HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W)PAMOJA NA MAIMAMU (A.S)

 
UMRI WETU TUUTUMIE VYEMA.
. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimwambia Abu Dhar, Bihar al-Anwaar, J. 77, Uk. 77: "Ewe Aba Dhar ! Faidi vitu vitano kabla ya vitu vitano: Ujana kabla ya uzee, Siha yako kabla ya magonjwa, Utajiri wako kabla ya umaskini, Ufaragha wako kabla hujawa mashughuli, na maisha yako kabla ya kifo chako."

. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., amesema Ghurar-ul-Hikam, Uk. 257: "Itakapofika siku ya Qiyamah, kikundi cha watu kitasimama na kuja kubisha hodi katika mlango wa Jannat. Nao wataulizwa ni nani wao, nao watajibu: Sisi ni watu wa subira na kwa hayo wataulizwa ni kitu gani walichokifanyia subira, nao watajibu sisi tumefanya subira kwa ajili ya Allah swt dhidi ya kumwasi Allah swt. Kwa hivyo Allah swt atasema kuwa hao ni wasema ukweli na atawaruhusu waingie Jannat. Kwani Allah swt amesema katika Qur'an Tukufu: Sura Az-Zumar, 39, Ayah 10: 'Sema: Enyi waja wangu mlio amini ! Mcheni Mola wenu Mlezi. Wale wafanyao wema katika dunia hii watapata wema. Na ardhi ya Allah swt ni kunjufu. Hakika wenye subira watapewa ujira wao bila ya hisabu.'"


. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., amesema Ghurar-ul-Hikam, Uk. 206: "Aliye na furaha ni yule ambaye hana matamanio na matarajio makubwa katika maisha yake na anafaidi kila fursa anayoipata."

DINI NA KUSOMEA MAMBO YAKE.
. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema, Bihar al-Anwaar, J. 1, Uk. 176: "Ole wake yule Mwislam ambaye habakizi siku moja katika juma zima kwa ajili ya kujifunza masuala ya dini yake na wala kujaribu kufanya uchunguzi na utafiti wa dini yake." . Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., amesema Al-Muhajjat-ul-Baidha, J. 1, Uk. 15: "Yeyote yule anayesomea dini ya Allah swt, basi kwa hakika ana uwezo mkubwa wa kuondoa matatizo yake na kumpatia yeye riziki kutokea mahala ambapo yeye alikuwa hata hajaweza kuwazia."

. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema Bihar al-Anwaar, J. 1, Uk. 214: "(Vijana wa Kish'ia lazima wawe na program au utaratibu wa kujifunza masuala ya dini). Mimi ninapomwona kijana wa Kishi'a ambaye hana program au utaratibu kama huu basi mimi nitamfundisha somo." . Al Imam Muhammad al-Baquir a.s., amesema Bihar al-Anwaar, J. 2, Uk. 29: "Wajulishe wafuasi wetu kuwa kwa hakika bila shaka wao watakuwa miongoni mwa wale watakao okoka siku ya Qiyamah kwa masharti iwapo wao watakuwa watimizaji wa yale wanayo amrishwa."

. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema, Bihar al-Anwaar, J. 2, Uk. 153: "Yeyote yule kutokea Ummah wangu atakaye hifdhi ( kariri ) hadithi arobaini ambazo zinahitajiwa na watu katika maisha yao ya kidini (kwa ajili ya Tabligh na muongozo), basi Allah swt atamwinua akiwa hakimu kutoka waliokufa Siku ya Qiyamah."

UPOLE NA MATOKEO YAKE MAZURI
. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ,Bihar al-Anwaar, J. 71, Uk. 373: "Kwa hakika mja anaweza kujipatia daraja la yule anayefunga saumu katika nyakati za mchana na anayesali usiku kucha, kwa tabia zake nzuri za upole." . Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. alimwambia mtoto wake Al Imam Hassan ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. ,Bihar al-Anwaar, J. 78, Uk. 111: "Ewe Mwanangu ! Hakuna utajiri uliona thamani kuliko akili na hakuna umasikini uliosawa na ujahili; hakuna ugaidi ulio mbaya kabisa kama kiburi,na hakuna maisha yenye raha kuliko kuwa mpole."


