ABU HURAIRAH

 
Hali Yake Kiakili Na Kimwili
1)- Baada ya Abu Hurairah kusilimu, alikuwa hana kitu chochote. Yeye alikuwa akiwaambia watu wasome Ayah ya Qur'an Tukufu, si kwamba alikuwa akitaka kufaidika nayo. Yeye alikuwa akitaka mtu huyo awe na hisia ya kidini na hivyo aweze kumwalika Abu Hurairah kwa ajili ya chakula cha mchana au usiku. Suala hili linajulika vyema kabisa kama "Kuchanganya Tumbo na Dini." ( Au kuchanganya Dini na pesa, tumbo, uwezo, au kwa vitu vya kawaida , au visivyo na maana).
2)- Hata watu hawaamini kuwa Abu Hurairah anaweza kuhadithia hadith kiasi hicho. ( Hakuna marejeo sasa : Imesemwa kuwa Abu Hurairah amehadithia Hadithi 40,000 katika uhai wake. Tukigawa Hadith hizo kwa kipindi cha miaka mitatu ya Usahaba wake, tunapata Hadith 36 kwa siku (!!! ). Marejeo niliyokwishayatoa hapo nyuma zinathibitisha kuwa, yeye mwenyewe Abu Hurairah, amekiri kuwa hakuna mtu yeyote miongoni mwa Masahaba ambaye amehadithia Hadith nyingi kama za kwake. Tukitambua ukweli huu kuwa yeye ndiye mtu wa pili katika kiwango cha kuhadithia wingi wa Ahadith katika Bukhari na Muslim, basi tunafikia uamuzi kuwa yeye Abu Hurairah atakuwa amehadithia Hadith nyingi mno zaidi ya hizo ambazo zimerekodiwa katika vitabu hivi viwili.Katika mojawapo ya Hadith, yeye Abu Hurairah mwenyewe, amekiri kuwa watu walikuwa wakimtuhumu yeye kwa ukichaa au mwenda wazimu.
3)- Jambo la kuvutia hapa ni kwamba hakuna hata Hadith moja iliyohadithiwa na mtu yeyote mwingine (mbali na yeye Abu Hurairah mwenyewe) kuzungumzia mema ya Abu Hurairah. Iwapo wewe utachunguza Bukhari na Muslim nzima kuhusu sifa ya Abu Hurairah, basi Hadith yoyote ile utakayoipata kuhusiana na Usahaba wake pamoja na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., na elimu yake basi itakuwa imehadithiwa na yeye mwenyewe (Abu Hurairah mwenyewe na wala si mtu mwingine)! Ambapo upande mwingine, wewe utakaposoma wema na sifa za Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ( na wengineo kama Salman, Umar, Zubair, .), basi utaona kuwa wapo wengine wanaomsifu Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. (na wengineo) kwa Hadith mbalimbali. Lakini haya vyovyote vile hayapatikani pamoja na Abu Hurairah. Hadith zote kama : Mimi nilikuwa mtoto mzuri, au nilifanya hivi na vile zimehadithiwa na Abu Hurairah mwenyewe tu (na wala si mtu mwingine).Mimi nakutaka unijibu iwapo utakubaliwa ushahidi wa mtu ajisemaye kuwa yeye ni mtoto mwema. Amehadithia Abu Hurairah: "Watu walikuwa na desturi ya kusema kuwa Abu Hurairah anahadithia Hadith nyingi mno." Kwa hakika mimi daima nilijiweka karibu mno na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na nilikuwa nikiridhika kwa kile kilichoshibisha tumbo langu. Mimi sikula mkate uliochachuka na wala sikuvaa mavazi yalirembeshwa kwa mistari, na kamwe hakuna mwanamme au mwanamke aliyekuwa amenihudumia mimi, na mara nyingi nilikuwa nikilibana tumbo langu kwa mawe kwa sababu za njaa, na mimi nilikuwa nikiwaambia watu wanisomee Ayah ya Qur'an Tukufu ingawaje nilikuwa nikiijua, ili kwamba anichukue nyumbani kwake na kunilisha chakula. Kwa hakika miongoni mwa watu waliokuwa wakarimu kwa masikini kuliko wote alikuwa ni Ja'far bin Abi Talib. Kwa hakika yeye alikuwa akituchukua nyumbani kwake na kutulisha chochote kile kilichokuwapo. Yeye vile vile alikuwa akitupatia mifuko (ya ngozi) tupu ya siagi ambayo alikuwa akiichana na tukilamba chochote kile kilichokuwamo ndani yake."Amehadithia Abu Hurairah:
"Mimi niliambatana na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kwa ajili ya kulijaza tumbo langu; na ndiyo kwa maana hiyo mimi sikula mkate uliochomwa wala kuvaa nguo za hariri. Na wala hakuna mtumwa kijakazi wala wa kiume aliyenihudumia mimi, nami nilikuwa nikijifunga mawe tumboni mwangu na nilikuwa nikimwomba mtu yeyote anisomee Ayah ya Qur'an Tukufu ingawaje nilikuwa nikiijua, ili kwamba inawezekana akanichukua nyumbani kwake na kunilisha chakula. Ja'far bin Abi Talib alikuwa mkarimu kwa masikini, yeye alikuwa akituchukua nyumbani kwake na kutulisha chochote kile alichokuwanacho nyumbani mwake, ( na kama kulikuwa hakuna chochote kile), yeye alikuwa akitupatia mifuko mitupu ya ngozi ( ya asali au siagi) ambapo sisi tulikuwa tukichana na kulamba chochote kilichokuwamo kimebakia."
Amehadithia Muhammad:
Sisi tulikuwa pamoja na Abu Hurairah pale alipokuwa akivaa nguo mbili za katani zilizokuwa zimetiwa rangi ya udongo mwekundu. Yeye alisafisha pua yake kwa nguo hiyo huku akisema, 'Hongera ! Vyema sana ! Abu Hurairah anasafisha pua yake kwa katani! Ulifika wakati ambapo mimi nilikuwa nikianguka bila fahamu baina ya Mimbar ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na nyumba ya 'Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa ambapo mtu aliyekuwa akipita hapo alinikanyaga shingoni kwa miguu yake, wakinichukulia mimi kuwa mwenda wazimu (kichaa), lakina kwa hakika, mimi sikuwa na ukichaa wowote, mimi sikuugua chochote kile isipokuwa njaa tu."


Amehadithia Abu Hurairah:
Wakati mmoja ambapo nilipokuwa katika hali ya ulegevu (kwa kutokana na njaa kali), nilionana na 'Umar bin al-Khattab, hivyo nilimwomba anisomee Ayah ya Qur'an Tukufu. Yeye aliingia nyumbani mwake na kunitafsiria. (Na mimi niliondoka zangu) baada ya kutembea umbali kidogo, nilidondoka chini juu ya uso wangu kwa sababu ya ulegevu wangu ambao ulitokana na njaa kali mno. Mara ghafla nikamkuta Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akiwa amesimama kichwani mwangu. Akaniambia, "Ewe Abu Hurairah!" Nami nikamjibu, "Labbaik ewe Mtume wa Allah swt na Siddiq!" kwa hayo akanishika mkono, na kuniinua. Ndipo alipokuja kujua kile kilichokuwa kikinisumbua. Hivyo akanichukua nyumbani kwake na akaniagizia bakuli kubwa la maziwa kwa ajili yangu. Mimi niliyanywa maziwa hayo, na ndipo hapo aliponiambia, "Kunya mengine, Ewe Abu Hurairah !!" Hivyo, mimi niliyanywa tena, kwa kumaliza, ambapo tena alisema, "Kunya zaidi." Hivyo mimi niliyanywa tena hadi pale tumbo langu lilipojaa na kuonekana kama bakuli.Baadaye mimi nilikutana na 'Umar na kumwelezea yote hayo yaliyotokea, na kumwambia, "Mtu fulani, ambaye anayestahiki zaidi yako wewe, alilichukua suala hili. Kwa kiapo cha Allah swt, mimi nilikwambia wewe unisomee Ayah ya Qur'an Tukufu wakati ambapo mimi ninazielewa vyema zaidi yako wewe." Kwa hayo 'Umar aliniambia, "Kwa kiapo cha Allah swt! Iwapo ningalikubali na kukushughulikia wewe, basi ingalinipendezea kwangu mimi kuliko kuwa na ngamia wazuri wekundu." Kujaaliwa kwa ghafla uwezo maalum