ABU HURAIRAH

 
Wapokezi wa Hadithi
Miongoni mwa Masahaba wote na wale waliokuwa wamemtembelea Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., ni wachache tu ambao walioziripoti Ahadith katika Sahih . Idadi yao ni ndogo kabisa hata kuliko idadi ya vidole. Wakati ambapo riwaya nyingine inasemwa kuwa kiasi cha watu 1400 walikwenda pamoja na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. huko Hudaibiyyah. Mji mtukufu wa Madina ulikuwa na wakazi zaidi ya 3000. Katika Vita vya Makkah (Fath-al-Mubin), zaidi ya watu 10,000 walishiriki. Katika Hajj ya mwisho ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. , kiasi cha watu idadi hiyo walikuwa pamoja na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Kutokea watu wote hawa, ni watu wachache mno waliotajwa katika Sahih. Miongoni mwa hao waliotajwa wapo watu kama Abu Hurairah ambaye alisilimu kiasi cha miaka mitatu tu kabla ya kifo cha Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Mtu mwingine ni 'Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa ambaye nae pia amenakiliwa Ahadith nyingi. Tuangalie alikuwa na umri gani :


Amehadithia babake Hisham: Bi.Khadija alifariki miaka mitatu kabla ya Hijrah ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kwenda Madina. Na huko Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliishi kwa muda wa miaka miwili au zaidi na ndipo hapo alipomwoa 'Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa aliyekuwa na umri wa miaka sita, na ndoa hiyo ilitimika pale alipokuwa na umri wa miaka tisa.


Mahisabu ya kirahisi yanasema:
1)- Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimposa 'Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa kabla ya Hijra ya kwenda Madina (mwaka mmoja kabla ya Hijra). Wakati huo 'Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa alikuwa na umri wa miaka sita. (Riwaya nyingineyo inasema kuwa 'Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa mwenyewe anasema kuwa yeye alikuwa bado akicheza na michezo ya kitoto katika siku hizo).
2)- Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. almwoa 'Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa katika mwaka wa pili wa Hijra, pale 'Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa alipokuwa na umri wa miaka tisa.
3)- Tukuchukulia kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliishi kwa miaka 10 baada ya Hijrah, 'Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa aliishi kwa muda wa miaka 8 tu ya utu uzima wake pamoja na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.Jambo moja napenda kuongezea hapa, nitatoa marejeo halisi, kuwa wanawake huwa ni watu wepesi kusahau maneno halisi au hata maneno yenyewe. Kwa hakika haya ni maumbile ya wanawake. Na hivyo kwa kuwa 'Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa alikuwa ni mwanamke hivyo ni jambo la kawaida kutegemea kuwa yeye pia atakuwa amesahau baadhi ya Ahadith katika hali ya uhalisi wake. Sasa naomba tuchunguze idadi ambazo mimi ninawaleteeni mbele yenu kuhusiana na watu mbalimbali waliozipokea ahadith. Mimi sidai kuwa idadi hiyo ni sahihi kabisa, kwani mimi mwenyewe sikuzihisabu kwa vidole. Ama kwa uhakika mimi binafsi nimezihisabu Ahadith zilizopokelewa na Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. na wana wake. Baadhi ya ahadith ambazo zimeandikwa na Imam Bukhari kwa kurejewa vile vile zimeingizwa katika idadi hiyo. Kimatokeo, itakubidi baadhi ya nyakati upunguze kwa 100 kutokea humo.