. Al Imam Hassan ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema, Khisal-i-Sadduq, Uk. 29: "Kwa hakika, bora ya bora zote ni tabia njema." . Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema, Bihar al-Anwaar, J. 71, Uk. 394: "Tabia njema ipo katika njia tatu: Kujiepusha na vitu vilivyo haramishwa, kutafuta yale yaliyo halalishwa, na kutendea haki wana nyumba wake."

. Al Imam Zaynul 'Abediin a.s., amesema Khisal-i-Sadduq, Uk. 317: "Kauli njema huongezea mali, utajiri, na riziki, na huahirisha ajali, na hutengeneza mapenzi miongoni mwa wenye nyumba, na humfanya mtu akaingia Jannat." . Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, Al-Kafi, J. 2, Uk. 103: "Yapo mambo matatu ambayo yeyote yule atakayezifikisha kwa Allah swt, basi Allah swt atamfaradhishia Jannat kwa ajili yake: Kutoa mchango katika umaskini, desturi nzuri pamoja na watu wote, na kujitendea haki nafsi yake." . Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema, Al-Kafi, J. 2, Uk, 100: "Kwa mambo ambayo umma wangu utajipatia Jannat ni hasa kwa mema yote, na desturi nzuri."


ATHARI MBAYA ZA HASIRA NA TABIA MBAYA.
. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema, Al-Kafi, J. 2, Uk. 302: "Hasira inaiharibu imani kama vile siki(huwa chachu) inavyoharibu asali." . Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, Al-Kafi, J. 2, Uk. 303: "Ghadhabu ni ufunguo wa kila aina ya shari." . Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s. amenakili kutoka kwa mzazi wake a.s. ambaye amenakili kutoka Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ambaye Amesema kuwa, Bihar al-Anwaar, J. 75, Uk. 27: "Mtu mmoja alimwijia Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ili afundishwe tendo ambalo litaondoa kizuizi baina yake na Jannat.


Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimwambia: Usiwe mkali; usiwaombe watu vitu, watakie watu kile ujitakiacho wewe mwenyewe." . Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, Al-Kafi, J. 2, Uk. 303: "Yeyote yule anayezuia ghadhabu zake, basi Allah swt atazificha siri zake." . Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema Al-Kafi, J. 2, Uk. 303: "Ghadhabu ni kitu kinacho teketeza moyo wa hakimu; kwani yeyote yule asiyeweza kudhibiti vyema ghadhabu yake basi kamwe hawezi kuitumia busara yake."


KUOMBA TAWBA YA ALLAH SWT.
. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., amesema Bihar al-Anwaar, J. 6, Uk. 22 : "Mjipake manukato ya Istighfar ili hata tone na mabaki ya madhambi yenu yasiwadhalilishe nyie." . Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. alimfundisha mtu mmoja kwa kumwomba Allah swt dua kwa kumwambia, Bihar al-Anwaar, J. 94, Uk. 242 : "Sifa zote ni za Allah swt kwa kila neema; na mimi ninamwomba kila la kheri na kila la wema; na naomba Allah swt aniepushe na kila aina ya shari; na ninamwomba Allah swt msamaha kwa madhambi yote."

. Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema kuwa, Khisal-i-Sadduq, Uk. 317: "Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliulizwa kuwa bora wa waja ni nani, naye alijibu: Wao ni: " Wanapofanya mema wanafurahia hayo; " wanapofanya mabaya basi wanaomba Tawba na Istighfar ; " wanapojaaliwa chochote wanashukuru; " wanapokuwa katika hali ngumu, wanaonyesha subira; " wao wanapo mghadhabikia mtu, humsamehe." . Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., amesema Makarim-ul-Akhlaq, Uk. 313: "Anapozidisha muumin Mwislam kwa kuomba Istighfar ya Allah swt, basi rikodi ya matendo yake mema yataongezeka na yatakuwa yaking'ara."


