HADITH

 

HADITH

Makala haya yametarjumiwa na :
AMIRALY M. H. DATOO
BUKOBA - TANZANIA
YALIYOMO

HADITH NI NINI ?................................................................................ 3

SHIAH NA HADITH ............................................................................. 4

MTUNZI NA HABARI ZAKE. ............................................................ 10

UTAMBULISHO WA MA'SUMIIN A.S. KATIKA AHADITH:....... 13
KUNIYYAT ...................................................................................... 13
1. ABUL QASIM.......................................................................... 13
2. ABU MUHAMMAD ................................................................ 14
3. ABU 'ABDILLAH ................................................................... 14
4. ABUL HASAN......................................................................... 14
5. ABU MUHAMMAD ................................................................ 14
6. ABU IBRAHIM........................................................................ 14
7. ABU IS-HAQ ........................................................................... 15
8. ABU JA'AFER......................................................................... 15
ALQAAB........................................................................................... 15

MWENYE KURIPOTI AHADITH AWEJE?....................................... 16

AINA ZA AHADITH ............................................................................ 17
1. HADITH SAHIH ........................................................................... 18
2. HADITH HASAN ......................................................................... 18
3. MUTAWATH-THAQ ................................................................... 18

HADITH ZILIZOTOLEWA ................................................................. 18

SIFA ZA KUZITAMBUA HADITH .................................................... 25
HADITH NI NINI ?

Mawaidha na Nasiha maneno aliyoyazungumza Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ni Hadith kwa kifupi, maneno yoyote yaliyotoka mdomoni kwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. mbali na ayah za Qur'an Tukufu, ama yale aliyoyatenda kuonyesha, hayo yote ni Hadith. Vile vile maneno na matendo yote ya Ma'asumin a.s. pia ni Hadith yaani yataingizwa katika Hadith. Kutokana na Hadith sisi tunaweza tukajua na kufuatilia na kutekeleza mambo ambayo ni usuli - Furu', Sunnah na faradhi. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. kwa maisha yake yote alikuwa pamoja na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Hivyo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. popote pale alipokuwa akiwapa watu nasiha na mawaidha katika mambo mbalimbali na kuwaongoza katika masuala mbalimbali basi Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. daima alikuwa akinufaika na hayo yaliyokuwa yakisemwa na kutendwa na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na ndivyo alivyosema "Sisi ndio dalili za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na vile vile ndio Sahaba wake halisi, na sisi ndio ufunguo wa hazina yake ya ilimu na mlango wa mji wake wa ilimu1 alioutangaza Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na mtu yeyote hawezi kuingia katika nyumba au mji isipokuwa kwa kupitia mlango wake." Kwa kiapo cha Allah swt ! Mimi nina ilimu na ma'arifa ya Utume na maneno ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Sisi Ahlul Bayt a.s. ni milango ya hekima na kwa hakika sisi ndio tunayo nuru ya hukumu za Allah swt. (Nahjul Balagha). Katika historia tunapata habari kuwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ndio aliyekuwa mtu ambaye amekusanya na kuwa na hazina kubwa ya Hadith za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Tumepata kuona kuwa 1 Ipo Hadith ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa "Mimi ni mji wa elimu na Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ni mlango wake" na vile vile amesema "Mimi ni hazina ya elimu na Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ni ufunguo wake." Na zipo Hadith nyingi kama hizo. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. yeye daima alikuwa akiziandika Hadith za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na kuzielewa na kuzikariri vyema kabisa. Na kwa amri ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ndipo Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. alitayarisha kitabu kimoja ambamo kumeandikwa Hadith za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na Sunnah zake, na kitabu hicho kinaitwa Sahifat Jami'a na kitabu kingine kinaitwa Kitabul Faraidh, ambamo katika vitabu hivyo vyote viwili kumeandikwa Ahkam za Sharia. Vitabu hivyo vimenakiliwa katika vitabu vingine mfano Sahih Buhari amenakili kwenye kitabu chake ambao ni upande wa Masunni. Na upande wa Mashi'ah Ma'ulamaa wa Kishi'ah Sheikh Sadduq a.r. amenakili katika kitabu kinachoitwa Manla yahdharulfaqih na Sheikh Tusi a.r. kinachoitwa Tahdhib na Thiqqatul Islam Quleyni r.a amenakili katika Al Kafi.