Jumla ya Ahadith zilizopo katika Juzuu 9 za Bukhari: 7,068
Na. JINA IDADI %
1 'Aisha bint Abu Bakr 1250 17.68
2 Abu Hurairah 1100 15.56
3 Ibn-Umar, mwana wa Umar 1100 15.56
4 Anas-Ibn-Malik 900 12.73
5 Abdullah-Ibn-'Abbas 700 9.9
6 Jobair-Ibn-'Abdullah 275 3.89
7 Abu-Musa-'Ashari 165 2.33
8 Abu-Said-Al-Khudhri 130 1.84
9 'Ali ibn Abi Talib 79 1.11
10 'Umar-Ibn-Khattab 50 0.71
11 Umm Salamah 48 0.68
12 Abdullah-Ibn-Masud 45 0.64
13 Muawiyah Ibn-Abu Sufian 10 0.14
14 Hassan ibn 'Ali ibn Abi Talib 8 0.11
15 Hussain ibn 'Ali ibn Abi Talib 2 0.03
16 Ali-Ibn-Husain 6 0.08
JUMLA 83
Kama vile uonavyo wewe mwenyewe katika jedwali la hapo juu, zimechukuliwa Ahadith chache kabisa zilizopokelewa na Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. na Watoto (Wajukuu wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ) wake. Mimi sijawapatieni bado majina ya wengine waliozielezea Ahadith. Mwandishi wa kitabu hiki cha Bukhari alikuwa akiishi katika zama za Al-Imam Muhammad al-Baqir a.s., mwana wa Al-Imam Zainul 'Abidiin a.s. na vile vile zama za Al-Imam Ja'afar as-Sadiq a.s. Kwa hakika yeye hakutaja hata Hadith moja kutokea hao. Kwa hakika hiki ndicho kilikuwa ni kipindi ambacho Al-Imam Muhammad al-Baqir a.s. na Al-Imam Ja'afar as-Sadiq a.s. walikuwa wakizielezea Ahadith zilizowafikia wao kutokea Wazazi (a.s.) wao hadi Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. na, mwisho ambapo ndipo kutokea kwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. mwenyewe. Katika maneno mengine, Imam Bukhari hakuwathamini hawa Watoto wa Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. iwapo walistahili kuzielezea Ahadith, na aliwadhania wao kuwa ni waongo. Kwa hakika ukipitia vianzio vya Kishi'a, utaona kuwa watu hawa hawakuwa kimya bali walikuwa ni waelezaji wakubwa wa Ahadith za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kutokea Wazazi a.s. wao hadi kufikia Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. mwenyewe. Je jambo hili si la kuvutia ?Kukiri ?
Hadithi ifuatayo si ngeni vile yaliyopo ndani mwa Hadith yanavyo kwenda. Mwanzani Abu Hurairah ananakili Hadith kutokea Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Na pale watu walipomwuliza iwapo yeye Abu Hurairah aliisikia mwenyewe hadith hiyo kutokea kwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. au sivyo, yeye alijibu kuwa yeye hakumsikia Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na akaielezea yeye mwenyewe.
1)- Kile nikuombacho wewe unisaidie kuigawa hadith hiyo ya kwanza katika sehemu mbili :
a)- Sehemu ya kwanza iwe ile ambayo imesemwa na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.
b)- Sehemu ile ambayo imesemwa na Abu Hurairah tu.
