Tatizo la
Kutafsiri
Wataliano wana usemo usemao "Wafasiri ni
waongo". Msemo huu una ukweli ndani yake na umetokana na uchunguzi
makini. Kuchukua kitu fulani kilichoandikwa katika lugha fulani na kujaribu
kukiingiza katika lugha nyingine huwa inaleta matatizo kwa sababu mara
nyingi wafasiri hupambana na maneno katika lugha moja ambayo hayamo katika
lugha nyingine. Neno jingine badala yake lazima litumike na matokeo yake ni
kubadilika kwa maana.
Agano la kale mwanzo kabisa liliandikwa kwa Kiebrania, lakini lilitafsiriwa
katika karne ya tatu kwenda katika lugha ya Kigiriki kwa ajili ya Wayahudi
waliokuwa wanaishi nje ya Palestina (ambao walikuwa wanaongea Kigiriki -
badala ya Kiebrania). Tafsiri hii iliitwa "septuagint" na ilitumika
sana hata na wakristo wa mwanzo.
Agano Jipya liliandikwa katika lugha ya Kigiriki lakini maadam Yesu mwenyewe
alitumia lugha ya kiaramaiki, hii ina maana kwamba maneno yake yalilazimika
kutafsiriwa na hivyo kusababisha uwezekano wa makosa.
Tafsiri ya kigiriki iliyokuwa ikiitwa Septuagint iliunganishwa na maandiko
ya Agano Jipya yaliyokuwa katika lugha ya kigiriki katika karne ya nne.
Maandiko haya yaliyounda Biblia kamili sasa hivi yanaeleweka kamaCodexsinaiticus"
na "Codex Vaticanus" na hizi ndio nakala za maandiko ya zamani
kabisa zilizopo leo. Hakuna maandiko ya mwanzo kuliko haya yaliyonusurika
kutupiliwa mbali.
Katika karne ya nne, Biblia ilitafsiriwa kwenda katika lugha ya Kilatini na
Mt. Jerome. Na hii ilibakia kuwa lugha ya Biblia hadi karne ya kumi
na sita ambapo watu wa Mageuzi kama John Wycliffe, William Tyndale na
Martin Luther walipoifasiri Biblia katika lugha mbalimbali za watu -
jambo ambalo lilikuwa haliruhusiwi kabisa na viongozi wa kanisa wa wakati
ule na ili kufanikisha lilimgharimu Tyndale maisha yake. Walifanya hivi ili
kuwazuia watu kuyasoma, kuyaelewa au kuyahisi maandiko yao Matakatifu - haya
yalifanywa makusudi na viongozi wa kanisa.
Tafsiri nyingine zilifuatia ndani ya muda mfupi. Karibu na mwisho wa karne
ya kumi na sita kulikuwa na tafsiri za lugha mbalimbali na tafsiri
mbalimbali za lugha moja ambazo zilileta malumbano na mabishano makubwa
jambo lililomfanya Mfalme James I wa Uingereza kuteua kamati ya
wanazuoni hamsini na nne ili kuandaa toleo "rasmi" na litakalotambulika na
mamlaka. Watu hawa (kamati) walizisoma tafsiri zote zilizokuwepo wakati ule
na, mnamo mwaka 1611, walitoa toleo lililoitwa "King James Versions of
the Bible" yaani toleo la Biblia la Mfalme James - ambalo lilikuwa ndio
toleo rasmi miongoni mwa Wakristo kwa mamia ya miaka.
Tatizo la uharibifu na upotoshaji lililoambatana na kutafsiri liliisha mwaka
1611, kwa kupatikana toleo la King James Versions of the Bible, tatizo la
marudio... "kuiboresha" au kuifanya kuwa ya "kisasa" limeikabili Biblia leo
hii.
Kiwango cha uharibifu na upotoshaji huu ni kama ifuatavyo:
katika mwaka 1952, makala yenye kichwa cha habari "Ukweli kuhusu Biblia"
yalionekana katika gazeti la "Look" (Tazama). Makala haya yalisema kwamba
kulikuwa makosa zaidi ya 20,000 (elfu ishirini) katika Agano Jipya
peke yake. Mashahidi wa Yehova walilizungumzia suala hili katika toleo la
Septemba, 1957 la gazeti lao la "Awake" (Amka) ambapo walisema
"...Wafasiri walifanya makosa katika kufasiri (Biblia) ambayo yamesahihishwa
na wanazuoni wa zama hizi… nao wakasema kuwa biblia ina makosa zaidi ya 50,
000…". Mtu anaweza kujiuliza ni jambo la ajabu wanazuoni hawa walilifanya!!
