUJAJI.
. Aliyebarikiwa ni yule ambaye anaelewaye vyema thamani yake na asiyevuka mipaka. . Kwa kupima kiasi ni nusu ya hifadhi. . Ufujaji unapotea kabla ya njaa. . Ufujaji unapoteza uwema na sadaka. . Tamaa ya mali kunaharibu ukiasi alionao mtu. . Kiasi kwa uangalifu kinabakia zaidi ya kile kilicho fujwa. . Hakuna ufahari katika ufujaji. . Kupima kiasi ni njia ya usalama na ya amani.


UWEMA ( HISANI )
. Heshima na ukukuzi hauwezi kamwe kulinganiswa na ubaya,sio yenye wema. . Mwenendo wa mtu ni diraja ya akili yake. . Urithi ulio bora kabisa ni uungwana wa mtu. . Hakuna chochote kile chenye thamani dhidi ya uungwana.

KUWAHESHIMU WAZAZI
. Kuwatazama wazazi ni fardhi iliyo kuu kabisa. . Kuwatunza na kuwastahi wazazi wako (kuwalea) na malezi ya watoto wako, ndiyo yatakayo kulea wewe na kukustahi.

PUPA
. Hakuna ushindi uliopo katika pupa. . Lawama huwa ni daima kwa yeyote aendeleae kwa pupa

HUSUDA
. Husuda humwibia mtu raha zake. . Silaha ya husuda ni malalamiko na mapingamizi. . Husuda huitafuna uwema kama vile moto iharibuavyo mbao.

KAZI
. Matendo ndiyo matokeo ya nia. . Uwemwaminifu katika kazi zako, kwami majaribio ya Allah swt yako macho sana juu yako. . Siku ya mwisho ni siku ya Qiyamah na wala si siku ya kufanya kazi. . Shauku ya uaminifu ni uharibifu mambo mema. . Upande ulio mgumu wa tendo, ni kuhifadhi utukufu wa jambo. . Bila ya uaminifu , kazi zote hazitakuwa na thamani yeyote ile. . Itakuwa ni wema iwapo mambo mema yawe rafiki yako na matilaba, adui yako. . Elimu kiasi kidogo huharibu mienendo na tabia. . Kazi nyingi zenye tamaa, zitaharibu zingine zote. . Hakuna aheshimiwaye zaidi kuliko wengine ila ni yule mwenye kufanya ibada. . Hakuna usalama ulio bora kuliko ibada . . Kumtii Allah swt ni sehemu ya busara ya mtu. . Ibadi ni pahala palipobora pa kujihifadhia. . Ibada ni mahala palipo bora pa kujihifadia. . Kujionesha au kujidai kunaharibu na pia kuighasi ibada.


KUFANYA GHIBA.
. Hakuna uwema au uamnifu katika kufanya ghiba. . Yeyote yule asikilizaye ghiba basi ndiye mfanya ghiba mwenyewe. . Yeyote yule awasemae wengineo kwako, ndivyo vivyo hivyo ujue wazi wazi kuwa ndivyo akusemaye wewe kwa wengineo.

KUCHEKA
. Kucheka kwa wastani (bila kutoa sauti) ni mcheko ulio bora kuliko vyote. . Kucheka kwa kupita kiasi kutamharibia mtu heshima yake. . Kucheka kwa kupita kiasi kunaiuwa bongo.

SIFA
. Majivuno yanadhihaki sifa na pia kuiharibu. . Uwema na ukarimu kunavuna sifa njema. . Yeyote yule akusifuaye ndiye akuuae.

MISEMO.
. Utakatifu huambatana na busara.
. Kutoridhika kwa mtu kutamfutia utulivu.
. Saumu ya akili ni kuiepusha kutoka matamanio yote yaliyo maovu.
. Uoga ni kutokana na moyo uliodhoofika na usio na uimara.
. Vitu vinavyotuharibu sisi ni karibu tu tutakavyo ungana navyo.
. Kufuatilia mateso na matatizo yamkabiliayo mtu, yanadhihirisha ukubwa wake na ustahimilivu na uwema wake.
. Yeyote asemaye maneno na misemo ya wale wenye busara, basi ndivyo anavyojivisha utukufu wao.
. Maisha marefu hukutana na matatizo mengi.
. Ardhi ni msafishaji bora.
. Makabiliano ndiyo yanayomsaidia sana mtu.
. Ukweli na mabishano ndiyo yaliyo bora kabisa.
. Mtu ajigambaye basi ndiye ajidhalilishaye yeye nafsi yake.
. Mtu mwenye mafanikio bora kabisa.. Yeyote yule mwenye kuhofu ndiye abakiaye salama.
. Tajiri hasemwi kwa kuongezeka kwa uwema na kuiendeleza subira.
. Uso wenye mcheko (mcheshi) huuepusha kutoka moto wa uadui.
. Kwa kukatalia zawadi ndiko kunamaanisha kutokuwa na shukrani.
. Hakuna chochote mbali na kule kufanya Tawbah ila ni kujipunguzia ule mwenendo unaofutilia.
. Usiligeuze tumbo lako likawa ni kaburi la wanyama.
. Ugonjwa ni moja wapo ya aina mbili za kifungo.
. Kuzuzuliwa kwa ghadhabu ni dhambi pia.
. Ndugu huongezea na kufurahikia furaha zetu na hutuondolea na kutuponya yale maumivu tuliyonayo.
. Ubongo (akili) huwa ni mfano wa ghala (stoo) ambayo ilifungwa kabisa na maswali tu ndio zifunguazo kutoka humo.
. Hata kama pazia itaondolewa mbele yangu ,basi hakuna chochote kile kitachoongezeka katika imani yangu.
. Pale Allah swt ampendeleapo Mja wake yeyote,Yeye humshugulisha katika mapenzi yake.
. Nywele za kijivu huelezea kuwa ni hatua ya kuikaribia mautiBAADHI YA DUA' ZA IMAM ALI (A.S.)
. Ewe Allah swt,mbariki yule ambaye hazina yake kuu ni imani na silaha zake ni machozi. . Ewe Allah swt, wewe ni mkuu kabisa kwa kumwangamiza yule ambaye umeshakwisha kumtukuza hapo awali. . Sala ni silaha ya mumini. . Je kuna yeyote yule ambaye anaelewa vyema uwezo wa Allah swt na tena asimwogope Allah swt? . Je kuna yeyote akuelewaye vile wewe ulivyo na tena asiwe na khofu yako? . Ewe Allah swt, ngozi hii yangu hafifu, haitaweza kustahimili moto mkali wa Jahannam. . Mishale yote hailengi penye kuheshimiwa na kwa kupatwa na shida na majaribio. . Ewe muumba ,wewe upo pekee mwenye kuheshimiwa na mwenye kudumu daima milele na umelazimishia viumbe vyako kwa kifo na kwa kupatwa na shida na majaribio.


