BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

 

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

 

IMEANDIKWA NA NDUGU ZETU WA KIISLAMU.

 

MALENGO YA DINI

 

UMUHIMU WA DINI KATIKA MAISHA YA MWANAADAMU

Kidokezo kuhusiana na dini:

Dini ni malengo ya mwanaadamu, na dini sio nyenzo inayomfikisha mwanaadamu katika njia isiyoendana sambamba na dini, dini imekuwa dini kwa ajili ya malengo ya wanaadamu wote, na sio kwa kundi au watu maalumu katika jamii, dini ya haki haiwezi kuwa lengo kwa kundi moja, na kuwa nyenzo kwa kundi jengine, malengo ya dini kwa wanaadamu wote ni mamoja, na sio kwa kundi moja kuwa ni lengo kwa ajili ya kudhibiti utawala, na kwa kundi jengine kuwa kama ni nyenzo kwa ajili ya kutawaliwa. Dini ni kwa ajili ya matabaka yote ya jamii, kwa bepari, mfanya kazi, mwanazuoni, tajiri, masikini, wasomi,n.k. Dini iko sawa kwa watu wote na kwa matabaka yote, basi dini haiwezi kuwa kama ni kigezo cha kushikilia kwa ajili kundi fulani, na kuwa kama ni nyenzo inayotumiwa na kikundi fulani kwa ajili ya kuziridhisha nafsi zao. Dini ni fungamano lililo kamili kwa ajili ya Mwenyeezi Mungu tu, na sio kwa ajili ya kundi au watu fulani, kwa mfano: mabepari, mutribu, muuguzi, muumikaji, n.k.

 Dini ni nyenzo ya kuweka uadilifu wa rasilimali katika jamii, kuzigawa haki za jamii kwa uadilifu na insafu, dini sio zana ya kueneza afyuni katika jamii. Kwa hiyo, ule ufafanuzi unaohusiana na dini uliotolewa na kitengo cha wanafiki sio sahihi na haukubaliki.

Kitengo hicho kimeifafanua dini kwa mtindo huu ufuatao:-

Dini imechukuliwa kama ni nyenzo inayoshikiliwa na tabaka la mabepari na wanyonyaji au hata watu wa kawaida inayotumiwa kwa ajili ya kupata mahitajio yao. Watu hao huitumia dini kama ni nyenzo ya kuridhisha nafsi zao, kwa hiyo dini ni afyuni ya jamii[1].

Ufafanuzi huo haukubaliki na sio sahihi, kutokana na dalili hizi zifuatazo:-

Hivi katika jamii ya dini, dini haikuwa sababu ya kupatikana mapinduzi? Au katika zama zote hizo hakujatokea mapinduzi yoyote yaliyopatikana kwa sababu ya dini? Hivi taasisi zote za wafuasi wasio na dini zimeweza kuleta usawa na kusawazisha baina tabaka na tabaka, au baina ya kabila na kabila n.k.? hivi kuna uwezekano wa kutumia nguvu za dini kwa ajili ya kuwaridhisha watu? Basi kwa siku ambazo hawatakuwa radhi au kutoridhika watapigana vita kwa dini gani, hivi kila mletaji mapinduzi hakuwa ni mwenye dini? Au kuna wanamapinduzi ambao walikuwa na dini, kama kuna wanamapinduzi walikuwa na dini, basi hakuna shaka kuwa dini sio nyenzo, wala dini haihusiani na kundi fulani tu, na dini haina nafasi ya unyonyaji au utumiaji wa nguvu kimagubegube.

Dini ina mtazamo mmoja kwa wanaadamu wote duniani, tofauti za makabila au rangi hazina nafasi yoyote kwa Mwenyeezi Mungu, nafasi ya dini katika jamii ni kuwaweka watu wote sawa na kuwafanyia insafu na uadilifu. Kwa hiyo mwenye thamani mbele ya Mwenyeezi Mungu ni yule anayemtii na kumcha Mola wake. Kama anavyosema Mwenyewe Mola Mtakatifu:-

[2]

Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari.

Basi watu wote ni sawa, na Mwenyeezi Mungu amewaumba waja wake katika mataifa na makabila mbali mbali ili watambuane, na sio kunyonyana au kudhulumiana

 Zingatio:

Ikiwa dini, ni dini ya kweli na ya uhakika, basi watu na jamii kwa ujumla ni lazima wawe wameshikamana na dini, dini bila ya watu wenye dini, au jamii isiyo na dini ni alama inayoonyesha upungufu wa dini hiyo. Kwa hiyo, dini ya haki ni dini ya Kiislamu, kwa sababu amali na matendo ya Waislamu walioshikamana na dini yanaonyesha haki ya dini hiyo.

Ni sahihi kuwa kuna tofauti baina ya dhati ya dini na washikamanaji wa dini, (tofauti baina ya dini na wanadini), kwa hiyo ni lazima tuzingatie kuwa, ni jambo lisiloingilika akilini kuitia upungufu dini kutokana na amali au matendo mabaya ya baadhi ya wanadini, tukitaka kuitambua dini na turejee kwa watu watukufu walioletwa na Mola Muumba kwa ajili ya kuwaongoza watu katika njia bora, watu hao watukufu wa Mwenyeezi Mungu (Mitume na Ahlulbayt a.s ) ndio kigezo bora cha dini ya haki. Kwani wao walishikamana na dini katika pande zote, kiamali na kimatendo, katika uhai wa watu hao watukufu, hakukuonekana tofauti yoyote baina ya amali na matendo yao, kwa hiyo kila Muislamu, na kila mwenye imani na Mitume ya Mwenyeezi Mungu na Ahlulbayt wake , ni lazima afanye jitihada zake zote ili kuiendeleza njia ya haki ya watukufu hao, na ni wadhifa wa kila Muislamu kufanya amali na matendo ya dini katika msingi wa haki unaoridhiwa na Allah (s.w), kwani, kwa kufanya hivyo tutaondoa ule umbali unaoonekana katika amali na matendo ya wanadini. Kwani kuvitenganisha vitu hivyo viwili ni kuitia dini athari mbaya, na kwa sababu hiyo basi Maimamu (a.s) walitilia mkazo suala la kuihifadhi dini, kama anavyosema mmoja wa Maimamu:-

ی ʘ ی

Kuweni ni pambo letu lenye kumurika (lenye kuakisi) sifa njema kutoka kwetu, wala msiwe picha mbaya ndani ya jamii zitakazowafanya watu kukirihishwa wanaposikia majina yetu.

Ibara hiyo ina maana hii ifuatayo:

(Msitutukanishe kwa sifa mbaya za matendo yenu, bali kuweni ni nuru na vigezo vyema kwa watu na katika jamii mnazoishi).


 

[1] Kitabu, njia ya Mitume ni njia ya wanaadamu. Kitengo cha wapiganaji jihadi, Irani. 

[2] Surat Al-Hujurati Aya ya 13.

 

 

 

MWISHO