zaidi Je hautaingiwa na shaka iwapo mtu akijaaliwa kwa ghafla uwezo maalum zaidi ya watu wengine, lakini sisi hatujawahi kusikia kuwa Abu Hurairah alikuwa na uwezo maalumu zaidi ya watu wengine. Ghafla anatokezea mbele ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na kuishi nae kwa muda wa miaka mitatu na tunaona kuwa anakumbuka kila kitu kwa nguvu fulani za kiajabu ?Jambo hili si la kumfanya mtu awe Msunni au Mshi'a kwa kuulizia je Abu Hurairah alikuwa akiropoka ? Mtu huyu alikuwa akiutumia muda wake mdogo huo pamoja na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kwa kujipatia faida zake binafsi na kuendelea kujipatia uhusiano kila pale palipojitokeza jambo ambalo lilihitaji ushauri na maoni, basi kwa nini yeye alijitokeza pamoja na Hadith ambayo yeye kwa haraka kabisa aliikumbuka kwa ukamilifu!! Hususan Abu Hurairah alikuwa akimchukia 'Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa na ni jambo la kuzingatiwa kuwa yeye alitunga hadith ambayo 'Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa aliipinga wazi wazi kabisa.Jambo la kustaajabisha ni kwamba ubongo wa Abu Hurairah uligeuka kuwa wa ajabu kabisa baada ya kifo cha Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Jambo lolote au suala lolote lililojitokeza wakati wowote ule, basi yeye alizungumzia mambo ambayo hakuna mtu mwingine aliyejua au kuyasikia hapo kabla. Wow! Kwa hakika tunaona wazi kuwa mtu huyu alikuwa akijitakia manufaa kwa ajili yake katika kujipatia nafasi na harakati zake za kisiasa na kijamii. Kuhadithia Hadith Nyingi Mno ? 'Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa amehadithia Hadith (1250) nyingi mno kuliko Abu Hurairah katika Sahih Bukhari. Ibn Umar amehadithia (1100) kiasi kama cha Abu Hurairah (1100) katika Bukhari. Idadi nimezitaja hapo awali katika jedwali. Mimi sikuulizia ni kwa nini 'Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa ameripoti hadith nyingi kiasi hicho kutokea kwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na wala sikuulizia kuhusu Ibn 'umar, au Ibn 'Abbas au wengineo.Lakini nilichokiuliza ni: Itawezekanaje kwa mtu aliyekuwa kasoro ya miaka mitatu aweze kuhadithia Hadith nyingi kiasi hicho? Tunayaachilia mengineyo. Abu Hurairah amehadithia hadith 5,374 tu. Iwapo tutachukua kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alikuwa miaka mitatu kamili pamoja na Abu Hurairah : 5,374/3 = 1791.33 Ahadith kwa mwaka, 1791.33/(365-11)= 5.06 Ahadith kwa siku.Wewe utaniuliza kwa vipi tena ? Je itawezekanaje kwa mtu kufanya hivyo kila siku ? Je kwa nini alikuwa amejitolea kiasi hicho ambapo kulikuwapo watu waliokuwa bora zaidi kuliko yeye, kama vile 'Umar, mtoto wake, Ibn 'Abbas na Abu Bakr hawakuweza kufanya hivyo ? ( Kwa uzani wa Abu Hurairah, hata Hadith 5 kwa siku ?) Bila ya kutaja kuwa Abu Hurairah amehadithia Hadith zaidi mno kuliko Sahaba yeyote, kutegemea kauli yake mwenyewe. Baadhi wanasema kuwa Abu Hurairah amehadithia kiasi cha Hadith 40,000. Hata watu walikuwapo karibu nae walishangazwa na mtu huyu kwa kuhadithia kwake huku ( kwa kutegemea kauli ya Abu Hurairah mwenyewe). Sehemu ya pili ni kwa nini mtu kama huyu amehadithia sawa na riwaya za Agano la Kale ? ( sehemu ambazo zimekanushwa na itikadi na imani za Kiislamu ?)