. Ewe muumba, nisamehee madhambi yangu pasipo mimi kujua kwangu . . Ewe mola , unisamehe madhambi yangu yale ambayo yanayoweza kuniteremshia juu yangu laana na adhabu na ghadhabu zako. . Ewe mola wangu, nisamehee madhambi yangu yale yanayoweza kuwa sababu ya kuharibu na kuzighasi zile baraka zako zilizo juu yangu. . Ewe mola, nisamehe madhambi yangu ambayo ndiyo yanayozuia na kuzipoteza ibada zangu kabla ya kukufikia wewe. . Ewe mola wangu, nisamehee madhambi yangu yale ambayo inanikatiza mimi katika imani yangu. . Ewe mola, mimi nakukaribia wewe kupitia kwa kukukumbuka wewe . . Ewe mola, mimi nakuomba wewe uniweke furaha na niwe nimeridhika na yale wewe uliyonijaalia maishani mwangu na katika bahati yangu (kwa ajili yangu). . Ewe mola wewe ni mwepesi sana wa kubariki na kurehemu, msamehe yule ambaye hana chochote ila ni ibada na sala zako tu. . Ewe Allah swt !, Je wewe utauachilia Moto uzikumbe nyuso ambazo ziko zimeangukia mbele yako kwa unyenyekevu? . Ewe Allah swt, zipatie nguvu mikono na miguu katika kutekeleza wajibu na huduma katika kazi zako. . Na uzipatie nguvu mbavu zangu ili nipate hali ya kukufikia wewe.


DUA.
. Al Imam Muhammad al-Baquir a.s., Bihar al-Anwaar, J. 91, Uk.6: "Ewe Mola wetu sisi kwa hamu kubwa utujaalie haki, Serikali ya Kiislam, (ambayo kwa hakika ipo uadilifu serikali ya Al Imam Mahdi Sahibuz-Zamaan a.s., tunamwomba Allah swt atuharakishie kudhihiri kwake). Kwa kupitia hii serikali takatifu, uihamasishe na kuipenda Islam na wafuasi wake ambao na papo hapo kuwadhalilisha unafiki na wanafiki. Na, katika kipindi hicho utuweke sisi miongoni mwa wale watu wanaowaita wengine katika utiifu wako na kuwaongoza katika njia yako utukufu; na, utujaalie heshima na ukuu katika dunia hii na Akhera. Aamin Ya Rabbal 'Alamiin.


. Kuna aina nne ya watu: " Wale wanaokula na kuwalisha wengine " Wale wanaokula na kuwanyima wengine " Wale hawali wenyewe na wala hawawapi wengine wale " Wale wanaowanyan'ganya wengine ili wale peke yao . Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amebainisha kuwa: "Mimi nimetumwa kuja kukamilisha maadili.

. Imenakiliwa kutoka kwa Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuwa: "Moyo ulio msafi- halisi ni ule ambamo hakuna chochote kile isipokuwa Allah swt tu" . Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ambamo twaambiwa: "Imani ya mtu haitokamilika hadi hapo mimi niwe mpenzi wake kuliko hata baba, mama, watoto wake, mali yake na hata kuliko maisha yake." . Allah swt abatuambia katika Qur'an Tukufu, Surah Qaaf, 50, Ayah 33: "Na anayemuogopa ( Allah swt Mwingi wa kurehemu, na hali ya kuwa humuoni na akaja kwa moyo ulioelekea ( kwa Allah swt)." (50:33)


. Qur'an Tukufu, Surah Attaghaabun, 64, Ayah 11, inatuambia: " Haufiki msiba wowote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na mwenye anayemwamini Allah swt huuongoza moyo wake. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu" . Amesema Allah swt katika Qur'an Tukufu, Surah Ar-Raa'd, 13, Ayah 28: "Sikiliza: Kwa kumkumbuka Allah swt nyoyo hutulia."

. Na vile vile mwishoni mwa Surah al-Fajr, 89, Ayah 28 twaabiwa "Ewe nafsi yenye kutua"! "Rudi kwa Mola wako, hali ya utaridhika, na umemridhisha." . Allah wt amesema katika Qur'an,Surah, Hajj , 22 , Ayah 32: Ndio hivyo! Na anayetukuza ibada za Allah swt, anayeziheshimu alama za (dini ya ) Allah swt, basi hili ni jambo la katika utawala wa nyoyo.

. Qur'an Tukufu, Surah Al Hajj, 22, Ayah 54: "Na ili walio pewa ilimu wajue kuwa hayo ni Haki itokayo kwa Mola wako Mlezi na waiamini, na ili zinyenyekee kwake nyoyo zao. Na hakika Allah swt ndiye anaye waongoa wenye kuamini kwenye Njia iliyo nyooka." . Allah wt amesema katika Qur'an, Surah, Ash-Shams, 91, Ayah 9-10: "Bila shaka amefaulu aliyeyeitakasa (nafsi yake) na bila shaka amejihasiri aliyeiviza (nafsi yake)" Qur'an Tukufu Tukufu inatuelezea: Qur'an Tukufu, Surah Al Qiyamah, 75, Ayah 1 - 2: "Naapa kwa siku ya Qiyamah. Tena naapa kwa nafsi inayojilaumu; (kuwa mtafufuliwa na mtalipwa)".