2)- Nitakuomba unieleze kwa uwazi kabisa ni kwa nini watu walimwuliza iwapo maneno hayo yalikuwa yametamkwa na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Hadi pale kiwango cha elimu yangu inapohusika, watu waliuliza hivyo pale walipoisikia Hadith ikiwa ngeni kwao, kama vile Hadith zinazozungumzia mambo ya maishani na baadhi ya matukio ambayo yalikuwa hayaaminiki kwao, na ambayo kwa hakika yanatokezea nyakati hizi. Je ni jambo gani la kustaajabisha katika Hadith hii, na ni kwa nini watu walimwuliza Abu Hurairah iwapo alikuwa akizungumza kile alichokisikia kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. au sivyo.3)- Nitapendelea iwapo wewe kwa uwazi utaniambia kile ambacho kisingelitokea iwapo watu wasingelimwuliza Abu Hurairah iwapo sehemu yoyote ile ya hadith ilikuwa kwa hakika imezungumzwa na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. au sivyo. 4)- Iwapo watu wasingelimwuliza Abu Hurairah iwapo Hadith hiyo ilikuwa imezungumwa na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. au sivyo, kidhahiri, watu wangeliichukulia Hadith nzima kama ni maneno aliyoyasema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Ukweli ni kwamba, vyovyote vile, Abu Hurairah amesema baadhi ya maneno yake mwenyewe na kuongezea baadhi ya maneno katika Hadith ambapo (inawezekana) imetamkwa na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Mimi nitapenda uniambie ni kwa nini unamwamini mtu kama huyo ambaye anaongezea baadhi ya maneno yake mwenyewe katika maneno ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.5)- Je unaweza kuniorodheshea Hadith zote ambazo zimeelezwa na Abu Hurairah na kwamba zimekubaliwa na Imam Bukhari na Muslim, na kuchora mstari ulio wazi kabisa baina ya maneno yaliyozungumzwa na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. au Abu Hurairah mwenyewe. Kwa hakika mimi sielewei vile mtu anavyojiruhusu mwenyewe kuzungumza kile ambacho hajakisikia kutokea Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na hata akathubutu kuziingiza katika maneno ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. hata bila ya kutoa tahadhari. Au ni kwa nini anazungumzia vya kwake mwenyewe kabla ya kuelezea wazi wazi hapo mwanzoni mwa maneno yake kuwa hayo yalikuwa ni maneno yake binafsi na kamwe si ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.? Mfano wa pili unaonyesha wazi wazi kuwa Abu Hurairah ameongezea (inawezekana) katika yale aliyoyazungumza Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Je itakuwaje pale ambapo hakuna mtu yeyote aliyetutanabahisha kuhusu kuongezewa maneno ya ziada ya Abu Hurairah ?


Amehadithia Abu Hurairah kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:
"Sadaqa iliyo bora kabisa ni ile ambayo itolewayo wakati mtu awapo tajiri, na mkono utoao ni bora kuliko mkono ule unaopokea, na wewe inakubidi uanze kuwasaidia kwanza wale wanaokutegemea.' Mke husema, 'Wewe ama unipatie chakula au talaqa.' Mtumwa husema, 'Nipe chakula na ufaidi huduma zangu.' Mtoto husema, 'Nipe chakula, je unaniachia kwa nani?' Watu wakasema, 'Ewe Abu Hurairah! Je hayo umeyasikia kwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ?' Naye akajibu, 'La, bali hayo ni kutokana mimi mwenyewe."


Nitapenda kujua ni kwa nini Abu Hurairah alizoea kuongezea mahala penginepo pia ? Anas bin Malik amesema kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:
"Msifanye vinywaji katika Ad-Dubba' wala katika al-Muzaffat. Abu Hurairah alizoea kuongezea zaidi maneno al-Hantam na An-Naqir. Imehadithiwa na Abu Hurairah kuwa mtu mmoja alimwijia Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na kusema :