SHIAH NA HADITH 2
Kwa hakika Mashiah wana mchango mkubwa sana katika uandishi wa Hadith na katika hali ambayo ni sahihi. Na wa kwanza kabisa ni mchango Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ambao hauna kifani wala usioelezeka, je litakuwa ni kosa gani iwapo wafuasi wake watamfuata yeye katika kuzidumisha na kuzihifadhi sirat na sunnah za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.? Katika historia vile vile tunapata mambo yaliyowazi kabisa kuwa kulikuwa na baadhi ya Ma-sahaba wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ambao walikuwa wakikataa kabisa kusiandikwe Hadith kwa sababu ya visingizio kuwa vilikuwa vikigongana na ayah za Qur'an Tukufu. Na wapo Ma-Sahaba wengine pia wameadhibiwa vifungo na adhabu mbalimbali kwa ajili ya kunakili na kusambaza Hadith za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Kwa hakika Ibn Hajar anaandika katika Futuh al-Bari utangulizi wake jambo moja la kustaajabisha, kuwa yeye anasema, "Mwanzoni mwa Waislam kulikuwa na utata katika uandishi wa Hadith, kwa sababu baadhi yao walikuwa wanasema kuwa ni karaha kuziandika. Na katika wale waliokuwa wakisema kuwa ni makuruh alikuwepo 2 Msomaji unaombwa kukisoma kitabu kwa ukamilifu nilichokitarjumu katika Kiswahili kinachoitwa Tadhwin al-Hadith historia ya ukusanyaji na uandishi wa hadith. 'Umar bin Al Khattab, Ibn Masoud na Abu Sai'd Al Khudhri. Na katika upande wa pili ambao walikuwa wakieneza Hadith kwa usahihi walikuwa ni Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., mtoto wake Al Imam Hassan ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. na vile vile Anas alikuwapo. Na kwa hakika Mashi'ah wamekuwa mbele katika kueneza Hadith zilizokuwa sahihi na miongoni mwao nawaletea majina yao: 1. Mtumwa wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliyekuwa akiitwa Abu Rafi', na ambaye alikuwa miongoni mwa wale Waislam wa mwanzoni kabisa. Bwana 'Abbas mjomba wake Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ndiye aliyekuwa amempa zawadi huyo, na wakati huyo mtumwa alipompa habari Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa mjomba wake huyo Bwana 'Abbas ameukubalia Uislam, basi Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kwa kusikia hiyo habari njema alimfanya huru huyo mtumwa kwa sababu ya kuleta habari hizo njema. Katika fadhila zake tunaona kuwa yeye alifanya Hijra mara mbili, na amesali katika Qibla zote mbili na amefanya Bay'a ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. mara mbili. Na vile vile ameshiriki katika vita vya Jihad vingi sana pamoja na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., na baada ya kifo cha Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. yeye hakumwacha Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. na daima alikuwa naye pamoja. Alikwenda na Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. hadi Kufa, Nchini Iraq na alishiriki naye katika vita vitukufu vyote vilivyotokea na alikuwa ni mtu mmoja aliyekuwa akiaminiwa sana na Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. kiasi kwamba yeye alikuwa akitunza Baitul Maal pia. Yeye alifariki akiwa na umri wa miaka themanini na tano. Na yeye ni miongoni mwa Rawi wa Kishi'ah 3 wanaoaminiwa na kusadikiwa, naye ameandika kitabu kimoja ambamo ameandika riwaya za Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. kinachoitwa Kitabu Sunan Wal-ahkam Wal- 3 Nimetarjumu orodha ya Rawi 100 wa Kishi'ah wanaojuikana na walio ma'arufu katika vitabu vya Ahl as-Sunnah. Kwani wengi wa Masunni wanadai kuwa Mashi'ah ni Rafidhi (walio asi ) na wengine majaheli kuthubutu kusema kuwa Mashi'ah ni Makafiri. Hivyo itakuwa vyema iwapo utapata makala hayo ukayasoma. Qadhaya. Katika vitabu vya 'ilmul Rijal kitabu hiki ni muhimu sana na chenye faida kubwa sana. 2. Bwana Salman Muhammad (Al Farsi) ambaye baada ya kifo cha Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliandika habari za Jasliq kwa niaba ya Mfalme wa Roma 3. Asbagh bin Nabata, aliandika usia wa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. alioumfanyia Bwana Malik Ashtar, vile vile aliandika Nasiha alizomfanyia mtoto wake Muhammad. Asbagh bin Nabata alikuwa ni mmoja wa Ma-Sahaba wa karibu sana wa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. 