. Twaambiwa katika Qur'an Tukufu Surah, Ash-Shams, 91, Ayah 8: " Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake" . Qur'an Tukufu, Surah Al Baqara, 2, Ayah 283, inazungumzia kulipa kwa amana: "Na atakaeficha basi hakika moyo moyo wake ni wenye kuingia dhambini." . Anaelezea Allah swt katika Qur'an Tukufu, Surah Al Kahf, 18, Ayah 28: "Wala usiwatii wale ambao tumezighafilisha nyoyo zao wakafuata matamanio yao yakawa yamepita mpaka."


. Allah swt katika Quran: : "Na watakaokuwa na uzani khafifu, basi hao ndio waliozitia hasarani nafsi zao kwa sababu ya kuzifanyia ujeuri Aya zetu." . Amesema Allah swt katika Qur'an Tukufu, Surah Al Hajj, 22, Ayah 46: "Kwa hakika macho hayapofuki, lakini nyonyo ambazo zimo vifuani ndizo zinapofuka. . Amesema Allah swt katika Qur'an Tukufu, Surah Al Baqara, 2, Ayah 10: "Nyoyoni mwao mna maradhi, na Allah swt amewazidishia maradhi."


. Allah swt anatuambia katika Qur'an Tukufu, Surah Al I'mran, 3, Ayah 7: "Wale ambao nyoyoni mwao mna upotofu wanafuata zile zinazobabaisha kwa kutaka kuwaharibu watu kutaka na kujua hakika yake vipi........" . Amesema Allah swt katika Qur'an Tukufu, Surah Al Maida, 5, Ayah 13: "Kwa sababu ya kuvunja agano lao tuliwalaani, na tukazifanya nyoyo zao kuwa ngumu. Wanayabadilisha maneno kutoka pahala pake, na wamesahau sehemu ya yale waliyo kumbushwa. Na huachi kuvumbua khiana kutokana nao, isipo kuwa wachache na miongoni mwao. Basi wasamehe na waache. Hakika Allah swt hawapenda wafanyao wema." . Amesema Allah swt katika Qur'an Tukufu, Surah, Al H'adiid, 57, Ayah 16: "Je! Wakati haujafika bado kwa walio amini zikanyenyekea nyoyo zao kwa kumkumbuka Allah swt na haki iliyo teremka? Wala wasiwe kama walio pewa Kitabu kabla yao, muda wao ukawa mrefu, kwa Kwa hivyo nyoyo zao zikiwa ngumu, na wengi wao wakawa wapotovu."


. Amesema Allah swt katika Qur'an Tukufu, Surah At Tawba, 9, Ayah 45: "Nyoyo zao zina shaka; kwa hivyo wanasitasita kwa ajili ya shaka yao." . Amesema Allah swt katika Qur'an Tukufu, Surah Al Mut'ffifiin, 83, Ayah 14: "Sivyo hivyo! Bali yametia juu ya nyoyo zao (maovu) waliokuwa wakiyachuma." . Twaambiwa katika hadith Tukufu kuwa: "Mtu mwenye furaha kuu katika siku ya Qiyama ni yule atakaye yaona maneno aliyokuwa akiyatamka 'naomba msamaha wa Allah swt' chini ya kila dhambi alilolitenda. Kwa hivyo inambidi kila Mwislam miongoni wetu apige msasa kila ovu alilolitenda ama sivyo, Allah swt azitowazo onyo zake za upole zitabadilika na kuwa ghadhabu kubwa sana.


. Qur'an Tukufu, Surah Yusuf, 12, Ayah 53 kuhusu Mtume Yussuf a.s., inazungumziwa Nafsi : "Nami sijitoi Nafsi yangu; kwa hakika (kila) Nafsi ni yenye kuamrisha sana maovu" Amesema Allah swt katika Qur'an Tukufu, Yusuf, 12, Ayah 53: "Nami sijitoi Nafsi yangu; kwa hakika (kila) Nafsi ni yenye kuamrisha sana maovu" . Amesema al-Imam Muhammad al-Baquir a.s. : Al-Kafi, j. 2, uk.330 "Zipo aina tatu za dhuluma: " Kwanza ni ile ambayo Allah swt anatoa msamaha na ya " pili ni ile ambayo haitolei msamaha na aina ya " tatu ni ile ambayo yeye haipuuzi."


ZAKA
. Allah swt katika Qur'an Tukufu, Surah al -Tawbah, Ayah 34 - 35 : Siku (mali yao) yatakapotiwa moto katika moto wa Jahannam , na kwa hayo vikachomwa vipaji vya nyuso zao na mbavu zao na migongo yao, "Haya ndiyo (yale mali) mliojilimbikia nafsi zenu, basi onjeni (adhabu ya ) yale mliyokuwa mkikusanya. . Amesema Allah swt katika Qur'an Tukufu, Surah Ali-Imran, 3 , Ayah 180 : Wala wasione wale ambao wanafanya ubakhili katika yale aliyowapa Allah swt katika fadhila Zake kuwa ni bora kwao. La ni vibaya kwao. Watafungwa kongwa za yale waliyoyafanyia ubakhili - Siku ya Qiyamah.


. Imeandikwa katika Minhaj-us-Sadiqiin kuwa imeelezwa katika Hadith kuwa : 'Yeyote yule aliyebarikiwa na Allah swt kwa mali na utajiri, lakini kwa sababu za ubakhili wake hakutoa Zaka na malipo mengine yaliyofaradhishwa kwake, basi Siku ya Qiyamah mali hiyo itatokezea kwake katika sura ya nyoka, ambaye atakuwa mwenye sumu kali kwani hatakuwa na unywele wowote juu ya kichwa chake na atakuwa na alama mbili za rangi nyeusi chini ya macho yake na hii ndiyo dalili ya kutambulisha kuwa nyoka huyo ni mkali sana na hatari kabisa. Basi nyoka huyo atajiviringisha shingoni mwa mtu huyo kama mnyororo. Katika hali ya kumsuta, nyoka huyo atasema: 'Mimi ni mali yako ile ambayo wewe ulikuwa ukijivuna na kujifakharisha duniani.'

. Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. amesema katika Wasail-as Shiah, mlango 3, J.6, Uk. 11: "Mtu yeyote ambaye hatatoa na kulipa Zaka ya mali yake basi Siku ya Qiyamah Allah swt atamwadhibu kwa miale ya mioto katika sura ya nyoka wakubwa ambao watakuwa wakinyofoa na kula nyama yake hadi hapo hisabu yake itakapokwisha."


. Vile vile Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. amesema katika Tafsir Minhaj as-Sadiqiin kuwa : "Iwapo mtu aliye na mali na utajiri atakapoijiwa na ndugu au jamaa yake kwa ajili kuomba msaada kutokea mali na utajiri huo alionao, na yeye kwa sababu ya ubakhili wake akimnyima, basi Allah swt atamtoa nyoka mkubwa kabisa kutokea mioto ya Jahannam ambaye huizungusha ulimi wake mdomoni ili kwamba mtu huyo amwijie ili aweze kujiviringa shingoni mwake kama mnyororo mzito."

. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema katika Wasa'il as-Shiah, Zakat,mlango 3, Hadith 1, J.6, Uk. 11 na Al-Kafi : "Mtu yeyote anayemiliki dhahabu na fedha na asipotoa Zaka yake iliyofaradhishwa (au Khums, kama vile inavyoelezwa katika Tafsir al-Qummi), basi Allah swt atamfunga kifungo katika mahala pa upweke na atamwekea nyoka mkubwa kabisa ambaye atakuwa amedondosha nywele zake kwa sababu ya sumu kali aliyonayo, na wakati nyoka huyo atakapotaka kumshika basi mtu huyo atakuwa akijarbu sana kukimbia lakini atkaposhindwa hatimaye na atakapotambua kuwa hataweza kujiokoa basi atamnyooshea mikono yake mbele ya nyoka huyo. Lakini nyoka huyo atazitafuna mikono hiyo kama vile anavyotafunwa mtoto mdogo wa ngamia na atajiviringisha shingoni mwake kama mnyororo. Na hapo Allah swt anatuambia kuwa 'Yeyote yule anayemiliki mifugo, ng'ombe na ngamia na siyetoa Zaka ya mali yake, basi Allah swt Siku ya Qiyamah atamfunga kifungo cha upweke na kila mnyama atamwuma na kila mnyama mwenye meno makali atampasua na yeyote yule ambaye hatoi Zaka kutokea mitende, mizabibu na mazao yake ya kilimo, basi huyo siku ya Qiyamah basi atafungwa shingoni mwake kwa mnyororo wenye urefu wa takriban magorofa saba."


. Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. amesema katika Wasa'il as-Shiah Mlango 3, J.6, Uk.11 : "Allah swt amefaradhisha Zaka pamoja na Sala. Ameamrisha kutekeleza Sala na kutoa Zaka hivyo iwapo mtu atasali bila ya kutoa Zaka, basi atakuwa hakukamilisha Sala." . Vile vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. Wasa'il as-Shiah, Zakat,mlango 3, Hadith 13, J.6, Uk. 11: amesema kuwa : "Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliingia katika Masjid an-Nabawi, na aliwataja watu watano kwa majina yao na akasema kuwa inukeni na mtoke humu Msikitini na wala msisali kwani nyinyi hamutoi Zaka. (Wasiolipa Zaka wamefukuzwa kutoka Msikitini !)


. Vile vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anasema katika Wasa'il as-Shiah, ZAKAT,mlango 3, Hadith 24, J.6, Uk 14 : "Mtu yeyote asiyelipa Zaka ya mali yake basi yeye wakati wa mauti yake atataka kurudishwa humu duniani ili aweze kutoa na kulipa Zaka, kama vile Allah swt anatuambia: 'Ewe Allah swt nirudishe tena ili nikafanye mema niliyokuwa nimeyaacha !' Yaani wakati wa kifo chake atasema kuwa arudishwe humu duniani ili akaitumie mali aliyoilimbikiza katika njia njema, lakini atajibiwa kuwa kamwe haitawezekana hivyo kurudi kwake." . Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ameelezea tafsir ya Ayah isemayo kuwa : 'Allah swt atawaonyesha matendo yao katika hali ya kusikitisha mno kuwa wao hawatatoka nje ya Jahannam' kama ifuatavyo katika Wasa'il as-Shiah,mlango 5, Hadith 5, J.6, Uk 21 :

"Mtu yule ambaye anakusanya na kulimbikiza mali yake na anafanya ubakhili katika kuitumia katika mambo mema na kwa kutoa zaka n.k., basi anapokufa huku amewaachia mali hiyo wale ambao watatumia mali hiyo katika utiifu wa Allah swt au kwa kutenda madhambi, basi iwapo itatumiwa katika utiifu wa Allah swt basi atakuwa mtu wa kujivuna na iwapo itatumiwa katika maasi na madhambi basi itamdhalilisha." . Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema, Wasa'il as-Shiah,mlango 5, Hadith 5, J.6, Uk21 : "Hakuna kitu kinachokimaliza Islam kama Ubakhili na njia ya Ubakhili ni sawa na njia ya sisimizi ambayo haionekani na yenyewe ipo kama Shirk ambayo inayo aina nyingi." . Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema katika Safinat al-Bihar, J.1 Uk. 155 : "Watu watakapokataa kutoa Zaka, basi baraka itakuwa imeondolewa kutoka ardhini kwa kutoa mazao na matunda kutoka mashamba yao,na madini."


