ABU HURAIRAH

 ABU HURAIRAH
YALIYOMO

" Abu Hurairah Na Hadith
" Idadi
" Kukiri
" Asili Ya Abu Hurairah
" Hali Yake Kiakili Na Kimwili
" Kuhadithia Hadith Nyingi Mno
" Abu Hurairah Kupata Fahamu Ya Ajabu


Abu Hurairah Na Hadith ?
Kila kitu, baadaye kilikuja kupitia yeye. Baadhi ya sheria na itikadi za Dini, yote hayo yalikuja kupitia sentenso zake ambazo hazikuwa katika dini asili hapo mwanzoni. Je ni sentenso ngapi unazozidhania wewe kuwa ziliwatenganisha Wakristo kuacha uasili wao ? Yupo mtu mmoja aitwaye ABU HURAIRAH ambaye historia yake mimi nitaweleteeni hapo mbele baada ya punde. Mtu huyu anasema mwenyewe : Amehadithia Abu Hurairah: Hakuna Sahaba hata mmoja wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kama mimi ambaye amehadithia Hadith zaidi yangu isipokuwa 'Abdallah bin Amr (bin al-'As) ambaye alikuwa akiziandika ambapo mimi sikufanya hivyo.


Juzuu zote tisa za Sahih Bukhari zina Ahadith 7,068. Kati ya hizo kiasi cha Ahadith 1100 zimenakiliwa na mtu huyu, yaani tuseme katika maneno mengine kuwa yeye amenakili Ahadith kiasi cha 15.56% za Ahadith zote za Sahih Bukhari (kiasi cha 1/6). (Hapa mbeleni nitawapatieni idadi sahihi za Ahadith alizozinakili Abu Hurairah katika Sahih Muslim).


Kama vile nilivyoonyesha juu ya "Abu Hurairah", yeye alijipinga mwenyewe na vile vile kisayansi. Hadith ifuatayo ni wazi ambapo yeye anainakili kwani inapingana na vile 'Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa na 'Umm Salamah walivyoipokea. Iwapo sisi tutakubali kuwa 'Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa na 'Umm Salamah walikuwa katika nyumba ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. wakati mwingi zaidi kuliko wake zake wengine, basi kwa urahisi tutambua pale penye tatizo.


Haya yapo katika ukurasa wa 81, katika sura: Iwapo mtu aliye katika hali ya saumu akiamka asubuhi akiwa katika Janaba (je saumu yake itakuwa sahihi ?) Hadith hii imetarjumiwa na mtarjumu tu hadi mwishoni mwa aya ya kwanza. Kufikia hapo, aliacha kutarjumu. Hata hivyo, bado ipo katika lugha ya Kiarabu. Kiasi kinachobakia ni tarjuma yangu. Iwapo wewe hautataka kuniamini, ninakushauri urejee katika maandishi ya Kiarabu. Zaid ya hayo, mimi nitakuletea vianzio zaidi kwa ajili ya kuelezea na tarjuma nilioyoifanya.


Amehadithia 'Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa na Umm Salamah: "Baadhi za nyakati Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alikuwa akiamka asubuhi huku akiwa katika hali ya janaba baada ya kujamiiana na wake zake. Yeye alikuwa akioga na kufunga saumu.Imehadithiwa na Abu Bakr bin 'Abdur-Rahman : Mimi na baba yangu tulimwendea'Aisha naye akasema : "Mimi ninatoa shuhuda kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. nyakati zingine alikuwa akiamka asubuhi akiwa katika hali ya Janaba kwa sababu ya kujamiiana, na wala si kutokwa manii usingizini na alikuwa akifunga saumu siku hiyo." Kutoka hapo alimwendea Umm Salamah ambaye nae pia alihadithia hivyo hivyo.