SALAA YA JAMA'A.
. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.,amesema Bihar al-Anwaar, J. 88, Uk. 4: "Allah swt huheshimu sana yule mja anayesali sala kwa Jama'a na baada yake anapoomba kitu chochote basi Allah swt lazima humtimizia." . Al Imam Musa al-Kadhim a.s., amesema Bihar al-Anwaar, J. 88, Uk. 4 na Wasa'il ush-Shi'ah, J. 8, Uk. 290: "Fadhila za sala ya Jama'a kwa sala ya mtu anayesali peke yake ni kila raka'a moja katika Jama'a ni bora kuliko raka'a elfu moja (1000) zinazosaliwa na mtu peke yake."


. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., amesema Mustadrak-ul-Wasa'il, J. 6, Uk. 446: "Sala moja ya mtu katika Jama'a ni bora kuliko sala za miaka arobaini anazosali akiwa nyumbani kwake (peke yake)." . Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema, Bihar al-Anwaar, J. 88, Uk. 6: "Safu ya mistari katika sala ya Jama'a inayosaliwa juu ya ardhi ni sawa na safu za Malaika huko mbinguni; na Raka'a moja inayosaliwa katika Jama'a ni sawa na Raka'a ishirini na nne na kila raka'a moja inayosaliwa na wapenzi wa Allah swt kuliko sala za miaka arobaini. Hivyo, siku ya Qiyamah ambayo ni siku ya uadilifu wakati Allah swt atakapo wakutanisha wanaadamu wote kuanzia mwanzoni hadi mwisho, basi hakutabakia na muumin yeyote ambaye amesali sala ya Jama'a, kwamba Allah swt atampunguzia shida zake za siku ya Qiyamah na ataambiwa aingie Jannat."


. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. siku moja aliijiwa na Kipofu mmoja ambaye alisema, At-Tahdhib, J. 3, Uk. 266: "Kulikuwa hakuna mtu yeyote wa kumchukua Msikitini ili aweze kushiriki katika sala ya Jama'a pamoja na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. pale aliposikia Adhana ikitolewa. Hapo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimwambia: "Funga kamba kutoka nyumbani kwako hadi Msikitini na ushiriki katika sala ya Jama'a." . Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema, Bihar al-Anwaar, J. 88, Uk. 11: "Mtu yeyote ambaye anaiacha sala ya Jama'a bila ya kuwa na Udhuri inayokubalika bali bila sababu yoyote, kwa misingi ya kutotaka kushiriki katika mkusanyiko wa Waislam, basi atakuwa hana Sala yoyote."

. Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s., amesema Bihar al-Anwaar, J. 88, Uk. 12: "Kwa hakika sala ya Jama'a imefaradhishwa ili kuwepo imani halisi katika umoja, katika Islam, na katika kumwabudu Allah swt kiwazi wazina ambayo imedhihirishwa kuwa bayana, kwa sababu, ili iweze kuwadhihirikia watu wa mashariki na wa magharibi (wa dunia hii). Hivyo ukweli na asili wa Uislam utadhihirika na kujulikana na makafiri na mapagani kabla ya Uislam utakuwa ni kama kiza mbele ya nuru, kiza ambacho hatimaye kinapotea. Vile vile sala ya Jama'a husababisha watu kutambuana na kuelewana na inawezekana wengine wakawa mashahidi kuhusu wengineo kuhusu Uislam wao, ambamo kuna uwezekano na vile vile kushirikiana katika mambo mema na ya kumfurahisha Allah swt mambo ambayo yanawazuia wasimuasi Allah swt kupita kiasi."


NEEMA NNE ZA ALLAH SWT
. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Amesema kuwa kila asubuhi, kila Mwislamu anatakiwa azikumbuke neema nne za Allah swt. Hofu yangu ni kwamba asipozikumbuka, kuna hatari ya kuzipoteza neema hizo: " Namshukuru Allah swt ambaye amenisaidia kumtambua Yeye na hakuuacha moyo wangu gizani. " Namshukuru Allah swt ambaye ameniweka pamoja na wafuasi wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. " Namshukuru Allah swt ambaye ameiweka riziki yangu kwake Yeye na si mikononi mwa watu. " Namshukuru Allah swt ambaye amezifunika dhambi zangu na aibu zangu na hakunidhalilisha mbele ya watu.

. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s.,Nur al-Absaar Shablanji. "Mwovu wa watu ni yule anayewawekea pingamizi na anakuwa mkali kwa watu wake wa nyumbani." . Allah swt amesema katika Qur'an Tukufu : "Enyi mlioamini! Ingieni katika hukumu za Uislamu zote, wala msifuate vyayo za Shaytani; kwa hakika yeye kwenu ni adui dhahiri."


SIFA ZA KUPENDEZA ZA MWANAMKE
. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., amesema Wasa'il ush-Shi'ah,Vo. 20, Uk.172 "Malipo ya mwanamke mcha Allah swt kwa kumpa mume wake bilauri moja ya maji ni zaidi ya kufanya ibada mwaka mzima ambamo mchana anafunga saumu na usiku zake anakesha katika kufanya ibada." . Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., amesema Al-Kafi, J.5, Uk. 508: "Ni kwa mwanamke kujiweka msafi kabisa kwa kujipaka manukato bora kabisa na kuvaa mapambo ambayo yatamfanya yeye amvutie bwana wake na ajiweke tayari kwa ajili ya bwana wake usiku na mchana."


. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., amesema Nahjul Balagha, Msemo 494: "Jihadi ya mwanamke (vita katika njia ya Allah swt ) ni kuwa na uhusiano mwema na kuwa mshiriki wa bwana wake." . Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., amesema Usuli kafi, J. 5, Uk. 327 "Iwapo ningetaka kukusanya mema yote ya dunia hii na Aakhera kwa ajili ya Mumin basi mimi ningeziweka kwa ajili ya moyo mnyenyekevu, ulimi wenye shukurani na isemayo mema, mwili ufanyao subira wakati wa shida na dhiki.


(Kwa ajili ya mwanamme Mimi ningempa) Mke mcha-Allah swt ili anapouona uso wake anajawa na furaha na yeye (mwanamke) anaihifadhi na kulinda mali yake, pale bwana wake anapokuwa hayupo." . Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., amesema Bihar al-Anwaar, J.103, Uk. 252 "Amelaaniwa! Amelaaniwa kabisa mwanamke yule ambaye anautonesha moyo wa mume wake na kumfanya akasirike. Lakini amebahatika kabisa mwanamke yule ambaye anamheshimu bwana wake wala hamghadhabishi na huwa mtiifu kwa bwana wake."


. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema Bihar al-Anwaar, J.103, Uk. 235 "Bora ya mwanamke ni yule anayezaa, mvutiaji kimapenzi, mtunza siri zenu, na mcha-Allah swt. Na humtii bwana wake na hupendwa na Jama'a na ndugu zake. Pale anapokuwa pamoja na bwana wake, anamwonyesha urembo na mavazi yake ambayo kwa hakika huyaficha kwa ajili ya wanaume wengine isipokuwa mume wake tu. Kwa hakika huwa msikivu na mnyenyekevu kwa mazungumzo yake na huzitii amri zake. Pale anapokuwa faragha anavaa vizuri kabisa na kutimiza mahitaji ya bwana wake kutoka kwake. Daima huwa anakuwa amevaa vizuri na kujirembesha kwa ajili ya bwana wake tu na kamwe huwa si mtu aliyejisahau kwa ajili ya bwana wake ( hujiweka tayari kwa ajili ya bwana wake.)."


. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., amesema Bihar al-Anwaar, J.104, Uk. 98: "Kutokea kwa furaha ya mwanamme Mwislamu ni kwamba ana mke mcha-Allah swt na nyumba kubwa ya kukidhi wananyumba, usafiri mzuri na watoto wema."


. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema "Vita vya Jihad kwa ajili ya mwanamke ni kuwa na uhusiano na kuwa mwema kwa mume wake na haki za mwanamme kwa mke wake ni zaidi ya haki za wote juu yake." . Allah swt amesema katika Qur'an Tukufu Surah Al-Baqara, 2, Ayah ya 231: Na mtakapo wapa wanawake talaka, nao wakafikia kumaliza eda yao, basi warejeeni kwa wema au waachilieni kwa wema. Wala msiwarejee kwa kuwadhuru mkafanya uadui. Na atakayefanya hivyo, amejidhulumu nafsi yake. Wala msizichukulie Aya za Allah swt kwa maskhara. Na kumbukeni neema ya Allah swt juu yenu, na aliyo kuteremshieni katika Kitabu na hikima anachokuonyeni kwacho. Na mcheni Allah swt , na jueni kwamba hakika Allah swt ni Mjuzi wa kila kitu.


. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., amesema Wasa'il ush-Shi'ah, J.22, uk.9: "Muoe na wala msitoe talaqa kwa sababu 'Arshi Ilahi hutetemeka kwa talaka." . Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., amesema Al-Kafi, J. 6, Uk. 54 "Allah swt hufurahishwa mno kwa nyumba ile ambamo harusi huwapo na hughadhabishwa kwa nyumba ile ambamo huwa na talaka. Na hakuna kinachomkerehesha Allah swt kama talaka."

SEMI ZA IMAM ALI IBN ABI TALIB a.s.
UADILIFU.
. Taji la mfalme ni uadilifu wake mwenyewe. . Utatawala iwapo nawe utakuwa mwadilifu. . Uadilifu huangamiza ulafi , uroho na tamaa. . Ngome ya Utukufu (ya Allah swt) huikinga nchi yenye mtawala mwadilifu.


SHURUTISHO NA SHARI
. Kulazimisha/Kushurutisha kunaifanya akili iwe kipofu. . Shari kunamfanya mtu awe mwoga wa uadilifu (ataiongopea) . Uchokozi ni hatua ya kukaribia maangamizi. . Kinachodhulumu haki ni kule kusaidia vilivyo batilifu. . Udhalimu kwa mwenye dhiki ni dhuluma kubwa kuliko zote zile. . Allah swt huharakisha kuanguka kwa wachokozi. . Ushidi wa mshari ni kushindwa kwa nafsi yake. . Kustarehe humu duniani kwa fidia ya akhera ni kujidhulumu nafsi yako. . Kuwakandamiza yatima na wajane kunaleta magonjwa na kupotea kwa ne'ema.


ULIMI NA USEMI:
. Mtu amehifadhika chini ya ulimi wake. . Ulimi mtamu/mzuri hupata marafiki wengi. . Ulimi wako utasema kile kilichozoeshwa. (Kwa hivyo jihadhari kabla ya kusema). . Akili ni busara. Akili ya mpumbavu ipo chini ya ulimi wake(anasema kabla ya kufikiri). . Ulimi ni mkalimani wa akili. . Ulimi wa mtu ni uzani wake mwenyewe. . Ulimi unaathari za kuchoma zaidi ya mkuki. . Usemi wa kweli ni ulimi mtukufu. . Jihadhari na ulimi, kwani ni sawa na mshale unaoweza kufyatuka kutoka upinde. . Mtu bila kusema (ulimi useme mema na kukataza mabaya) ni ama sanamu au mnyama. . Ulimi wa mwenye busara ipo akilini mwake (huongea na akili yake na hufikiria zaidi na kusema kwa uchache kwani ni yenye manufaa). . Kuujaribu (kucheki) ulimi ni afadhali kuliko kulitazama tumbo. . Yeyote yule asiye uhifadhi ulimi wake basi ataujutia mbeleni.


UKIMYA NA KUSEMA.
. Kila vile busara ya mtu iongezekavyo ndivyo vivyo hivyo maneno yake hupunguavyo. . Ukimya ni majibu ya maswali mengi sana. . Ukimya ni jibu bora kabisa kwa mpumbavu. . Mazungumzo bora ni yale yaliyo mafupi na yenye manufaa. . Bora ya misemo ni ile iliyochujwa na kuhakikishwa. . Ukae kimya ili ukae salama. . Kusema kupita kiasi kunamdharaulisha mtu. . Urefu wa mazungumzo huidhoofisha hotuba. . Hotuba ni kama dawa; kiasi kidogo kinaponya na kwa kuzidi kiasi kunaweza kumwua mgonjwa. . Usimpuuzie yule asemaye bali wewe uyatilie maanani yale ayasemayo. . Kusema kidogo ndivyo kukosolwa kidogo.