. Vile vile Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema katika Wasa'il as-Shiah, Mlango 1, Hadith 13 : "Muwatibu wagonjwa wenu kwa kutoa Sadaka na mutokomeze balaa, maafa kwa Du'a na muhifadhi mali zenu kwa kutoa Zaka." . Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema Wasa'il as-Shiah,mlango 5, Hadith 10, J.6, Uk23 : "Allah swt anazo mahala pengi humu ardhini ambazo huitwa 'kilipiza kisasi' hivyo Allah swt anapomjaalia mtu mali na utajiri, na huyo mtu haitumii kwa kutoa malipo aliyofaradhishiwa, basi huwekewa nafasi mahala hapo. Mali ambayo anakusanya kwa mbinu zake zote,inapomtoka na anaiachia wengine."


. Zipo riwaya nyingi ambazo zinazumngumzia kukufurishwa kwa mtu asiyetoa Zaka kwa sababu za ubakhili wake. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema katika Wasa'il as-Shiah,mlango 4, Hadith 2, J.6, Uk 18 : "Bila shaka Allah swt amewawekea hisa mafukara na wenye shida katika mali za matajiri ambayo imefaradhishwa. Faradhi ambayo inapotimizwa inakuwa ni yenye kuwafakharisha matajiri hao na ni kwa sababu ya kutoa huko Zaka kunakoharamisha kumwagwa damu yao na wanaolipa zaka wanaitwa Waislamu."


. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, Wasa'il as-Shiah,, J.6, Uk 18 : "Mtu yeyote yule ambaye hatatoa Zaka hata lau kwa kiasi cha Qirat (1.20 Dinar yaani punje nne za Shayiri) basi huyo si Mumin wala si Mwislamu na watu kama hawa ndivyo alivyoelezea Allah swt kuwa watakuwa wakitaka warudishwe humu duniani ili watekeleze mema." . Vile vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ameeleza katika Wasa'il as-Shiah,, J.6, Uk 18: "Mtu yeyote yule ambaye hatatoa Zaka hata kwa kiasi cha Qirat moja (sawa na punje nne za Shayiri) basi huyo atakuwa bila imani na kufa kwa mauti ya Myahudi au Mnasara.". Amesema vile vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. katika Wasa'il as-Shiah, Zakat, mlango 3, Hadith 1, J.6, Uk. 19 na Kafi : "Allah swt ameruhusu kumwagwa damu ya watu wa aina mbili ambapo hukumu hii itatekelezwa pale atakapodhihiri Al-Imam Muhammad Mahdi, Sahibuz-Zamaan, a.s. na hivyo mmoja miongoni mwa watu hao wawili ni yule anayefanya zinaa ilhali anayo mke wake hivyo atauawa kwa kupigwa mawe hadi kufa kwake na wa pili ni yule asiyetoa Zaka, huyo atakatwa kichwa." . Vile vile amesema, katika Wasa'il as-Shiah,mlango 5, Hadith 8, J.6, Uk 20 : "Mali haipotei katika majangwa na Baharini isipokuwa ile isiyolipiwa Zaka na atakapodhihiri Al-Imam Muhammad Mahdi, Sahibuz-Zamaan, a.s. basi wale wote wasiolipa Zaka watasakwa na kukamtwa na watakatwa shingo zao."


. Amesema Allah swt katika Quran: Surah al -Fussilat, 41, Ayah 6-8 : "Ole wao wanaomshirikisha, ambao hawatoi Zaka na wanaikataa Aakhera." . Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. , katika Al-mustadrak : "Kwa kiapo cha Allah swt ambaye anayo roho ya Mtume Wake katika kudura yake, kuwa hakuna mtu anayemfanyia khiana Allah swt isipokuwa Mushrikina kama hawa ambao hawatoi Zaka kutoka mali zao."


. Vile vile Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimwambia Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., katika Al-Khisal, Uk. 450, Mlango Kumi : "Ya Ali ! Katika Ummah wangu wapo makafiri wa makundi kumi : Mfitini na mchonganishi Mchawi Dayyuth yaani mwanamme yule ambaye anajua kuwa mke wake anazini lakini hajali bali anapuuzia, Mwanamme yule ambaye anauroho wa kiharamu wa kutafuta wanawake mbalimbal kwa kulawiti, Anayewalawiti wanyama Anayezini pamoja na wale walioharamishwa kwake yaani ambao ni mahram kwake, Anayechochea na kuzidisha moto wa fitina na chuki miongoni mwa watu, Anayewasaidia makafiri kihali na mali kupigana dhidi ya Waislamu, Asiyetoa Zaka Asiye Hijji ilhali ana uwezo kamili na kutimiza masharti yake na akifa katika hali hiyo."


. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema katika kuzungumzia faida za utoaji wa Zaka, katika Kafi na Wasail, Mlango 1, Hadith 9 : "Bila shaka Zaka imefaradhishwa kwa ajili ya kuwajaribu (mtihani) matajiri na wenye mali na kuwatimizia mahitaji ya wenye shida na kwa yakini, iwapo watu wangalikuwa wakitoa Zaka ipasavyo, basi kusingalikuwapo na Waislamu masikini na wenye shida na wala kusingalikuwa na mmoja kumtegemea mwingine na wala kusingalikuwapo na wenye kuwa na njaa au wasiokuwa na nguo. Lakini taabu na shida zote walionazo masikini ni kutokana na wenye mali na utajiri kutotimiza wajibu wao wa kutoa Zaka na Sadaka. Hivyo Allah swt humtenga mbali na neeema na baraka Zake yule ambaye hatimizi wajibu wake huo. Nami naapa kwa kiapo cha Allah swt ambaye ameumba viumbe vyote na anawapatia riziki zao, kuwa hakuna kinachopotea katika mali katika nchi kavu au majini isipokuwa ile isiyotolewa Zaka. Faida ya tatu, Nafsi yetu inatoharishwa kwa udhalilisho wa ugonjwa sugu wa ubakhili na hivyo inatubidi sisi lazima tuutibu ugonjwa huu unaoangamiza na kutumaliza.