4. Suleim bin Kais Al Hilali yeye ameandika kitabu chenye Ahadith ambacho kinatumika mpaka sasa hivi na kwa mara ya mwisho kilikuwa kimechapwa huko Najaf Al Ashraf, nchini Iraq. Hadith zake zimetokana na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. mwenyewe na vile vile Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ; Miqdad, Salman, Abudhar na wapenzi wa Ahlul Bayt a.s. 5. Mitham al-Tammaar yeye alikuwa mmoja wa Ma-Sahaba mashuhuri na mshupavu wa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. yeye naye ameandika kitabu ambacho Sheikh Sadduq amekitumia katika 'Aamali na vile vile Tabari ametumia katika Basharatul Mustafa. 6. Zaid bin Wahab Aljahni ambaye ametunga kitabu kimoja ambamo ameandika hotuba zote za Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. alizokuwa akizitoa siku za Ijumaa na Idi, kwa hakika ameufanyia 'umma huu ihsani kubwa sana. Ibn Hajar na Ma'ulamaa wengine wanasema kuwa huyu bwana Zaid bin Wahab Thiqqah na wanampa Ukuu. Yeye amefariki katika mwaka takribani 96 Hijriyyah. 7. Mkusanyiko mkubwa kabisa wa semi na Dua za Ma'sumin a.s. yanayojulikana kama Sahifa al-Kamila na vile vile inajulikana kama Zaburi Al Muhammad. Kitabu hicho kimekuwa tangia uhai wa Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. na humo kumeandikwa semi zao n.k. ambayo yalikuwa yamesimamiwa kikamilifu na Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ndiye aliyefanya mpango huo. 8. Jabir bin Yazid bin Al Harith Al Jaufi, yeye ameziandika yaani yeye katika nuru ya ahadith za Masumin a.s. ameandika Tafsiri, vita vya Jamal, Siffin, na Naherwaan, na vile vile ameandika kuuawa kwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. na Al Imam Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. Yeye amefariki katika mwaka 128 Hijriyyah. 9. Bwana Abu Hamza Thumali (aliyefariki mwaka 150 Hijriyyah) alikuwa mmoja Sahabi mashuhuri mwaminifu kabisa wa Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. na Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. na ameweza kutunga kitabu kiitwacho Annawadir Wa-Dhuhud. Vile vile amefanya tafsiri ya Qur'an Tukufu pia. 10. Vile vile miongoni ma Ma-Sahaba wa Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. na Al Imam Muhammad al- Baquir a.s. alikuwa akiitwa Muhammad bin Keis Al Bijalli ambaye ameandika kitabu kiitwacho Qadhaya Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. 11. Aban bin Taghlib (aliyefariki mwaka 141 Hijriyyah) ni kwamba wote wanaafikiana kuwa yeye ameishi katika zama za Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s., Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. na Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., na Hadith zao alizozileta huyu Aban bin Taghlib zinasemwa kuwa ni Asili. Yaani inamaanisha kuwa Hadith zake hizo yeye alizoziandika zimetoka moja kwa moja kutoka kwa Maimamu a.s. na si kwa kupitia watu wengine walizozisikia inamaanisha kuwa ni yeye mwenye amezisikia hizo. 12. Takriban waliosomea ilimu ya Hadith ilifikia elfu nne au na zaidi kuanzia katika zama za Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. na Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. Siku moja Hassan bin Ali Alwashakhi yeye alikutana na wale watu waliokuwa wakizoea kuzisema Hadith si chini ya mia tisa katika Masji Al-Kufa, na wengi wa wale waliokuwa wakizisema hizo Hadith walikuwa wakisema tumeambiwa Hadith hii na Ja'afar bin Muhammad yaani zilikuwa ni Hadith asili ambazo huyo mtu amezisikia moja kwa moja kutoka kwa Maimamu a.s. 13. Ibn Nadhir katika kitabu chake Fahrist amemwandikia yule Yunusu bin 'Abdul Rahman na habari zake kuwa ni mtu mmoja mwaminifu na mwenye kutegemewa kabisa ambaye miongoni mwa Ma-Sahaba wa Al Imam Musa al-Kadhim a.s. na Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s. Kwa hakika kitabu hiki ni chenye manufaa sana kiitwacho Jawamiul Aasar. 