KIFO (MAUTI).
. Watu wako wamelala hali wako hai na huwa macho baada tu ya kufa. . kujielekeza kwa mabaki ya matamanio ya mtu ndiko kujiuwa haraka. . Ufe kabla ya kifo kukuijia. . Mauti inaidhihaki tamaa. . Mauti ni kutenganisha toka kitakachoisha na kuelekea kule pasipokwisha. . Kuikumbuka mauti kila mara kutampunguzia mtu tamaa za duniani. . Wale watembeao juu ya ardhi siku moja watazikwamo. . Tamaa hukuongoza katika njia ya upotofu. . Wakati hatuna matumaini huwa hatuhuzuniki.

. Kufadhaika huwa pamoja na tamaa. . Kinachoipatia madhara na hasara dini ni tamaa. . Waroho ni watumwa wa matilaba yao. . Kutokuwa na mategemeo kunaituliza na kuipumzisha roho. . Uroho huuangamiza uadilifu . Ubinadamu ni wa aina mbili; wale wenye matamanio matupu na wale watakao kuja kuwa wasioridhika. . Tamaa huingamiza hadhi ya mtu bila ya kuongezeka kwa bahati yake. . Hata kama wakiwa uchi na wenye njaa, hao walioridhika huwa ni wenye furaha. . Kuridhika ni hazina isiyo na kifani. . Kuridhika ni hadhi na heshima isiyodidimia milele. . Mwenye kuridhika tu ndiye aishiee kwa amani na usalama.


USTAHIMILIVU, UVUMILIVU NA UTULIVU.
. Kutokuwa na saburi ya akili ni yenye madhara kuliko ustahimilivu. . Chifu ya sababu ya Islam ni utulivu kwa Allah swt . Ustahimilivu ni matunda ya Imani. . Ujue kuwa utulivu ni hatua ya awali katika dini halisi na uaminifu ni mwili . Kwa ustahimilivu, bahati mbaya huwa sivyo tena bahati mbaya. . Ule uwezo wa uvumilivu wa ghadhabu (hasira) ni bora kuliko kuchukua kisasi.


MALI (UTAJIRI).
. Mapenzi ya mali inachochea tamaa na kuharibu wema. . Usia unawafariji warithi . Mali ni chanzo cha hamaki. . Bora ya akiba ni pale ambapo kazi zinatawanywa vyema. . Fedha haimnufaishi mwenye kuwa nayo hadi hapo anapotengana nayo.

AKILI NA UPUMBAVU.
. Uadui ni kazi ya wapumbavu. . Dhana ya mwenye akili ni mafumbo. . Kwa kumtii Allah swt ni sawa kwa hisa ya akili na hekima ya mtu. . Kupigana vita dhidi ya matakwa yake mtu ni jihad kubwa kabisa. . Sababu ya busara na akili ni kukubalia ujinga wake mwenyewe. . Mwerevu hulenga pale na thabiti. . Mpumbavu hulenga pale penye mali. . Dhana ya mtu inategemea akili yake ilivyo.


. Dhana ya mwenye busara na hekima ni sahihi kabisa kuliko kithibitisho cha mpumbavu . Kwa kujitenganisha na vitu vya muda na kujiweka tayari kwa maisha ya kudumu ndiko kunako busara na hekima hisa kubwa. . Mtu huyo ni mwenye busara ambaye matendo yake yanathibitisha yaliyoyasema. . Mtu mwenye busara hasemi ila pale penye dharura au penye sababu. . Kila mtu aliye mwenye busara na hekima huwa yuko masikitikoni. . Mwenye busara ni mwenye faida hata kama akiwa katika hali gani ile. . Kujihusisha na wapumbavu ni kuitesa Roho. . Mpumbavu yupo peke yake hata kama akiwa katika jamii. . Kutoka kupata hekima (matakwa yake) hayawezi kufidiwa na fedha. . Hakuna ugojwa ulio mbaya kabisa kuliko kutokwa kwa hekima.