. Hivyo Amesema Allah swt katika Qur'an Tukufu, Surah al-Tawba, Ayah 103 : "Chukua Sadaka katika mali yao, uwasafishe na kuwatakasa kwa ajili ya hizo (Sadaka zao na kuwataja kwa vizuri (mbele yangu) na uwaombee dua. Kwa hakika kuwaombea kwako kutawapa utulivu, na Allah swt ndiye asikiaye na ajuaye." . Vile vile Amesema Allah swt katika Qur'an Tukufu, Surah al - Hashri, 59, Ayah 9: "Na walio na maskani zao na Imani yao kabla yao, wanawapenda waliohamia kwao, wala hawaoni choyo katika vifua vyao kwa waliyopewa (Wahajiri), bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji. Na mwenye kuepushwa uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufanikiwa."


. Amesema Allah swt katika Qur'an Tukufu, Surah al -Baqarah, Ayah 28 : "Allah swt huongezea katika Sadaka" . Allah swt amesema katika Qur'an Tukufu, Surah al - Sabaa, 34, Ayah 39 : 'Chochote kile mtakachokitoa (katika njia yake), basi Atawalipeni (humu humu duniani) malipo yake, Naye ni Mbora wa wanao ruzuku.' . Amesema Allah swt katika Qur'an Tukufu, Surah al -Rum, 30, Ayah 39 : 'Na mnachokitoa kwa riba ili kiongezeke katika mali ya watu, basi hakiongezeki mbele ya Allah swt . Lakini mnachokitoa kwa Zaka kwa kutaka radhi ya Allah swt, basi hao ndio watakaozidishiwa.'


. Amesema Bi. Fatimah az-Zahra a.s. bintie Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika hotuba aliyoitoa kuzungumzia Fadak katika Bihar al-Anwaar, J.8, Uk 109 : "Kwa ajili ya kujitakasa na dhambi la Shirk, Allah swt ametufaradhishia kuikamilisha imani yetu (yaani mtu yeyote anayetaka kujitakasisha na unajisi basi inambidi kuleta imani kwa moyo wake kamilifu), na Sala inamwepusha na magonjwa ya kiburi na kujifakharisha, na Zaka inamwepusha mtu kwa magonjwa ya ubahili ili mwanadamu awe mkarimu na mpenda kutoa kwa ajili ya mema ili atakasike) na hii pia ndiyo sababu kuu katika kujiongezea riziki ." . Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ameripotiwa akisema katika Al-Kafi: "Yeyote yule anayetumia kutoka mali yake katika njia ya kheri, basi Allah swt anamlipa mema humu duniani na kumwongezea katika malipo yake."


. Vile vile ameripotiwa akisema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. katika Wasa'il as-Shiah : Mlango Sadaka, Hadith 19, J.6, Uk. 259 : "Tafuteni riziki yenu kwa kutoa Sadaka." . Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ameripotiwa katika Kitab 'Uddatud-Da'i kuwa alimwuliza mtoto wake : "Je nyumbani kuna kiasi gani kwa ajili ya matumizi?"

Naye alimjibu : "Zipo Dinar arobaini tu." Imam a.s. alimwambia "Dinar zote hizo zigawe Sadaka." Kwa hayo mtoto wake alimwambia Imam a.s. "Ewe Baba ! Mbali na Dinar hizi arobaini, hatutabakia na akiba yoyote." Imam a.s. alimwambia : "Nakuambia kuwa zitoe Dinar zote Sadaka kwani ni Allah swt tu ndiye atakayetuongezea kwa hayo. Je wewe hauelwei kuwa kila kitu kina ufunguo wake ? Na ufunguo wa riziki ni Sadaka ( kutolea mema )."


Kwa hayo, mtoto wake aliyekuwa akiitwa Muhammad, alizitoa Sadaka Dinar hizo na hazikupita siku kumi, Imam a.s. alitumiwa Dinar elfu nne. Hapo Imam a.s. alimwambia mwanae : "Ewe Mwanangu ! Sisi tulitoa Dinar arobaini tu na Allah swt ametupa Dinar elfu nne badala yake." . Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema katika Nahjul Balagha kuwa : "Mtu anapokuwa masikini au mwenye shida basi fanyeni biashara pamoja na Allah swt kwa kutoa Sadaka."

. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema : "Zakat-i-Fitrah inakamilisha saumu za mwezi Mtukufu wa Ramadhani." . Amesema Allah swt katika Qur'an Tukufu, Surah al - Tawbah, 9, Ayah 60 : "Wa kupewa Sadaka ni mafakiri, na masikini, na wanaozitumikia, na wa kutiwa nguvu nyoyo zao, na katika kukomboa watumwa, na wenye madeni, na katika Njia ya Allah swt , na wasafiri. Huu ni wajibu uliofaradhiwa na Allah swt . Na Allah swt ni Mwenye kujua Mwenye hikima."

. Vitu saba vina Zaka Sunnah : " Mali ya biashara au mtaji Mali ambayo mtu anataka kuitumia katika kufanyia biashara " Aina za nafaka : Mfano mchele, dengu, dengu iliyoparazwa. Lakini mbogamboga kama vile biringanya, matango, matikimaji, maboga hayana Zaka. " Farasi jike " Vito vya dhahabu na mawe Vitu vilivyotengezwa vya kuvaa na mawe kama almasi n.k. " Mali iliyozikwa au kufichwa Iwapo mtu atakuwa na mali aliyoizika au aliyoificha ambayo hawezi kuitumia basi kwa misingi ya uwezo inambidi kutoa Zaka ya mwaka mmoja. " Kukwepa kutoa Zaka Iwapo mtu atauza sehemu ya mali kiasi fulani kabla ya kuisha kwa mwaka kwa misingi ya kukwepa kulipa Zaka, basi itambidi uanzapo mwaka mpya, alipie Zaka sehemu hiyo aliyokuwa ameuza kwa ajili ya kukwepa Zaka yake. " Mali ya kukodisha Mtu anayepokea malipo kutokana na kukodisha majumba, maduka, mashamba, mabustani au hamaam (mabafu yanayotoza malipo kwa kutumia ).