14. Ibn Nadiim katika kitabu chake Fahrist amewaandika watoto wawili wa Sa'id bin Himad ambao ni Hussein na Hassan na vile vile ameandika habari zao pia, kuwa hawa watu walikuwa ni hodari kabisa katika 'ilimu ya Hadith,Fiq-h na Manaqib. Hao wote walikuwa wana kitabu walichokitunga juu ya Hadith na walikuwa ni miongoni mwa Ma-Sahaba wa Al Imam Muhammad Taqi Al Jawad a.s. na Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s. 15. Fadhl Bin Shaazan Nishapouri (aliyefariki 260 Hijriyyah) yeye amewahi kuwa Sahaba wa Maimam watatu a.s. ambao ni, Al Imam Muhammad at-Taqi a.s., Al Imam 'Ali an-Naqi a.s. na Al Imam Hassan al-'Askari a.s. Naye ameandika vitabu vitatu: o Cha kwanza Kitabul Faraidh Al Akbar, o cha pili Kitabu Faraidh Al Awsat, o cha tatu Kitabu Faraidh Al-Asghar ambacho ni mashuhuri. 16. Na baada ya hapo hii kazi ya ukusanyaji na uandishi wa Hadith ulikuwa umeendelezwa na Ma-Sahaba na wazee na wameweza kuleta kazi nne zilizo kubwa kabisa. Kazi hizo nne ambazo mpaka leo zinajulikana kwa jina la mashuhuri Kutub Al-'Arbi'a yaani inajulikana kwa jina la vitabu vinne. Kitabu Cha kwanza kabisa ni Al Kafi, ambacho kimetayarishwa na kuandikwa na Thiqqatul Islam Al Quleyni a.r. (amefariki mwaka 329 Hijriyyah) katika kitabu hiki zipo Hadith takribani elfu kumi na sita. Vile vile kuna kitabu kingine kinachoitwa Man la haydharul faqih ambacho kimeandikwa na Bwana Abu Ja'afer As-Sadduq humo takribani Hadith elfu sita zinapatikana. Vile vile kulikuwa na kitabu chake kingine kijulikanacho kwa jina Madinatul 'Ilm ambacho Shahid a.r. amekizungumzia. Na kwa kutokana na fitina za zama hizi kitabu hiki hakipo yaani hakipatikani Na Sheikh Sadduq a.r. katika mwaka 381 Hijriyyah. Vile vile tunapata vitabu viwili mashuhuri na vyenye faida sana ambavyo vinavyoitwa Tahdhibul Ahkam na kingine Al-Istibsaar vyote vikiwa vya Sheikh Taifah Bwana Ja'afer Muhammad bin Hassan Tusi (aliyefariki mwaka 460 Hijriyyah). Kwa kuunganisha vitabu vyote viwili zipo Ahadith elfu kumi na nane zilizo andikwa. Kwa hakika katika zama zote hizi ilimu hii ya Hadith na katika nuru ya Ayah za Qur'an Tukufu na Sunnah ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. 'ummah umeweza kuwatambua na kuwafuata Ahlul Bayt a.s. na kuweza kujipatia ma'arifa yao na Ma-Sahaba. Katika kila zama kazi zilikuwa zikifanyika kwa kiwango fulani katika kuendeleza jitihada hizi za Hadith lakini katika mwaka wa 11 Hijriyyah kulifanywa kazi moja kwa kiasi kikubwa sana cha kutungwa kwa kitabu kiitwacho Bihal Al Anwar ambacho kilitungwa na Muhaqqiq 'Allama Majlisi a.r. (aliyefariki 1111 Hijriyyah), kitabu hicho ambacho kilikusanya Hadith kwa wingi. Kwa hakika kitabu hiki kimoja yaani Bihal Al Anwar sisi hatujakipa heshima kiasi inavyotakiwa na wala sisi hatujafaidika nacho kiasi tunachotakiwa kufaidika nacho. Bihal Al Anwar ni kitabu ambacho Hadith ambazo hazikuandikwa katika Kutub Al-'Arbi'a basi hizo Hadith zinapatikana katika kitabu hiki cha Bihar Al Anwar. Kwa hakika kitabu hiki kina Juzuu ishirini na sita lakini katika Jamhuri ya Kiislam ya Iran na Beirut wamejaribu kukipanga katika vitabu vidogo zaidi ambavyo vimefikia Juzuu mia moja na kumi, ambavyo hata mimi ninavyo. Katika zama hizi vitabu hivyo na vingine vingi vinapatikana kwa urahisi katika CD za compyuta ambavyo mtu hana haja ya kujitwisha vitabu hivyo na inakuwa rhisi kutafuta masuala atakayo. Kwa hakika Maulamaa wamefaidika sana na Hadith zilizo andikwa katika Bihar Al Anwar na vile vile inadhihirisha vile wanavyoonyesha kuisifu na kuiheshimu kazi hiyo na hapa nimejaribu kuwaletea baadhi ya majina yao ambao wamekuwa katika zama zake hizo na mmoja miongoni mwao kama Marhum 'Allamah Majilisi alipewa ruhusa ya kunakili yaani 'ijaza ya riwaya. 1. Muhammad bin Hassan Hurri 'Aamili aliyefariki mwaka 1104 na mwandishi wa kitabu kinachoitwa Wasa'il as-Shi'ah, nacho kimechapwa si chini ya Juzuu ishirini. 2. Mullah Muhsin Faiz Khashani aliyefariki 1091 na ambaye ni mwandishi wa Al-wafi Kitabu hiki kina Juzuu kumi na nne kinazungumzia juu ya Usul, Furu', Sunan, na Ahkam. 3. Mulam 'Abdullah bin Nurullah Bahrani mwandishi wa kitibu kiitwacho Al Awalim kitabu hiki kiko katika Juzuu mia moja. 4. Sheikh Muhammad Ridha bin Abdul Latif Tabrizi, aliyefariki mwaka 1158 na ni mwandishi wa kitabu kiitwacho As-Shifa'.