Katika karne ya kumi na tisa, Wakristo waliamua kuiboresha lugha
ilivyotumika katika King James Version. Jitihada zao zilizaa toleo jipya la
Biblia liitwalo "American Standard Version" lililotolewa mwaka 1901.
Wakristo waliolifanyia kazi toleo hili sio tu kwamba waliikuza na kuiboresha
lugha bali pia walifanya mabadiliko katika Biblia yenyewe:
Katika kuuthibitisha ukweli kwamba baadhi ya maneno yaliondolewa na mengine
kuongezwa, tunaweza kuangalia katika maandiko ya mwanzo ya Biblia yaliyokuwa
katika lugha ya kigiriki toleo la Biblia la King James Version 1Yohana
5:8 ambapo imeandikwa "Baba, Mwana na Roho Mtakatifu". Lakini
toleo jipya la American Standard Version, wanazuoni walibadilisha na badala
yake wakatumia maneno "Roho, Maji na Damu". ( " Angalia Nukuu hapo juu
kabisa)
Katika kukubali ukweli mwingine juu ya uongezaji na upunguzaji wa baadhi ya
maneno katika Maandiko Matakatifu (Biblia), vifungu vya vingi vimefungiwa
mabano na katika sherehe yake (maelezo ya ziada) wameeleza kwamba vifungu
hivi "havipatikani katika Biblia (Maandiko matakatifu) nyingi za zamani".
Baada ya miaka kadhaa viongozi wa kanisa walikutana wakaamua kuliboresha
toleo la Biblia la American Standard Version. Matokeo ya jitihada zao
ilikuwa ni kupatikana toleo jingine la Biblia linalojulikana kama "The
Revised Standard Version" - yaani toleo la Biblia la kiwango bora na
lililofanyiwa marekebisho. Toleo hili lilitoka rasmi mwaka 1952.
Katika dibaji ya Toleo hili kuna maelezo haya: "…Toleo la King James
(King James Version) lina makosa na mapungufu mengi mno na hatari sana kiasi
kwamba kuna haja kubwa ya kulifanyia marudio na marekebisho toleo zima...".
(Tafadhali angalia dibaji ya Revised Standard Version)
Katika toleo la Biblia la 'The Revised Standard Version' tunakuta kwamba aya
katika injili ya Marko zinazozungumzia juu ya kupaa kwa Yesu (Marko
16: 9-20) zimeondolewa kwa madai kwamba aya hizi hazipatikani katika
Biblia (maandiko) za zamani kabisa.
Katika mwaka 1989, toleo la Biblia la 'The Revised Standard Version' la 1952
liliboreshwa tena na hivyo likapatikana toleo jipya "The New Revised
Standard Version". Na katika toleo hili aya zinazozungumzia
juu ya kupaa kwa Yesu katika Marko 16 zilirejeshwa. Kwa vile Wakristo
wengi hawakufurahia "kumomonyolewa" kwa moja ya imani zao za msingi
kulikofanywa na Wahariri wa "The Revised Standard Version", ilibidi aya hizi
zirejeshwe ili kuwaridhisha.
Kwa kuhitimisha, tunaweza kusema, kutokana na marudio ya mara kwa mara
yaliyofanyika kwa miaka mingi wakati wa kufasiri na "Matoleo" mbalimbali
mapya katika Biblia tuliyonayo leo maandiko ya wanadamu ndio mengi zaidi
kuliko ufunuo kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Wakristo Wenyewe Wanasemaje Juu ya Tatizo
Hili
Huko nyuma katika karne ya nne, Mt. Augustino aligundua
makosa mengi, ndani ya Biblia. Akizungumzia juu ya suala hili katika barua
yake Na. 82 Alisema kwamba… makosa katika uelewaji ndio sababu ya tatizo
hili (la kuona aya zinapingana, na nyingine zipo katika toleo hili,
lakini katika toleo jingine hazipo na utatanishi mwingine mwingi).
Anasema yeye haamini kwamba watu kuongeza, kupunguza na kubadilisha baadhi
ya mambo katika Biblia kuwa ni tatizo ila tatizo ni uelewaji mbaya katika
usomaji. Kwa maneno mengine anasema kwamba baada ya msomaji kukumbana na
mikorogano hii katika Biblia anatakiwa abuni maelezo fulani yatakayokuwa ni
msamaha wa makosa haya.