KHUMS
. Allah swt anavyotuelezea katika Qur'an Tukufu, Surah al-Anfaal, 8, Ayah 41 : NA JUENI ya kwamba ngawira mnayoipata, basi khums (sehemu moja katika tano) ni kwa ajili ya Allah swt na Mtume, na jamaa, na mayatima, na masikini, na wasafiri, ikiwa nyinyi mmemuamini Allah swt na tuliyoteremsha kwa mja wetu(Muhammad) siku ya kipambanuo (katika Vita vya Badr), siku ( Waislamu na Makafiri ) yalipokutana majeshi mawili. Na Allah swt ni Muweza wa kila kitu. . Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, katika Man la yahdhurul Faqih, J.2, uk.41 "Kwa kuwa Allah swt ametuharamishia Zaka sisi Ahlul-Bayt a.s.hivyo ametuwekea Khums kwa ajili yetu na hivyo Sadaka pia ni haram kwetu na zawadi imeruhusiwa kwa ajili yetu."


. Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. amesema, katika Usuli Kafi, J. 1, Uk.545 : "Hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kununulia chochote kutoka kifungu ambacho Khums haijalipwa na hadi pale wasipoifikisha kwa wanaostahiki kwetu." . Vile vile Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. amesema, katika Al-Kafi, J.1, Uk. 546 : "Siku ya Qiyamah wakati ule utakuwa mgumu kabisa pale wanaostahiki Khums watakapotokezea kudai haki zao kutoka wale wasioilipa." . Miongoni mwa marafiki tajiri mmoja kutokea Uajemi alimwandikia barua Al-Imam 'Ali ar-Ridha a.s. na alimwomba Imam a.s. ruhusa ya kuitumia ile mali ambayo khums haijatolewa. Basi Imam a.s. alimwandikia majibu kama ifuatavyo : Imenakiliwa kutoka Al-Wafi, Al-Kafi na Tahdhib "Bila shaka Allah swt ni Wasi' na Mkarimu na amechukua dhamana ya kumlipa thawabu na malipo mema yule mtu ambaye atatekeleza hukumu zake na ameweka adhabu kwa yeyote atakayekwenda kinyume ya hayo.


Bila shaka mali iliyo halali kwa ajili ya mtu ni ile ambayo Allah swt ameihalalisha na kwa hakika Khums ni dharura yetu na ni hukumu ya Dini yetu na ni njia ya kujipatia kipato kwa jili ya riziki sisi na wenzetu na imewekwa kwa ajili ya kulinda hishima zetu dhidi ya wapinzani wetu. Hivyo kamwe musiache kutoa na kulipa Khums. Na kila inapowezekana kusijikoseshe Du'a zetu na kwa hakika kwa kutoa Khums kunazidisha riziki yenu na kutoharisha na ni hazina kubwa kwa ajili ya Siku ile ambayo kutakuwa na taabu tupu na mateso (Siku ya Qiyamah). Na kwa hakika Mwislamu sahihi ni yule ambaye amemwahidi Allah swt kwa ahadi na 'ibada, basi atimize kwa ukamilifu. Na iwapo atakubali kwa mdomo tu ilhali moyoni anakataa na kupinga basi atambue kuwa yeye si Mwislamu.


. Imeripotiwa kutoka Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. katika Al-Kafi J.5, Uk. 144 kuwa : "Iwapo mimi nitapenda kumpatia kitu rafiki yangu basi mimi nitampa zawadi kwani ninaipenda zaidi kuliko Sadaka." . Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. kwa muda wa siku saba hakupata mgeni nyumbani kwake basi alisema huku akilia : "Nasikitika mno na ninakhofu kuwa isije Allah swt akaniondolea rehema na baraka zake." . Amesema Allah swt katika Qur'an Tukufu Surah al- Ma'arij,70, Ayah 24 - 25 : Na ambao katika mali yao iko haki maalumu. Na mwenye kuomba na anaye jizuilia kuomba…

. Al Imam Musa bin Ja'afer a.s. amepokelewa riwaya kuwa : "Katika ukoo wa Bani Israil kulikuwa na mtu mwema ambaye alikuwa na mke aliye mwema pia. Siku moja aliota ndoto ambamo aliambiwa kuwa Allah swt amempangia kiasi fulani cha umri wake ambapo nusu ya umri huo utapita katika raha na mustarehe wakati nusu ya umri uliobakia utapita katika shida na dhiki na umasikini. Hivyo Allah swt amekupa fursa wewe kuchagua iwapo utapenda kupitisha umri wako wa nusu ya awali ya raha na mustarehe na baadaye dhiki na umasikini ? Hivyo chagua mojawapo. Kwa hayo mtu huyo alijibu kuwa : 'Mimi ninaye mke wangu aliye mwema na hushirikiana naye katika maswala yote, hivyo nitapenda kupewa muda wa kuweza kuongea naye kabla sijatoa uamuzi wa chaguo langu.'


Mke wake alimshauri mumewe kuukubalia umri ule wenye neema uwe ndio wa kuanzia kwani: 'Inawezekana Allah swt anataka kututeremshia neema na baraka zake hivyo tukaongoka.' Hivyo usiku uliofuatia, bwana huyo aliulizwa jibu alilolifikia katika uamuzi wake. Naye akajibu : 'Mimi ninataka kuupitisha nusu ya umri wangu katika neema, raha na mustarehe.' Kwa hayo akajibiwa kuwa hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa mujibu wa chaguo lake. Kuanzia hapo yeye alijaaliwa kila aina ya raha na akawa tajiri mkubwa mwenye mali na milki nyingi.


