BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

 

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

 

IMEANDIKWA NA NDUGU ZETU WA KIISLAMU.

 

MAKUNDI YA WANAADAMU SIKU YA KIAMA NO.2

 

* wanaadamu watagawika makundi mangapi katika siku ya malipo na jazaa?

 

Katika makala iliyopita inayohusiana na makundi watakayogawika wanaadamu siku ya Kiama, katika makala hiyo tulilielezea kundi la mwanzo, katika

 

makala hii tutaendelea kuelezea makundi mengine.

 

Siku ya Kiama walimwengu watagawiwa katika makundi totfauti kwa mujibu wa itikadi na amali zao walizozifanya duniani.

 

*Kundi la watu watakaoelekea upande wa kulia. 

 

Neno یی ndani ya Qur-ani limekuja likiwa na maana ya upande wa kulia, na watu watakaoelekea upande wa kulia ni wale ambao siku ya Kiyama watapewa daftari ya amali zao walizozitenda kwa mkono wa kulia,

 

basi hiyo ni alama inayoonyesha saada njema ya watu hao, kama tunavyosoma ndani ya qur-ani kuhusiana na watu hao.

. . [1]  

Ama atakaye pewa daftari lake kwa mkono wa kulia, Basi huyo atahisabiwa hisabu nyepesi, Na arudi kwa ahali zake na furaha.

 

Watu hao watabakia Peponi milele na kunufaika na neema zake Allah (s.w), wengi wao wa kundi hilo watakaofaidika na neema hiyo ni kutoka katika uma wa Hadharati Muhammad (s.a.w.w) kama tunavyosoma

 

ndani ya qur-ani:-

. . [2]

Kwa ajili ya watu wa kuliani. Fungu kubwa katika wa mwanzo, Na fungu kubwa katika wa mwisho.

 

Watu hao ni waumini, na waliishi duniani kwa kutekeleza maamrisho ya Mol wao, na walipokuwa wakikutwa na tabu au mashaka hunasihiana na kuhimizana kuwa na subra, na walikuwa wakifanya jitihada zao zote

 

ili kuwaondolea matatizo yao wale waliokuwa wakihitajia misaada kutoka kwao, basi waliwasaidia na kuwapa himaya mafakiri, mayatima, na masikini, Mwenyeezi Mungu anawaarifisha watu hao kwa kusema:-

. [3]

Tena awe miongoni mwa walio amini na wakausiana kusubiri na wakausiana

 

kuhurumiana. Hao ndio watu wa kheri wa kuliani.

 

*Kundi la watu wanaosonga mbele katika mambo ya kheri.

 

Kundi litakalosonga kuelekea mbele ni lile kundi la watu ambao, baada ya

 

 

kuwadhihirikia haki hawakupinga wala kufanya uvivu, bali walimuamini Mwenyeezi Mungu na waliyaamini yale waliyokuja nayo Mitume, na walivuka hatua ya kufanya amali njema nzuri na kutii maamrisho na

 

desturi za Mola wao, katika qur-ani tunasoma:-

[4]

Basi wote hao ndio wanao kimbilia katika mambo ya kheri, na ndio watakao tangulia kuyafikia.

 

Watu hao waliotangulia katika kufanya yale ambayo wameamrishwa na Mola wao, na wakamtii Mwenyeezi Mungu na Mitume yake, na walipokutwa na tabu walivuta subira, na wakapigana jihadi katika njia ya

 

Mwenyeezi Mungu, hapana shaka kuwa watu hao ndio watu bora kulinganisha na watu wengine

 

[5]

 

Na mna nini hata hamtoi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na hali urithi wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu? Hawawi sawa miongoni mwenu wenye kutoa kabla ya Ushindi na wakapigana vita.

 

Hao wana daraja kubwa zaidi kuliko wale ambao walio toa baadae na wakapigana. Na wote hao Mwenyezi Mungu amewaahidia wema. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda.

 

Watu waliotangulia katika mambo ya kheri ni wale walio karibu na Mola wao, kama anavyosema Allah (s.w):

. [6]

Na wa mbele watakuwa mbele. Hao ndio watakao karibishwa .

 

Watu hao watapata jazaa na malipo mema, hata utakapofika muda wao wa kuitika wito wa Mola wao (yatakapowafikia mauti) hawatakuwa na hofu wala woga wowote, na watanufaika na kila neema ya Mwenyeezi

 

Mungu katika makazi yao huko Peponi. kama tunavyosoma ndani ya Qur-ani:-

. . [7]

 

Basi akiwa miongoni mwa walio karibishwa, Basi ni raha, na manukato, na Bustani zenye neema. Na akiwa katika watu wa upande wa kulia, Basi ni Salamu kwako uliye miongoni mwa watu wa upande wa kulia.

 

*Kundi la watu wenye (Ikhlasi) waliozitakasa na kuzisafisha nafsi zao na maovu.

 

Kundi hilo ni kundi la waja wema na watiifu wa Mwenyeezi Mungu (s.w), watu wa kundi hilo mbali ya kumuamini Mwenyeezi Mungu, na kutangulia katika kufanya mambo mema, vile vile wana utukufu maalumu

 

mbele ya Allah (s.w), utukufu ambao hauwezi kuonekana katika viumbe wengine, Mwenyeezi Mungu huwaepusha waja wake hao na kila maovu na machafu, kama tunavyosoma kuhusiana na Nabii Yussuf (a.s):-

 

ٰ [8]

 

Na hakika yule mwanamke alimtamani, na Yusuf angeli mtamani lau kuwa hakuona ishara ya Mola wake Mlezi. Hayo hivyo ni kwa ajili tumuepushe na uovu na uchafu. Hakika yeye alikuwa katika waja wetu walio

 

safishwa.

 

Watu hao wema watukufu walio na Ikhlasi wametukuka na wako katika daraja ya juu kabisa, kiasi ya kwamba hawawezi kufanya maasi hata kwa kukosea au kusahau, wako katika amani,  na wamesalimika na wasi

 

wasi wa shetani na iblisi. Mwenyeezi Mungu Mtukufu kuhusiana na watu hao anasema hivi:-

. [9]

Akasema (Iblisi): Naapa kwa utukufu wako, bila ya shaka nitawapoteza wote,

 

Isipo kuwa wale waja wako miongoni mwao walio khitariwa.


 

[1] Surat Inshiqaaq Aya ya 7-9.

[2] Suratul-Waqiah Aya ya 38-40.

[3] Suratul Balad Aya ya 17-18.

[4] Surat Al-Muuminuun aya ya 61

[5] Suratul-Al-Hadiyd Aya ya 10.

[6] Surat-Al-Waqiah Aya ya 10-11

[7] Surat Al-Waqiah aya ya 88-91

[8] Surat Yussuf Aya ya 24

[9] Surat sad Aya ya 82-83.

 

 

MWISHO