Utafiti unaojaribu kuangalia na kuonyesha makosa katika Maandiko Matakatifu,
tofauti na watu wengi wanavyofikiri, umeanza hivi karibuni. Kwa mamia ya
miaka Biblia ilikubalika tu "kama ilivyo". Ilichukuliwa kuwa ni dhambi kubwa
sana kujaribu kukosoa kosa, hata dogo lililomo ndani ya Biblia na viongozi
wa kanisa walifanikiwa sana kuyazima majaribio yoyote ya kujaribu kuikosoa
Biblia.
Kitabu cha kwanza kuonyesha na kukosoa makosa katika Biblia kilichoandikwa
na Richard Simon kiitwacho Critical History of the Old Testament
(Historia inayojaribu kuonyesha na kukosoa makosa yaliyomo katika Agano
la kale), kilitoka mwaka 1678. Kitabu hiki kilileta tafrani na mtafaruku
mkubwa lakini kilisaidia sana kufungua njia kwa wale waliokuja baadaye
katika karne ya 18 na 19 kwa dhumuni la kufanya utafiti juu ya makosa
yaliyomo katika Agano la Kale.
Kutokana na ukweli mwingi usiopingika uliotolewa na watu mbalimbali,
Halmashauri ya awamu ya Pili ya Vatican (1962- 1965) ilitoa maelezo
yanayoshangaza juu ya jambo hili "…Vitabu vya Agano la Kale vina
(ndani yake) habari zisizo sahihi na zenye mapungufu mengi..."
Agano Jipya pia lina kasoro na mapungufu mengi. Ingawa Halmashauri ya awamu
ya pili ya Vatican inashikilia kwamba Injili "kihistoria ni ya kweli " na
kwamba wao "kwa uaminifu kabisa wanaeneza yale ambayo Yesu alifanya na
kufundisha watu wakati wa maisha yake". Wanazuoni wengine wamekuwa na
maelezo ambayo ni kinyume kabisa na msimamo wa Vatican.
Katika kitabu chake "The Call of the Minaret" (Wito kutoka katika
mnara wa msikiti, Adhana), Dr. Kenneth Cragg anasema kwamba
kuna "mambo yaliyoongezwa na kupunguzwa" katika Agano Jipya Injili na
ni kazi ya akili ya viongozi wa kanisa ikiongozwa na waandishi, na kwamba
katika kazi zao wanatumia uzoefu na historia."
Padre Kannengiesser, Profesa katika taasisi ya kikatoliki
katika mji wa Paris, alionya katika kitabu chake "Faith in
Resurrection" (Imani juu ya ufunuo), kwamba watu wasijaribu "kuyatafsiri
na kuyaelewa maneno kama yalivyo" juu taarifa za kweli kuhusiana na Yesu
katika Injili - onyo ambalo pia lilitolewa na Padre Rognet wa Paris
katika kitabu chake "Initiation to the Gospels".
Carl Andrey, profesa wa falsafa na masomo ya dini katika Chuo kikuu
cha Ball State kilichopo Indiana anasema kwamba vitabu vinne vya Injili: "…viliandikwa
na watu wenye shauku wa harakati za mwanzo za kikristo na kwamba wanatupatia
nusu tu ya habari kamili na kwa kiasi kikubwa ni mazao ya fikra za waandishi
wao"
Mwisho tuna maelezo ya Dr. W. Graham Scroggie wa "Prestigious
Moody Bible Institute" ambaye anasema: "Ndiyo, Biblia ni zao la kazi
iliyofanywa na binadamu …vitabu hivyo vimetokana na akili za watu,
vimeandikwa kwa mikono ya watu, na fani ya uandishi wake ni ya kibinadamu.
Kama huu ndio msimamo wa
wanazuoni wa Biblia, wakristo wa "kawaida" watakuwa na lipi la kusema juu ya
jambo hili?
Wengi (wa wakristo wa kawaida) hata hawajui lolote juu ya kasoro nyingi
zilizomo ndani ya Biblia kwa sababu waandishi wa utangulizi na
washereheshaji (wanatoa maelezo ya ziada) wa Biblia. Wanatumia mbinu
mbalimbali za kijanja ili kuwafanya Wakristo wasiyajali na wajisahaulishe na
maswali ambayo wangejiuliza juu ya kasoro nyingi zilizomo ndani ya Biblia.
Pamoja na mambo mengine, waandishi hawa:
1) Wanaandika mambo kama ukweli uliothibitika wakati ukweli na uthabiti wake
una mashaka, na
2) Wanayafunika makosa na kasoro zilizomo ndani ya Biblia kwa kutoa nyudhuru
na kuomba radhi mbinu ambayo inaondoa umakini wa msomaji kutoka kwenye
dosari na kasoro zilizomo ndani ya Biblia na badala yake kuangalia mambo
mengine.