Katika kutajirika huku, mke wake akamwambia, 'Ewe Bwanangu! Usiwasahau kuwasaidia na kukidhi haja za majamaa zetu na mafukara na masikini na uwe na uhusiano mwema pamoja nao. Na uwazawadie watu fulani fulani wakiwemo majirani na marafiki, zawadi mbalimbali.' Mtu huyo alizingatia na kutekeleza ushauri uliokuwa umetolewa na mke wake. Na hivyo alifungua milango ya kugawa mali yake katika masuala hayo hadi ulipofika wakati wa kuisha kwa nusu ya umri wake wa awali. Kuisha huku kwa nusu ya kwanza ya umri wake, aliota ndoto tena ambamo aliambiwa kuwa : 'Kwa kutokana na uwema wako wa kuwasaidia wenye shida na dhiki imekuwa kipaumbele kwako, basi Allah swt amekubadilishia sehemu hii ya pili kuwa katika raha na mustarehe kama ilivyo sasa.'"


. Wakati wa mavuno kwa kiwango kile ambacho bado Zaka haijapigiwa hisabu, inagawiwa kwa kuchota mkono moja kwa wapita njia kama vile alivyosema Allah swt katika Qur'an Tukufu, Surah al -Al-An-'Aam 6, Ayah 141 : Na Yeye ndiye aliye ziumba bustani zenye kutambaa juu ya chanja, na zisiyo tambaa, na mitende, na mimea yenye matunda mbali mbali, na mizaituni na mikomamanga inayo fanana. Kileni matunda yake inapo zaa, na toeni haki yake siku ya kuvunwa kwake. Wala msitumie kwa fujo. Hakika Yeye hawapendi watumiayo kwa fujo.

. Yaani kuwakopa Waislamu ambao wanashida ya kukopa deni ili kukidhi masuala yao. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, katika Al-Kafi : "Katika mlango wa Jannat kumeandikwa 'Yapo mema kumi kwa mtoa Sadaka na mema kumi na nane kwa mkopeshaji madeni.'" . Vile vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, katika Al-Wafi : "Wakati Mumin mmoja anapomkopesha Mumin mwenzake deni kwa ajili ya kutaka ridhaa ya Allah swt , basi Allah swt anamhisabia deni hilo katika Sadaka hadi kuja kulipwa kwake."

. Vile vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ameripotiwa akisema kuwa : "Kwa kupuuzia 'Ma'un' (mambo ya nyumbani ) ambayo Allah swt ameahidi katika Qur'an Tukufu adhabu, basi si Zaka inayozungumziwa, bali ni kuwasaidia kwa kuwakopa wale wenye shida na wenye shida wanapokuja kuazima vitu vya nyumbani, basi inabidi kuwa azima vitu vya nyumbani." . Abu Basir amemwambia Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuwa "Majirani zetu wanapokuja kuazima vyombo au vitu vingine vya nyumbani, na tunapo waazima basi huvunja vunja na kuviharibu vitu vyetu na hivyo sisi tunalazimika kuwakatalia kwa misingi hiyo, sasa je kuwakatalia huku ni dhambi ?"


. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alimjibu : "Iwapo watu hao wanatabia kama hiyo, basi si dhambi kuwanyima." . Inabidi kuwapa muda au kuwasamehe madeni wale ambao hawana uwezo wa kuyalipa madeni hayo. Na kuhusiana na swala hili Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema : "Iwapo mtu anataka asidhalilishwe Siku ambayo hakuna mwingine wa kuwaokoa isipokuwa Allah swt , basi inambidi awape muda wa kulipa madeni wadaiwa wake au kuwasamehe madeni yao."


. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema : "Yeyote yule atakayempa muda wa kulipa madeni ambaye hana uwezo wa kulipa ( basi kwa ajili yake ) thawabu zake mbele ya Allah swt ni sawa na thawabu za kutoa Sadaka kila siku kwa kiasi hicho hadi atakapolipwa." . Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. aliambiwa kuwa : "Abdur Rahmaan bin Sababah anamdai deni marehemu mmoja, nasi twamwambia yeye kuwa amsamehe lakini yeye anakataa kata kata kumsamehe deni lake."


. Kwa hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akasema : "Ole wake, je haelewi kuwa iwapo atamsamehe marehemu deni lake basi Allah swt atamlipa Dirham kumi kwa kila Dirham yake moja. Na iwapo hatamsamehe basi atalipwa Dirham moja kwa Dirham yake moja." . Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, Al-Kafi, J.2,Uk. 204 : "Mtu yeyote atakayemsaidia Mumin kwa mavazi wakati wa baridi au joto basi Allah swt atamjaalia mavazi ya Jannat (Peponi au Paradiso ) na atampunguzia shida kali wakati wa kutoa roho yake (wakati anapokufa ) na atampanulia kaburi lake na Siku ya Qiyamah atakapotoka nje ya kaburi lake atakuwa akitoka katika hali ya furaha kwa kuonana na Malaika."

. Vile vile Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema, Al-Kafi, J.2, Uk.205 : "Iwapo Mwislamu yeyote atamsaidia mtu asiye na mavazi kwa mavazi au aliye na dhiki ya mali, akasaidiwa ( nyumba,mali n.k ) basi Allah swt anamwekea Malaika elfu saba hadi Siku ya Qiyama kwa ajili ya kumwombea maghfirah kwa kila dhambi lake." . Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, katika Al-Wafi, al-Kafi na kunakiliwa pia katika Tahdhiib : "Baada ya kufariki kwa mtu, huongoka kwa mambo matatu " Sadaka ambayo aliitoa humu duniani na ambayo inaendelea baada yake, " Sunnah ambayo aliitekeleza kwa mfano Adhan ambayo baada ya kifo chake ingali ikiendelea, " Kuacha mtoto mwenye tabia na mienendo mizuri ambaye atakuwa akimwombea dua na usamehevu kwa ajili yake ( na akifanya mema kwa niaba ya baba yake, kama inavyoelezwa katika vitabu vingine.