MTUNZI NA HABARI ZAKE.
Kitabu hiki cha sadaqah ambacho kipo kwa mikononi mwenu, Hadith zake zimetolewa kutoka Wasa'il as-Shi'ah na tunaona vyema kuwaleteeni habari chache kuhusu kitabu na mtunzi wake. Sheikh Hurri Aamili baada ya jitihada zake nyingine kwa muda wa miaka ishirini mfululizo amekigawa kitabu hicho katika sehemu sita katika fani mbalimbali na kuzigawia Hadith kimpangilio mzuri kabisa kwa na hakika anastahili pongezi kubwa sana kwa jitihada zake zote katika kuzipanga Hadith kimpangilio mnavyouona katika kitabu hiki pia. Mwandishi wa Al-Mizaan fi Tafsir al-Qur'an yaani As-Sayyid Muhammad Hussein Tabatabai kuhusu Wasa'il as-Shi'ah anaandika : Kwa hakika kitendo hicho ni kipeo cha hali ya juu kabisa katika maswala ya Fiq-h na Mafuqahaa na Mujtahidiin wanakitegemea sana. Wao katika kutoa waftwah zao wanakitumia na kukitegemea sana na kitabu hiki ambacho kinawafaidisha na hawana shaka na hawana shaka yoyote kwenye kitabu hiki. Mambo yote ambayo yameisha zungumzwa humu kwa hakika yana mapana yake, kwa hakika kutokana na zama zao hizo mpangilio na utaratibu uliotumika kunasaidia na wenye manufaa sana. Kwa hakika inatubidi sisi tujali na kutekeleza na kuipa muhimu sana matamshi na maneno matakatifu yaliyozungumzwa na watu watukufu kabisa. Sheikh Hurri Aamili alikuwa ni mwandishi yaani ni mtu mwenye habari, na ni mmoja wa waandishi wa vitabu vinne vya kutegemewa kabisa ambavyo vimeisha kwisha kuelezwa hapo nyuma. Kwa hakika katika zama zetu hizi kuna pengo kubwa sana la ma'ulamaa kama hao ambalo haliwezi kuzibwa kwa hakika athari ya mapengo hayo yanaonekana katika zama zetu na zile zitakazo kuja kwa sababu mapango yamebakia wazi yanaongezeka na maulamaa wengi wametumia kazi ya Bwana Hurri 'Aamili kama vile Said Abul Qasim Al-Khui ametumia katika Mu'jamur Rijaal na kumtaja kuwa Bwana Sheikh 'Aamili alikuwa ni mtu wa maswala ya habari pia. Hivyo hivyo hali kadhalika Sheikh 'Aamili alizaliwa katika Jabal 'Aamil kijiji kimoja kijulikanacho kama Mashgharah (Mwezi wa Rajab mwaka 1033 Hijriyyah) na amefariki na amezikwa Mashhad al-Muqaddas katika mwaka 1104 Hijriyyah. Katika sehemu mwisho ya Wasa'il as-Shi'ah 'Aamili anaandika kuhusu Alama Majlisi a.r. anaandika kuwa: Yeye ni mwisho katika wale waliokuwa wamenipa idhini, nami nilimpa idhini. Mbali na kitabu cha Wasa'il as-Shi'ah, Sheikh 'Aamili ameandika vitabu vingine ishirini na sita ambavyo vingi vyake vina Juzuu mbalimbali. Kwa hakika mwanga wake huo mkubwa alioutoa