Kina wanachokwenda washereheshaji (Commentators) katika kujaribu kutetea
kasoro na dosari zilizomo ndani ya Biblia ni alama na ushahidi tosha juu
kutojisikia kwao vizuri na ugumu wanaoupata katika jitihada zao za kujaribu
kutetea makosa, dosari na kasoro zilizomo ndani ya Biblia.
Pamoja na ukweli huu juu ya kasoro na dosari zilizomo ndani ya Biblia, ajabu
ni kwamba mtu anapojaribu kuzionyesha hataambulia chochote kutoka kwa
wakristo isipokuwa uadui.
Watu wengi waliwahi kupeleka makaratasi yenye utafiti juu ya kasoro na
dosari mbalimbali zilizomo ndani ya Biblia katika mishenari ya kikristo,
lakini wanacho ambulia kushutumiwa kwa kufanya "uvamizi dhidi ya Biblia, na
utawasika wakisema "Biblia imefanyiwa uvamizi (imevamiwa) kwa karne nyingi,
lakini bado ipo. Imestahimili vishindo (vyote) vya nje na ndani".
Nastaajabu vipi mtu awe na msimamo kama huu mbele ya mifano tele inayoweza
kuthibitishwa, sielewi anamaanisha nini katika neno "vishindo". Labda
linaendeleza lile linalopatikana katika "kazi bora " ya vitabu vinavyotetea
dosari na kasoro zilizomo katika vitabu vya Kikristo iliyomo katika kitabu
kiitwacho "Is Bible Reliable. (Je, Biblia inaaminika?).
Katika kitabu hiki, mwandishi Bjug Horstal anasema kwamba
Mungu "aliwashawishi" waandishi wa Maandiko Matakatifu " …kuandika kasoro na
dosari zilizoambatana (zinazotokana) na lugha, na kwamba tunatakiwa tuliache
jambo hili kwa Mungu mwenyewe, awe huru kutumia idadi yoyote ile ya fani na
hata udhaifu wa kibinadamu kama anavyotaka mwenyewe…".
Mashahidi wa Yehova wameandika kitabu kizima kiitwacho:
Bible: God's Word or Man's? (p. 97) (Biblia: Ni neno la Mungu
au la Mwanaadamu?), ambacho kinazungumzia kasoro na dosari zilizomo ndani ya
Biblia. Katika kitabu hiki, wamelizungumzia suala hili kwa namna tofauti na
ya pekee kwa kusema kwamba: 'kuna baadhi ya "kasoro na dosari za wazi"
katika Biblia ambazo "ni vigumu kuzitetea". Hata hivyo tusizichukulie dosari
na kasoro hizi kuwa ni kugongana na kupingana kwa aya za Biblia; mara nyingi
ni kwa sababu ya ukosefu wa taarifa na habari kamili'.
Nilibahatika kupata nakala ya tafsiri ya Biblia ya Mashahidi wa Yehova "The
New World Translation of the Holy Scriptures". Nilimuuliza mjumbe
mmoja wa ngazi za juu kuwa ana maelezo gani juu ya aya ya Mathayo 17:21,
ambayo inasomeka: "Hakuna aya, kuna namba tu mstari mrefu ulio wazi". Mjumbe
yule alibabaika sana alipoangalia sehemu hiyo. Akaahidi kuwa angekuja
kuniona kwa mara nyingine tena ningependa kujua anasemaje kuhusiana na suala
hili.
Kwa kifupi, Wakristo hawako tayari kuukubali ukweli kwamba Maandiko yao
Matakatifu yamepotolewa kwa madai kwamba, ikiwa msingi utayumba na kutokuwa
na uhakika, je tutasimama juu ya nini katika siku za masaibu na mashaka?"
(Is the Bible Reliable?)
Sio hayo tu, bali kuna aya inayozungumzia juu ya kuyabadilisha maandiko
matakatifu katika maandiko hayo hayo:
"...ikiwa mtu yeyote ataongeza (au kufuta) neno lolote katika kitabu
hiki, Mungu atamuongezea balaa zilizoandikwa katika kitabu hiki".
(Ufunuo 22:18,19)
Ushahidi uko hapo, upo wazi na rahisi kwa kila mtu kuelewa. Ikiwa Mungu
aliwaongoza kwa ufunuo kuandika vitabu vya Biblia, hakuna shaka kwamba
wanadamu wameingilia na kubadilisha mambo mengi. Swali muhimu kabisa la
kumuuliza Mkristo ni kwamba:
Inawezekanaje kwa neno la Mungu
kubadilishwa, kuondolewa na hata kutupiliwa mbali kwa matakwa ya
mwanaadamu??
MWISHO