Abu Hurairah Kupata Fahamu Ya Ajabu?
Sasa ndipo wewe unaanza kuhisi nakisi ya elimu yako. Je unajua kuwa Sahaba na Ndugu wa Kijamaa wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Abdullah Ibn Abbas alipewa baraka za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na siku moja alimpiga kwa mkono kifua chake na alimwomba Allah swt akisema : "Allahumma faqqihhu fiddini wa 'allimhu min ta'uwili l kitabi" ( Ewe Allah swt ! Mjaalie elimu ya Dini na mfanye mfasiri wa Kitabu (yaani Qur'an Tukufu)? Na kwa muujiza, Ibn 'Abbas akawa Hibr l umma (Imam wa 'Ummah), hiyo ilikuwa ni muujiza mojawapo wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Vivyo hivyo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alivyomwombea Abu Hurairah wakati alipolalamikia udhaifu wa kukumbuka kwake: Kama vile ulivyojionea kuwa Ibn 'Abbas (R) anatambuliwa hata na Masahaba wengineo kuwa yeye alikuwa akiijua taawil (tafsiri) ya Qur'an Tukufu. Kwa hakika huku ni tofauti na kukariri ! Leo hii tunawaona watu wengi wakikariri Qur'an Tukufu nzima, lakini haimaanishi kuwa wao wanajua maana halisi iliyomo.Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ni mtu mwingine ambaye alisema kuwa hakuna Ayah yoyote katika Qur'an Tukufu ambayo yeye alikuwa haijui ilipoteremshwa na sababu ya kuteremshwa kwake na nini kilichokuwa kikimaanishwa. Kwa hakika Masahaba wengi walitambua haya kuhusu Shakhsiyyah hizi na zipo Ahadith zinazosadikiwa katika kuthibitisha elimu yao hiyo. Sasa, tukirejea kwa Abu Hurairah, sisi hatuoni mahala popote kuwa Abu Hurairah aliipata kipaji hiki cha maajabu yoyote baada ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kumwombea dua !!!Vile vile nitapenda kuongezea usahihisho kuwa Abu Hurairah baada ya kuishi kwake kwa kipindi kasoro ya miaka mitatu pamoja na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., hakuhadithia au alijiepusha na kuzisema Ahadith katika zama za makhalifa watatu Abu Hurairah alianza kuhadithia Hadith hususan katika kipindi cha Mu'awiyah ibn Abu Sufian yaani takriban miaka 30 baada ya kifo cha Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Hivyo yeye alijiwekea kifuani mwake Hadith hizo 3000 na zaidi kwa kipindi chote hicho bila ya kumwambia mtu yeyote.


Ushahidi nilionao ni kwamba Abu Bakr, Umar na 'Uthman hawakuruhusu usemaji na uandishi wa Hadith. Imeripotiwa kuwa Abu Hurairah aliulizwa iwapo alihadithia Hadith katika zama za 'Utman bin 'Affan ? Abu Hurairah alijibu kuwa yeye asingelithubutu kufanya hivyo, kwani wao wangalimpiga iwapo angelithubutu kuhadithia Hadith !!


Kwa hakika si kosa kuchunguza maisha na mienendo ya Sahaba yeyote, hususan Abu Hurairah. Kwani wote hao ni wanaadamu tu ambao wanaweza kukosea kwa madaraja mbalimbali, na wala hatusemi kuwa Allah swt hawezi kuwasamehe makosa yao, iwapo Allah swt mwenyewe ataamua kufanya hivyo. Hivyo ni wajibu wetu kutambua wazi kuhusu wale tunaowafuata iwapo kweli ni waaminifu ili tusije tukapotoka kwani Allah swt ametujaalia neema kubwa mno ambayo ni fahamu na akili. Hivyo iwapo tutawaona kuwa hawafai au wapo mashakani, basi tujiepushe nao ili tusije tukaiharibu Akhera yetu. M W I S H O