kwa ajili ya madhehebu ya Ahlul Bayt a.s. ni mkubwa sana na wenye kustahili kusifiwa na kupewa heshima zote. Tunaomba Allah swt awajaalie kila la heri Ma'ulamaa wakubwa waliojitolea mhanga kuinusuru dini hii tukufu ya Islam. Kwa hakika kitabu hiki cha sadaka ni sehemu moja tu ndogo au tunaweza kusema ni sura mojawapo katika Juzuu ishirini za Wasa'il as- Shi'ah katika sura inayoitwa Kitabu cha Zakah. Mkiangalia kazi yake yote hiyo kwa hakika hamtakuwa na la kusema. Na surah hii inaitwa Kitabu cha Sadaka ambacho kinazunguzia mambo juu ya sadaka na humo zipo surah hamsini na nne sasa mfikirie kama yeye kwa swala moja dogo hili amechukua kwa hakika uzito mkubwa kama huo je mfikirie kazi yote hiyo itakuwa imechukua uzito gani? Kwa hiyo ndugu msomaji sababu ya kupenda kuchukua maudhui haya ni mambo mawili, Kwanza kabisa ni kuweza kuwadhihirishia na kuwaonyesha mchango wa Ma'ulamaa wa Kishi'ah katika ilimu hii ya Hadith na vile vile kuteketeza uvumi kuwa Mashi'ah wanaikubali Qur'an Tukufu lakini hawakubali na hawana Hadith zozote wao na kwa hakika hilo ndilo litakalo kuwa jibu letu. Kwa hakika ukiweza kuangalia utaona kuwa ilimu ya Hadith imehifadhiwa na kuendelezwa na hii Madrssah ya Ahlul Bayt a.s. ambapo kwa wengine jambo hili halikupewa uzito wala tahadhari ya aina yoyote ile. Leo ukiangalia katika ulimwengu wa Masunni utaona kuwa vitabu vyao vilivyopo wamshukuru 'Umar ibn 'Abdul Aziz na kama akiwa kiongozi mtawala asingetia msisitizo katika swala hili basi hawa watu ambao wamejitenga na Ahlul Bayt a.s. wangekuwa hawana chochote, hazina yao ingekuwa tupu kabisa. Vile vile mtarjumu wa kitabu hiki ambaye yeye ametokea 'Umma huu na amesomea, hivyo ameona afadhali kuwa kazi aifanye ili aweze kuleta mbele ya umma huu na kwa ajili ya manufaa ya wana-'umma huo kwa hivyo itasaidia pia kumtaarufisha mwandishi wa kitabu hiki. Sote kwa pamoja tunaomba kwa Allah swt nguvu zetu na jitihada zetu hizi azikubalie. Iwapo kumetokezea au kumebakia kasoro zozote katika kutarjumu basi tunamwomba Allah swt atusamehe na ninawaomba Wanazuoni na wenye Ilimu wajaribu kusaidia turekebishe kwa sababu katika kukitarjumu kitabu hiki hapakuwapo na matayarisho kamili kuanzia awali. Na kazi hii imefanywa kwa nia njema kwa matarajio kuwa itatumika kwa nia njema na itafaa kutukupeleka mahala pema. Inshallah. Naomba kazi yangu hii niiweke mbele kwa idhini ya Allah swt. Na kuiweka mbele ya Al Imam Muhammad Sahibuz-Zamaan a.s. iwe ni kama zawadi kwake.