Marwan alimwambia Abdu-Rahman ibn Harith: Kula kiapo kwa kuyasikia haya, Abu Hurairah atapiga makelele. Wakati huu, Marwan alikuwa mjini Madinah. Abu Bakr akasema: Abd-Rahman hakupendezewa na haya. Baadaye ikatokezea kuwa tukakutana Dhi-Hulaifah ambapo Abu Hurairah alikuwa na kipande cha ardhi. Abd-ar-Rahman akamwambia Abu Hurairah: Mimi nakwambia haya, na iwapo Marwan asingelikuwa ameniuliza mimi ( kwa kula kiapo) haya, basi mimi nisingelizungumzia hayo kwako wewe. Ndipo hapo alipoitaja Hadith hiyo aliyoelezwa na 'Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa na Umm Salamah. Yeye (Abu Hurairah) alisema: al-fadhl Ibn Abbas ameninakili mimi hivyo yeye ni mtu aliye elimika zaidi. Hammam na Ibn Abdullah Ibn Umar wamenakili kutokea Abu Hurairah kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliamrisha kufunguliwa kwa saumu (na msifunge), (ni dahiri) kuwa mapokezi ya mnyororo huo (ni kutokea 'Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa na Umm Salamah ) unaaminiwa zaidi.Swali :
Abu-Hurairah (RA) alikuwa karibu mno na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kwa miaka michache, hata hakwenda sokoni. Jibu :
Je unaelewa ni kwa kipindi gani Abu-Hurairah alikuwa pamoja na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.? Jibu la swali linapatikana kutokea marejeo ya Ki-sunni:
1. al-Milala wa al-Nihal, ya ibn al-Jawzi, Pub. Egypt.
2. Sirat Ibn Hisham, Pub. Egypt.
Abu-Hurairah alisimu miaka miwili tu kabla ya kifo cha Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Hivyo, itawezekanaje kwake yeye kuripoti Ahadith 2000 katika Sahih al-Bukhari peke yake, wakati ambapo zipo Ahadith chache kabisa zilizoripotiwa na Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., Al-Imam Hassan ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s., Al-Imam Hussain ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. au Bi.Fatimah az-Zahra a.s. Je utaelezaje masuala kama haya? Mimi kwa hakika ninapendelea katika malengo na majibu yako ya kisayansi huku ukisaidiwa na baadhi ya marejeo.


Jibu :
1) Abu Hurairah alikuwa pamoja na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kwa muda wa masaa 24 !!! Na hivyo ndivyo alivyoweza kuzielezea Ahadith zaidi .
2) Yeye alizielezea Ahadith nyingi mno kwa sababu ya kuwa pamoja na Masahaba wengineo . Kwa hakika Masahaba walikuwa ni Waislamu wema na waliokuwa wakiaminiana, na hivyo ndivyo alivyoweza kuzichukua baadhi ya ahadith kutokea Masahaba .


Jibu:
Ama kwa kuhusiana na upinganashi unaotolewa, kile niwezacho kukisema mimi ni kwamba inambidi msomaji arejee vitabu vya Fiq-h!!!! Na haya nimeyasema kwa mara nyingi zilizopita .. kwani kwa kuutolea uamuzi Hadith, inakubidi urejee vitabu vya Fiq-h . Kwani si jambo la moja kwa moja. Mfano wa kitabu cha Fiq-h al-Sunnah.

Kwa upande wa pili, iwapo wewe utakuwa na kitabu cha Fiq-h al-Sunnah naomba uzingatie kuwa wakati Said Sabiq (mmoja wa Wanazuoni wa Kisunni anayeheshimiwa na vile vile mwandishi wa vitabu vinavyotambulikana kama kitabu tulichokitaja hapo juu ) anapozungumzia baadhi ya masuala, mara nyingine yeye huzungumzia kimtazamo wa Kishi'a kwa suala hilo. Kwa mfano: Zawaj al-Mut'ah, Qanun al-Hawal al-Shakhsiyyah (Kanuni za Ndoa).


Vile vile chunguza mwelekeo wake pale anapowazungumzia Waislamu Mashi'a au Wanazuoni wa Ki-Shi'a! Tafadhali sana naomba unijulishe kile unachokifikiria baada ya kupitia Sura mbili za kitabu hicho.