"Mimi nilijamiiana na mke wangu katika siku ya Mwezi wa Ramadhani (akiwa katika saumu)." Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimwuliza:"Je unaweza kumfanya mtumwa mmoja awe huru?" Mtu huyo akajibu kuwa hawezi. Ndipo hapo tena Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alipomwuliza:"Je unaweza kufunga saumu kwa muda wa miezi miwili mfululizo ?"Tena mtu huyo akajibu kuwa asingeweza. Basi Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akamwuliza: "Je unaweza kuwalisha masikini 60 ?" Hapa tena mtu huyo akajibu kuwa asingeliweza kuwalisha masikini sitini. (ABU HURAIRAH AKAONGEZEA): Ndipo hapo kikapu kilichokuwa kimejaa tende kilipoletwa mbele ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na akamwambia mtu huyo, "Walishe (masikini) kwa haya kama kaffarah."Mtu huyo akasema, (Je niwalishe haya) masikini kuliko sisi wenyewe? Hakuna nyumba ya wa masikini kuliko sisi baina ya milima ya Mji wa Madina." Kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akasema, "Basi walishe watu wa nyumba yako kwa hayo." Asili Ya Abu Hurairah Masunni kwa kawaida huzitaja baadhi ya Ayah za Qur'an Tukufu kuonyesha kuwa Masahaba ambao walishiriki katika Viapo vya Hudaibiyyah wanalo daraja la juu (mema) na wanaheshimiwa mno. Vyema, hapa, mimi sitaki kujiingiza katika usahihi wa kuitafsiri na kuielewa kwake. Je wewe unajua kuwa wakati huo Abu Hurairah hakuwa Mwislamu, na wala hakuwa miongoni mwa wale walioshuhudia Viapo vya Hudaibiyyah ? Naam ! Abu Hurairah kamwe hakushuhudia Viapo vya Hudaibiyyah ! Abu Hurairah alikuwa Myahudi, na alisimu Siku ya Khaibar ambayo ilikuwapo mwaka mmoja baada ya Viapo vya Hudaibiyyah, na aliishi miaka mitatu tu pamoja na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.1)- Abu Hurairah alisilimu siku ya Khaibar. Haya yanathibitishwa na Jabir ibn 'Abdullah (Hadith ya pili). Abu Hurairah alimwijia Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika siku ya Khaibar Mimi sihitajiki kusisitiza suala hili kuwa Vita vya Khaibar vilikuwa baina ya Waislamu na Mayahudi. Abu Hurairah alikuwa Myahudi kabla ya kusilimu.
2)- Abu Hurairah alikuwa pamoja na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kwa kipindi cha miaka mitatu tu (yeye mwenyewe anathibitisha hayo katika Hadith ya kwanza) "Nilikuwa pamoja na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kwa kipindi cha miaka mitatu"3)- Labda, wewe unaelewa vyema vile wengineo walivyomsalimia pale aliposilimu siku hiyo. Amehadithia Abu Hurairah: Mimi nilikuwa pamoja na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kwa muda wa miaka mitatu, na katika miaka iliyokuwa imebakia katika umri wangu nilikuwa na shauku kubwa ya kuzielewa ahadith za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kama vile nilivyokuwa katika miaka mitatu ile. Mimi nimemsikia akisema, akionyesha kwa mikono yake hivi, : 'Kabla ya Saa, utapigana na watu ambao watakuwa na viatu vya manyoa na wakiishi al-Bariz.' (Sufiani, mnakili wa mnakili, alisema mara moja, "Na hao ndio watu wa al-Bazir."Amehadithia Ja'bir bin 'Abdullah:
"Kuwa yeye alipigana katika Ghazwa kuelekea Najd pamoja na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na wakati Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliporejea , naye pia, alirejea nae. Wakati wa usingizi wa mchana uliwachukua wakati walipokuwa katika bonde lililokuwa limejaa miti ya miiba. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliteremka chini ya farasi wake na hivyo ndivyo walivyokuwa watu wote wakatawanyika katikati ya miti hiyo ya miiba, wakijistiri katika vivuli vya miti hiyo. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alijipatia kivuli chini ya mti wa Samura na kuuning'iniza upanga wake juu ya mti huo. Sisi tulilala kidogo ambapo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alituita kwa ghafla, na tulipomwendea tukakuta kuwa Mbedui mmoja alikuwa ameketi pamoja nae. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akasema kuwa Mbedui huyo aliuchukua upanga wake kutokea ala yake wakati yeye akiwa amelala. Wakati nilipoamka, nikaukuta upanga huo upo mkononi mwake na akiniambia "Je ni nani anayeweza kukuokoa kwangu?" Mimi nikamjibu, "Allah swt" Na sasa huyu hapa ameketi." Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. hakumwadhibu (kwa hayo).Kwa kupitia kundi lingine la waelezaji wengine wa riwaya, Ja'bir alisema : "Sisi tulikua pamoja na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. (katika Vita vya) Dhat-ul-Riqa', na tulitokezea chini ya mti wenye kivuli na tukamwachia Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. (apumzike chini ya kivuli chake). Alitokezea Mapagani mmoja huku upanga wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ulipokuwa ukining'inia mtini. Mpagani huyo aliutoa upanga huo kutokea ala yake kwa kisiri na alimwambia Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. 'Je waniogopa mimi?' Kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimjibu, 'hapana.' Ndipo hapo Mpagani huyo aliposema,'Je ni nani anayeweza kukuokoa wewe kutoka kwangu?' Kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimjibu, 'Allah swt .' Masahaba wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. walimtishia huyo, na mara Iqamah ya Sala ilisemwa, na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alisali raka'a mbili za Sala ya Khofu pamoja na kundi mojawapo ya makundi mawili, na kundi hilo lilikwenda pembeni, na hapo tena Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alisali Raka'a mbili zinginezo pamoja na kundi lingine. Hivyo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alisali jumla ya Raka'a nne ambapo watu walisali raka'a mbili tu."(Mwelezaji wa mwelezaji) Abu Bishr aliongezea, Mtu huyo alikuwa Ghaurath bin al-Harith na Vita vilipiganwa dhidi ya Muharib Khasafa." Jabir akaongezea, "Sisi tulikuwa pamoja na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. hapo Nakhl ambapo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alisali Sala ya Khofu." Abu Hurairah akasema, "Mimi nilisali sala ya Khofu pamoja na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. wakati wa Ghazwa (yaani Vita) vya Najd." Abu Hurairah alimwijia Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. siku ya Khaibar !! Amehadithia 'Anbasa bin Said:
Abu Hurairah alimwijia Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na kumwuliza (kutaka hisa katika mali iliyopatikana katika Vita vya Khaibar au ngawira ). Kwa hayo, mmoja wa wana wa Said bin al-'As alimwambia Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. 'Ewe Mtume wa Allah swt ! Usimpe huyo (Abu Hurairah ).' Kwa hayo Abu Hurairah alimwambia Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. 'Huyu ndiye mwuaji wa Ibn Qauqal.' Mwana wa Sa'id akasema, 'Maajabu gani ! Jitu dogo (au mwovu) litokalo Qadum Ad-Dan!" Amehadithia Abu Hurairah : Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimtuma Aban kutokea Madina kwenda Najd akiwa Kamanda wa Sariya. Aban na wenzake walimwijia Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. huko Khaibar baada ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akiwa ameishaikomboa Khaibar, na mafigo ya farasi zao zilitengenezwa kwa moto wa mitende. Mimi nilisema, 'Ewe Mtume wa Allah swt ! Usiwape hisa ya Ngawira.' Kwa hayo Aban akasema ( kuniambia mimi), "Maajabu ! Wewe unashauri jambo ingawaje wewe ni wewe, ewe mtu mdogo (au mwovu) utokeae Ad-Dal (myungiyungi)!" Kwa kuyasikia hayo, Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akasema, "Ewe Aban, kaa chini!" Na hakuwapa hisa yoyote.Amehadithia Said: Aban bin Said alimwijia Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na kumsalimia. Abu Hurairah akasema, Ewe Mtume wa Allah swt ! Huyu (Aban) ni mwuaji wa Ibn Qauqal." (Kwa kuyasikia hayo), Aban alimwambia Abu Hurairah, "Usemayo wewe yanavyostaajabisha! Ewe, mtu mdogo ( au mwovu) ukitokea Qadum Dan, ukinituhumu mimi kwa (mauaji) ya mtu ambaye Allah swt amemjaalia (shahada) kwa mikono yangu, na kwamba Allah swt ameharamisha udhalilisho wangu mikononi mwake.'