UTAMBULISHO WA MA'SUMIIN A.S. KATIKA AHADITH:

KUNIYYAT
Mara nyingi tunaposoma vitabu vya riwaya tunapata majina mengine yaliyotofauti na majina ya asili. Hivyo tunaona katika Ahadith kuwa Ma'asumiin a.s. wanatambulishwa kwa majina yanayoitwa Kuniyyat au Iaqab, kwa mfano: Qala Abul Hasan ( yaani amesema Abul Hasan ) au Qala Abu 'Abdillah (yaani amesema Abu 'Abdillah) n.k. na hapo ndipo tunakuwa hatuelewi ni Ma'sum a.s. yupi ambaye amesema hayo. Waarabu wanayo desturi ya kuwaita wazee wao si kwa majina yao bali kwa majina mengineyo yaan Kuniyyat au Alqaab. Hivyo inatubidi tupate ufafanuzi zaidi kuhusu majina hayo yanayotumiwa kwa ajili ya Ma'sumiin a.s zaidi ya mara moja. Na hivyo Maulamaa wetu wametuelewesha ilivyo sahihi kabisa. Wakati wa kujaribu kufafanua juu ya Laqab au Kuniyyat kunatiliwa maanani kuhusu maneno na maana ya Hadith, zama za kusemwa na habari za wale wanaoziripoti, ndipo hapo panapoweza kutambuliwa kwa Alqaab au Kuniyyat katika Hadith hiyo kunatambulishwa Ma'sumiin a.s. yupi. Hivyo kuelezea hayo na mengineyo, maelezo yafuatayo yatasaidia kutoa mwanga katika swala hili kwa ujumla: 1.
ABUL QASIM
Kuniyyat hii inatumika kwa ajili ya Mtume Muhammad s.a.w.w. na Imam al-Mahdi a.s. Iwapo kutaripotiwa riwaya kuwa Abul Qasim tu, basi ijulikane kuwa ni Imam al-Mahdi a.f
2.
ABU MUHAMMAD
Zipo Hadith chache mno zinazojulikana kuwa Imam Hasan a.s. Hata hivyo hiyo ndiyo Kuniyyat yake.
3.
ABU 'ABDILLAH
Kuniyyat hii inatumika kwa ajili ya Imam Hussein a.s na vile vile inatumika kwa ajili ya Imam Ja'afer as-Sadiq a.s.
4.
ABUL HASAN
Kuniyyat hii inatumika kwa ajili ya Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. , Imam Musa ibn Ja'afer a.s., Imam Ali ibn Musa al-Ridha a.s. na Imam Ali an-Naqi a.s. Iwapo kutakuwapo na Abul Hasan tu katika riwaya, basi kutatambuliwa Imam Musa ibn Ja'afer a.s. Na iwapo kutaandikwa Abul Hasan Thani (Abul Hasn wa pili) basi kutakuwa kumefanywa ishara ka Imam Ali ar-Ridha a.s. na pale panapoandikwa Abul Hasan Thalith (Abul Hasan wa tatu) basi tujue kuwa kunamaanishwa Imam Ali an-Naqi a.s.
5.
ABU MUHAMMAD
Kuniyyat hii inatumika kwa ajili ya Imam Hasan a.s., Imam Zaynul Aabediin a.s na Imam Hasan al-'Askari a.s. lakini iwapo kutaandikwa riwaya kwa Abu Muhammad tu tutatambua kuwa riwaya hiyo ni kutoka Imam Hasan al-'Askari kwa sababu riwaya za Imam Zaynul Aabediin a.s. zinatajwa kwa jina lake tu, bali zipo riwaya chache mno tu kwa Kuniyyat yake.
6.
ABU IBRAHIM
Katika Hadith Kuniyyat hii inatumika hasa kwa ajili ya Imam Musa ibn Ja'afer a.s.
7.
ABU IS-HAQ
Kuniyyat hii inatumika kwa kumtambulisha Imam Ja'afer as-Sadiq a.s.
8.
ABU JA'AFER
Kuniyyat hii inatumika kwa ajili ya Imam Muhammad al-Baquir a.s. na Imam Muhammad Taqi a.s Lakini iwapo kutakuwapo na Abu Ja'afer tu au Abu Ja'afer Awwal, (Abu Ja'afer wa kwanza) basi ijulikane kunamaanishwa kwa Imam Muhhammad al-Baquir a.s. Na iwapo kutaandikwa Abu Ja'afer Thani (Abu Ja'afer wa pili) basi kutambuliwe kuwa ni Imam Jawad a.s. Kwa mara chache mno Abul Hasan inatumika kwa ajili ya Imam Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. lakini mahala pengi mno kunatumika Kuniyyat yake mahsusi ya Abul Hassanain.