UWEMA NA MATENDO MEMA.
. Kwa uwema mtu anaweza kumteka mtu aliye huru. . Wema haufi kamwe. . Kazi iliyo bora zote ni kujijumuisha pamoja na walio wema. . Kuwa mwema kwa mema ni uwema na hii ndiyo fahamu ya mtu ya hali ya juu. . Thamani ya mtu inategemea uzani wa uadilifu wake. . Angukia ndani kwa wema na uangukie nje kwa matakwa.


TAMAA
. Mapenzi ya mali (utajiri) yanachochea tamaa na kuupoteza uwema. . Tamaa haielewi mipaka yake. . Kuwa na imani ya Allah swt ni jitihada iliyo bora kabisa. . Tamaa iliyo kuuu kabisa ya wanyama ni kule kushibisha tumbo lao wenyewe. . Tamaa iliyo kuu ya wanyama porini kule kuwanyanyasa wengineo. . Tamaa kuu ya mwanamke ni kuivutia dunia kwake na kuchochea fujo humo. . Jitihada kuu kabisa ya Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s.humu duniani ni kuiongoza dunia. . Tamaa yako iwe ni ile kwa ajili ya akhera na hapo utajirekebisha. . Thamani ya mtu inategemea utukufu wa jitihada zake. . Ukuu na ufahari wa mtu unategemea utukufu wa jitihada zake na wala sio pale penye kuozapo mifupa ya mababu zetu.


REHEHMA NA MSAMAHA:
. Kusamehe ni taji la ukubwa na fahari. . Rehema inaitukuza nguvu. . Itakuwa ni vyema iwapo rehema itashirikishwa pamoja na ukubwa. . Itakuwa ni adhabu kubwa itakayotolewa mbali na kuombwa msamaha. . Unyenyekevu inatangaza ukubwa. . Unyenyekevu ni matunda ya elimu na hekima. . Unyenyekevu bila ya kutazama panapostahili ni sawa na huna uwezo. . Majivuno huangamiza na kumharibia sifa mtu. . Kwa kuwa na majivuno au kiburi ni sawa na kuipa akili sumu. . Kiburi hukandamiza mwenendo wa maendeleo. . Majivuno huua na kuudhalilisha ukubwa. . Unyenyekevu ni sawa na wavu uliotandwa kwa ukubwa. . Kujivuna na kule kujideka ni matokeo ya wale wenye akili kasoro.


ULIMWENGU:
. Ulimwengu huu ni sawa na daraja ituvushayo kwenda akhera. . Dunia hii ni sawa na duka la maovu. . Mapenzi ya dunia ni chanzo (mizizi) cha matatizo na maovu yote. . Ufahari wa wapumbavu na walio wajinga ni mapenzi ya dunia. . Dunia ni chungu mno zaidi kuliko ule utamu wake ulio nao. . Kuipatia dunia hii talaka ni sawa na kupanga harusi na Akhera. . Dunia hii ni sumu na wale wailao sumu ni majahili. . Uishi kwa kiwiliwili chako humu duniani na uifanyishe kazi nafsi(imani) yako kwa ajili ya akhera.


WATU
. Watu ni zaidi ya vile walivyokuwa awali na huishi zaidi ya walivyokuwa wakiishi mababu zao. . Mtu aliye jasiri kuliko wengine ,atulizaye matamanio yake (subira). . Itakuwa ni jambo la upuuzi iwapo nafsi itakuwa imedhoofika hali mwili wa mtu bado ana siha nzuri na iliyo njema. . Yule aijuaye na kuelewa ubinadamu huchagua upweke. . Yule ampandae Allah swt hupigana na aibu za watu. . Yeyote yule asiyejifikiria na kujithamini mwenyewe basi amepotoka.


MATAKWA YA SUBIRA
. Hekima iliyo kuu kabisa ni kule kupingana na matakwa na matamanio ya mtu. . Atakuwa ni mtu mwenye furaha kuu iwapo ataishinda nafsi yake mwenyewe. . Adui wa kupindukia wa mtu ni yale matakwa yake. . Vita vilivyo bora kuliko vyote ni vile vita dhidi ya nafsi ya mtu. . Ulafi wa sehemu zetu za siri ndizo nyavu zilizo tegwa na Shaytani.